Hamas; Iran ni mshirika wetu wa kweli mashariki ya kati

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
9,784
20,155
Mwakilishi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) hapa Tehran amesema kuwa njia pekee ya kukabiliana na utawala wa Kizayuni ni kuendeleza muqawama na kwamba ishara ya wazi zaidi ya mapambano hayo ni Intifadha.

Khalid al Qaddumi Mjumbe wa Hamas hapa Tehran amesema katika kikao cha wataalamu chini ya anwani 'Palestina na Mustakbali Wake,' hapa Tehran katika kukaribia tarehe 18 Januari ambayo ni siku ya 'Ghaza Nembo ya Muqawama wa Palestina' kwamba, harakati ya Hamas inaendesha harakati zake za muqawama katika ngazi zote kuanzia watoto hadi watu wazima, na kuwa vyama na makundi ya mapambano kutokana na kuweko umoja na mshikamano wa ardhi yote ya Palestina, kamwe harakati hiyo haitaruhusu Palestina igawanywe vipande vipande.

Khalid al Qaddumi amesema njia pekee ya kukabiliana na utawala wa Kizayuni ni kundesha muqawama na Intifadha na kwamba, katika njia hiyo muungaji mkono wao wa pekee katika eneo ni Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Mwakilishi wa Harakati ya Hamas hapa Tehran amesema kuwa misimamo ya ukingaji kifua ya serikali ya Marekani kuhusu utawala wa Kizayuni na mipango ijayo ya rais wa nchi hiyo Donald Trump ambayo imeitia wasiwasi jamii ya kimataifa, inaonyesha namna Marekani ilivyo bega kwa bega katika kuusaidia utawala wa Kizayuni na kuwapinga Wapalestina.

Khalid al Qaddumi amekosoa pia kitendo cha baadhi ya nchi za Kiarabu cha kuhuisha uhusiano na utawala wa Kizayuni; na kusisitiza kuwa migogoro na mapigano yanayoshuhudiwa katika nchi za Kiislamu za eneo la Mashariki ya Kati yamepelekea kutopatiwa kipaumbele kadhia ya Palestina kimataifa.

Source: IRIB
 
Ndiyo Iran amekuwa akimsaidia Hamas na Hizbollah muda sasa. Na ipo wazi tu. Lakini nini hatima ya hii mambo? Hao Hamas wakiishia kulipua watu haitasaidia sana kuwashinda Israel. Kila siku Israel wanaongeza makazi yao. Wanazidi kujiimarisha. Wanazidi kushinda vita. Hamas wanabaki na taswira ileile yakuonwa magaidi. Au wanataka wawe wanaharakati wakujitoa muhanga miaka nenda rudi bila kuaccompkish jambo kubwa kwa watu wao/interests zao wanazotetea? Bora watafute njia nyingine tu. Kukaa chini nakupatana kama binadamu? Au ndiyo itakuwa udhaifu? Israel nao vinjwa ngumu kwelikweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…