blessedester
New Member
- Jun 8, 2024
- 1
- 0
Ni nini sababu ya uwepo wa hili giza? Nani aliitaka nuru na wakati ni giza hilohilo liliwaficha dhidi ya uovu wao , Pengine giza lilitengenezwa liulinde mfumo nufaika. Nini ni kikwazo cha waokutoka maofisini na kwenda barabarani kuhubiri kuhusu kodi? Abadani! na mashati meupe waliyovaa hayaruhusu wao kufanya hivyo ni bora pia hawakutoka maana siku waliyotoka ilikuwa ni mshikemshike kwa wafanyabiashara , ni huzuni kwa taifa langu.
Hivi Mamlaka haina kurugenzi ya elimu kwa umma juu ya suala zima la ulipaji kodi. Mamlaka inalo panga mkononi na lina makali kweli kweli tunaona hasa lakini Inafanya nini kuhakikisha inazalisha walipa kodi wapya na kuhakikisha wanakuwa wakubwa bila kusahau ustawi wa wafanyabiashara wakongwe, au ni uhasimu unaopelekea mpaka kukosekana kwa uaminifu na hatimaye janjajanja kuzaliwa ili mambo yaende. Ni huzuni siku atakayokamatwa bila kuangalia mimba ya hili tatizo ilipotungiwa kama si biashara kutaifishwa basi atakiona cha mtema kuni .
Lakini vipi kuhusu makadirio anayofanyiwa mtu anayetaka kuanza biashara ni kilio kikubwa bado mizunguko na danadana anazopigwa mtu mpaka apate leseni ya biashara , ilipaswa iwe rahisi mno !vipi kama jopo lote linalohusika na kodi na leseni mngekaa pamoja kwa kila wilaya? Nidiriki kusema kuanza biashara na kulipa kodi hakitakiwi kuwa kitu chenye ukakasi katika nchi yangu.
Mfanyabiashara akipatiwa elimu na mazingira wezeshi atalipa kodi kwa tabasamu na kwa wakati. Na makadirio kwa mfanyabiashara anayechipukia isiwe ndio kiyama chake tumeona watu wengi wakifunga au kuacha biashara kwa sababu ya kodi kuwa mzigo mzito kwao! Ni huzuni mno.
Wakati umefika sasa mtoke maofisini mkatoe elimu kuhusu kodi mzunguke kila mahali kuanzia shule za msingi mpaka vyuoni, maofisini, masokoni makanisani na misikitini na hata barabarani ndio barabarani tuweke maspika mabango na matamasha kwa wingi mpaka tutakapo hakikisha Mtanzania ana uelewa kuhusu Kodi na kazi ya mamlaka na kwamba mamlaka sio adui kwake. Amani ya kukaa maofisini mkipulizwa na viyoyozi mnaitoa wapi wakati mteja wetu hana taarifa za kutosha kuwahusu?
Soko limekuwa gumu wafanyabiashara wanadiriki kuoga barabarani kufanya matangazo’ Wafanyabiashara ni wateja wenu mnatakiwa muwape thamani kwenu inatakiwa iwe sehemu ya kimbilio iliyo salama kwao muumie mkisikia au kuona biashara imefungwa .Inashangaza tena mno na inafikirisha na mlangoni mwa ofisi zenu kuna ulinzi mtu akichelewa kufika haruhusiwi kuingia.
Ajabu mno na tatizo la mtandao lisipokuwepo basi ni bahati, hamuwezi kuwa na huduma ya masaa 24? Kuzalisha na kuwalea wafanyabiashara wachanga mpaka wakue badala ya kuziua hizo biashara wanazo anzisha ?
Kutoa elimu kuhusu kodi na kuandaa mazingira wezeshi kwa wafanyabiashara ili kodi ilipwe kwa tabasamu? Mmezidiwa nguvu na wauza viwanja na watoa mikopo walioweka maspika na mabango kila sehemu’ Tuingaze Nuru kwa ajili ya Tanzania yetu ya leo na kesho kwaajili ya vizazi vyetu .
Tujifunze kwa wenzetu waliotuzidi ama hakika si vibaya kukiri udhaifu tujitafute tujue wapi tulipokosea badala ya kummulika mfanyabiashara mithili ya mwizi na kufanya magendo kuzaliwa, fedha kufichwa ndani, na mengine mengi yasiyo na afya kwa Taifa hutokea.
Ukweli usemwe mtu kuanza biashara kumekuwa kunawazisha mno hasa kwa sababu watu hawana uelewa juu ya nini kianze nini kinafuata mpaka hitimisho lake huwa ni kukata tamaa, Tokeni maofisini !
Vitu vya msingi vimekaliwa kimya purukushani, kutokuwajibika,ukandamizaji na unyonyaji unaendea kimyakimya, wakati MTANZANIA akijipambania ajikwamue dhidi ya hali ngumu ya maisha mara anapoanza kuangaza giza nalo humnyemelea limmeze.
Je ni mamlaka imefeli au ni hakuna anayejali ? Lazima mamlaka itakuwa chini ya wizara Je wizara haioni? au hakuna anayejali, si kweli kwamba wizara haioni, lakini lazima kwa pamoja tujifunze kujali maana huko ndiko shida zetu nyingi zitatatuliwa, huko ndiko ajira zitazaliwa kwa watu kuanza biashara kutakapo pelekea kodi kulipwa kwa wakati hatimaye shule na hospital zitajengwa, miundombinu na upatikanaji wa maji na umeme hautakuwa wa maruweruwe tutakwenda mbali zaidi ambapo hatutakwenda kuomba mikopo kwa ajili ya maendeleo kama inavyosemwa’ ndio mikopo na misaada tunayoomba kila uchwao basi kama hatuacha kabisa walau kwa kiasi fulani kidogo.
Nafahamu hakuna nchi iliyoendelea bila mikopo basi angalau tuwe na kiwango. Giza lifike tamati Nuru itawale tuandae watoto kwa kuwapatia elimu na namna nzuri za kulipa kodi ziwekwe. Watanzania ni wazalendo hakika na wanajivunia hilo basi mfumo usiwanyime haki yao ya msingi ya kulipa kodi tokeni huko kwenye mahandaki yenu muwaelimishe, mazingira rafiki na wezeshi yaandaliwe kwa ajili ya kulipa kodi tutafika mbali hata kupokea gawio kutoka Mamlaka! ni kama inachekesha lakini inawezekana’
Mashati meupe na suti mzivue sasa tujivikwe magwanda tuingie kazini, kazi ya ndoto ya kila kijana sasa muifanye kwa uchungu mnajua hasa panapovuja mpazibe tufike nchi ya ahadi kwa kuliondoa Giza hili lililodumu kwa miongo sasa, itachukua muda pengine inaweza ikawa ngumu pia maana Nuru inaweza kuziba mianya na hamjazoea ukata mjitahidi kuwa Wazalendo kama ambavyo mnatuambia tukija ofisini kwenu.
Picha kutoka ukurasa wa instagram wa masoud kipanya chapisho la 27 may 24