Hatimaye sasa ni Gabon mpaka Karume Stadium na siyo tena Gabon mpaka Kombe la dunia!

Mkuu nadhani hujanizidi Mimi kwa kufurahi kutolewa Kwetu. Manake sasa ilikuwa Kero humu mitaani na katika Maredio kwani kila mara tu utasikia Gaboooooooon.....mpaka......Kombe la dunia na bila shaka kuanzia Kesho tutasikia kauli mbiu mpya ya Gaboooooooon........mpaka........Karume Stadium.

Wewe Timu hata bado haijawa na Mafanikio tayari Kamati Kibao zimeundwa kumbe Kamati zenyewe ni za kupiga / kula tu Pesa.
Hahahahaaaaa
 
Wewe Kocha kafundisha tu kwa muda Timu ya VPL JKT Ruvu mechi 8 kafungwa 6 na katoa sare 2 tu halafu leo mnampa Timu ya Taifa akafundishe wakati wapo Makocha bora zaidi yake ambao pengine wangetufikisha mbali kama Seleman Abdallah Matola a.k.a Veron a.k.a Mzambia au Mzee Abdallah King Kibaden na Serengeti Boys ingefika mbali na hata kumbe Kombe la dunia nchini India tungeenda.

Eti Bakari Shime nae ni Kocha kabisa wa mpira wa miguu. Akhsante sana Niger kwa kututoa Tanzania kwani tayari Timu yenyewe ilishaanza kufanywa kama vile Kitega Uchumi cha Kundi fulani la Watu huku wengine wakiitumia kama ngazi yao ya Kisiasa na kulikuwepo na Unafiki mtupu ndani ya Timu, Uongozi wa TFF na Kamati nzima ya Saidia Serengeti Boys.

Gaboooooooooooon..........mpaka...........................Karume Stadium..................kudadadeki.

Leo nimeamka na furaha sana na sasa nakuwa Mshabiki wa Timu ya Taifa ya Niger.
 
Ila wamejitahidi vijana wetu pamoja na kutoka. Binafisi nawakubali hawa kuliko kaka zao.
Wakiendelezwa vizuri watatutoa
Hakuna atakayewakumbuka tena. Hata yule aliyesimamia michango.
Nilivyowaona tu leo wanaingia pale Uwanjani hasa vyumbani huku wakiwa wanashangilia kizembe kizembe na kuimba nyimbo za Mafirauni fulani hivi wa Bongo Fleva nikajua mapema tu kuwa tayari nuksi imeshatukuta na hatuna chetu. Halafu kuna Vichezaji fulani hivi viwili vya Serengeti Boys vilikuwa vimeshaanza kujiona kama vile akina Messi na Ronaldo kwa kuwa na mapozi ya hovyo hovyo na kuota majipu ( kuanza kuringa na kujisikia ) kana kwamba wameshafika Kombe la dunia.

Warudi tu kwakweli tuendelee tu kula nao bamia, kisamvu, matembele yetu na maharage kwani ndicho tunachokiweza na siyo mpira. Mnatusumbua tu kila siku katika Radio na Tv kuwa tuwachangieni halafu tunajinyima mnaenda huko mnaishia tu kumbwela mbwela. Tena TFF na Malinzi kesho asubuhi tu nakuja Karume hapo Ofisi zenu za TFF kuchukua Pesa yangu ya mchango kwani nilitoa ili Timu ifanikiwe na siyo iishie njiani kama hivi. Kesho nataka Pesa yangu tafadhali!
 
Haya ni matunda ya siasa na upendeleo ktk soka na ubinafsi ktk nchi yetu.hatuwezi fanikiwa kwa jambo llt maana nchi yt haina baraka toka kwa mungu.
 
Sidhani kama ni sahihi kuwatukana kiasi hiki, kwakuwa ndo mara yao ya kwanza kushiriki tuwapongeze hapo walipofikia.

Kwani tulitegemea waishie hatua gani??
 
Kitendo cha Kocha cha kuingia na mkakati wa kulinda huku akijua ile mechi ilimpasa kushinda kwakweli hata nilitabiri kufungwa baada tu ya dk 5 kuchezwa. Huwezi weka mtu mmoja tu mbele na huku wenzio wanajua wana nafasi pia ya kufuzu. Hii mechi lawama ni Kwa kocha
 
Back
Top Bottom