sinza pazuri
JF-Expert Member
- Aug 16, 2014
- 2,953
- 8,465
Wote tunajua kwenye mchezo wa boxing hajawai kutokea bondia mwenye uwezo wa kupigana ngumi hapa bongo kama Mwakinyo.
Dunia nzima inajua Hassan ndio alama ya boxing hapa Tanzania. Ndio biashara kubwa ya ngumi East Africa ukitaka kufanya biashara ya ngumi na upate hela isiyo na longolongo basi mtumie Mwakinyo.
Mwakinyo kaitoa boxing kwenye fight za kwenye bar za Keko na Manzese mpaka ngumi zinapigwa Masaki.
Huwezi mpandisha Hassan ulingoni eti apiganie gari anaijua thamani yake.
Na tatizo ndio linaanzia hapo watu wanashindwa kumtumia kwa urahisi hivyo wanapigana vita ya kumpoteza.
Mnataka mpoteza Mwakinyo ili mbaki na nani?
Anachopitia Mwakinyo alishawai kukipitia Diamond.
Kuna wakati Diamond alipigwa vita na kila mtu kama sio mashabiki wake kusimama nae leo hii tungekuwa tunaongea mengine na sababu walizotoa ni hizi hizi.
Anaringa sana, anajiona mkubwa, anavimba, muda wake umeisha ila aliwaprove wrong na wengine kwa sasa wapo kwenye team yake wanajifanya wanampenda kuliko ndugu zake amebaki kuwachora na kuwagawia riziki.
Mwakinyo awe makini sana na acheze game yake very smart, yupo kwenye nchi iliyojaa watu wenye chuki na roho mbaya zisizo na sababu.
Waswahili ni watu wa kuyakadilia mafanikio, kuna mstari wa mafanikio ukiuvuka hata wale waliokupeñda wanageuka kukupiga vita upotee. Huo ndio uhalisia. Na sasa Mwakinyo ana mtihani wa kupambana na ili kundi ambalo limekuwa kubwa likifanya jitihada apotee kabisa.
Tanzania ni nchi iliyojaa watu wajinga, ujinga ukaleta ugonjwa wa roho mbaya na husda na ikifika wakati wa kumuadabisha mtu mwenye mafanikio uwa wanaungana wanakuwa wamoja.
Kwa sasa asipokuwepo Mwakinyo hakuna mwingine wa kukaribia brand yake ila wenye chuki wanaona bora tubaki na kina Kaoneka. So sad ila ndio taifa letu lilivyo.
Naamini ili suala la Mwakinyo litaisha ila inabidi awe makini sana, na fight yake atayopambana hana option nyingine zaidi ya kushinda. Bila hivyo itakuwa ni sherehe kubwa kwa wenye chuki na roho mbaya.