Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,410
Dar es Salaam. Bei ya hisa za kampuni ya uchimbaji wa madini ya Acacia imeshuka katika masoko ya hisa ya London (LSE) na Dar es salaam (DSE) ikiwa ni muda mchache baada ya kampuni hiyo kutangaza ripoti ya matokeo ya hesabu za fedha kwa miezi 12 iliyoishia Desemba, 2017.
Kampuni hiyo ilitangaza matokeo yake Jumatatu ya wiki hii sanjari na kumtangaza aliyekuwa Meneja Mkuu wa uendelevu, Asa Mwaipopo kuwa Mkurugenzi Mtendaji kwa Tanzania.
Kilio cha ukata kutokana na zuio la usafirishaji wa mchanga wa ‘makinikia’ kilitawala katika ripoti hiyo iliyotolewa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Peter Geleta .
Baada ya kutangazwa kwa ripoti hiyo, bei ya hisa za Acacia katika soko la hisa la DSE zilishuka kwa asilimia 0.92 kutoka Sh5,460 kwa mauzo ya mwisho siku ya Ijumaa ya wiki iliyopita hadi Sh5,410 Jumatatu jioni na kuporomoka tena kwa asilimia 0.74 hadi Sh5370 kwa bei ya mwisho ya siku ya Jumanne.
Kwa kawaida kudondoka kwa bei huakisi ufanisi uliofikiwa na kampuni husika ndiyo maana hata katika soko la asili la kampuni hiyo (LSE) bei ilishuka kutokana na wawekezaji wengi kutoonyesha nia ya kununua hisa hizo.
Katika soko la LSE Jumatatu saa mbili asubuhi kabla ya kutangazwa kwa matokeo hayo ya hesabu, hisa moja ya Acacia iliuzwa kwa GBX 175.65 (Sh5,484.02) lakini baada ya matokeo hayo bei ilishuka hadi kufikia GBX 142.75 (Sh4,449.9), bei ya mwisho siku ya Jumanne ilikuwa GBX 160.10 (Sh5013.9)
Kwa mujibu wa ripoti hiyo iliyotolewa na Geleta, Mwaka 2017 biashara katika kampuni hiyo iligubikwa na changamoto nyingi zilizosababisha kushindwa kutoa gawiwo kwa wanahisa wake kwani, akiba ya fedha ilishuka kutoka Sh700 bilioni hadi Sh180 bilioni, upungufu wa Sh520 bilioni kwa mwaka ukijumuisha ongezeko la kodi ya thamani.
Alisema kwa kuzingatia viwango vinavyotumika vya kihasibu, wamerudia mahesabu ya thamani ya mali zao kwa kulinganisha na vipengele vichache vya mpango uliyotangazwa na Barrick na Serikali ya Tanzania wakati wa makubaliano yao, matokeo yameonyesha kupungua kwa thamani ya mali zao zote.
“Athari kubwa ipo katika mgodi wetu wa Bulyanhulu kutokana na hatua ya kupunguza uzalishaji na uhai wa mgodi wenyewe. Upungufu huu umesababisha thamani ya sasa ya mgodi kushuka kutoka Dola za Marekani 1.2 bilioni hadi Dola 600 milioni,” alisema Geleta katika ripoti hiyo.
Chanzo: Mwananchi