Juzi niliandika thread hapa jamvini yenye kichwa cha habari kisemacho: Waziri Nape, hizi kelele za kulipishwa vifurushi kutizama local channel kwenye ving'amuzi huzisikii?. JamiiForums wakamtafuta Waziri Nape naye akaahidi kulifanyia kazi.
Itakumbukwa kwamba channel zote za ndani ziliondoka hewani kwa zaidi ya mwezi sasa na ili uzipate ulilazimika ununue kifurushi jambo ambalo ni kinyume na tamko ambalo serikali ililitoa kwa makampuni ya ving'amuzi kwamba local channel zote zipatikane bila malipo.
Hatimaye king'amuzi cha Startimes kimerudisha channel zote na ndani na zinapatikana bila yakununua kifurushi.
Tunaishukuru serikali lakini pia hili lisiiishie kwa startimes pekee, tunaomba Waziri wa Habari, Mh. Nape na Waziri wa Mawasiliano, Mh. Mbarawa kwa umoja wao wahakikishe na makampuni mengine ya ving'amuzi kama AZAM na wengineo nao warudishe hizi channel za ndai zionekane bila malipo.