LGE2024 Frank Nyalusi: Katibu wa CHADEMA Kata ya Ilala (Iringa) amechomwa visu mbele ya Askari na Msimamizi wa Uchaguzi

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Don Gorgon

Member
Nov 21, 2024
33
61
Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Jimbo la Iringa Mjini, Frank John Nyalusi, amezungumzia hujuma zilizojitokeza katika upigaji kura wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika jana, tarehe 27 Novemba 2024.

Nyalusi ameeleza kuwa Chama kimeshuhudia vitendo vya vurugu na hujuma, ikiwa ni pamoja na tukio la katibu wa CHADEMA katika Kata ya Ilala (Iringa) kukatwa visu mbele ya polisi na afisa wa Usimamizi wa Uchaguzi, ambapo hakukuchukuliwa hatua yoyote dhidi ya wahusika. Ameelezea pia kwamba walishuhudia rafu nyingi, ikiwa ni pamoja na mawakala wa chama kuzuiliwa kuingia kwenye vituo vya kupigia kura.

"Kwa kuwa Chama ni taasisi, tutaitisha vikao tutajadili taarifa hizi na kutoa tamko la pamoja. Tumeshuhudia mambo mengi yasiyofaa, ikiwa ni pamoja na kutofanywa kwa hatua yoyote kuhusu matukio hayo. Kama Chama, tutaizungumzia hali hii baada ya kukusanya taarifa kutoka kwa viongozi wetu wa kata zote 18, kisha tutatoa tamko la pamoja," alisema Nyalusi.

Viongozi wa CHADEMA wanaendelea kuchunguza na kukusanya taarifa kutoka kwa mawakala na wanachama wa chama ili kuhakikisha haki inatendeka na matukio hayo yanachunguzwa kwa umakini.

 
Back
Top Bottom