Hili ni funzo jamani

Huyu kijana ambae ni kaka mshikaji kiaina kwa sasa baba yake alikua mfanya biashara. Biashara ilianza kunenepa wakati wa awamu wa pili, awamu ya tatu biashara ilikua nzuri kiasi ambacho msure aliamua kijana akasome nje baada ya six.
Alisoma first degree huko nchi za wenzetu. Akiwa mwaka wa pili katika masomo yake, hali ya afya ya mzee ilianza kuzorota. Akiwa kama mtoto mkubwa ilibidi arudi nyumbani. Amerudi Masters ilibidi aingie UDSM. Wakati yuko pale alikutana na mdada mmoja, baba yake akiwa waziri wa awamu ya nne. Mdada alibabaika na swaga za mamtoni za jamaa.


Mtaani kuna binti amemaliza six nae anamzimikia kaka vibaya sana mshikaji akawa anajipoza akija home lakini roho yake yote ilikuwa kwa mtoto wa waziri ambae alishampeleka mpaka kwao.
Wakati anafanya research yake alikuwa nyumbani muda mwingi, baba yake alimshauri kheri aoe kwakua ndiye kijana mkubwa na baba alisema kama sitaona wajukuu zangu angalau nishuhudie harusi yako, kama unavyoona afya yangu inaleta matata.

Lile wazo lilimuingia kijana. Amerudi Dar akaanza kumtafuta mpenzi, alipropose moja kwa moja. Binti kwa dharau sana alimwambia, khe wewe vipi, zaidi ya hivyo vi nguo, sijui simu, na laptop una nini cha maana, unaweza kunitunza mimi wewe? Kwa fedheha kaka wa watu aliondoka. Alirudi kwao weekend ile na kupropose kwa yule dada wa form six mtaani kwao. Kumbe mdada alikua anafunga na kusali lile jambo litokee.

Harusi ilikua nzuri kwani baba aliigharamia kwa uwezo wake wote, kijana alimaliza shule na kupata ajira nzuri. Alianza kumsomesha mke wake, mke yuko chuo bado anasoma, mtoto wa waziri analia anadai jamani ulikua ni utoto, mimi nina kazi yangu basi niko tayari kuzaa tu na wewe.

Nipe namba ya mtoto wa waziri. Kwanza waziri mwenyewe hakutumbuliwa hii awamu ya 5
 
stori za kutunga nimemanya hilo kutokana na uandishi wako,
lakin ni funzo zuri,
Nakumbuka mim iliwah kunitokea hiyo kuna dada nilitokea kuwa ktika mahusiano kwa muda kidgo mala akaanza visa vya hapa na pale mwisho akanitema kwa dharau na kejeli kibao nikambembeleza lakin wap kwa kwel niliteseka sana
nikapga moyo konde nikaanza maisha mapya nikakaa karibia mwez hiv mara naanza kumuona na gia na misele ya fujo kutka kuja kwangu,mpaka leo hii bado ananiambiaga kuwa bdo ananipenda but mi nilishamtoaga moyoni kitambo sana kwani sasa nina kimwana kingine kizuri tu tena kuliko yeye huu ni mwaka wa kwanza tangu niwe nae hajawah niletea maringo wala dharau na ananipenda sana
ndo huwa nakumbuka huu msemo"ULISEMA CHA NINI WENZIO WANASEMA WATAKIPATA LINI"
 
Sasa hapo tujifunze nini, hiyo ni life scenario ya kawaida
1. Mtoto wa waziri alikua yuko sawa kukataa ndoa cause life aliyokuliwa kuamini before ndoa ndoa lazima uwe independent. jamaa harusi yote alifanyiwa na baba yake

2. Dada wa form six inaonekana alitokea maisha ya kawaida kuamini ndoa ndio mkombozi so jamaa alikua anakaa nae mtaa mmoja so alimuona wa kishua sanaa.

3. Jamaa ni wale mali kazikutaa.
4. Kuna utoto flan( hakuna ukomavu wa akili) Decision nyingi zilikua zinafanyika na wazazi
 
Mie ilishanitokea pia wakati niko kigori haswaaa. ... sikumkataa jamaa kwasababu hakuwa na mbele wala nyuma laah bali nilimkataa kwa sababu ya inheritance disease kwenye uko wao. Thank God alikuwa mawazo sana maana aliniambia kila kitu yeye mwenyewe.... jamaa alinizimikia sana pamoja na mengine mengi nyingine ya sababu ya kumwaga ni kuwa na mahusiano ya urafiki wa wadada wengi wazi wazi akijitetea just friends hamna kitu na mie ndo namba one wake........ Wivu ulinishinda nikaona siwezi mitaala mapema hii. Pia alikuwa mtu wa kabila ambao kwao wanavalue sana kuoana wao kwa wao. Mie akaniambia wewe hakuna atayekugusa wewe ni mimi na mimi ni wewe. Ila akaniwarn kuwa mama yake mzazi anaweza asipende pamoja na dada yake..... nikaona cha kuanza stress kabla ya mahusiano nini..... nikamwambia I just want to be among your friends tuu nothing else.

Maskini jamaa hakuamini. .... hadi mwaka juzi alikuwa hajaoa sijui kwa miaka 2 hii sijasikia habari zake.

A friend in deed and a friend in need with no string attached!!

Kasie.
ulinifanya kitu mbaya sana we binti ila any way bado sijaoa nakusubiri tu
 
Yaani kama wanaona nilipotea kutokuwa na wao shauri yao kusema kweli. Wabarikiwe wawe matajiri na wawe fresh tu.
Mi na maisha yangu na wangu. Nakomaa kivyangu
 
Binti kwa dharau sana alimwambia, khe wewe vipi, zaidi ya hivyo vi nguo, sijui simu, na laptop una nini cha maana, unaweza kunitunza mimi wewe? Kwa fedheha kaka wa watu aliondoka.

Umenikumbusha T.O mmoja wa HESABU 4m4 na 4m6 alifika UDSM, akapenda mwanamke akapeleka vyeti badala ya maneno

"Mimi ndio T.O wa hesabu 4m4 na six, nakupenda sana dada"

Dada alichomjibu.., " uT.O wako huko huko na mama yako.."

Kijana akaondoka kwa fedheha kubwa kuliko huyo
 
Yaani hapo mwishoni ndo pamenoga haswa! Hata mimi ilishanitokea binti hataki kwenda na mimi wala hataki kunisindikiza nikienda home kwao kisa sipendezi kuambatana nae mwisho wa siku akawa yeye ndo wa kuja home bila chenga na yeye ndo anakuwa wa kwanza kusema nimsindikize.
 
Back
Top Bottom