Fahamu matumizi ya gia L, 2 na 3 katika gari automatic

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
280,657
729,768
Katika gari za Automatic kuna gia za L, 2, na 3. Watu wengi hawafahamu kiundani matumizi ya gia hizi hivyo mara nyingi hujikuta wanakosea wapi na namna ya kuzitumia. Katika maelezo haya hapa chini, tumekufafanulia namna ya kutumia gia hizo.

Kwanza kabisa ujue katika hali ya kawaida gari lako linapaswa kuwa katika D (Drive) na hii inategemeana na mazingira ya barabara na hali ya hewa kama ni nzuri. Lakini 2, 3, hutumika tu pale unapokuwa aidha unateremka au unapanda mlima mkali na unataka ushuke au upande kwa spidi isiyozidi 40/60, hapo ndipo unaruhusiwa kutumia 2, na 3.

Namba 2, 3 na L ina maana kuwa unalock giaboksi (gearbox) ili gia zisibadilike (+/-) kama ambavyo zinabadilika ukiweka D. Itambulike kuwa unaweza kubadili kutoka D kwenda 2 au 3 wakati wowote gari inapokuwa katika mwendo ila hakikisha usiwe katika mwendokasi wa zaidi ya 40/60. Maana kinachofanyika ni kwamba D inasababisha sahani (disk) zilizomo ndani ya gearbox kufanya kazi na hii husababisha ile hydrolick iliyomo kupata joto linalotoka katika zile sahani ambalo joto lile husababisha gearbox kutokuwa na nguvu ile ile (Constant velocity) na ndiyo maana ukiweka 2, 3 au L, Gearbox inakuwa kwenye lock na sahani hazisuguani maana inakuwa inatumika sahani (Disk) moja tu.

Hii inasaidia hydrolick kupoa pia na ndiyo maana gari huongeza nguvu kwa ghafla.

Gia L inatumika pale unapokuwa aidha umekwama au unavuta gari jingine au tela, lakini inapaswa itumike kwa muda mfupi sana maana ina nguvu na inaongeza ulaji wa mafuta. Kama ukishatoka katika mkwamo na unaona bado barabara siyo nzuri labda utelezi au unavuta mzigo kwa mwendo mrefu basi unaweka 2 au 3 na wakati huo huo unaweza kuweka hata D kama hali ya njia na mzigo vinaruhusu na unaweza kuongeza walau spidi 40/60 au zaidi kama utaweka D.

Kwa maana rahisi zaidi ni kwamba, gia 2, 3 na L zinafanya kazi kama gari ya manual transmission na hii inakuwa rahisi kwa yeyote ambaye anafahamu kuendesha manual.

FB_IMG_1690823212049.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Katika gari za Automatic kuna gia za L, 2, na 3. Watu wengi hawafahamu kiundani matumizi ya gia hizi hivyo mara nyingi hujikuta wanakosea wapi na namna ya kuzitumia. Katika maelezo haya hapa chini, tumekufafanulia namna ya kutumia gia hizo...
Mkuu jana niliona umetupia link ya kujiunga telegram kwa madereva tupeane ujuzi nimedownlaod naingia leo sion tena link uliyoieka
 
Katika gari za Automatic kuna gia za L, 2, na 3. Watu wengi hawafahamu kiundani matumizi ya gia hizi hivyo mara nyingi hujikuta wanakosea wapi na namna ya kuzitumia. Katika maelezo haya hapa chini, tumekufafanulia namna ya kutumia gia hizo...
Ntarudi
 
nasikia kuna nyuzi ukipatia kati ya D na P gari inakwenda bila ya mafuta hata tone
 
Kuna watu kadhaa nimewaona wanajaribu hiki ulichokiandika baada ya kusoma huu uzi 😀
 
Back
Top Bottom