ibanezafrica
JF-Expert Member
- Oct 23, 2014
- 7,261
- 6,552
Pamoja na jitihada zinazofanywa na serikali kujitahidi kupunguza adha ya foleni jijini,nichukue nafasi hii kuipongeza serikali kwa juhudi zote lakini pia nishauri hatua zaidi zichukuliwe.
Foleni za Dar zinasababisha upotevu mkubwa wa muda na pia nishati nyingi inapotea kwa magari ku kwama barabarani kwa masaa mengi.
Huwa inanichukua takriban 3 hrs+ kusafiri toka mbagala hadi bunju! Kwa usafiri wa umma Na hunichukua 3 hrs toka magomeni hadi morogoro msamvu kwa private car.
Ukitathmini muda wa safari hizo uliotumika utagundua kweli kua pana shida kubwa jijini Dar na muda mwingi mtu anapoamua kutoka point A kwenda point B kitu ambacho ni hatari.
Ushauri;
~ Njia nyingi zitanuliwe.
~ Njia ya Tabata hadi segerea
Airport terminal 2 hadi gongo la mboto.
~ Tegeta kibaoni hadi bunju b darajani.
~ Mbagala kokoto hadi kisemvule.
~ Mtaa wa uhuru mnazi hadi buguruni.
~ Kutoka mataa ya morocco kupitia tmj mikocheni, mbezi ya chini kwa zena hadi africana mataa.
Flyover ya Tazara iongezewe njia nyingine juu kwa gari zitokazo bandari kuelekea ubungo.
Mwenge,Morocco pawekwe flyovers,pia buguruni chama/shell patafutiwe suluhishi japo pawekwe round about.
Tanroads wafanye tafiti za kuja na barabara za chini ya ardhi(subway) kwani tunakoelekea hali ya sasa itazidi mara dufu pasipo kubuni mikakati mikubwa.
Nawasilisha.