Kuelekea 2025 Gazeti la Mwananchi: Sekretarieti ya CCM Imejaa Watu "Machawa"

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
58,795
69,460
Kwa mujibu wa maelezo ya gazeti la Mwananchi wakinukuu maoni ya Luqman Moloto anasema Sekretarieti ya CCM Imejaa Watu "Machawa" au Tegemezi ambao wanakitegemea chama kuliko Chama kuwategemea wao ukilinganisha na Wapinzani.

My Take
CCM ni chama Pendwa, maoni haya yanaonesha Mwananchi ni Mwanachama wa CCM hivyo kuelekea Uchaguzi angependa kwenye Sekretarieti ya chama wajae watu wenye majina.

Maoni haya yachukuliwe Kwa tahadhari.

====

1728990176919.png

Dhana ambayo Hayati John Magufuli aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) alianza nayo, kwamba yeyote anaweza kuwa kiongozi CCM, tena akatamba kupitia uvumi kuwa Bashiru alikuwa mwanachama wa Cuf, kwa sasa inaonekana kuchukua sura mbaya. Hivi sasa sekretarieti ya CCM inaundwa na wajumbe ambao hawajulikani. Watakiuzaje chama?

Hivi karibuni aliyekuwa Katibu Mkuu CCM, Daniel Chongolo, alijiuzulu wadhifa wake kwa kashfa ya mambo binafsi ya kijamii. Hata ungemrejesha Chongolo leo ofisini, bado humwoni kama alitosha kupimana ubavu na viongozi wa kariba yake waliopo upinzani.

Katibu Mkuu Chadema, John Mnyika, kiongozi wa idara za chama kwa muda mrefu. Akawa Naibu Katibu Mkuu, mbunge vipindi viwili kabla ya kuwa Katibu Mkuu.

Chongolo, alikuwa msaidizi binafsi wa Nape, alipokuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi, akawa mkuu wa wilaya, kisha katibu mkuu. Je, unaweza kuwalinganisha Mnyika na Chongolo?

Naibu Katibu Mkuu Bara, Anamringi Macha, Katibu wa Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Rabia Hamid, Katibu wa Oganaizesheni, Issa Gavu, Katibu wa Uchumi na Fedha, Frank Haule, wana msuli wa kuiuza CCM au wao ndiyo wanaotegemea chama kijenge wasifu wao wa kisiasa?

Mwananchi
 
Kwa mujibu wa maoni ya gazeti la Mwananchi ni kwamba wanasema Sekretarieti ya CCM Imejaa Watu "Machawa" au Tegemezi ambao wanakitegemea chama kuliko Chama kuwategemea wao ukilinganisha na Wapinzani.

View: https://www.instagram.com/p/C1oAZelIWG7/?igsh=NmJiYWZiY2E0Mg==

My Take
Ccm ni chama Pendwa,maoni haya yanaonesha Mwananchi ni Mwanachama wa ccm hivyo kuelekea Uchaguzi angependa kwenye Sekretarieti ya chama wajae watu wenye majina.

Maoni haya yachukuliwe Kwa tahadhari.

Ccm kama chama hakina nguvu yoyote nje ya siasa za kubebwa na Dola. Hata hao inaosemakana hawana ushawishi, hawana lolote la kuhofia maana wanajua hicho chama hakishindi kwa ushawishi, Bali kwa nguvu ya Dola. Dhalimu magu alikuja kudhibitisha hilo.
 
Kwa mujibu wa maoni ya gazeti la Mwananchi ni kwamba wanasema Sekretarieti ya CCM Imejaa Watu "Machawa" au Tegemezi ambao wanakitegemea chama kuliko Chama kuwategemea wao ukilinganisha na Wapinzani.

View: https://www.instagram.com/p/C1oAZelIWG7/?igsh=NmJiYWZiY2E0Mg==

My Take
Ccm ni chama Pendwa,maoni haya yanaonesha Mwananchi ni Mwanachama wa ccm hivyo kuelekea Uchaguzi angependa kwenye Sekretarieti ya chama wajae watu wenye majina.

Maoni haya yachukuliwe Kwa tahadhari.

Dah ni uchambuzi mzuri sana. Hakika Dkt Magufuli aliharibu chama. Pamoja na nia yake nzuri ila kuleta mamluki ndani ya chama imekigharimu chama sana
 
Liko wazi kabisa!
 
Dah ni uchambuzi mzuri sana. Hakika Dkt Magufuli aliharibu chama. Pamoja na nia yake nzuri ila kuleta mamluki ndani ya chama imekigharimu chama sana
maji yako shingoni nini? Magifuli alitengeneza taswira ya chama kutoka zomea zomea mpaka jezi za mitoko na akashinda kwa 84% na 99.9% wabunge na 99.5%madiwani na wenyekiti usiige kunywa kwa tembo utapasuka msamba
 
Kampeni Yako imeishia wapi? Mbona umekata moto mapema sana? 😆😆😆😆

Mwendazake ni hovyo tuu aliharibu chama
 
Kwa mujibu wa maoni ya gazeti la Mwananchi ni kwamba wanasema Sekretarieti ya CCM Imejaa Watu "Machawa" au Tegemezi ambao wanakitegemea chama kuliko Chama kuwategemea wao ukilinganisha na Wapinzani.

View: https://www.instagram.com/p/C1oAZelIWG7/?igsh=NmJiYWZiY2E0Mg==

My Take
Ccm ni chama Pendwa,maoni haya yanaonesha Mwananchi ni Mwanachama wa ccm hivyo kuelekea Uchaguzi angependa kwenye Sekretarieti ya chama wajae watu wenye majina.

Maoni haya yachukuliwe Kwa tahadhari.

Ni kweli wamejaa machawa na wafitinishaji ili wapate tu maslahi yao sio kwa maslahi ya Chama !!
 
Hahahaha ila inawezekana maana hata Dkt Samia kuwa makamu haikuwa sahihi kuna watu kibao ambao wamekipiganiq chama enzi na enzi, hata Dkt Mpango au Majaliwa. Nadhani CCM inajijua yenyewe na inaonekana anayeiongoza CCM siyo CCM
Duh 🙄 !!
Yaani wapo waliokipigania Chama kufa na kupona lakini mpaka sasa wametupiliwa mbali out of systems. ???!!!
Kwa kweli na Mimi ni mmoja wao 🙈😀✌️👍🙏🙏😂
Sisi wengine tunaamini haya ni maisha tu !! 🙏🙏👍
 
Kwa mujibu wa maoni ya gazeti la Mwananchi ni kwamba wanasema Sekretarieti ya CCM Imejaa Watu "Machawa" au Tegemezi ambao wanakitegemea chama kuliko Chama kuwategemea wao ukilinganisha na Wapinzani.

View: https://www.instagram.com/p/C1oAZelIWG7/?igsh=NmJiYWZiY2E0Mg==

My Take
Ccm ni chama Pendwa,maoni haya yanaonesha Mwananchi ni Mwanachama wa ccm hivyo kuelekea Uchaguzi angependa kwenye Sekretarieti ya chama wajae watu wenye majina.

Maoni haya yachukuliwe Kwa tahadhari.

Soma vizuri hayo ni maoni ya Luqman Maloto ndiko wamechukua hiyo taarifa.
 
Dah ni uchambuzi mzuri sana. Hakika Dkt Magufuli aliharibu chama. Pamoja na nia yake nzuri ila kuleta mamluki ndani ya chama imekigharimu chama sana
Una miaka mingapi?,unaijua CCM ya mwaka 2010-2015 ilivyokuwa inapingwa na Wananchi mpaka walikuwa wanaogopa kuvaa sare za CCM?
Magufuli na timu yake akina Bashiru na Polepole ndiyo Walikuja kurejesha Imani ya CCM kwa Wananchi ila hawa wa Sasa ndiyo wanao irudisha CCM ilikotoka.
Makonda amerudi na style waliyoitumia akina Polepole na mumeona muitikio wa Wananchi,sasa endeleeni kusikiliza ushauri wa matapeli wa Msoga alafu mtufurahishwa kwenye Uchaguzi!
 
maji yako shingoni nini? Magifuli alitengeneza taswira ya chama kutoka zomea zomea mpaka jezi za mitoko na akashinda kwa 84% na 99.9% wabunge na 99.5%madiwani na wenyekiti usiige kunywa kwa tembo utapasuka msamba

Watanzania tumekuwa na roho mbaya sana. Kwa hivyo na wewe ule uharibifu unaita uchaguzi. Punguza unafiki. Mtu anaengua karibia nusu ya wagombea na kuzima internet kwa wiki mbili halfu inakuja kutoa sifa za kijinga. Bahati nzuru alipata kinachomstahili.
 
Una miaka mingapi?,unaijua CCM ya mwaka 2010-2015 ilivyokuwa inapingwa na Wananchi mpaka walikuwa wanaogopa kuvaa sare za CCM?
Magufuli na timu yake akina Bashiru na Polepole ndiyo Walikuja kurejesha Imani ya CCM kwa Wananchi ila hawa wa Sasa ndiyo wanao irudisha CCM ilikotoka.
Makonda amerudi na style waliyoitumia akina Polepole na mumeona muitikio wa Wananchi,sasa endeleeni kusikiliza ushauri wa matapeli wa Msoga alafu mtufurahishwa kwenye Uchaguzi!
Magufuli alitumia mtutu kunyamazisha Wapinzani
 
Back
Top Bottom