babu M
JF-Expert Member
- Mar 4, 2010
- 5,222
- 3,172
Mkuu,Kuna weza kukawa na sababu nyingi zinazopelekea kushuka kwa bei ya hisa za NMB, lakini hoja ya taasisi za serikali kupeleka pesa zao BOT lazima itakua ni mojawapo.
Kwakuwa sasa wewekezaji wanakadiria kupungua kwa faida ya NMB siku za mbeleni kutokana na NMB kupungukiwa na kiasi cha fedha ambacho alikuwa akizitumia kwenye masoko ya fedha kujipatia faida.
Sababu ingine inaweza kuwa ni mwelekeo wa serikali katika kubana matumizi lakini na mpango wa serikali wa kuhakikisha halmashauri pia zinaweka fedha zake BOT yaani Trasury Single Account.
Uwanzishwaji wa benki ya walimu unaweza kuwa umechangia kwa kuzingatia kwamba labda wateja wengi wa NMB ambao ni walimu sasa wataanza kupokea pesa zao kupitia benki hio, hivyo kuendelea kupunguza uwezo wa kifedha wa NMB.
Sababu zote hizi, pamoja na zingine zimepelekea watu kuamini kuwa faida ya NMB itapungua, gawio litapungua hivyo ni busara kuuza hisa kwa sasa, na supply imeizidi demand na matokeo yake bei ndio inashuka.
Soma watu wengine walichoandika. Hisa NMB zimeshuka kwa asilimia kubwa kati ya Feb15 na April15 wakati sababu ulizotoa unaihusisha serikali ya awamu hii ambayo aina hata miezi minne.
Chuki zako kwa serikali zinakufanya uanze kujidanganya wewe mwenyewe.