FIFA Women's World Cup 2023 | Kombe la Dunia kwa Wanawake

Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
16,665
21,870
Mashindanoa ya FIFA kombe la dunia la wanawake litaanza kesho Alhamisi July 20, 2023 na kumalizika August 2nd.

Round za kwanza zitachezwa Sydney, Australia na Auckland, New Zealand huku fainali ikichezwa Sydney Australia.

Mashindano haya mwaka huu yamehusisha timu 32 tofauti na huko nyuma zilikuwa timu 24 tu. Nchi zitakazoshiriki kutoka mabara mbalimbali ni kama ifuatavyo:

Africa-CAF (Timu 4): Morocco, Nigeria, South Africa na Zambia

Asia- AFC (Timu 5): China, South Korea, Japan, Phillipines na Vietnam

Ulaya- UEFA (Timu 12): Denmark, England, France, German, Netherlands, Norway, Portugal, Ireland, Spain, Sweden, Italy na Switzerland

North America-NAF ( Timu 2): Canada na USA

Central America -UNCAF (Timu 1): Panama

Carribean- CFU ( Timu 3): Jamaica, Costa Rica na Haiti

South America-CONMEBOL (Timu 3): Argentina, Brazil na Colombia

Oceania- OFC (Timu 2): Australia na New Zealand

Watu wengi huyajua sana mashindano ya CONCACAF na wanaweza kujiuliza CONCACF iko wapi, laikini ileleweke kuwa CONCACAF huunganisha NAF, UNCAF, na CFU nadhani kwa sababu za kibishara tu, lakini bodies zinazotambulika na FIFA ni hizo nilizoweka hapo juu.

Timu machachari za Chile na Scotland hazikufuzu mwaka huu.

Kombe hili lilichukuliwa na Marekani katika mashindano ya 2019 na 2015, lakini vile 2011 waliingia fainali na kutolewa kwa chupupuchu na Japan.

Je mwaka huu tusubilie kombe hilo kuhamia Africa au litarudi Marekani?

Timu ya Marekani itakayotetea taji hilo ni hii hapa



Kesho kuna michezo mitatu tu kama ionekanavyo hapa: muda huo unaoonyeshwa ni Central Standar time ya Marekani (ambao ni pungufu ya masaa matano kwenye GMT).

1689789158769.png

Michuano hii imefikia hatua ya Robo Fainali kama ionekanavyo kwenye picha hapo chini
IMG_7060.jpeg
 
Timu zitakazowakilisha Afrika ni hizi hapa chini (Tanzania haimo).
Zambia (Copper Queens)


Morocco (Lionesses of Atlas)


Nigeria (Super Falcons)


South Africa (Banyana Banyana)
 
Leo wameanza wenyeji New Zealand na Australia ambapo New Zealand ilicheza na Norway wakati Australia ilicheza na Ireland. Michezo yote miwili ilikuwa ya kusisimua lakini wenyeji walijishindia bao moja kwa sifuri kama inavyoonekana kwenye highlights hizi



 
Leo wameanza wenyeji New Zealand na Austratilia ambapo New Zealand ilicheza na Norway wakati Australia ilicheza na Ireland. Michezo yote miwili ilikuwa ya kusisimua lakini wenyeji walijishiandia bao moja kwa sifuri kama inavyoonekana kwenye highlights hizi




Wanacheza mida gani kwa saa za huku kwetu?
 
Wanacheza mida gani kwa saa za huku kwetu?
Ngoja nitaunganisha schedule yote hapa; naona imeandikwa katika msaa ya kwao. Michezo inachezwa kwenye viwanja tisa ambavyo viko katika time zones tofauti kama ifuatavyo. UK(BST) ndiyo GMT na Tanzania tuko mbvele ya GMT kwa masaa matatu; Kwa hiyo mcehazo wa kesho kati ya Nigeria na Canada utakaochezwa Melbourne saa 12:30, itakuwa ni itakuwa ni saa 12.30-9.00= 3:30 GMT kwa scale ya BST, na hivyo Tanzania itakuwa 3:30GMT + 3:00=6:30 Asubuhi. Sijui kama hesabu hizo zimeelewak

1689894337492.png


Sasa ratiba Kamili iliyotolewa na FIFA kwa kutumia muda wa venua nimeiambatanisha hapa, ujue kupiga mahesabu ya muda local kwako. https://digitalhub.fifa.com/m/2c830...en-s-World-Cup-Australia-New-Zealand-2023.pdf
 
Mpira kati ya Nigeria na Canada ulisisimua sana. Kuna Wakati yule mshambuliaji mashuhuri wa Canada Sinclair alijiangusha ndani ya kulazimisha penalty na akaipata, Lakini Nnadozie golikipa wa Nigerai akaipangua penalty hiyo kama Diarra alivyopangua penaly ya Aligeria. Katika mchezo wote Nigeria walilishambulia sana goli la Canada ingawa mchezaji mmoja wa Nigeria alipewa red card katika dakika za mwisho mwisho mwisho. Hadi kipenga cha mwisho, timu hazikuweza kufungana.

 
Kama kuna mchezo ulikatisha tamaa sana leo ni ule kati ya Phillipines na Switzeralnd. Wasichana wa Phillipineas walicheaza mpira wa hali ya juu sana lakini kwa bahati mbaya Switzerland wakaibuka na ushindi wa magoli mawili huku goli moja likiwa golia la penalty. Kwa bahati mbaya hii clip ya highlights haionyesi zile moments nzuri za Phillipines.

 
Kama mnakumbuka, kwenye FIFA world cup ya wanaume huko Qatar mwaka jana, Spain iliiadhibu sana timu ya Costa Rica kwa jumla ya mabao 7-0 ambayo ilikuwa ni rekodi mojawapo kubwa kwenye mashindano hayo. Leo mambo hayakuwa hivyo kwa wanawake ingawa bado Spain ilishinda kwa mabao mengi ya 3-0 ikiwa ndiyo timu ya kwanza kufunga zaidi ya mabao mawili kwenye mashindano hayo. Kwa vyovyote Spain waliielemea sana Costa Rica.

Highlights za mchezo huo ni hizi hapa.

 
mchezo unaofuatia wakati naandika post hii ni kati ya Marekani na Vietnan; utaanza baada ya dakika 18 tokea sasa.
 
Marekani kashashinda, Kwenye Soka la wanawake hii timu iko vizuri sana
Marekani kashinda 3-0 ingawa golikipa wa Vietanam alipangua penalty6. Hata hivyo fowrad line ya Marekani haikuwa nzuri sana safari hii. Meagn Rapijnoe kakosa magoli ya wazi mawili.

 
Mchezo ulionikatisha tamaa ni ule wa Japana dhid ya Zambia. Timu ya Zambia iloianza vizuri sana lakini kipindi cha pili ikaelewa hadi kufungwa mabao 5-0 ingawa kuna magoli mawili ya Japan yalikataliwa; ingekuwa saba. Hata hivyo hii sheria ya penaly kukaa kwenye msitali siyo nzuri kwani kipa wa Zambia alikuwa amepangua penaltu moja lakini ikarudiwa na kuwapa japan goli la tano.

 
Kwa upande wa Uingereza (England) walikuwa na wakati mgumu sana dhid ya nchi maskini ya Haiti. Waliponea chupuchupu na kuifunga Haiti goli 1-0

 
Mchezo wa Mwisho kwa leo ulikuwa Denmark dhidi ya China. Timu zote mbili zilikuwa zinapewa uzito sawa kwenye mshindano hayo. Hata hivyo Denmark iliifunga China 1-0. Kwa jumla mchezo huo ulikuwa mgumu kwa pande zote mbili.

 
Mchezo wa leo baina ya Sweden na South Africa ulikuwa mkali sana na South Africa iliutawala cizuri sana, ila beki namba mbili wa South Afrika hakuwa makini kiasi cha kuwafanya Sweden wasawazishe na katika dakika ya mwisho Sweden wakapata bao la ushindi.

 
Mchezo mgumu ulikuwa baina ya Uholanzi na Ureno. Hata hivyo pamoja na upinzani mkubwa sana kutoka ureno, Uholanzi ilishambulia kama nyuki na hadi dakika ya mwisho Uholanzi iliongoza kwa bao 1-0

 
Back
Top Bottom