KENZY
JF-Expert Member
- Dec 27, 2015
- 30,263
- 69,502
Angalizo: bandiko hili linahitaji utafakari wako na sio hisia ama uchama na uchawa!.
Binafsi sina Imani sana na vyama vya siasa katika makuzi ya nchi haswa kiuchumi. hii nikutokana na namna vinavyoenenda,hulka za wanachama wengi wa vyama hivyo n.k.
Nimeuangalizia upinzani kwenye nchi yetu kwasababu ccm tayari tushaijua!,kama namna yauendeshwaji wa chama hichi tawala haina tofauti sana na vyama hivi pinzani sitashangaa siku upinzani ukishika nchi nayo ikafanya yaleyale!.
Imani yangu ktk pumzi za nchi naamini inashikiliwa na usalama wa taifa (engineering in everything), wakishirikiana na jeshi lakujenga taifa na vyombo vyengine vya usalama.
Hivi vyombo vyote vya usalama ndio ngao, njia na ni kama Sheria ya yeyote yule atakaepata cheo cha kisiasa lazima aenende na matakwa ya nchi kama ilivyoelekezwa na Sheria.. hawa watabaki kuwa waangalizi wa mwenendo, washauri na wasimamizi wa masilahi ya taifa.
Kelele tunazosikia za upinzani sitokuja kushangaa siku wakipata madaraka nao wakaufyata halafu ccm ndio akawa mbwatukaji!.
Kama vyama vyetu vinanjaa tusitegemee shibe watakaposhika usukani!.
Kama hakuna wakuvisimamia hivi vyama kivitendo basi maendeleo tutayaona kwa nchi zilizoendelea!.
Ukiona mtu yupo kwenye chama chochote na chama chake kikakosea jambo nae asifanye lolote kuhusu hilo kosa,aidha kulitatua,ama kuwajibisha n.k ndugu jua huyo mtu yupo kimasirahi hana uzalendo wala upendo..
Wewe mwanachama mdogo wa chama chochote nikupe tu taarifa jua unatumika sana tu kuwasukuma waliokuzidi wazidi kukaa juu yako!. Wewe utakalishwa kwenye vikao vya uzalendo halafu wao watakaa pembeni wakutenge kwenye vikao vyao vya namna yakuila nchi!..
Nakumbusha tena hili andiko ni la utafakari....
Watu huongozwa kutokana na namna walivyoendelea ktk nyanja mbalimbali aidha walivyoendelea kiuchumi na kielimu!,na ndio maana huwezi kusikia siasa za maji taka na madawati kwenye siasa za nchi kama USA!.
wao waambie kuhusu usalama,uchumi,sayansi n.k ktk namna ambayo imeendelea sio uchumi wakuuziana mitumba!.
Tunapigwa na hawa wanasiasa wetu kwasababu wanajua bado tumelala!,laiti kama tutabadirika sisi hata wao hawatakuwa nabudi yakubadirika waendane nasi!.
Muda mwengine sisi wananchi wakawaida tunayakwamisha maendeleo yetu wenyewe kwasababu tunashikilia bendera za vyama na sio bendera ya taifa!.
Hatuzungumzi kuhusu Tanzania tunazungumza kuhusu vyama!.
Kaa ukijua kelele unazowasaidia kupiga wewe hautanufaika nazo bali wao!.. kesho yako itadidimia na yao itaimarika!.
Si walikuambia kura yako inathamani?
Ndio inathamani lkn haitakuwa na thamani kama itatumika kutuletea mijitu ya hovyo!,kura yako lazima iwe inamatokeo ya kesho yako na vizazi vijavyo!.
Tutoke kwenye fikra za kupata nabii wakisiasa ndio aje atubadilishie upepo ambapo kesho asipokuja nabii tunalia na nyimbo zilezile!.
Tunapotakiwa hivi Sasa ni kufika kule ambapo hata lisimamishwe jiwe ama boya kwenye kiti kikuu,basi tule na tunywe kama inavyotakikana kwamaana mfumo hautegemei nabii mmoja ambae ataharibu au atapatia!.
Siamini kwenye kunywa maji yabendera ya chama chochote cha siasa bali naamini kwenye kunywa maji yabendera ya taifa langu.