Heko Rais Magufuli kwa msimamo thabiti. Shikilia hapo hapo. Kelele za Mlango Zisikukoseshe Usingizi!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
52,669
119,297
Wanabodi,
Kama nilivyowahi kushauri huko nyuma, mazuri tupongeze na mabaya tukosoe, hili ni bandiko la pongezi kwa Rais wetu mpendwa, Mhe. Dr John Pombe Joseph Magufuli, kwa misimamo thabiti na isiyoyumbishwa na kelele za mitandao kuhusu mmoja wa wateule wake, mchapakazi hodari, mtu jasiri anayejituma kwa bidii, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda, kutuhumiwa na mitandao ya kijamii na mchungaji wa kanisa moja kuwa ni mhalifu, mwizi, ameiba jina la mtu mwingine, na pia amefoji vyeti!

Kitendo cha rais Magufuli, kupuuzia tuhuma hizi, fitna hizi, majungu haya, kinahitaji pongezi za dhati. Hapa rais Magufuli, anatufundisha somo la uthabiti na kushikilia msimamo bila kuyumba, ni moja ya sifa muhimu za kiongozi bora.

Rais wa nchi anatakiwa kuwa ni mtu wa msimamo imara na sio kusikiliza majungu!.
Ila ikitokea kwako rais Magufuli, pamba za masikioni zikalegea, na sauti za kelele hizi zikapenya, ukazisikia na ukaamua kuzifanyia kazi kelele hizi na kuzifanyia uchunguzi, nakuomba sana umtendee haki Makonda kwa sababu hayuko peke yake anayetumia majina bandia ambayo sio majina yake halisi. Kwa haraka haraka wako mawaziri wako watatu ambao wote ni wanachama wa mtandao huu wa JF, nao pia hawakufaulu darasa la saba na wakasomea majina ya watu wengine ambayo wanayatumia hadi leo. And to be fair, clean and just, itisha vyeti vya shule ya msingi vya wateule wako wote, utashangaa!.

Kwenye hili la majina bandia, kwa vile wote ni watendaji wazuri, fanya kama alivyofanya rais Kikwete kwa mafisadi wa EPA, toa msamaha wa jumla kwa wote waliotumia majina ya bandia au majina ya wengine, waende tuu wakaape upya kwa majina yao halisi, kisha tengua teuzi zao za majina ya bandia na kuwateua tena kwa majina mapya, hakuna haja ya kuapa upya kwa sababu aliyeapishwa ni mtu yule aliyetamka "mimi" ile fulani bin fulani it's immaterial.

Hivyo nawaomba wana jf wenzangu tuungane nami kumpongeza rais wetu Magufuli kwa misimamo thabiti ya kutoyumbishwa na kelele za mitandaoni.

Jumanne njema.

Paskali
 
Siku hizi umebadili gia angani mkuu hongera sana.
 
Kaka, Msomi mwenzangu Pascal Mayalla, mitandao hujenga na kubomoa. Mitandao huibua na kufunika. Mitandao huanzisha na kumaliza. Mitandao hushtaki, kutoa nafasi ya kujitetea na kuhukumu. Mitandao ni nchi inayojitegemea, si ya kuibeza hata kidogo. Ujumbe wako umefika kama unavyotaka ufike.
 
walimu wetu mliohakiki vyeti vyao na kuona majina yao sio na kuwatemesha kazi zao bila kuwalipa chochote, muwarejeshe, la sivyo tutaonana 2020
 
Wizara ya ardhi kupitia Msajiri wa hati,ina jukumu la kusajiri "DEED POLL", hati za kubadilisha jina,na baada ya kuzisajiri,hulazimika kutangaza usajiri huo wa mabadiliko ya jina katika gazeti la serikali " GOVERNMENT GAZZETTE "

Hati hii huonyesha jina la zamani,na jina jipya la muhusika.

Tunataraji waziri lukuvi pia atakuwa sehemu ya mawaziri ambao watalitolea tamko suala hili,na maofisa wake waanze kupekua kumbukumbu husika na pia TCU,Vyuo vya uvuvi Nyegezi,Mbegani,Chuo cha Ushirika Moshi,

Pia UVCCM ambako aliwahi kuajiriwa,Wizara ya Utumishi wa Umma ambao alipata ajira ya Mkuu wa Wilaya,na sasa Ukuu wa Mkoa wasaidie kwa kuwa watakuwa na nyaraka zote.

Pia Wizara ya elimu kupitia NECTA wasilale usingizi,waandae nyaraka hizi.

Pia kamishna qa kiapo aliyemuapisha pia ajiandae kisaikolojia kufafanua jinsi muhusika alivyokuja kwake,na lengo lake la kubadili jina
 
Mayala maana yake ni njaa, huyu tayari keshanunuliwa, anatumia style ya " mixed Signals" ili kutuhadaa hapa JF, wakati kumbe anatetea upuuzi through confusing the subconscious minds.

Katika uandishi wa namna hii, msimamo wa mwishoni mwa makala ndo huwa lengo la mwandishi na siyo ule wa mwanzoni mwa makala, lakini mwandishi anatuhadaa hapa kwa kuwa anajua hapa JF tutamshukia kama mwewe akijireveal wazi.

Hii technique ya huyu jamaa ni kubuild the domino and destroy them
 

we paskali wewe, yani umeng'ata na kupuliza, hahahaha watz bana
 
Naamini yule Pasco wa zamani asinge andika hivi ,ila baada ya kuwa Pasco Mayala uwoga umekuwa mwingi, ndiyo maana umeamua kutumia fasihi .Anayejua kaelewa nini unamaanisha .Asante Pasco kaka mkubwa ni Mpenzi wa Mungu atasikia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…