Hali ya Fedha mfukoni ni mbaya kwelikweli, Kwenu vipi waungwana?

Jamani siasa ni maisha, Ebu tuelezane wajasiria mali wenzangu.

Hii hali ya mfukoni mnaionaje? Mbona mifuko ya watu nahisi imetoboka sana. Namaanisha mfukoni hela wengi hawana. Nina ka biashara kangu sehemu flani ki ukweli pato limeshuka mpaka naingia uoga.

Tatizo nini haswa? Kila ninayemuuliza analia kama mimi. Baadhi wanasema nisubiri Bunge la bajeti lipitishe 2016/2017 najiuliza upo uhusiano kweli?

Hali ikiendelea hivi, Pango linaweza kuwa mtihani achia mbali watoto shule na mahitaji yao muhimu.

Naomba Mungu na kule Zanzibar patokee maridhiano maana wafadhili nao wakifunga koki ndio balaa zaidi.

Mungu atusaidie wakuu hali ni ngumu kweli kweli sijuwi tu kwenu.

Hii inaweza kuwa ni habari nzuri sana kupostiwa humu kwa muda mrefu; kama ni kweli.
 
Mkakati wa serikali kupeleka account zake BOT unalenga kuzuia/kupunguza ufisadi na kuifanya pesa kuwa "adimu".

Lengo; sarafu ya Tanzania walau ipande thamani.

Sasa itakapofikia kipindi pesa haikamatiki kabisa hapo tutaanza kutafutana mijini. Halafu bei ya bidhaa itashuka sana mpaka kina dd poa nao wataona uchumi hawajaukalia tena.
.
.
 
Jamani siasa ni maisha, Ebu tuelezane wajasiria mali wenzangu.

Hii hali ya mfukoni mnaionaje? Mbona mifuko ya watu nahisi imetoboka sana. Namaanisha mfukoni hela wengi hawana. Nina ka biashara kangu sehemu flani ki ukweli pato limeshuka mpaka naingia uoga.

Tatizo nini haswa? Kila ninayemuuliza analia kama mimi. Baadhi wanasema nisubiri Bunge la bajeti lipitishe 2016/2017 najiuliza upo uhusiano kweli?

Hali ikiendelea hivi, Pango linaweza kuwa mtihani achia mbali watoto shule na mahitaji yao muhimu.

Naomba Mungu na kule Zanzibar patokee maridhiano maana wafadhili nao wakifunga koki ndio balaa zaidi.

Mungu atusaidie wakuu hali ni ngumu kweli kweli sijuwi tu kwenu.
acha kutuzuga hapa wewe kizalia cha mafisadi. Mramba yuko uraiani.
 
Ukiona mafuta yameshuka bei,Dollar imeshuka na stock market haiendi vizuri basi ujuwe mbele kuna giza nene. mwaka huu vijana fungeni mikanda tupo kilimani twapanda
 
Hali unafanya wtu wote kumuabudu mtu mmoja, na yeye anajiona, tunamfeel shida sana!
 
Yaan nina kagoli sehemu.wadau wamekuwa wakutoa tu pesa kwenye line zao hamna kuweka, tena pesa zenyewe kumi kumi kushuka, sjui nn tatizo???
 
Nimepita juzi kinondoni B Nikashangaa jinsi vishowroom vikiwa tupu hakuna gari ndani vimefungwa.
Kwan nn tatzo??
 
Mwanangu nimeajiriwa mpaka leo tar 8 macho kodo!,no mshahara!;Nshapiga mizinga mpaka mzunguko imeisha!,leo sikwenda mzigoni nimesingizia naumwa lo!,sijui hii hali itakuwaje coz mshahara ukiingia tu imeishia kulipa madeni.
 
Hali sio mbaya kwa wote. Mie kwangu hali ilikuwa ngumu mwezi wa 1 tu. Ila ilipoingia mwezi wa 2 mambo yako poa. Napata pesa vizuri.
Nachofanya ni kuweka akiba tu. Dili zikikata nisilie lie.
 
Kashata zinekuwa dili mjini hapa.......ukipata kahawa yako na kashata mbili...mbili zingine unaziweka za akiba......siku imekwisha hivyo....
 
Ngoja leo nikaongee na kinyozi anikopeshe huduma ya kuninyoa maana mzuzu unazidi kuwa mkubwa balaa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom