Android kila mara wanazidi kuwa imara sana tutegeme feature mpya Kali amazing zitakuja kwenye simu zetu za Android kuanzia version 14
1) Notification flashes
Kwenye Android 14 utakua na uwezo wa kutumia flash ya kamera Ikiwaka kuonyesha ishara ya kupokea notification toka sehemu mbalimbali. najua mwanzoni hii feature ilikuwepo kwenye baadhi ya simu za Android kama vile Infinix, Samsung pamoja iphone uwezo wa kuweka flash notification kwenye simu.
Lakini hii inakuja na operating system ya version 14 Ikiwa uwezo kuweka Rangi mbili yellow flash au white wakati wa notification inapotokea au kupigiwa simu hii imekuja kusaidia wakati umepoteza simu au umeweka kwenye mazingira magumu ni rahisi kuonekana pia unaweza kuweka vibrate au kuondoa.
2) Satellite Connectivity
apple walikua watu wa mwanzo kutambulisha huu mfumo wa Satellite emergency Sos kupitia Satellite inakupa uwezo wa kukusaidia kupata huduma ya dharura kwenye maeneo ambayo akuna mtandao kabisa. Android nao wameamua kuleta huu mfumo kwenye simu za Android version 14.
Utaweza kutoa taarifa polisi au kwa ndugu Ikiwa kwenye eneo ambalo akuna mtandao alafu umepatwa na majanga.
3) App cloning
Kutumia akaunti mbili za app Zako kwenye simu moja ni jambo la kipee sana kuweza kupunguza Matumizi ya kupakua app mara mbili mbili najua mwanzoni ilikuwepo hii feature ila kwa app baadhi tu kama vile Facebook, Instagram, Whatsapp nk.
sasa kwa app zote utaweza kuzitengeneza app moja ziwe mbili Kisha kuweza kutumiwa na mtu Zaidi ya mmoja kwa urahisi tu.
4) Drag and drop
Aisee kwenye Android 14 utakua na uwezo wa kuhamisha kitu chako toka sehemu moja kwenye nyingine bila kubonyeza sehemu ya copy we unaishikilia tu picha Kisha unaipeleka sehemu unayotaka kama kwenye status Whatsapp au message nk bila kubonyeza copy yani drag na ku drop kama unatumia mouse vile
.
5) Data sharing
Hii ni feature itaweza kukusaidia kujua kama Kuna app inatumia data Zako kushare baadhi ya taarifa na app nyingine bila wewe kujua mfano location, sms, call logs nk utakua unapewq taarifa labda Whatsapp inatumia taarifa ya location Zako kwenye app Fulani au sehemu Fulani.
Hii itasaidia sana kupata zile app ambazo sio Salama kwako kuweza kufuatilia bila wewe muhusika kujua.