Fanya Haya ili Kumsahau mtu Uliyempenda sana.

Peter Mwaihola

JF-Expert Member
Jun 23, 2022
263
429
Kuachwa, kuachana na kifo ni miongoni mwa mambo ambayo huwaacha watu katika wakati mgumu pindi yanapotokea.

Kwa leo tuzungumzie jambo moja tu kati ya hayo ambalo ni namna gani unaweza Kumsahau mtu uliyempenda sana pindi ambapo haupo nae tena.

Watu wengi wanapopatwa na jambo Kama hili huchanganyikiwa wengine hufika mbali zaidi kwa kuwaza kujinyonga au kunywa sumu kabisa.

Kuchukua uamuzi mgumu wa kujitoa uhai kisa mtu uliempenda Sana sio sahihi bali kuna mambo na mbinu kadhaa Unaweza kuzitumia ili kujinusuru uweze Kumsahau na uendelee na maisha mengine.

Mbinu ya kwanza ni kupotezea kumbukumbu zote zinazomhusu yeye kwa mfano kufuta picha zake kwenye Simu yako ama kubandua picha mlizopiga pamoja kama ulizibandika ukutani kwenye chumba chako.

Kufanya hivyo kutakusaidia kuondoa taswira yake katika mawazo yako wakati wote na kukufanya uanze kufikiria mambo mapya.

Pili, baada ya kugundua kuwa umempoteza ni vizuri ukachukua hatua ya kufuta uwezekano wa mawasiano Kati yako na yeye kwa mfano kufuta namba yake ya simu, kuacha kabisa mazoe ya kumtafuta mara kwa mara na kama unaishi kwenye nyumba ya kupanga unaweza kuhamia mtaa wa mbali kidogo ambao hautafanya uonane nae mara kwa mara.

Pia hakikisha unazuia mianya ya mawasiano mbadala mfano "kublock" barua pepe yake "Email" na kufuta kumbukumbu zote za mawasiano yenu.

Pia unatakiwa kujiweka mbali nae kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii kwa kuzuia Kurasa zake ama kuondoa urafiki Kati yenu ndani ya hiyo mitandao ya kijamii ili usijue nini anafanya na anaishije.

Kama wewe ulikua mtu wa kupiga stori Sana na rafiki zake basi anza kwa kupunguza mazoea kidogo kidogo ili hata mazungumzo yenu yasiwe marefu sana kufanya hivyo kutasaidia kuepuka kumzungumzia yeye katika mazungumzo yenu.

Aidha kama una marafiki wa upande wako wapenda mipasho hao ni wa kuwaepuka katika kipindi hiki, wafanye waishi unavyotaka usiruhusu wakuletee maneno na umbea kuhusu mtu huyo ili kukuvuruga.

Kwa kipindi hicho jibidishe sana ili uwe bize na shughuli zako hii itakusaidia kupunguza msongo wa mawazo na upweke.

Kwa bahati mbaya ikitokea umemkumbuka fikiria sana uovu ama makosa aliyokufanyia kipindi upo karibu nae.

Hii itakuongezea hasira na kukufanya uzidi kumpotezea zaidi.

Wakati huo huo epuka kutembelea maeneo ambayo pindi mlipokuwa karibu mlikua mnaenda pamoja mara kwa mara kwa mfano Klabu na kumbi za sinema ili kuepuka kumkuta huko ama kuulizwa kuhusu yeye.

Ufanye moyo wako ufikirie kuwa wewe ni wa thamani kuliko mtu yeyote na hakuna anaeweza kukufanya ujihisi mnyonge.

Epuka matumizi makubwa ya vilevi na madawa ya kulevya Kama njia ya kupunguza mawazo, kwani inaweza kupelekea ukaharibikiwa zaidi kisaikolojia na kiafya.

Ukifanya hayo yote sara iwe silaha yako muombe Mungu akupe uimara wa kuendelea na maisha mapya yenye matumaini.

Peter Mwaihola Ni Mwandishi na Mchambuzi wa masuala ya Siasa na Jamii
1660985385509.jpg
 
Kweli social media inaraha zake. Amini usi amini mkuu Leo j.mosi imetimia week mbili tangu shemeji Yako anipige na kitu kizito kichwani. Sijaweza kuamini Kwa MTU Niliempenda Kwa dhati amenipiga tukio la kutisha saikolojia yangu ilivurugika kabisa. Nikajikuta naangukia kwenye ulevi. Na msongo mkali wa mawazo shuguli zangu za kujiiigizia kipato zikasimama kifupi nilikuwa nusu mfu nusu hai. LAKINI Leo j.mosi imetimia siku ya tatu tangu nifanye hivi ulivyo andika naanza kuona Nuru inarejea taratibu. Hatua nilizo chukua ni kufuta pic zake zote kwenye sim yangu na ku block ac zake zote za social media. Numefuta namba yake ya sim japo amepiga missed call Zaid ya 95 sijapokea Wala kujibu sms pia nawaza kutafuta room sehemu nyingine. Pia nimetoa onyo KALI Kwa rafiki zake wa karibu KAMWE wasiniambie chochote juu yake.
 
Pole Boss
 
Back
Top Bottom