100 others
JF-Expert Member
- Aug 5, 2017
- 4,766
- 16,168
Mwezi huu wale wazee wa torrent imetoka hii filamu ya James Bond kwa jina la no time to die ,katika kutazama hii filamu nimeona scene ambayo imenifikirisha kwa nini na kuna maana gani?
Mapema land rover walitoa video fupi ya no time to die ambayo ipo YouTube, cha kushangaza ni James Bond kwenye video anaendesha land Cruiser prado old model ya 90's ambayo ilifanikiwa kuwakabili vyema maadui kwenye rough road na kuziharibu hizo range rover SVR vibaya...
Ipo wazi hizo RR ni moja ya top perfomance ranger rovers ambazo zina 575 hp, V8, 5.0 L..
Gari ambayo Bond alikuwa nayo ni Prado ya kizamani sana J90, cha kustaajabisha RR zilifanywa vibaya sana na Land Cruiser ambayo ipo wazi katika matoleo yake yenye nguvu kubwa ni 190hp huku RR SVR zikiwa na 575hp..
Au ndio kuonyesha ufundi wa agent wa MI6 jinsi anaweza kuendesha gari?
Kampuni kubwa kama Land Rover wanapowekeza kwenye filamu kubwa kama hii natarajia waonyeshe uwezo wa gari zao kwenye maneuverer, stability na kila kitu kama gari za off road zaweza fanya lakini mambo yamekuwa tofauti.
Land Cruiser old model imeonekana ikizifanya vibaya RR kitu ambacho natafakari hii imekaaje wazee?
Au kuna kitu sielewi?
Halafu sijawahi kuona James Bond anaendesha Toyota, hii ndio mara ya kwanza..
Hebu wajuzi wa mambo tufahamishane hii imekaaje?