Hii ni ishara tosha kuwa rais magufuli atakuwa na shida uchaguzi wa mwaka 2020

Mda kama huu ilibidi waanze kujiimarisha mapema sana sehemu za vijijini na ambako walipoteza kura nyingi kwa kunadi chama na sera katika maeneo hayo,kushirikiana iapasavyo katika shughuki za maendeleo,kuanza kupima wagombea wao kwa ngazi zote wanaokubalika na wananchi na kuwaandaa mapema kwa kampeni zijazo,inabidi waone kila saa moja inayopita kuwa ya thamani sana na kila dakika isipite bila kupata member mpya countrywide kwa njia yoyote, wasiishie kutatua kesi mahakamani na kuharibu muda mwingi katika kesi hizo,wenye nyadhifa wote katika chama inabidi wawe disciplined ili kuepuka usumbufu wa kukamatwa na kupoteza muda mwingi kwenye kesi,wahakikishe wamwjijenga ipasavyo vijijini ambako wanaonekana kupuuzia na kuishia kukosa kura muhimu.
Muhimu pia(japo linaonekana kutowezekana kiurahisi) vile vyama ambavyo vinajua vinakuwa wasindikizaji kila election waamue sasa kujiunga na wenzao walio juu yao kwa vyote ili kuongeza nguvu na kupunguza wastage of votes na voters distribution, ikiwezekana kuwe na vyama viwili tuu vya upinzani lakini chini ya makubaliano sahihi na yenye maslahi kwa uma na sio kikundi cha watu.
Pia huu mwaka ndo mwaka wa kuanza kupigania marekebisho mbalimbali katika vipengele muhimu vya katiba kama tume huru ya uchaguzi na hii ishu ya wakurugenzi makada kuhusika kwenye kutangaza matokeo since bwana yule haonekani kuipa sapoti katiba mpya.hapa ndo penye shida,at least wakiweza huu mfupa basi hata wakishindwa 2020 watakuwa wamepiga hatua kubwa kuelekea ikulu.inabidi waanze mapema hili swala na sio kusubiri few months before election ndo wademand free and fair electoral commission.
Tumechoka na vilio vyao kila uchaguzi,sasa ni mda wa kuanza ku-pave the way kuelekea kushika dola,warekebishe mifumo ndani ya chama ili kupunguza weakness zitakazopunguza idadi ya kura,huu ni mda wa kupalilia chama kionekane chama kweli na sio watafuta ruzuku or else wataishia kulialia every election.
 
Hata yeye hana mpango wa kuishi magogoni milele!yaani aendelee kulea watoto 50 million?no way!tena walalamishi hivi.baba mkopo halipi,njaa,dawa,nk atakuwa hayuko sawa.
 
Kwa nchi za kiafrika Kuingia Ikulu ni jambo moja na maamuzi ya wananchi ni jambo lingine na hapa mimi nazungumzia maamuzi ya wananchi na si nani ataingia Ikulu.
Wananchi wanaamua kulingana na aina ya wapinzani waliopo.
Kama tumewawekea wasanii,unategemea nini
 
Mwenye akili huhitaji kufanya utafiti mkubwa kujua kinachojiri nchini. Rais wangu tangu aingie madarakani ameonekana kutojali sana wana nchi. Pamoja na kwamba kuna mambo anafanya lakini kutojali walio mweka alipo imewakatisha tamaa wengi. Muda utaongea.

Nisemacho ni kwamba labda kama kuna namna nyingine ya kujipatia ushindi vinginevyo 2020 tuna taabu sana maana hata upande wetu kuna watu wamepoteza imani.
 
Kama anapopoteza mvuto ndo furaha kwako kwani 2020 unaweza na ww ukala nyama badala ya kumeza mate.
 
weka matokeo ya utafiti wako kuthibitisha,vinginevyo ni porojo tu
 
bado sarakasi zinaendelea wenzenu huku bara kuna mtu alianza kuwa na ndoto za kuwa RAIS tokea mwaka 1995 lkn mpaka leo bado anaota,mwezake kaingia kwenye kinyanganyiro mwaka 2015 na ameupata.
 
Nchi hii!kila mtu ni mtabiri,mwalimu,mwanasiasa,mwanasheria,daktari.....yote yawezekana tanzaniani.
 
Watanzania bora tupigane damu imwagike tupate katiba mpya itakayoleta Tume huru... Hz dhihaka za Juma Ponda Mali kwa wananchi ni kwa kuwa mahakama, vyombo vya ulinzi na usalama, NEC anaweza kuviamrisha anayo taka... Yaliyotokea Zanzibar kama hayajatupa funzo basi....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…