Hii naita 'upende utanunua usipende utanunua'. Mwaka wa kufosi watu hawana mchezo

MtotoKautaka

JF-Expert Member
Jul 16, 2018
274
737
๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚ Wakuu majuzi nilienda kumchek anko bush flani hivi one time.

Nilifika mida ya jioni, nikalala kesho yake asubuhi nikaamka ile kutoka nje nikaona msululu wa ma pikipiki na baiskeli watu wamebeba mafurushi.
Nikamuliza nikaambiwa ni wafanyabiashara na siku ile ilikuwa siku ya gulio au mnada.

Mida ya mchana kama saa 6 hivi nikamwambia anko tukazunguke zunguke kwenye mnada tunaweza pata cha kununua.

Tupo katika mizunguko mnadani tukaona kundi la watu wamekusanyika na katikati kukawa na majamaa wanapiga kelele na filimbi wakiuza nguo.

Sasa walikuwa wanatumia kauli ambayo ni tata yani walikuwa wanachukua nguo mbili mbili kama ni pens za watoto wanachukua mbili au wanachanganya pens na fulana halafu wanasema "hizi zote mbili jero, hizi zote mbili jero".

Sasa hapa mtu alikuwa akinyoosha mkono anarushiwa zile nguo na ukizidaka tu pesa unalipa.

Hii kauli ya zote mbili jero ilikuwa inautata mtu anakurupuka akidhani nguo zote mbili ni tsh mia5 kumbe majamaa wanauza zile nguo mbili tsh 2500 maana yake ni mbilijero.

Watu wanambinu katika biashara wazee hii ilinishangaza na kunifurahisha sana ๐Ÿ˜†๐Ÿ˜†
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom