NALIA NGWENA
JF-Expert Member
- Oct 6, 2016
- 10,571
- 13,399
".... Kila kipato kinapoongezeka na matamanio nayo yanaongezeka, hiki ndicho kinachosababisha ugumu wa maisha.
..... Nilipita hapa mjini juzi, kila baada ya gari mbili unakutana na namba 'E' zinafululiza kama tano ndiyo zinakuja namba nyingine.Nenda kalinganishe na miaka miwili au mingine huko nyuma"
"Zipo hatua tumepiga.Nenda hata benki unakuta viti vimejaa na wengine wengi wamesimama.
... Nenda kwenye harusi kaangalia, huko nyuma hata michango tu ya harusi ilikuwa inatupiga chenga wakati huo.
"Hili jambo la ugumu wa maisha kuanzia tu unapozaliwa ni mpaka unapomaliza. Ndio maana wanasema mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke siku zake za kuishi ni chache tena zilizojaa tabu.
Hamna siku hilo la ugumu litaisha ndio maana hata matajiri wakubwa duniani wanajirusha na kujiua."
Kubwa zaidi tunaloliangalia kama serikali ni uwekezaji mkubwa unaoelekezwa kwenye shughuli za uwekezaji kwasababu huo unaenda kupunguza pengo kati ya walionacho na wale wasionacho.
"...Uwekezaji unaolenga kwenye kukuza sekta binafsi na kwenye sekta inayoajiri watu wengi zaidi ndio unaotoa jawabu la kudumu kwenye maisha na ustawi wa watanzania.
- Mwigulu Nchemba
Waziri wa fedha Tanzania
Maswali yangu: je ni kweli uchumi wa nchi hupimwa kwa kutazama kumbi za harusi, namba E za magari barabarani?!
Kama ni hivi tuna safari ndefu sana katika taifa let hili (Tanzania).