Raia Fulani
JF-Expert Member
- Mar 12, 2009
- 11,328
- 3,486
Gazeti lenu la leo tar 10/10/2024 ukurasa wa 18 kuna makala inasema "Kiasi cha mwinuko kinachofaa kwa basement kwenye ujenzi".
Sasa nikawa natafuta kiasi hicho cha mwinuko wa kitaalamu ambao utakuwa umeelezewa kwenye makala na ndugu mleta makala.
Anaweka maelezo mengi na ajabu anamalizia kwa kusema ikiwa unahitajikufahamu kama eneo lako limetimiza vigezo unapaswa kuchukua mtaalam wa usanifu majengo na kufika nae eneo hilo.
Sasa nini maana ya kuweka makala yenye kichwa hicho.cha habari? Nilidhani mleta angemtafuta huyo mtaalam na kufanya nae mahojiano na angalau tupate kwa muhtasari huo utaalam.
Mwananchi nao wakachukua habari kama ilivyo na kuiweka gazetini. Mbona kuna makala nyingi tu huwa mnaweka zenye uchambuzi wa kina hadi msomaji anaridhika?