FRANC THE GREAT

JF-Expert Member
May 27, 2016
5,500
8,061
1591794739577.png

Habari!

Karibu ili kujuzwa na pia kupata taarifa (masasisho) mbalimbali ya kile kinachojiri kuhusiana na kirusi cha Corona (Coronavirus) almaarufu kama "kirusi cha Wuhan" kutoka nchini China.

Katika uzi huu utapata kufahamu mambo mbalimbali hususani hali ya ongezeko na ukuaji, jitihada zinazofanyika kukabiliana na kirusi hiki na mengine mengi yanayoibuka duniani kote katika muda wowote kuanzia sasa.

Nikukaribishe sana!

PIA SOMA: Coronavirus: Fahamu kiundani kuhusu Virusi hivi | Usambaaji, Dalili na Kinga - JamiiForums

====

Coronaviruses ni virusi vinavyopatikana zaidi kwa wanyama, lakini katika matukio machache virusi hivyo ninavyoitwa Zoonotic, Kisayansi, vinaweza kuambukizwa kutoka kwa mnyama kwenda kwa binadamu.

Virusi hivi vinaweza kuwafanya watu wakaugua, mara nyingi katika sehemu ya juu ya mfumo wa upumuaji sawa kabisa na mafua ya kawaida.

1581111142114.png

Virusi husambaa kutoka kwa binadamu mmoja hadi mwingine kwa njia ya hewa kwa kukohoa au kupiga chafya, kugusana na mtu mwenye virusi hivyo.

Njia nyingine ni kugusa kitu au sehemu yenye virusi na kisha kujigusa mdomo, pua au macho kabla ya kunawa na mara chache huambukiza kupitia kinyesi.

Dalili za kuwa umepata virusi hivi ni pamoja na pua kudondosha mafua mfululizo, kuumwa kichwa, kukohoa, kupata homa na muwasho katika koo ila kwa wenye kinga ndogo ya mwili kama wazee au watoto wanaweza kupata Nimonia (Pneumonia).

Hakuna Kinga ya virusi hivyo kwa sasa, ila usambaaji wake kwa binadamu unaweza kupunguzwa kupitia kuosha mikono yako mara kwa mara kwa maji na sabuni na epuka kugusa macho, mdomo na pua kwa mikono isiyooshwa.

Pia, unaweza kupunguza usambazaji wake kwa kukaa mbali na mtu aliyethibitika kuwa na maambukizi. Ukianza kuona dalili hizo unashauriwa kumuona daktari.

Ukithibitika kuwa na maambukizi ya virusi hivyo, funika mdomo na pua yako wakati wa kupiga chafya au kukohoa na safisha sehemu au kitu ulichokigusa.

====

Kirusi hiki cha Corona, kinaaminika kuwa kilianza katika soko la bidhaa za baharini mwishoni mwa mwaka 2019, katikati ya jiji la Wuhan, China ambalo lilikuwa likiuza nyama ya porini.

1580315252357.png

Kirusi hiki kimepatiwa jina la SARS-CoV-2 (Severe Acute Respiratory Syndrome Coronavirus 2) ambacho ni sehemu ya familia ya kirusi corona ambacho kinauhusiano na virusi vya SARS na MERS ambavyo vilisababisha milipuko siku za nyuma.

Mpaka sasa, kirusi hiki kimeenea katika nchi mbalimbali duniani. Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kuwa kuenea kwa virusi vya corona katika mataifa mbalimbali duniani hivi sasa kumefikia kuwa janga la kimataifa.

Hapo kabla, China ilitoa tahadhari kuwa kirusi hiki kinaweza kusambaa kwa watu wengi zaidi.

Waziri wa Kamisheni ya Afya ya Taifa nchini China, Ma Xiaowei, akizungumza na vyombo vya habari, alisema kuwa, uwezo wa serikali wa kufahamu kirusi hiki kipya ni finyu na hawajui hatari zinazoweza kuambatana na kubadilika kwa kirusi hiki.

Ma Xiaowei alisema muda ambao kirusi hiki cha corona huchukuwa hadi kujitokeza ni kati ya siku mmoja hadi 14, na kuwa kirusi hiki kinaambukiza hata wakati kinajijenga mwilini, kitu ambacho kilikuwa tofauti kwa homa kali ya mafua, SARS, kirusi corona kilichoibuka China na kuua takribani watu 800 duniani mwaka 2002 na 2003.

Mpaka sasa juhudi zilizokwisha kufanyika ili kudhibiti kuenea kwa kirusi hiki ni pamoja na katazo la usafirishaji na kusafiri na kusitisha matukio ya sherehe kubwa. China imetoa makatazo kadhaa ya kusafiri katika maeneo yaliyoathiriwa vibaya sana katika nchi hiyo ili kuzuia kuenea kwa kirusi hicho.

Muendelezo wa haya pamoja na yatakayokuwa yakijiri tutapata kuyafahamu kwa kina.

Baki hapa!

====
SASISHO: Mei 12,
Hadi kufikia leo kesi za coronavirus duniani zimefikia 4,342,847 huku wagonjwa 46,342 wakiwa katika hali mbaya zaidi.

Mpaka sasa idadi ya vifo 292,899 tayari vimeripotiwa duniani kote. Waliopona ni 1,602,118.

Mpaka sasa COVID-19 imeathiri nchi na ‘territories’ 212.

SASISHO: Mei 11, Marekani imerekodi jumla ya vifo 80,807 vya #COVID19 huku ikiwa na jumla ya visa 1,387,047 kutoka katika Majimbo yote 50 na sehemu zilizochini ya nchi hiyo

Taifa hilo ambalo kwa sasa ndilo linaongoza kwa idadi ya vifo na watu walioathirika na virusi hivyo limerekodi jumla ya Wagonjwa 234,916 waliopona hadi kufikia sasa

Aidha, Uhispania imerekodi vifo vipya 123 na kwa mujibu wa Wizara ya Afya idadi hiyo ya vifo ni ndogo kutokea kwa ndani ya wiki 7. Jumla ya Vifo imefikia 26,774

Idadi ya visa nchini humo imeongezeka kutoka 224,390 kwa jana, Jumapili hadi visa 268,143 kwa siku ya leo Mei 11, 2020 huku idadi ya Wagonjwa waliopona ikifikia 177,846

Huko Uturuki, maduka, saluni za aina zote zimeruhusiwa kufunguliwa baada ya kufungwa kwa takriban miezi miwili huku nchi hiyo ikihimiza masuala ya usafi zaidi

Hadi kufikia leo, nchi hiyo imerekodi jumla ya visa 138,657, vifo 3,786 huku kukiwa na zaidi ya Wagonjwa 92,691 waliopona ugonjwa huo

SASISHO: Mei 10, Visa 4,120,788 vya COVID19 vimeripotiwa ulimwenguni huku wagonjwa waliopona wakiwa 1,388,920 na jumla ya vifo ikiwa 280,144

Marekani inaendelea kuwa nchi iliyoathirika zaidi ikiripoti maambukizi 1,369,245 na vifo 80,068 huku waliopona wakifikia 217,636

Mataifa mengine ni Uhispania (262,783), Italia (218,268), Uingereza (215,260) na Urusi (198,676)

Barani Afrika, taifa la Afrika Kusini limerekodi visa 9,440, Misri (8,964), Morocco (5,911), Ghana (4,263) na Nigeria (4,151)

SASISHO: Mei 03, Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa cha Marekani (CDC) kimetoa sababu za kutofananisha mafua ya kawaida na #COVID19 ili kuweka sawa wanaopinga na kutaka shughuli za kiuchumi ziendelee kwa kuamini mafua ni sawa na #COVID19

Kituo hicho kimesema, Mafua ya kawaida yanaweza kuambukiza kwa wastani watu 1.28 wakati #CoronaVirus huambukiza wastani wa watu 2 hadi 3.Pia, Mafua ya kawaida yana chanjo, #CoronaVirus haina chanjo

Aidha, tafiti za CDC zinaonesha kati ya Oktoba 2019 hadi mwanzoni mwa Aprili 2020 mafua yameua wastani wa watu 331 kwa siku huku #COVID19 kuanzia Februari 6 hadi Aprli 30, ikiwa imeua wastani wa watu 769 kwa siku huko Marekani

Pia, Mafua ya kawaida watu huugua siku moja hadi nne baada ya kupata maambukizi, na huchukua siku mbili kuonesha dalili jambo linaloweza kuwafanya wakae nyumbani mara tu wajihisi wagonjwa lakini #COVID19 huchukua siku 4 hadi 5 kuanza kujionesha na kupevuka kwa dalili huchukua hadi siku 14
#JFCOVID19_Updates

SASISHO: Mei 01, Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaonesha #COVID19 imeathiri takriban watu milioni 3,392,451 huku zaidi ya Wagonjwa 229,000 wakifariki dunia na wengine zaidi ya 923,000 wakipona

Marekani ndilo Taifa lililoathirika zaidi Ulimwenguni likiwa na jumla ya visa 1,159,028, vifo 62,631 huku wagonjwa waliopona wakiwa ni zaidi ya 91,447

SASISHO: Aprili 30, Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaonesha #COVID19 imeathiri takriban watu milioni 3.3 huku zaidi ya Wagonjwa 229,000 wakifariki dunia na wengine zaidi ya 923,000 wakipona

Marekani ndilo Taifa lililoathirika zaidi Ulimwenguni likiwa na jumla ya visa 1,159,028, vifo 62,631 huku wagonjwa waliopona wakiwa ni zaidi ya 91,447

Jumla ya visa hivyo inajumuisha katika Majimbo yote 50, na maeneo yote yaliyochini ya nchi hiyo pamoja na Wagonjwa waliorudi nchini baada ya kugundulika katika nchi nyingine, walio Magerezani na Jeshini

Jana, Aprili 29, 2020 Marekani imerekodi visa vipya 27,327 na vifo 2,611 ndani ya saa 24. Hata hivyo, namba hii inaweza kuongezeka sana kwa siku zijazo kutokana na kwamba nchi hiyo inaanza kuhesabu vifo vinavyodhaniwani vya #COVID19

Vifo vinavyodhaniwa ni vya #COVID19 ni vilivinavyotokea ambapo watu waliofariki wanahusishwa na #COVID19 na Madaktari kujiridhisha hivyo lakini bila mgonjwa kupimwa maabara

Idadi hiyo ya vifo inayoelezwa kupita idadi ya vifo vya Wanajeshi wa Marekani walikufa katika vita ya Vietnam (47,434), imepita makadirio ya vifo yaliyowekwa ambapo ikadiriwa vifo 60,000 vingevika Agosti 2020.

SASISHO: Aprili 29, Hadi kufikia leo kesi za coronavirus duniani zimefikia 3,139,588 huku wagonjwa 56,970 wakiwa katika hali mbaya zaidi.

Mpaka sasa idadi ya vifo 218,024 tayari vimeripotiwa duniani kote. Waliopona ni 958,664.

Mpaka sasa COVID-19 imeathiri nchi na ‘territories’ 210.

SASISHO: Aprili 28, Hadi kufikia leo kesi za coronavirus duniani zimefikia 3,113, 587 huku wagonjwa 56,382 wakiwa katika hali mbaya zaidi.

Mpaka sasa idadi ya vifo 215,575 tayari vimeripotiwa duniani kote. Waliopona ni 944,350.

Mpaka sasa COVID-19 imeathiri nchi na ‘territories’ 210.

SASISHO: Aprili 27, Hadi kufikia leo kesi za coronavirus duniani zimefikia 3,004, 887 huku wagonjwa 57,623 wakiwa katika hali mbaya zaidi.

Mpaka sasa idadi ya vifo 207,257 tayari vimeripotiwa duniani kote. Waliopona ni 882,315.

Mpaka sasa COVID-19 imeathiri nchi na ‘territories’ 210.

Aidha, katika nchi ya Marekani Wagonjwa 55,000 wamefariki Mpaka kufikia leo

Waziri Mkuu Boris Johnson anatarajiwa kurudi kazini leo baada ya kupona #COVID19

Baadhi ya biashara kama maduka ya maua na vipodozi zitafunguliwa leo Uswizi

SASISHO: Aprili 26, Hadi kufikia leo kesi za coronavirus duniani zimefikia 2,923, 783 huku wagonjwa 57,881 wakiwa katika hali mbaya zaidi.

Mpaka sasa idadi ya vifo 203,319 tayari vimeripotiwa duniani kote. Waliopona ni 837,017.

Mpaka sasa COVID-19 imeathiri nchi na ‘territories’ 210.

Mataifa yaliyoathirika zaidi duniani ni Marekani, Uhispania, Italia, Ufaransa, Ujerumani na Uingereza

Kwa upande wa Afrika, nchi zenye idadi kubwa ya waathirika mpaka sasa ni Afrika Kusini, Misri, Algeria, Cameroon na Ghana

SASIHO: Aprili 25, Hadi kufikia leo kesi za coronavirus duniani zimefikia 2,910,634 huku wagonjwa 58,178 wakiwa katika hali mbaya zaidi.

Mpaka sasa idadi ya vifo 202,853 tayari vimeripotiwa duniani kote. Waliopona ni 831, 939.

Mpaka sasa COVID-19 imeathiri nchi na ‘territories’ 210.

Vifo vipya 813 vilivyotokea Hospitali vimetangazwa nchini Uingereza na idadi ya Wagonjwa wa COVID19 waliofariki dunia katika Hospitali mbalimbali imefikia 20,319

Takwimu za vifo za Serikali hazihusishi vifo vilivyotokea nyumbani, nyumba za uangalizi au sehemu nyingine kwenye jamii.

Takwimu hizo hukusanywa tofauti na Ofisi ya Taifa ya Takwimu kulingana na Hati za vifo.

Kwa upande wa Kenya, wagonjwa wapya 16 watamgazwa na kufanya idadi katika nchi hiyo kufikia 336.

Wagonjwa wapya 11 wanatoka Nairobi na 5 ni kutokea Mombasa

Wizara ya Afya imetangaza kuwa waliopona wamefikia 95 baada ya wagonjwa wengine watano kuponawagonjwa

Aidha, Uingereza imerekodi maambukizi 148,377 hadi kufikia leo.

Kwa upande wa Tanzania inaelezwa kuwa wagonjwa wapya 37 wamepona.

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema hadi sasa jumla ya Wagonjwa waliopona ni 48

Waliopona ni kati ya Wagonjwa 108 waliothibitika kuwa na Ugonjwa huo, ila sasa hawana dalili.

SASISHO: Aprili 24, Hadi kufikia leo kesi za coronavirus duniani zimefikia 2,799,787 huku wagonjwa 58,259 wakiwa katika hali mbaya zaidi.

Mpaka sasa idadi ya vifo 195,119 tayari vimeripotiwa duniani kote. Waliopona ni 774,910.

Mpaka sasa COVID-19 imeathiri nchi na ‘territories’ 210.

Aidha, inaelezwa kuwa katika nchi ya Bangladesh Madaktari zaidi ya 200 wameambukizwa Covid 19.

Takriban Madaktari 251 wameambukizwa #CoronaVirus na wagonjwa kutokana na ukosefu wa vifaa kinga (PPE)

Nchi hiyo imerekodi visa 4186, vifo 127 na waliopona ni 108.

SASISHO: Aprili 23, Hadi kufikia leo kesi za coronavirus duniani zimefikia 2,734,102 huku wagonjwa 58,712 wakiwa katika hali mbaya zaidi.

Mpaka sasa idadi ya vifo 191,189 tayari vimeripotiwa duniani kote. Waliopona ni 774,910.

Mpaka sasa COVID-19 imeathiri nchi na ‘territories’ 210.

Aidha, katika nchi ya Kenya wagonjwa wapya 17 watangazwa nakufanya jumla ya visa vyote katika nchi hiyo kufika 320.

Inaelezwa kuwa katika wagonjwa hao17 wote ni Wakenya, kati yao 12 wametokea Mombasa na watano ni kutoka Nairobi

Vilevile, wagonjwa wengine 6 wamepona na jumla ya waliopona ni 89

SASISHO: Aprili 22, Hadi kufikia leo kesi za coronavirus duniani zimefikia 2,674,994 huku wagonjwa 57,216 wakiwa katika hali mbaya zaidi.

Mpaka sasa idadi ya vifo 178,658 tayari vimeripotiwa duniani kote. Waliopona ni 703,473.

Mpaka sasa COVID-19 imeathiri nchi na ‘territories’ 210.

Aidha, kwa upande wa Tanzania visa vipya 30 vyathibitika na kufanya jumla ya visa vyote vilivyotangazwa katika nchi hiyo kufikia 284

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema idadi hiyo ni hadi kufikia jana, Aprili 21, 2020

Aidha, Wagonjwa 256 wanaendelea vizuri, 7 wako katika uangalizi maalum, 11 wamepona na 10 wamefariki

SASISHO: Aprili 21, Hadi kufikia leo kesi za coronavirus duniani zimefikia 2,543,556 huku wagonjwa 57,254 wakiwa katika hali mbaya zaidi.

Mpaka sasa idadi ya vifo 176,533 tayari vimeripotiwa duniani kote. Waliopona ni 686,440.

Mpaka sasa COVID-19 imeathiri nchi na ‘territories’ 210.

Aidha, kwa upande wa Afrika Mashariki nchi ya Kenya idadi ya waathirika yafikia 296 huku ikielezwa wagonjwa wengine watano wamepona.

Visa 11 vimeripotiwa leo ambapo 11 ni Wakenya na 4 ni wageni, wote hawajasafiri karibuni

Idadi ya wagonjwa waliopona nchini humo imefikia 74

SASISHO: April 20, Hadi kufikia leo kesi za coronavirus duniani zimefikia 2,459,749 huku wagonjwa 55,613 wakiwa katika hali mbaya zaidi.

Mpaka sasa idadi ya vifo 168,193 tayari vimeripotiwa duniani kote. Waliopona ni 617,304.

Mpaka sasa COVID-19 imeathiri nchi na ‘territories’ 210.

Aidha, Waziri Mkuu wa Ufaransa, Edouard Philippe amesema mwenendo wa ugonjwa wa COVID19 nchini humo unabadilika taratibu. Amesema dalili mojawapo kuwa mlipuko huo unaanza kupungua ni kushuka kwa idadi ya wagonjwa Hospitali

Ufaransa ni nchi ya nne kwa vifo vingi zaidi duniani kutokana na Corona Virus ikiwa imerekodi vifo 19,718 na maambukizi 152,894 hadi kufikia leo.

Kwa upande wa Tanzania Waziri wa Afya wa nchi hiyo ametangaza ongezeko la kesi mpya 84 za watu waliathiriwa na Covid-19 katika nchi hiyo na kufanya jumla ya kesi zote katika nchi hiyo kuwa 254.

SASISHO: Aprili 19 Hadi kufikia leo kesi za coronavirus duniani zimefikia 2,399,849 huku wagonjwa 54,215 wakiwa katika hali mbaya zaidi.

Mpaka sasa idadi ya vifo 164,0939 tayari vimeripotiwa duniani kote. Waliopona ni 615,332.

Mpaka sasa COVID-19 imeathiri nchi na ‘territories’ 210.

Kwa upande wa Tanzania, Zanzibar wametangaza kesi mpya 23 za wagonjwa wa Corona na kufanya jumla ya visa katika taifa hilo kufikia 170.

SASISHO: Aprili 18, Hadi kufikia leo kesi za coronavirus duniani zimefikia 2,283,090 huku wagonjwa 58,741 wakiwa katika hali mbaya zaidi.

Mpaka sasa idadi ya vifo 158,010 tayari vimeripotiwa duniani kote. Waliopona ni 593,306.

Mpaka sasa COVID-19 imeathiri nchi na ‘territories’ 210.

SASISHO: Aprili 17, Hadi kufikia leo kesi za coronavirus duniani zimefikia 2,190,010 huku wagonjwa 56,601 wakiwa katika hali mbaya zaidi.

Mpaka sasa idadi ya vifo 147,010 tayari vimeripotiwa duniani kote. Waliopona ni 553,306.

Mpaka sasa COVID-19 imeathiri nchi na ‘territories’ 210.

Aidha, katika nchi ya Kenya imeripotiwa kuwapo kwa visa vipya 12 vya Ugonjwa wa Covid-19 na kufanya jumla ya visa vyote katika taifa hilo kufikia 246.

Habari ya kushitua nchini Marekani leo imetangaza vifo 4,491 ndani ya saa 24

Idadi hiyo ya vifo ni kubwa zaidi kutangazwa ndani ya saa 24 na sasa vifo nchini humo vimefikia 32,917 kwa mujibu wa takwimu za Chuo Kikuu John Hopkins

Hata hivyo, vifo hivyo vinaweza kuwa vinajumuisha watu waliofariki wakihusishwa kuwa na #COVID19 na Madaktari kujiridhisha hivyo lakini bila mgonjwa kupimwa maabara

Awali, Marekani ilikuwa ikitangaza idadi ya vifo vya wagonjwa waliopimwa maabara na kuthibitika kuwa na Ugonjwa huu

SASISHO: Aprili 16, Hadi kufikia leo kesi za coronavirus duniani zimefikia 2,083,590 huku wagonjwa 51,142 wakiwa katika hali mbaya zaidi.

Mpaka sasa idadi ya vifo 134,632 tayari vimeripotiwa duniani kote. Waliopona ni 510,309.

Mpaka sasa COVID-19 imeathiri nchi na ‘territories’ 210.

Aidha kwa upande wa Tanzania kumetangazwa visa vipya 6 ambvyo vyote vimetokea Zanzibar.

Kati ya Wagonjwa hao, Watano ni Wanaume na mmoja ni Mwanamke. Wana umri kati ya miaka 23 na 58. Wote ni Watanzania na hawana historia ya kusafiri nje ya nchi kwa siku za karibuni

Kwa upande wa Kenya visa vingine 9 vimetangazwa leo na kufanya jumla ya visa vya Covid19 kufikia 234

Watu hao wana umri kati ya miaka 2 hadi 64

Aidha, Rais Uhuru Kenyatta amesema mtu mmoja amefariki kwa #COVID_19 na kufanya idadi ya vifo kufikia 11

SASISHO: Aprili 15, Hadi kufikia leo kesi za coronavirus duniani zimefikia 2,034,438 huku wagonjwa 51,405 wakiwa katika hali mbaya zaidi.

Mpaka sasa idadi ya vifo 129,929 tayari vimeripotiwa duniani kote. Waliopona ni 495,434.

Mpaka sasa COVID-19 imeathiri nchi na ‘territories’ 210.

Marekani imerekodi idadi kubwa ya vifo 2,228 ndani ya saa 24 na kufikia vifo 28,368 hadi sasa kwa mujibu wa Chombo cha Habari cha Reuters. Idadi kubwa ya awali ilikuwa Ijumaa ambapo vifo 2,069 vilirekodiwa

Nchi hiyo ambayo ni ya tatu kwa idadi kubwa ya watu duniani imerekodi Waathirika 606,194 hadi kufikia mapema leo idadi ambayo ni kubwa kwa mara tatu kwa nchi inayoifuata kwa Waathirika wa #COVID19

Ongezeko la vifo 2,228 halijumuishi makusudio ya Jiji la New York kujumuisha idadi ya vifo vinavyodhaniwa vimetokana na #CoronaVirus bila kupimwa

Mamlaka za New York zimeripoti vifo 3,778 vinavyodhaniwa ni kwasababu ya corona ambapo madaktari walijiridhisha ni kutokana na ugonjwa huo, na vifo 6,589 vilivyothibitishwa maabara. Ukijumlisha idadi hiyo ya vifo inafika zaidi ya 10,000.

Aidha, kwa Afrika Mashariki nchini Kenya Idadi ya waliopata maambukizi ya #COVID19 imeongezeka na kufikia 225 baada ya wagonjwa wapya 9 kuthibitika na virusi hivyo kufuatia kupimwa kwa sampuli 803 ndani ya saa 24

Waziri wa Afya, Mutahi Kagwe amesema wagonjwa wote wapya ni raia wa Kenya na hawana rekodi ya kusafiri nje ya nchi hiyo kwa hivi karibuni. Ni miongoni mwa watu waliokuwa wakifuatiliwa

Ameeleza kuwa kati ya wagonjwa hao wapya, watano wanatokea Nairobi na wanne wanatokea Mombasa na umri wao ni katika ya miaka 9 na miaka 69

Aidha, watu 12 wamepona ugonjwa huo na kuruhusiwa kutoka hospitalini; Idadi ya waliopona imefikia 53. Mtu mmoja amefariki kwa ugonjwa huo

Waziri amebainisha kuwa jumla ya watu 2,336 waliokutana na waathirika wamekuwa wakifuatiliwa, huku 1,911 wakiachiwa na wengine 455 wakiwa bado wanafuatiliwa

Kwa upande wa Tanzania, mamlaka imeripoti kuwapo kwa visa vipya 29 na kufaya jumla ya waathirika wa #COVID19 katika nchi hii kufikia 88 ambapo Wagonjwa hao wamebainika kutoka kwenye majibu ya sampuli zilizopimwa Aprili 14 na 15 mwaka huu

Wagonjwa wote ni Watanzania na 26 wapo Dar es Salaam, Wawili wapo Mwanza na mmoja yupo Kilimanjaro.

SASISHO: Aprili 14, Hadi kufikia leo kesi za coronavirus duniani zimefikia 1,926,277 huku wagonjwa 50,943 wakiwa katika hali mbaya zaidi.

Mpaka sasa idadi ya vifo 125,338 tayari vimeripotiwa duniani kote. Waliopona ni 466,284.

Mpaka sasa COVID-19 imeathiri nchi na ‘territories’ 210.

Aidha kwa upande wa Tanzania Waziri Mkuu atangaza kuongezeka kwa visa vipya vinne na kufanya jumla ya visa katika nchi hii kufikia 53.

SASISHO: Aprili 13, Hadi kufikia leo kesi za coronavirus duniani zimefikia 1,985,083 huku wagonjwa 49,151 wakiwa katika hali mbaya zaidi.

Mpaka sasa idadi ya vifo 117,670 tayari vimeripotiwa duniani kote. Waliopona ni 432,903.

Mpaka sasa COVID-19 imeathiri nchi na ‘territories’ 210.

Aidha, kwa upande wa Tanzania visa vipya 14 vimethibitishwa leo na kufanya jumla ya visa katika nchi hii kufikia 14.

Wizara ya Afya imesema kuna ongezeko la Wagonjwa wapya 14 wa COVID19 na kufanya idadi ya Waathirika kufikia 46 kutoka 32 waliotangazwa awali.

Wagonjwa wote ni Watanzania na kati yao waliopo Dar ni 13 na mmoja Arusha. Wote wanaendelea na matibabu chini ya uanglizi wa Wataalam wa Afya.

Hii ni idadi kubwa kuwahi kutangazwa na Serikali tangu kutokea kwa mlipuko wa ugonjwa huo nchini.

Kwa upande wa nchi ya Kenya, Wizara ya Afya imetangaza visa vipya 11 vya #COVID19 na kufanya idadi ya visa nchini humo kufikia 208

Watu 14 wameruhusiwa kurudi nyumbani baada ya kupona huku vifo 9 vikiripotiwa hadi sasa.

Aidha, kwa upande wa Marekani, takriban Polisi 6,522 wa Idara ya Polisi ya New York hawakuweza kufika kazini siku ya jana kwa mujibu wa ripoti ya kila siku ya #CoronaVirus ya Idara hiyo

Ripoti hiyo imeeleza kuwa hadi sasa Polisi 2,344 na Wafanyakazi wasio Polisi 489 wa Idara hiyo ndio wamethibitika kuwa na ugonjwa wa #COVID19

Ongezeko la Wagonjwa 5,695 kwa siku ya jana kumefanya New York kuwa na zaidi ya Waathirika 104,000 na takriban vifo 6,182 vilivyorekodiwa

Kwa ujumla Marekani ndio nchi iliyoathirika zaidi duniani na virusi hivi ikiwa na jumla ya Waathirika 560,433 huku ikiwa imesharipoti vifo 22,115

SASISHO: Aprili 12, Hadi kufikia leo kesi za coronavirus duniani zimefikia 1,830,321 huku wagonjwa 50,513 wakiwa katika hali mbaya zaidi.

Mpaka sasa idadi ya vifo 104,560 tayari vimeripotiwa duniani kote. Waliopona ni 382,073.

Mpaka sasa COVID-19 imeathiri nchi na ‘territories’ 210.

Aidha, kwa upande wa Afrika Mashariki Nchi ya kenya yafikisha jumla ya visa 197 huku vifo vikiwa 8.

Kenya imethibitisha visa vipya 6 vya #COVID19 na kupelekea nchi kuwa na jumla ya visa 197 ya ugonjwa huo

Visa 6 hivi ni vijana wa miaka kati ya 25-29 waliopatikana baada ya sampuli 766 kupimwa ndani ya saa 24.
Zaidi ya hayo, kwa upande wa nchi ya Marekani inaelezwa idadi ya vifo vilivyotokea vyaipiku ile ya nchi ya Italia mbayo ilikuwa ikiongoza kwa kuwa na vifo vingi vya Covid 19 ulimwenguni.

Marekani imerekodi vifo 20,602 vya wagonjwa wa #COVID19 na Italia ina vifo 19,468

Wyoming ni Jimbo pekee ambalo halijatangaza kifo huku #USA ikiwa na Waathirika takriban 529,740.

SASISHO: Aprili 11, Hadi kufikia leo kesi za coronavirus duniani zimefikia 1,710,798 huku wagonjwa 49,913 wakiwa katika hali mbaya zaidi.

Mpaka sasa idadi ya vifo 103,512 tayari vimeripotiwa duniani kote. Waliopona ni 382,073.

Mpaka sasa COVID-19 imeathiri nchi na ‘territories’ 210.

SASISHO, Aprili 10, Hadi kufikia leo kesi za coronavirus duniani zimefikia 1,684,281 huku wagonjwa 49,774 wakiwa katika hali mbaya zaidi.

Mpaka sasa idadi ya vifo 102,053 tayari vimeripotiwa duniani kote. Waliopona ni 375,221.

Mpaka sasa COVID-19 imeathiri nchi na ‘territories’ 210.

Kwa upande wa Tanzania imeripotiwa visa vipya vitano vya Covid 19 na kufanya idadi kufikia 34 huku vifo viwili vikiongezeka ambavyo vimepelekea utimia kwa vifo 3 vinavyotokana na Covid 19

SASISHO, April 09, kwa siku ya leo kesi za coronavirus duniani zimefikia 1,605,729 huku wagonjwa 49,145 wakiwa katika hali mbaya zaidi.

Mpaka sasa idadi ya vifo 95,799 tayari vimeripotiwa duniani kote. Waliopona ni 357,003.

Mpaka sasa COVID-19 imeathiri nchi na ‘territories’ 210.

Waziri Mkuu wa Uhispania, Pedro Sanchez amesema nchi hiyo inatarajia kulegeza masharti ya karantini yaliyowekwa ili kudhibiti maambukizi na Virusi vya Corona

Sanchez ambaye pia ameombe Bunge kupitisha ombi lake la kuongeza muda wa hali ya tahadhari mpaka Aprili 26 amesema kutokana na athari zilizosababishwa na janga la Covid-19, mchakato wa maisha kurejea kama zamani utachukua wa taratibu

Uhispania ni nchi ya pili iliyoathirika zaidi na janga la Corona Virus baada ya Marekani. Maambukizi 152,446 na vifo 15,238 vimerekodiwa huku wagonjwa 52,165 wakipona hadi kufikia leo

Mbali na Uhispania, mataifa mengine ya Ulaya nayo yanakifikiria kulegeza masharti mapema iwezekanavyo kutokana na wasiwasi wa uchumi kuathirika kwasababu ya kuwekwa kwa amri ya karantini

SASISHO: April 08, kwa siku ya leo kesi za coronavirus duniani zimefikia 1,501,435 huku wagonjwa 48,017 wakiwa katika hali mbaya zaidi.

Mpaka sasa idadi ya vifo 87,835 tayari vimeripotiwa duniani kote. Waliopona ni 319,263.

Mpaka sasa COVID-19 imeathiri nchi na ‘territories’ 209.

Huko nchini Romania inaelezwa watoto 10 wapata maambukizi ya Covid 19 huku wazazi wao wote wakiwa salama

Aidha, kwa upande wa afrika Mashariki nchi ya Kenya imetangaza maambukizi mapya 7 na kufanya idadi ya maambukizi katika nchi hiyo kufikia 179

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya amesema wagonjwa wote saba ni raia wa Kenya

Kati yao, Wawili wametokea Marekani, mmoja alitoka Congo na mwingine Uingereza

SASISHO: Aprili 07, kwa siku ya leo kesi za coronavirus duniani zimefikia 1,411,332 huku wagonjwa 47,882 wakiwa katika hali mbaya zaidi.

Mpaka sasa idadi ya vifo 81,048 tayari vimeripotiwa duniani kote. Waliopona ni 300,759.

Mpaka sasa COVID-19 imeathiri nchi na ‘territories’ 209.

Aidha ripoti zinaeleza kuwa katika nchi ya Italia hadi kufikia jana Aprili 06, 2020 jumla ya Wafanyakazi 12,681 wa sekta ya Afya walikuwa wanaugua ugonjwa huo

Inaelezwa kuwa ukosefu wa vifaa vya kujikinga na virusi vya corona umesababisha idadi ya wafanyakazi wanaougua ugonjwa huo kuongezeka

Mojawapo ya miundombinu bora ya afya barani Ulaya ipo Kaskazini mwa Italia lakini imeshidhwa kukidhi kuhimili wingi wa wagonjwa wa #COVID_19 wanaogundulika nchini humo

Italia imeripoti jumla ya waathirika 132,547, idadi ya vifo 16,523 na waliopona hadi sasa ni 22,837.

Kwa upande wa Kenya idadi ya waathirika wameongezeka waathirika 14 huku mmoja akiwa ametokea Tanzanua na kufanya idadi kufikia 172, hadi sasa Kenya imepima watu zaidi ya 5,000 maana kasi ya kupima imeongezeka, mbinu zinatumika kwa umakini kufuata kila aliyekutana au kuhusiana na waathirika.

SASISHO, Aprili 06, kwa siku ya leo kesi za coronavirus duniani zimefikia 1,312,628 huku wagonjwa 46,216 wakiwa katika hali mbaya zaidi.

Mpaka sasa idadi ya vifo 72,636 tayari vimeripotiwa duniani kote. Waliopona ni 275,087.

Mpaka sasa COVID-19 imeathiri nchi na ‘territories’ 209.

Kwa upande wa Afrika mashariki inaelezwa kuwa nchini Kenya maambukizi yamefikia 158, ambapo Rais Kenyatta ametangaza maambukizi mapya 16 na vifo viwili.

aidha, kwa upande wa Tanzania Waziri wa Afya ametangaza kuwapo kwa maambukizi mapya manne na kufanya jumla ya watu walioathirika katika nchi hii kufika 24.

Zaidi ya hayo, Inaelezwa kuwa maamubukizi ya Virusi vya Corna yameshuka kwa takribani siku nne katika nchi ya Hispania.

Vifo 637 vimeripotiwa leo na idadi ya waliofariki dunia imefikia 13,055

Idadi ya vifo kupungua inaleta matumaini kuwa Uhispania imemaliza kipindi kigumu.

SASISHO, Aprili 05 kwa siku ya leo kesi za coronavirus duniani zimefikia 1,245,741 huku wagonjwa 45,015 wakiwa katika hali mbaya zaidi.

Mpaka sasa idadi ya vifo 67,628 tayari vimeripotiwa duniani kote. Waliopona ni 256,760.

Mpaka sasa COVID-19 imeathiri nchi na ‘territories’ 206.

Marekani imetangaza idadi kubwa ya vifo vilivyotokana na #COVID19 kwa siku moja huku Wataalam wakitahadharisha kuwa wiki mbili zijazo zitakuwa mtihani mkubwa katika kupambana na maambukizi nchini humo

Nchi hiyo imetangaza jumla ya vifo 1,344 vilivyorekodiwa kutokea jana Aprili 04, ikiwa ndio idadi kubwa ya vifo kutokea ndani ya saa 24 kwa Taifa moja tangu kulipuka kwa Ugonjwa huo

Idadi hiyo inapelekea Marekani kuwa na jumla ya vifo 8,496 huku kukiwa na jumla ya Waathirika 312,076, idadi kubwa ya Waathirika kuliko Taifa lolote

Aidha, inaelezwa kuwa Zanzibar yatangaza wagonjwawapya wawili na kufanya idadi ya Waathirika visiwani humo imefikia 7 kwa sasa

Wagonjwa hao wapya wametoka Tanga kwa nyakati tofauti na kuingia Zanzibar kupitia Bandari ya Mkokotoni

SASISHO, Aprili 04 kwa siku ya leo kesi za coronavirus duniani zimefikia 1,222,990 huku wagonjwa 42,066 wakiwa katika hali mbaya zaidi.

Mpaka sasa idadi ya vifo 68,080 tayari vimeripotiwa duniani kote. Waliopona ni 268,331.

Mpaka sasa COVID-19 imeathiri nchi na ‘territories’ 206.

Aidha, kwa upande wa Afrika Mashariki nchi ya Kenya imetangaza waathirika wapya wanne na kufanya jumla ya kesi za Covid19 katika nchi hiyo kufikia 126.

Watatu kati yao ni raia wa Kenya na 1 ni raia wa Pakistani. Wagonjwa wote wana umri kati ya miaka 34 hadi 44

Aidha, Botswana imeweka zuio la wananchi kutoka nje kwa siku 28 baada ya kurekodi visa 4 vya maambukizi ya #Covid19

SASISHO, Aprili 03, Siku ya leo kesi za coronavirus duniani zimefikia 1,083,843 huku wagonjwa 39,252 wakiwa katika hali mbaya zaidi

Mpaka sasa idadi ya vifo 64,231 tayari vimeripotiwa duniani kote. Waliopona ni 242,099.

Mpaka sasa COVID-19 imeathiri nchi na ‘territories’ 203.

Aidha, kwa upande wa Hispania Kwa mujibu wa data zilizotolewa na Wizara ya Afya nchini humo leo Aprili 03, 2020, jumla ya Watu waliofariki dunia baada ya kuugua #COVID19 imefikia 10,935

Idadi hiyo imefikiwa baada ya vifo 932 vya Wagonjwa wa #Corona kurekodiwa katika saa 24 zilizopita. Jana, Wizara hiyo ilitangaza vifo 950 vilivyotokea ndani ya saa 24

Aidha, data za Wizara hiyo zinaonesha kuwa kuna Wagonjwa 76,262 kwa sasa nchini humo, ikiwa ni ongezeko la Wagonjwa 2,770 kutokea idadi ya jana lakini pia ni ongezeko dogo tangu Machi 20

Uhispania ni moja ya nchi iliyoathirika vibaya na mlipuko wa Ugonjwa huu, ikiwa ni ya pili kwa idadi ya vifo nyuma ya Italia yenye vifo 13,915. Inashika nafasi ya pili kwa Waathiriki ikiwa na Waathirika 117,710 nyuma ya Marekani (245,380).

SASISHO, Aprili 02, Hadi mapema leo kesi za coronavirus duniani zimefikia 936,829 huku wagonjwa 35,770 wakiwa katika hali mbaya zaidi

Mpaka sasa idadi ya vifo 47,263 tayari vimeripotiwa duniani kote. Waliopona ni 194,604

Mpaka sasa COVID-19 imeathiri nchi na ‘territories’ 203.

Taarifa zinaeleza kuwa katika nchi ya Kenya walioambukizwa Covid 19 wafikia 110.

Idadi ya wagonjwa wa #Covid19 imeongezeka kwa wagonjwa 29 ndani ya saa 24 zilizopita

Wagonjwa hao wamepatikana kwenye sampuli 662 zilizopimwa. 28 kati yao ni raia wa Kenya na 1 ni raia Congo.

Nchi tano zenye Waathirika wengi waliorekodiwa ni Marekani (215,362), Italia (110,574), Uhispania (110,238), China (81,589) na Ujerumani (80,641)

Lakini pia nchi tano zenye idadi kubwa ya vifo vilivyoripotiwa ni Italia (13,155), Uhispania (10,003), Marekani (5,113), Ufaransa (4,032) na China (3,318)

SASISHO, Aprili 01, Hadi mapema leo kesi za coronavirus duniani zimefikia 750,890 huku wagonjwa 33,092 wakiwa katika hali mbaya zaidi

Mpaka sasa idadi ya vifo 42,364 tayari vimeripotiwa duniani kote.

Mpaka sasa COVID-19 imeathiri nchi na ‘territories’ 203.

Kwa upande wa Afrika Mashariki nchi ya Kenya imepata jumla ya maambukizi 81 ambapo wagonjwa Wapya 22 wamethibitishwa na kufanya jumla hiyo kufikiwa.

Aidha, kati ya 22, 18 ni raia wa Kenya, 2 ni raia wa Pakistan na 2 ni raia wa Cameroon.

SASISHO Machi 31, Jumla ya kesi za Covid 19 duniani zimefikia 750,890 huku wagonjwa 31,488 wakiwa katika hali mbaya zaidi

Mpaka sasa idadi ya vifo 36,405 tayari vimeripotiwa duniani kote.

Mpaka sasa COVID-19 imeathiri nchi na ‘territories’ 200.

Aidha, kwa upande wa Tanzania, Waziri wa Afya alitangaza kifo cha kwanza kilichotokana na Virus vya Covid 19 katika nchi hii.

Wakati nchi ya China yatangaza wagonjwa wapya wa Covid-19 48 huku vifo vipya vikiwa 4.

Nchi ya Kenya imetangaza maambukizi mapya 9 huku ikipelekea jumla ya maambukizi katika nchi hiyo kufikia 59 huku kifo kilichoripotiwa ni 1 tu.

SASISHO: MACHI 30, Mpaka kufikia leo kuna kesi 693282 duniani kote huku watu wapatao 26,149 wakiwa mahututi.

Mpaka wakati huu vifo vilivyorekodiwa duniani kote ni 33106.

Mpaka leo COVID-19 imeathiri nchi na ‘teritorries’ 198.

Taarifa zinaeleza kuwa watu wapatao 756 wamefariki ndani ya saa 24 katika nchi ya Italia huku idadi ya vifo katika nchi hiyo ikiwa 10,779.

Aidha, kwa vifo hivyo kitakwimu vinachukua takriban 1/3 ya vifo vyote vya #Covid19 duniani (33,982).

Zaidi ya hayo kwa upande wa Tanzania inaelezwa kuwa mpaka kufikia sasa idadi ya maambukizi yaongezeka na kufikia jumla ya waathirika 19 baada ya kupatikana kwa wagonjwa wapya watano.

Inaelezwa kuwa katika wagonjwa hao, wagonjwa Watatu wanatoka Dar na wawili wanatoka Zanzibar.

SASISHO: Machi 29, Mpaka kufikia leo kuna kesi 634,813 duniani kote huku watu wapatao 24,329 wakiwa mahututi.

Mpaka wakati huu vifo vilivyorekodiwa duniani kote ni 29,891 waliopona wamefikia 142,366

Mpaka leo COVID-19 imeathiri nchi na ‘teritorries’ 198.

Aidha, taarifa kubwa inaeleza kuwa katika nchi ya Italia Idadi ya inazidi kuwa kubwa zaidi ikilinganishwa na nchi yoyote nyingine na vifo hivyo vinachukua theluthi moja ya jumla ya vifo vyote vya #Covid19 duniani ambavyo ni 33,982

Licha ya kutokea kwa vifo 756 Jumapili, idadi ya vifo nchini humo imeonekana kupungua ambapo Jumamosi kulirekodiwa jumla ya vifo 889 na Ijumaa vifo 969 vilirekodiwa.

Aidha, Idadi ya maambukizi kwa Jumapili yalifikia 97,689 kutoka 92,472 ikiwa ni kiwango kidogo cha maambukizi kuongezeka tangu Jumatano Machi 25, 2020.

SASISHO: Machi 28, Mpaka kufikia leo kuna kesi 571,659 duniani kote huku watu wapatao 19,189 wakiwa mahututi.

Mpaka wakati huu vifo vilivyorekodiwa duniani kote ni 26, 493 huku waliopona wakiwa 140,903.

Mpaka leo COVID-19 imeathiri nchi na ‘teritorries’ 197.

Aidha, katika idadi hiyo, inaelezwa kuwa katika nchi ya Marekani kuna maambukizi mapya 15,537 na linakuwa Taifa linaloongoza duniani kwa kasi ya maambukizi.

Mpaka sasa, watu 1,557 wamefariki dunia huku 2,465 wakipona maradhi ya #COVID_19 nchini humo.

Kwa upande wa nchi ya Hispania inaelezwa kuwa Idadi ya walioambukizwa imefikia 65,719 na katika hao 9,444 ni watumishi wa sekta ya afya.

Uhispania ina idadi kubwa zaidi ya watumishi wa afya waliopata #COVID_19 duniani.

SASISHO: Machi 27, Mpaka kufikia leo kuna kesi 509,164 duniani kote huku watu wapatao 18,929 wakiwa mahututi.

Mpaka wakati huu vifo vilivyorekodiwa duniani kote ni 23,335 ambapo waliopona wakiwa ni watu 116,223.

Mpaka leo COVID-19 imeathiri nchi na ‘teritorries’ 196.

Zaidi ya hayo mpaka kufikia sasa, Nchi ya Marekani yawa nchi yenye maambukizi mengi zaidi, yaizidi China.

Ina jumla ya maambukizi 85,594 huku China ikiwa na maambukizi 81,340 na Italia maambukizi 80,589

Italia inaongoza kwa vifo, ikiwa na vifo 8,215, Marekani kuna vifo 1,300 na China vifo 3,292

Kwa upande wa Afrika Mashariki, Nchi ya Rwanda imeripoti maambukizi mapya 9 huku idadi ya jumla ikiwa waathirika 50.

Aidha, inaelezwa kuwa katika maambukizi hayo 9, watano wametoka Dubai, 1 Marekani, 1 Uholanzi na 2 wameambukizwa nchini humo

SASISHO: Machi 26, Hadi mapema leo kesi za coronavirus duniani zimefikia 471,820 huku wagonjwa 14,795 wakiwa katika hali mbaya zaidi

Mpaka sasa idadi ya vifo 21,297 tayari vimeripotiwa duniani kote huku watu wapatao 114,703 wakiripotiwa kupona kabisa

Mpaka sasa COVID-19 imeathiri nchi na ‘territories’ 198

Katika juhudi za kuudhibiti ugonjwa huu, nchi ya Ethiopia inawaachia huru wafungwa zaidi ya 4,000 kuanzia leo, miongoni mwao wakiwa ni wenye makosa madogo, wanawake wajawazito na wale waliobakiza mwaka 1 kukamilisha vifungo

SASHIHO: Machi 25, Mpaka kufikia leo kuna kesi 425,059 duniani kote huku watu wapatao 13,129 wakiwa mahututi.

Mpaka wakati huu vifo vilivyorekodiwa duniani kote ni 18,944 ambapo waliopona wakiwa ni watu 109,225.

Mpaka leo COVID-19 imeathiri nchi na ‘teritorries’ 194.

Katika juhudi za kupambana na ugonjwa huu, Rais Uhuru Kenyatta aagiza mishahara ya maafisa wa juu wa Serikali, Rais na Makamu wa Rais kupunguzwa kwa 80%. Aagiza pia Wakenya wanaolipwa mshahara chini ya TZS 500,000 kusamehewa kodi.

Uhispania yaipiku China kwa vifo vingi zaidi. Idadi imefikia 3,434 baada ya vifo vipya 738 kuripotiwa. China ina vifo 3,281 hadi sasa. Nchi hiyo inakuwa ya 2 kwa idadi ya vifo ktk mlipuko huu wa Corona baada ya Italia

SASISHO: MACHI 24, Mpaka kufikia leo kuna kesi 408,913 duniani kote huku watu wapatao 12,547 wakiwa mahututi.

Mpaka wakati huu vifo vilivyorekodiwa duniani kote ni 18,289 ambapo waliopona wakiwa ni watu 107,073.

Mpaka leo COVID-19 imeathiri nchi na ‘teritorries’ 196.

SASISHO: Machi 23, Mpaka kufikia leo kuna kesi 332,930 duniani kote huku watu wapatao 13,886 wakiwa mahututi.

Mpaka wakati huu vifo vilivyorekodiwa duniani kote ni 14,510 ambapo waliopona wakiwa ni watu 101,423.

Mpaka leo COVID-19 imeathiri nchi na ‘teritorries’ 195.

SASISHO: Machi 22, Mpaka kufikia sasa kuna kesi 335,403 duniani kote huku watu wapatao 10,640 wakiwa mahututi.

Mpaka wakati huu vifo vilivyorekodiwa duniani kote ni 14,611 ambapo waliopona wakiwa ni watu 95,892.

Mpaka leo COVID-19 imeathiri nchi na ‘teritorries’ 192.

Aidha, kwa upande wa Afrika Mashariki Wizara ya Afya Uganda amethibitisha kisa cha kwanza cha Covid19 nchini humo. Waziri wa Afya Dkt Ruth Aceng amesema mgonjwa huyo ni mganda mwenye miaka 36 aliyerudi kutoka Dubai 21 Machi, saa nane usiku.

Mtu huyo alienda Dubai Machi 17, alitumia siku nne huko kwa masuala ya kibiashara. Alikuwa na afya njema wakati anaenda Dubai Dkt Aceng alisema.

Mtu huyo ametengwa, abiria wote waliosafiri nae wako karantini na passport zao zinashikiliwa na serikali ya Uganda.

Kwa upande wa Tanzania, mpaka sasa wagonjwa wamefika 12 huku wagonjwa 4 wakiwa raia wa kigeni na wengine 8 wakiwa Watanzania.

Zaidi ya hayo, inaelezwa kuwa mgonjwa wa kwanza kubainika na virusi Tanzania amepimwa tena na kukutwa hana viriusi hivyo.

SASISHO: Machi 21, Mpaka kufikia sasa kuna kesi 304,986 duniani kote huku watu wapatao 9,381 wakiwa mahututi.

Mpaka wakati huu vifo vilivyorekodiwa duniani kote ni 12,987 ambapo waliopona wakiwa ni watu 94677.

Mpaka leo COVID-19 imeathiri nchi na ‘teritorries’ 188.

Aidha kwa upande wa Afrika: DR Congo na Mauritius zimeripoti kifo cha kwanza kila moja

Mawaziri 4 wa Burkina Faso wamepata #Covid_19 huku Raia wa Italia aliyekuwa Mgonjwa wa kwanza Nigeria amepona

Pia, Misri imetangaza kufunga Misikiti kwa wiki 2 na kuzuia makundi ya sala

Kwa upande wa Rwanda inaelezwa mtoto wa miezi kumi aambukizwa Covid 19

Wizara ya Afya ya nchi hiyo jana imetangaza, watu wengine 6 wameambukizwa #CoronaVirus miongoni mwao ni mtoto wa miezi 10

Rwanda hadi sasa ina visa 17 vya maambukizi wote wametoka nchi za nje hivi karibuni

SASISHO: Machi 20, Mpaka sasa kuna kesi 246,020 duniani kote huku watu wapatao 7,388 wakiwa mahututi.

Mpaka wakati huu vifo vilivyorekodiwa duniani kote ni 10,049 ambapo waliopona wakiwa ni watu 88,483.

Mpaka leo COVID-19 imeathiri nchi na ‘teritorries’ 182.

Kwa mujibu wa Chuo Kikuu Johns Hopkins, (Baltimore, Marekani ) takwimu zinazoonesha hadi 20 Machi 2020 (GMT+1) vimeripotiwa visa 245,061. vya maambukizi na vifo 10,037. ikiwemo Tanzania.

TAIFA. MAAMBUKIZI. VIFO.
1. Uchina- Maambukizi -81,193 Vifo- 3,252
2. Italia- Maambukizi- 41,035 Vifo- 3,405
3. Iran- Maambukizi- 18,407 Vifo- 1,284
4. Uhispania- Maambukizi- 18,077 Vifo- 833
5. Ufaransa- Maambukizi- 10,997 Vifo- 372
6. Marekani- Maambukizi- 14,161 Vifo- 205
7. Uingereza- Maambukizi- 3,269 Vifo- 144
8. Korea Kusini- Maambukizi- 8,652 Vifo- 94
9. Uholanzi- Maambukizi- 2,460 Vifo- 76
10. Ujerumani- Maambukizi- 15,320 Vifo- 44

SASISHO: Machi 19, Hadi kufikia sasa jumla ya mataifa yaliyoathirika ulimwenguni yafikia 176. Jumla kesi za Covid 19 zilizohibitishwa ni 230,041 huku ikielezwa kuwa watu wapatao 6,942 wakiwa na hali mbaya.

Sambamba na hilo, vifo vya watu kutokana na Covid 19 vyafikia 9,386 huku watu waliofanikiwa kupona baada ya matibabu wakiwa 86,256.

Aidha, katika takwimu hizo za kiulimwengu nchini Tanzania kesi 3 mpya zimeripotiwa leo na kufikia jumla ya kesi 6 ndani ya siku tatu. Kesi tatu zote zilizoripotiwa leo zinatoka kwa Raia wa kigeni. Tahadhari inaendelea kuchukuliwa katika nyanja mbalimbali.

Italia yaipiku Uchina kwa idadi ya vifo vilivyotokana na virusi Corona. Italia, ikiwa na raia milioni 60, imerekodi vifo 3,405, au takriban 150 zaidi ya Uchina, nchi ambayo ina idadi kubwa ya watu zaidi ya mara 20 ya Italia

SASISHO: Machi 18, Virusi hivyo vimeendelea kusambaa huku nchi takriban 39 Duniani zikizuia safari za Kimataifa (kuingia na kutoka) hususan kutoka Nchi zenye Maambukizi - Hadi kufikia mapema leo, Wagonjwa walikuwa 198,426, vifo vilikuwa 7,987 huku watu 82,763 wakipona Ulimwenguni.

Aidha, kwa upande wa Tanzania mpaka sasa zimeongezeka kesi mbili za Watu waliokutwa na virusi vya Corona huku mmoja akiwa raia wa Ujerumani na mwingine raia wa Marekani. Kwa ujumla mpaka tarehe ya leo Tanzania kuna jumla ya kesi 3.

SASISHO: Machi 17, Wagonjwa wafikia 179111 ulimwenguni kote huku wagonjwa wapya wakiwa 11525.

Vifo vimefikia 7426 huku vifo vipya kuripotiwa ni 475. Mataifa mbalimbali yazidi kuchukua tahadhari huku baadhi yake yakifunga mipaka na kukataza mikusanyiko.

Aidha, kwa upande wa Tanzania kisa cha kwanza cha virusi vya Corona kimeripotiwa kutoka mkoani wa Arusha ambapo Mwanamke mwenye umri wa Miaka 40 ameripotiwa kukutwa na virusi hivyo. Taarifa zinadai kuwa mwanamke huyo alitokea nchini Ubelgiji.

SASISHO: Machi 16, Wagonjwa wafikia 169,605, vifo 6,518 na Watu 77,775 wakiripotiwa kupona

Virusi vyasambaa katika Mataifa 157 Duniani kote yakiwemo Mataifa 26 ya Afrika, huku nchi mbalimbali zikiendelea kuchukua tahadhari kwa kufunga shule, Vyuo/Taasisi na kuzuia safari za Kimataifa

SASISHO: Machi 15; Italia yarekodi vifo 368 kwa siku moja. Visa 24,747 vyarekodiwa huku vifo kwa nchi nzima vikifikia 1,809

Duniani kote, idadi ya visa vyote yafikia 167,307 huku vifo vikiwa ni 6,455

SASISHO: Machi 14; China imekwisha ripoti visa 80,824 vikiwemo vifo 3,189 nchini humo mpaka sasa.

Wagonjwa wapatao 65,541 mpaka sasa wametibiwa dalili za COVID-19 na kupata ahueni huku 3,610 wakiwa katika hali mbaya zaidi.

Duniani kote, idadi ya visa vyote imefikia 147,019 vikiwemo vifo 5,524 huku wagonjwa wapatao 73,428 wakitibiwa dalili za COVID-19 na kupata ahueni.

SASISHO: Machi 7; Idadi ya visa vyote nchini China imefikia 80,695 huku idadi ya vifo vyote kutokana na ugonjwa wa virusi vya Corona (COVID-19) ikifikia 3,097.

Jumla ya visa 105,912 vimeripotiwa kote duniani huku watu wapatao 3,597 wakipoteza maisha ulimwenguni kote kutokana na ugonjwa wa virusi vya Corona (COVID-19) kulingana na takwimu rasmi.

Wagonjwa wapatao 59,866 wameripotiwa kupata ahueni huku visa vya COVID-19 vikizidi kuongezeka zaidi katika sehemu mbalimbali duniani.

SASISHO: Machi 2; Wizara ya afya ya China imeripoti visa vipya 125 pamoja na vifo vipya 31 nchini humo. Visa 114 kati ya hivyo pamoja na vifo vyote 31 ni kutoka katika mkoa wa Hubei pekee.

Hadi hivi sasa, visa vya COVID-19 vipatavyo 90,917 vimeripotiwa duniani huku idadi ya waliokufa kutokana na ugonjwa wa virusi vya Corona ikifikia 3,123 ulimwenguni kote kulingana na takwimu rasmi.

SASISHO: Machi 1; Wizara ya afya ya China imeripoti visa vipya 202 pamoja na vifo vipya 42 nchini humo. Visa 196 kati ya visa vipya vilivyoripotiwa pamoja na vifo vyote 42 ni kutoka katika mkoa wa Hubei pekee.

Mpaka sasa, watu wapatao 3,045 wameripotiwa kufariki dunia duniani kote kutoka na virusi vya Corona huku visa vipatavyo 89,067 vikiripotiwa ulimwenguni.

SASISHO: Februari 29; Wizara ya afya nchini China imeripoti visa vipya 573 pamoja na vifo vipya 35 nchini humo huku visa 570 na vifo 34 vikiripotiwa katika mkoa wa Hubei pekee.

Hadi hivi sasa, China imekwisharipoti visa vipatavyo 79,824 pamoja na vifo 2,870 nchini humo tokea mlipuko wa ugonjwa wa virusi vya Corona (COVID-19) ulipoanza huku wagonjwa wapatao 41,825 wakiripotiwa kupata nafuu na wengine 7, 365 wakiwa katika hali mbaya zaidi.

SASISHO: Februari 28; Wizara ya afya ya China imeripoti visa vipya 427 pamoja na vifo vipya 47 nchi nzima. Kati ya hivyo, visa vipya 423 pamoja na vifo vipya 45 vimeripotiwa mkoani Hubei pekee.

Kulingana na takwimu zilizo rasmi, visa vipatavyo 84,587 vimeripotiwa duniani kote hadi sasa huku idadi ya waliokufa kutokana na virusi vya COVID-19 duniani ikifikia 2,923.

SASISHO: Februari 27; Wizara ya afya ya China imeripoti visa vipya 327 pamoja na vifo vipya 44 huku visa 318 na vifo 41 kati ya hivyo vikiripotiwa mkoani Hubei pekee.

SASISHO: Februari 26; Wizara ya afya ya China imeripoti visa vipya 433 pamoja na vifo vipya 29 nchini humo.

Ongezeko hilo linapelekea idadi ya visa vyote ulimwenguni kufikia 82,147 huku idadi ya vifo vyote kutokana na virusi vya Corona ikifikia 2,772 duniani kote kwa mujibu wa takwimu rasmi.

SASISHO: Februari 25; Wizara ya afya ya China imeripoti visa vipya 406 pamoja na vifo vipya 52.

Hadi hivi sasa, idadi ya watu waliokufa kutokana na virusi vya Corona duniani imefikia 2,763 huku visa 80,955 vikiripotiwa ulimwenguni kote.

SASISHO: Februari 24; Wizara ya afya ya China imeripoti visa vipya 508 pamoja na vifo vipya 71 nchini humo. Visa tisa (9) pamoja na vifo vitatu (3) kati ya hivyo vimeripotiwa nje ya mkoa wa Hubei.

SASISHO: Februari 23; Wizara ya afya ya China imeripoti vifo vipya 150 pamoja na visa vipya 409 nchini humo. Idadi ya visa vyote ulimwenguni imefikia 79,558 huku idadi ya vifo ikiwa ni 2,619 duniani kote kwa mujibu wa takwimu rasmi.

SASISHO: Februari 22; Hubei imeripoti visa vipya 630 pamoja na vifo vipya 96 kutokana na virusi vya Corona mkoani humo. Mpaka sasa visa takribani 78,754 vimeripotiwa ulimwenguni huku idadi ya waliokufa kutokana na virusi vya Corona ikifikia 2,460 duniani kote.

Takwimu hizo ni kulingana na ripoti rasmi.

SASISHO: Februari 21; Wizara ya afya ya China imeripoti visa vipya 397 nchini humo pamoja na vifo vipya takribani 109 huku vifo 106 kati ya hivyo vikitokea katika mkoa wa Hubei pekee.

Virusi vya Corona hadi sasa vimekwishapoteza maisha ya watu wapatao 2,360 duniani kulingana na takwimu rasmi huku visa takribani 77,812 vikiripotiwa ulimwenguni kote.

SASISHO: Februari 20; Vifo vipya 115 vimeripotiwa Hubei nchini China huku visa vipya 411 vikiripotiwa mkoani humo.

Idadi ya visa vyote ulimwenguni imefikia 76,188 hadi sasa huku watu wapatao 2,245 wakipoteza maisha.

Wagonjwa takribani 11,728 wako mahututi huku wagonjwa wapatao 15,827 wakipata nafuu. na kuruhusiwa kutoka hospitalini.

SASISHO: Februari 19; Hubei nchini China imeripoti vifo vipya 108 kutokana na virusi vya Corona huku visa vipya takribani 349 vikiripotiwa mkoani humo.

Kulingana na takwimu rasmi, jumla ya visa 75,640 vimeripotiwa ulimwenguni huku idadi ya waliokufa kutokana na virusi vya Corona ikifikia 2,121 hadi sasa.

SASISHO: Februari 18; Vifo vipya 132 pamoja na via vipya 1,693 vimeripotiwa Hubei nchini China huku maeneo mengine ndani ya China yakiripotiwa kuwa na visa vipya 48 pamoja na vifo vipya viwili (2).

Watu wapatao 2,010 wamekufa kutokana na virusi vya COVID-19 huku watu zaidi ya 75,000 wakibainika kuwa na maambukizi ya virusi hivyo ulimwenguni.

SASISHO: Februari 17; Hubei imeripoti visa vipya 1,807 pamoja na vifo vipya 93 kutokana na virusi vya COVID-19.

Nchini China, nje ya mkoa wa Hubei vimeripotiwa vifo vipya vitano (5) pamoja na visa vipya 79, kulingana na wizara ya afya nchini humo.

Mpaka sasa, watu takribani 1,873 wamekufa kutokana na virusi hivyo huku visa zaidi ya 73,000 vikiripotiwa duniani kote.

SASISHO: Februari 16; Hubei imetangaza vifo vipya 100 kutokana na virusi vya COVID-19.

Pia, visa vipya 1,933 vimeripotiwa mkoani humo huku idadi ya walioambukizwa virusi hivyo ikipindukia 70,000 ulimwenguni kote.

SASISHO: Februari 15; Hubei imeripoti ongezeko la vifo 139 ambavyo ni sawa na ripoti ya siku iliyopita pamoja na visa vipya 1,843 mkoani humo huku jumla ya waliokufa kutokana na virusi vya Corona (SARS-CoV-2) wakifikia 1,666.

SASISHO: Februari 14; Hubei imetangaza vifo vipya 139 pamoja na visa vipya 2,420 vya COVID-19.

Ripoti ya leo inapelekea ongezeko la visa vyote ulimwenguni kufikia 66,887 huku idadi ya waliokufa kutokana na virusi hivyo ikifikia 1,523.

SASISHO: Februari 13; Mkoa wa Hubei nchini China umetangaza vifo vipya takribani 116 pamoja na visa vipya 4,823 mkoani humo.

Idadi ya visa vyote nchini China imefikia 64,627 huku idadi ya visa vyote ulimwenguni ikifikia 65,210.

Jumla ya watu 1,483 wamekufa kutokana na virusi hivyo nchini humo na 1,486 duniani kote.

SASISHO: Februari 12; Mkoa wa Hubei nchini China umetangaza vifo vipya 242 kutokana na virusi vya Corona.

Visa vipya 14,840 vimeripotiwa mkoani humo na kufikisha visa 60,016 duniani kote.

Idadi ya waliokufa kutokana na virusi hivyo kwa mujibu wa ripoti rasmi mpaka sasa wamefikia 1355 ulimwenguni huku idadi kubwa ya vifo hivyo vikitokea nchini China.

SASISHO: Februari 11; Mkoa wa Hubei umeripoti vifo vipya 94 pamoja na visa vipya 1,638.

Katika mkoa huo pekee, idadi ya vifo imeongezeka mpaka kufikia 1,068.

Kutokana na ongezeko la vifo 94, jumla ya vifo vyote mpaka sasa kutokana na virusi vya Corona ni 1,112 duniani kote huku watu takribani 44,754 ulimwenguni wakigundulika kuwa na maambukizi ya virusi hivyo.

SASISHO: Februari 11; Shirika la afya duniani WHO limetangaza kuupatia jina jipya ugonjwa mpya unaotokana na virusi vya Corona.

Kwa mujibu wa shirika la afya duniani WHO, ugonjwa huo sasa utaitwa COVID-19.

SASISHO: Februari 10; Idadi ya vifo kutokana na virusi vya Corona yafikia 1013 ulimwenguni.

Mamlaka ya afya ya mkoani Hubei imeripoti kuwa watu 103 zaidi wamekufa kwa ugonjwa wa Corona katika mkoa wa Hubei Jumatatu, na kuongeza idadi ya vifo katika mlipuko wa janga hilo kufikia 974 mkoani humo.

Visa vipya takribani 2,097 vimeripotiwa katika mkoa huo.

SASISHO: Februari 9; Mkoa wa Hubei nchini China umeripoti visa vipya 2,618 pamoja na vifo vipya 91.

Kutokana na ongezeko hilo, idadi ya vifo duniani kote imefikia 904 huku zaidi ya watu 40,000 wakibainika kuwa na maambukizi.

SASISHO: Februari 8; Idadi ya vifo imeongezeka mpaka kufikia 719 huku zaidi ya watu 34,000 wakigundulika kuwa na maambukizi ya virusi vya Corona.

Mkoa wa Hubei nchini China ambao ndiyo kitovu cha mlipuko wa virusi vya Corona umeripoti vifo vipya 80 pamoja na visa vipya 2,841.

SASISHO: Februari 7; Idadi ya waliokufa kutokana na virusi vya Corona yaongezeka mpaka kufikia 638.

China imethibitisha vifo vipya 73 pamoja na visa vipya 3,143 kwa siku ya jana pekee. Vifo vipya 69 pamoja na visa vipya 2,447 ni katika mkoa wa Hubei pekee.

SASISHO: Februari 6; Mkoa wa Hubei nchini China umeripoti vifo vipya 70 na visa vipya 2,987 vya virusi vya Corona.

Idadi ya jumla ya vifo vyote imepanda mpaka kufikia 564 huku visa vyote vikiongezeka mpaka kufikia 27,648 duniani kote. Wagonjwa wapatao 911 wamepata nafuu.

SASISHO: Februari 5; Jumla ya visa vote kutokana na virusi vya Corona yafikia 23,858 mpaka sasa huku idadi ya vifo ikifikia 492 kutoka 426 ikiwa ni ongezeko la vifo 66.

China bara pekee ni jumla ya visa 23,648 na idadi ya vifo ni 490.

SASISHO: Februari 4; Ripoti mpya yaonesha ongezeko la visa mpaka kufikia 19,852 duniani kote huku idadi ya vifo ikifikia 426 mpaka sasa.

Jumla ya visa 19,668 pamoja na vifo takribani 425 ni ndani ya China bara pekee.

SASISHO: Februari 3; Watu karibu 17,500 wamekwisha thibitika kuwa na maambukizi ya virusi vya Corona duniani kote huku watu takribani 362 wamepoteza maisha kutokana na virusi hivyo.

SASISHO: Januari 30; Idadi ya vifo kutokana na virusi vya Corona yafikia 169.

Hili ni ongezeko la vifo 37 toka ripoti ya mwisho ya vifo 132 ilipotoka huku vikiripotiwa visa vipya zaidi ya 1000. Vifo 162 kati ya hivyo ni kutokea mkoa wa Hubei pekee.

SASISHO: Januari 28; Idadi ya vifo kutokana na virusi vya Corona imeongezeka kutoka 106 hadi 131.

Taarifa ya vifo vipya 25 ni kutoka katika mkoa wa Hubei pamoja na visa vipya takribani 840 kwa siku ya jana pekee (Januari 28).

SASISHO: Januari 27; Idadi ya vifo kutokana na virusi vya Corona (Coronavirus) imekwisha fikia 106 hivi sasa kutoka idadi iliyoripotiwa mara ya mwisho ya 82.

Mkoa wa Hubei, China pekee umeripoti visa vipya takribani 1291 na vifo vipya 24.

Wagonjwa wapatao 690 wana hali mbaya zaidi.

SASISHO: Beijing, China imetangaza kifo cha kwanza kabisa katika jiji hilo kutokana na kirusi cha Corona, mwanamume wa miaka 50 aliyekuwa amesafiri kwenda Wuhan tarehe 8, Januari na kurejea jijini Beijing tarehe 15. Idadi ya vifo imefikia 82.

SASISHO: Kifo kingine kimeripotiwa kutokana na kirusi cha Corona katika mkoa wa Hainan nchini China. Hicho ni kifo cha kwanza kabisa katika mkoa huo. Jumla ya vifo kutokana na kirusi hicho ni 81 mpaka sasa.

SASISHO: Idadi ya vifo nchini China kutokana na virusi vya Corona imeongezeka na kufikia 80 mpaka sasa huku idadi ya wenye maambukizi ikifikia zaidi ya 2700 ikijumuisha Hong Kong, Macau pamoja na Taiwan.

UPDATES NYINGINEZO KUHUSU GONJWA HILI PITIA HAPA

MORE UPDATES:

View attachment 1401219

APRILI 16, 2020
CALIFORNIA: WAUZAJI WA MAZIWA WAYATUPA KWA KUKOSA SOKO

Wauzaji wa maziwa katika Jimbo la California wanalazimika kutupa maziwa hayo baada ya soko kupungua kutokana na kufungwa kwa migahawa na shule

Mkurugenzi Mtendaji wa Western United Dairies, Anja Raudabaugh ambaye anawakilisha takriban Wafugaji 860 amesama baada ya agizo la kukaa ndani kutolewa, migahawa ilifungwa na asilimia 50 ya Wateja ilipotea kwa usiku mmoja

Amesema migahawa mikubwa kama TGI Friday’s na Applebee’s iliyokuwa ikichukua maziwa mengi na kuwa Wateja wakubwa kwa wafugaji, iliacha kununua maziwa tangu katikati ya mwezi Machi

Aidha, Wafugaji walipata pigo zaidi baada ya Shule kufungwa na vyakula vya mchana kutotolewa shuleni jambo linalowafanya kuwa na hifadhi kubwa ya maziwa kuliko mahitaji

APRILI 15, 2020
MAREKANI YAWEKA REKODI MPYA, WATU 2,228 WAFARIKI KWA SIKU 1

Marekani imerekodi idadi kubwa ya vifo 2,228 ndani ya saa 24 na kufikia vifo 28,368 hadi sasa kwa mujibu wa Chombo cha Habari cha Reuters. Idadi kubwa ya awali ilikuwa Ijumaa ambapo vifo 2,069 vilirekodiwa

Nchi hiyo ambayo ni ya tatu kwa idadi kubwa ya watu duniani imerekodi Waathirika 606,194 hadi kufikia mapema leo idadi ambayo ni kubwa kwa mara tatu kwa nchi inayoifuata kwa Waathirika wa #COVID19

Ongezeko la vifo 2,228 halijumuishi makusudio ya Jiji la New York kujumuisha idadi ya vifo vinavyodhaniwa vimetokana na #CoronaVirus bila kupimwa

Mamlaka za New York zimeripoti vifo 3,778 vinavyodhaniwa ni kwasababu ya corona ambapo madaktari walijiridhisha ni kutokana na ugonjwa huo, na vifo 6,589 vilivyothibitishwa maabara. Ukijumlisha idadi hiyo ya vifo inafika zaidi ya 10,000

KENYA: IDADI YA WAATHIRIKA YAFIKIA 225. VIFO VYAFIKIA 10

Idadi ya waliopata maambukizi ya #COVID19 imeongezeka na kufikia 225 baada ya wagonjwa wapya 9 kuthibitika na virusi hivyo kufuatia kupimwa kwa sampuli 803 ndani ya saa 24

Waziri wa Afya, Mutahi Kagwe amesema wagonjwa wote wapya ni raia wa Kenya na hawana rekodi ya kusafiri nje ya nchi hiyo kwa hivi karibuni. Ni miongoni mwa watu waliokuwa wakifuatiliwa

Ameeleza kuwa kati ya wagonjwa hao wapya, watano wanatokea Nairobi na wanne wanatokea Mombasa na umri wao ni katika ya miaka 9 na miaka 69

Aidha, watu 12 wamepona ugonjwa huo na kuruhusiwa kutoka hospitalini; Idadi ya waliopona imefikia 53. Mtu mmoja amefariki kwa ugonjwa huo

Waziri amebainisha kuwa jumla ya watu 2,336 waliokutana na waathirika wamekuwa wakifuatiliwa, huku 1,911 wakiachiwa na wengine 455 wakiwa bado wanafuatiliwa

APRILI 14, 2020
KUNDI LA WACHUNGAJI LAMSHTAKI GAVANA WA CALIFORNIA KWA KUZUIA MIKUSANYIKO YA KIDINI

Kundi la Wachungaji kutoka Kusini mwa Jimbo la California limemshtaki Gavana Gavin Newsom na baadhi ya Watendaji kwa kuzuia Waumini kwenda Kanisani kutokana na #CoronaVirus

Mashtaka hayo yamefunguliwa jana katika Mahakama ya huko California na Kampuni ya Kisheria ya Dhillon, kwa niaba ya Walalamikaji wanne na watatu kati yao ni Wachungaji

Walalamikaji ni Dean Moffatt, Mchungaji katika Kanisa la Indio anayedaiwa kupigwa faini ya $1,000 kwa kuongoza Ibaya ya Jumapili ya Matawi; Brenda Wood, Mchngaji wa Kanisa la Riverside; Patrick Scales, Mchungaji wa Kanisa la Fontana na Wendy Gish Muumini wa kanisa la Fontana

Walalamikaji hao pia wanamshtaki Mwanasheria Mkuu wa Jimbo, Xavier Becerra na baadhi ya Watendaji wa Kaunti za Riverside na San Bernardino wakiwemo Polisi na Wafanyakazi wa sekta ya Afya

Machi 19, Newsom alitoa agizo la kwanza la kuwataka Wakazi takriban milioni 40 wa California kukaa nyumbani ili kupunguza kusambaa kwa virusi hiyo

APRILI 13, 2020
ASILIMIA 18 YA POLISI WA NEW YORK WAHOFIWA KUUNGUA #COVID19

Takriban Polisi 6,522 wa Idara ya Polisi ya New York hawakuweza kufika kazini siku ya jana kwa mujibu wa ripoti ya kila siku ya #CoronaVirus ya Idara hiyo

Ripoti hiyo imeeleza kuwa hadi sasa Polisi 2,344 na Wafanyakazi wasio Polisi 489 wa Idara hiyo ndio wamethibitika kuwa na ugonjwa wa #COVID19

Ongezeko la Wagonjwa 5,695 kwa siku ya jana kumefanya New York kuwa na zaidi ya Waathirika 104,000 na takriban vifo 6,182 vilivyorekodiwa

Kwa ujumla Marekani ndio nchi iliyoathirika zaidi duniani na virusi hivi ikiwa na jumla ya Waathirika 560,433 huku ikiwa imesharipoti vifo 22,115

APRILI 12, 2020
MAREKANI YAIZIDI ITALIA KWA VIFO

Marekani imeipita Italia kwa vifo ikiwa imerekodi vifo 20,602 na ikiwa na Waathirika takriban 529,740 kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Chuo Kikuu cha Johns Hopkins

Waathirika hao wapo katika Majimbo yote 50 ikiwemo ‘District of Columbia’ hadi sasa Jimbo pekee ambalo halijatangaza kifo cha mgonjwa wa #COVID19 ni Wyoming pekee

Takriban nusu ya vifo hivyo vimetokea New York ambapo Gavana wa sehemu hiyo, Andrew Cuomo amesema Jana kuwa Ijumaa kulitokea vifo 783 na kufanya Jimbo hilo kuwa na vifo 8,627

Aidha, kwa mujibu wa takwimu, Marekani ilikuwa na vifo 58 wiki nne zilizopita, na katika wiki 3 zilizopita ilikuwa na vifo 323. Katika wiki mbili zilizopita vifo vilifika 2,043 na wiki moja iliyopita kulikuwa na vifo 8,488

Jana, Aprili 10, 2020 Italia ilitangaza jumla ya vifo 619 vipya vinavyohusiana na #COVID_19 na kufanya Taifa hilo la Ulaya kuwa na jumla ya vifo 19,468

KENYA: MAAFISA 6 WA AFYA WAPATA MAAMBUKIZI YA #COVID19 WAKIWA KAZINI

Kwa mujibu wa Umoja wa Maafisa Kliniki wa Kenya (Kenya Union of Clinical Officers), maafisa afya wapatao 6 wamepata maambukizi ya #COVID19 wakiwa kazini

Utafiti uliofanywa hivi karibuni nchini humo umebaini 68% ya wafanyakazi wa sekta ya afya ya jamii hawana mafunzo maalum ya kukabiliana na wagonjwa wa #CoronaVirus

Katibu wa Umoja huo amesema upungufu wa barakoa na glovu ni miongoni mwa vyanzo vikubwa vilivyochangia maafisa hao sita kupata maambukizi

APRILI 11, 2020
ITALIA: TAKRIBAN MAPADRI 100 WAFARIKI DUNIA KWA CORONA VIRUS

Mapadri hao wamefariki dunia baada ya kupata maambukizi ya COVID-19. Imeelezwa kuwa asilimia kubwa ya Viongozi hao wa Dini walikuwa wastaafu

Mapadri wamekuwa wakiweka maisha yao hatarini kwa kutoa huduma za kiroho kwa wazee na Waumini walioathirika zaidi na Ugonjwa huo katika maeneo mbalimbali

Nchi ya Italia ni miongoni mwa mataifa yaliyoathirika zaidi na mlipuko wa Coronavirus ikiwa na maambukizi 147,577 na vifo 18,849 hadi kufikia jioni ya leo

MAREKANI: CORONA VIRUS YAGHARIMU MAISHA YA WATU 2000 NDANI YA SIKU MOJA

Watu 2,018 wamefariki dunia kutokana COVID-19 ndani ya siku moja, idadi hiyo ya vifo ni kubwa zaidi kurekodiwa duniani

Huenda nchi ya Marekani yenye waathirika 503,177 na vifo 18,761 hadi sasa ikaipiku Italia ambayo imerekodi vifo 18,849 kufikia leo kwa kuwa na vifo vingi zaidi

Licha ya ongezeko hilo la vifo, Wataalamu wa Kikosi Kazi cha COVID-19 kutoka Ikulu wanasisitiza kuwa makali ya mlipuko huo yameanza kupungua

Rais Donald Trump naye amesema anatarajia kuona vifo vichache zaidi vikirekodiwa tofauti na makadirio yaliyotolewa awali

KOREA KUSINI: WAGONJWA 91 WALIOPONA COVID-19 WAPATA MAAMBUKIZI

Mamlaka za Korea Kusini zimeripoti kuwa takriban watu 91 waliopona Corona Virus wamepata maambukizi kwa mara ya pili

Mkurugenzi wa Kituo cha Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa nchini humo, Jeong Eun-kyeong amesema kuna uwezekano mkubwa virusi hivyo vilikuwa vimelala (dormant) na sio kwamba watu hao wameambukizwa upya

Aidha, Wataalamu wanasema huenda vipimo walivyofanyiwa watu hao vilionesha majibu ya uongo au baadhi ya virusi vilibaki mwilini ila havikuwa na madhara

Hata hivyo, Wataalamu wa Afya wa Korea Kusini bado hawajafahamu kinachosababisha hali hiyo na undani wa jambo hilo unaendelea kuchunguzwa

Hali ya wagonjwa wa Corona kupata maambukizi baada ya kupona ni suala ambalo linahofiwa kimataifa kwakuwa nchi nyingi zinatamani walioathirika watakuwa na kinga ya mwili ya kutosha itakayowazuia kuambukizwa tena

ITALIA KUBAKI KARANTINI HADI MWEZI MEI

Waziri Mkuu wa Italia, Giuseppe Conte ametangaza kuwa muda wa wananchi kutotoka nje umeongezwa hadi Mei 3 ili kudhibiti maambukizi mapya ya COVID-19

Italia ambayo imerekodi maambukizi 147,577 na vifo 18,849 hadi kufikia leo tayari imekuwa chini ya amri hiyo kwa mwezi mmoja ma wananchi wametakiwa kubaki nyumbani

Akitangaza uamuzi huo, Conte amesema wakiacha kuchukua tahadhari zaidi, watahatarisha maendeleo waliyopata mpaka sasa na kusababisha vifo zaidi

APRILI 10, 2020
UINGEREZA: BORIS JOHNSON ATOLEWA ICU

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson ametolewa katika Chumba cha Uangalizi Maalum (ICU) na kuhamishiwa wodini huku bado akiendelea kuwa chini ya uangalizi maalum

Taarifa iliyotolewa na Ofisi yake imeeleza kuwa Johnson ambaye alilazwa baada ya hali yake kubadilika ghafla anaendelea vizuri hivi sasa.

Wanasayansi wametahadharisha kuwa Uingereza inaingia katika hatua mbaya zaidi ya mlipuko wa #Covid19 na wanatarajia vifo vingi zaidi kurekodiwa kuelekea sikukuu ya Pasaka

Jumla ya maambukizi 65,077 na vifo 7,978 vimerekodiwa hadi kufikia leo

APRILI 09, 2020
UHISPANIA KULEGEZA MASHARTI, WAZIRI MKUU ASEMA KIPINDI KIGUMU KINAPITA

Waziri Mkuu wa Uhispania, Pedro Sanchez amesema nchi hiyo inatarajia kulegeza masharti ya karantini yaliyowekwa ili kudhibiti maambukizi na Virusi vya Corona

Sanchez ambaye pia ameombe Bunge kupitisha ombi lake la kuongeza muda wa hali ya tahadhari mpaka Aprili 26 amesema kutokana na athari zilizosababishwa na janga la Covid-19, mchakato wa maisha kurejea kama zamani utachukua wa taratibu

Uhispania ni nchi ya pili iliyoathirika zaidi na janga la Corona Virus baada ya Marekani. Maambukizi 152,446 na vifo 15,238 vimerekodiwa huku wagonjwa 52,165 wakipona hadi kufikia leo

Mbali na Uhispania, mataifa mengine ya Ulaya nayo yanakifikiria kulegeza masharti mapema iwezekanavyo kutokana na wasiwasi wa uchumi kuathirika kwasababu ya kuwekwa kwa amri ya karantini

APRILI 08, 2020
UINGEREZA: WAZIRI MKUU BORIS JOHNSON APATA NAFUU

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson (55) aliyewekwa Chumba cha Uangalizi Maalum (ICU) katika Hospitali ya Mtakatifu Thomas jijini London baada ya afya yake kubadilika ghafla anaendelea vizuri baada ya kupatiwa Oxygen

Johnson aliyegundulika kuwa na maambukizi ya #Covid19 wiki mbili zilizopita alifikishwa Hospitali Jumapili. Alihamishiwa ICU baada ya hali yake ilizidi kuwa mbaya zaidi. Taarifa iliyotolewa na Ofisi yake imesema anaendelea vizuri na hajawekewa mashine za kupumulia

Kwa muda ambao Johnson amelazwa Waziri wa Mambo ya Nje, Dominic Raad ataongoza harakati za kudhibiti maambukizi ya Corona na amepewa baadhi ya mamlaka ya Waziri huyo. Hata hivyo, maamuzi yote makubwa ikiwemo kusitisha karantini yatapitishwa na Baraza

Endapo Raad atashindwa kazi hiyo, Waziri wa Fedha Rishi Sunak (39) atapewa mamlaka

MAREKANI: WATU 1,736 WAFARIKI DUNIA NDANI YA SAA 24

Marekani imeripoti vifo 1,736 vilivyotokea Jumanne, idadi kubwa zaidi kurekodiwa ndani ya siku moja, ambapo asilimia kubwa ya vifo hivyo vimetokea Jijini New York

Jumla ya waliofariki kutokana na Virusi vya Corona imefikia 12,854. Maambukizi yaliyorekodiwa nchini humo mpaka sasa ni 400,412, idadi ambayo ni kubwa zaidi duniani

Rais wa Marekani Donald Trump ametishia kusitisha kutoa fedha kwa Shirika la Afya Duniani (WHO) huku akilishutumu Shirika hilo kwa kuipendelea China na kushindwa kudhibiti mlipuko huo ambao umegharimu maisha ya watu 82,080 duniani kote

Trump amesema WHO imefanya makosa na ilitakiwa kutangaza tahadhari mapema zaidi huku akidai kuwa walitakiwa kufahamu athari za mlipuko wa #Covid19 mapema zaidi, hivyo Marekani itafanya tathmini juu ya fedha ambazo inatoa kwa Shirika hilo

APRILI 07, 2020
MADAKTARI 94 NA WAUGUZI 26 WAFARIKI DUNIA

Taarifa hiyo imetolewa leo Aprili 07, 2020 na Umoja wa Madaktari nchini humo huku Shirikisho la Wauguzi likisema licha ya Wauguzi 26 kufariki wengine 6,549 wanaugua #COVID19

Kwa mujibu wa Taasisi ya Afya nchini humo, hadi kufikia jana Aprili 06, 2020 jumla ya Wafanyakazi 12,681 wa sekta ya Afya walikuwa wanaugua ugonjwa huo

Inaelezwa kuwa ukosefu wa vifaa vya kujikinga na virusi vya corona umesababisha idadi ya wafanyakazi wanaougua ugonjwa huo kuongezeka

Mojawapo ya miundombinu bora ya afya barani Ulaya ipo Kaskazini mwa Italia lakini imeshidhwa kukidhi kuhimili wingi wa wagonjwa wa #COVID_19 wanaogundulika nchini humo

Italia imeripoti jumla ya waathirika 132,547, idadi ya vifo 16,523 na waliopona hadi sasa ni 22,837

MAREKANI: WATU ZAIDI YA 10,000 WAFARIKI DUNIA

Idadi ya vifo ambayo imerekodiwa Marekani hadi asubuhi ya leo ni 10,876. Nchi hiyo inakuwa ya tatu kwa vifo vingi zaidi duniani baada ya Uhispania (13,341) na Italia (16,523)

Wataalamu wa Afya kutoka Ikulu ya Marekani wametabiri kuwa watu 100,000 hadi 240,000 wanaweza kupoteza maisha kutokana na ugonjwa wa COVID-19 hata kama maagizo ya kukaa nyumbani yakifuatwa

Marekani imesema hali inaweza kuwa mbaya wiki hii, ambapo maambukizi na vifo vingi vitarekodiwa. Miji ya New York, New Jersey, Connecticut na Detroit inatajwa kuwa katika hatari zaidi

Hadi sasa, takriban asilimia 90 ya Wamarekani wanatekeleza agizo la kukaa nyumbani na kuepuka mikusanyiko huku majimbo nane yakiwa bado hayajatoa tamko hilo

NEW ZEALAND: WAZIRI WA AFYA ASHUSHWA CHEO BAADA YA KUIPELEKA FAMILIA BAHARINI WAKATI WA KARANTINI

Waziri Mkuu wa New Zealand, Jacinda Ardern amemshusha cheo Waziri wa Afya David Clarke kwa kukiuka taratibu zilizowekwa kudhibiti maambukizi ya #Coronavirus nchini humo na kuipeleka familia yake baharini

Waziri Ardern amesema katika mazingira ya kawaida angemfukuza kabisa kazi Clarke kwasababu kitendo alichofanya sio sawa na alitarajia atakuwa mfano kwa wengine

Clarke ametolewa katika nafasi yake ya Waziri wa Afya na sasa atakuwa katika nafasi za chini za Baraza. Katika taarifa yake, amesema hakutumia busara na anaelewa kwanini watu wamekasirishwa

New Zealand yenye watu Milioni 5 ilitangaza karantini ya nchi nzima mwishoni mwa mwezi uliopita na kufunga mipaka yake, shule, migahawa pamoja na sehemu nyingine zenye mikusanyiko ya watu

Idadi ya maambukizi iliyoripotiwa nchini humo ni 1,160 na mpaka sasa kifo kimoja kimerekodiwa

APRILI 06, 2020
UHISPANIA: IDADI YA VIFO YAPUNGUA KWA SIKU NNE MFULULIZO

Idadi ya vifo vilivyorekodiwa kutokana na maambukizi ya #Covid19 imeendelea kupungua kwa siku ya nne sasa, hali ambayo inaleta matumaini kuwa Uhispania imemaliza kipindi kigumu

Uhispania yenye jumla ya waathirika 135,032 ina idadi kubwa zaidi ya maambukizi Ulaya. Vifo 637 vimeripotiwa leo na idadi ya jumla waliofariki dunia hadi sasa ni 13,055

Mbali na Uhispania, vifo nchini Italia, Ufaransa na Ujerumani pia vimeendelea kupungua. Hii inaashiria kuwa mkakati wa watu kuwekwa karantini na kuzuia mikusanyiko umesaidia kupunguza maambukizi

Maambukizi 1,287,168 ya Virusi vya Corona yameripotiwa duniani. Watu 70,530 wamepoteza maisha kutokana na Virusi hivyo na waliopona hadi leo ni 271,887

APRILI 05, 2020
MAREKANI: WATU 1,344 WAFARIKI NDANI YA SAA 24. HALI MBAYA ZAIDI YAHOFIWA

Marekani imetangaza idadi kubwa ya vifo vilivyotokana na #COVID19 kwa siku moja huku Wataalam wakitahadharisha kuwa wiki mbili zijazo zitakuwa mtihani mkubwa katika kupambana na maambukizi nchini humo

Nchi hiyo imetangaza jumla ya vifo 1,344 vilivyorekodiwa kutokea jana Aprili 04, ikiwa ndio idadi kubwa ya vifo kutokea ndani ya saa 24 kwa Taifa moja tangu kulipuka kwa Ugonjwa huo

Idadi hiyo inapelekea Marekani kuwa na jumla ya vifo 8,496 huku kukiwa na jumla ya Waathirika 312,076, idadi kubwa ya Waathirika kuliko Taifa lolote

Mratibu wa Timu ya kukabiliana na CoronaVirus ya Ikulu ya Marekani, Dkt. Deborah Birx ametahadharisha kuwa siku chache zijazo Marekani itashuhudia mtihani wake mkubwa na zitakuwa siku muhimu sana katika mapambano hayo

Amesema “Hizi ni siku za kutokwenda dukani, kutokwenda duka la dawa, na fanya lolote uwezalo unalodhani litaiweka familia yako na marafiki zako salama na hii ni kila mtu kuhahikisha anakaa umbali wa Mita 2 kutoka kwa mwenzako na unanawa mikono”

Aidha, Rais Donald Trump ameaambia Wamarekani kujiaandaa na ongezeko kubwa la vifo vitokanavyo na #Corona katika kile alichokiita wiki mbili ngumu zijazo katika mapambano na mlipuko huo

UHISPANIA: WATU 674 WAFARIKI KWA SIKU 1. IDADI NDOGO KUTOKEA TANGU MAPEMA MACHI

Watu wengine 674 wamefariki kwa #COVID19 nchini humo kwa siku ya jana Aprili 04, ikiwa ni idadi ndogo zaidi kutokea ndani ya saa 24 tangu mwezi Machi 2020

Nchi hiyo kwa sasa ina jumla ya vifo 12,418 vilivyorekodiwa ikiwa ni nchi ya pili kwa vifo vingi baada ya Italia iliyorekodi jumla ya vifo 15,362

Pamoja na kuwa ya pili kwa vifo, takwimu zinaonesha Taifa hilo linaelekea kumaliza kipindi kigumu zaidi cha mlipuko wa ugonjwa huo ambapo sasa idadi ya vifo na Waathirika wapya inayorekodiwa inapungua

Wizara ya Afya imesema leo kuna jumla ya Wagonjwa 80,261 wa #COVID19, ikiwa idadi hiyo imeongezeka kwa Wagonjwa 1,488 kutoka Jumamosi lakini pia ndio ongezeko dogo kwa siku tangu Machi 17

Ila pia Wizara hiyo imeripoti kuwa jumla ya Wagonjwa 38,080 wamepona ugonjwa huo ikiwa ni ongezeko la Wagonjwa 4,000 kutoka idadi iliyoripotiwa jana Aprili 04, 2020

APRILI 03, 2020
#CORONAVIRUS-UPDATE:
Idadi ya Watu walioathirika na maambukizi ya virusi vya #COVID19 imezidi milioni moja Ulimwenguni kwa mujibu wa Chuo Kikuu Cha Johns Hopkins

Nchi tano zenye Waathirika wengi waliorekodiwa ni Marekani (245,184), Italia (115,242), Uhispania (112,065), Ujerumani (84,794) na China (81,620)

Lakini pia nchi tano zenye idadi kubwa ya vifo vilivyoripotiwa ni Italia (13,915), Uhispania (10,348), Marekani (6,088), Ufaransa (5,387) na China (3,322)

UHISPANIA: WATU 932 WAFARIKI NDANI YA SAA 24

Kwa mujibu wa data zilizotolewa na Wizara ya Afya nchini humo leo Aprili 03, 2020, jumla ya Watu waliofariki dunia baada ya kuugua #COVID19 imefikia 10,935

Idadi hiyo imefikiwa baada ya vifo 932 vya Wagonjwa wa #Corona kurekodiwa katika saa 24 zilizopita. Jana, Wizara hiyo ilitangaza vifo 950 vilivyotokea ndani ya saa 24

Aidha, data za Wizara hiyo zinaonesha kuwa kuna Wagonjwa 76,262 kwa sasa nchini humo, ikiwa ni ongezeko la Wagonjwa 2,770 kutokea idadi ya jana lakini pia ni ongezeko dogo tangu Machi 20

Uhispania ni moja ya nchi iliyoathirika vibaya na mlipuko wa Ugonjwa huu, ikiwa ni ya pili kwa idadi ya vifo nyuma ya Italia yenye vifo 13,915. Inashika nafasi ya pili kwa Waathiriki ikiwa na Waathirika 117,710 nyuma ya Marekani (245,380)

APRILI 02, 2020
UHISPANIA: WATU 950 WAFARIKI NDANI YA SAA 24

Kwa mujibu wa data zilizotolewa na Wizara ya Afya nchini humo leo Aprili 02, 2020, jumla ya Watu waliofariki dunia baada ya kuugua #COVID19 imefikia 10,003

Idadi hiyo imefikiwa baada ya vifo 950 vya Wagonjwa wa #Corona kurekodiwa katika saa 24 zilizopita. Hii ni idadi kuwa ya vifo kwa siku moja kutokea nchini humo

Uhispania ni moja ya nchi iliyoathirika vibaya na mlipuko wa Ugonjwa huu, ikiwa ni ya pili kwa idadi ya vifo nyuma ya Italia yenye vifo 13,155. Pia, ikiwa na maambukizi 110,238 inazifuata nchi za Marekani (215,344) na Italia (110,574) kwa maambukizi mengi

BALOZI WA UFILIPINO NCHINI LEBANON AFARIKI KWA #COVID19

Bernardita Catalla aliyekuwa Mwanadiplomasia kwa miaka 27, amefariki katika hospitali iliyopo Beirut baada ya kuugua ugonjwa wa #Covid_19

Miezi kadhaa nyuma, Balozi huyo aliongoza mpango wa kuwaondoa takriban Wafilipono 2,000 nchini Lebanon, wengi wakiwa ni Wanawake waliokuwa wakifanya kazi za ndani

Tangu Oktoba 2019, Lebanon imekuwa na migogoro ya Kisiasa na Kifedha na Wakimbizi wengi wa Kiafrika na bara la Asia wanaofanya kazi nchini humo wanalalamika kulipwa kidogo au kucheleweshewa mishahara

APRILI 01, 2020
AFRIKA: WATU 203 WAFARIKI DUNIA KWA #COVID19

Kituo cha udhibiti na kuzuia magonjwa vya Umoja wa Afrika kimesema kuwa watu 203 wamepoteza maisha baada ya kuambukizwa virusi vya #Covid19

Hadi sasa #CoronaVirus imeenea katika nchi 50 barani Afrika na jumla ya maambukizi 5,886

Mpaka sasa hakuna taarifa zozote za maambukizi nchini Lesotho, Sudani Kusini, visiwa Sao Tome na Principe, Comoro na Malawi

Afrika Kusini ina idadi kubwa ya maambukizi, ikiwa imefikia 1,353, huku watu saba wakiwa wamethibitishwa kufariki kwa #Covid19

KENYA: WAGONJWA WAPYA 22 WATHIBITISHWA. MAAMBUKIZI YAFIKIA 81

Waziri wa Afya, Mutahi Kagwe amethibitisha kuwa watu 22 wamekutwa na #CoronaVirus leo ambapo idadi hii inafanya jumla ya maambukizi kufikia 81

Kati ya wagonjwa hao 22, 18 ni raia wa Kenya, 2 raia wa Pakistan na 2 ni raia wa Cameroon. Aidha 13 kati yao ni wanaume na 9 ni wanawake

Waziri amesema wagonjwa hao wapya wamepatikana baada ya Watu 300 kupimwa na kuwa kati ya hao 22, 21 walikuwa Karantini tayari

MACHI 30, 2020
ITALIA: WATU 756 WAFARIKI NDANI YA SAA 24. IDADI YA VIFO ILIYOREKODIWA YAFIKIA 10,779

Idadi ya vifo kwa Italia ni kubwa zaidi ikilinganishwa na nchi yoyote nyingine na vifo hivyo vinachukua theluthi moja ya jumla ya vifo vyote vya #Covid19 duniani ambavyo ni 33,982

Licha ya kutokea kwa vifo 756 Jumapili, idadi ya vifo nchini humo imeonekana kupungua ambapo Jumamosi kulirekodiwa jumla ya vifo 889 na Ijumaa vifo 969 vilirekodiwa

Aidha, Idadi ya maambukizi kwa Jumapili yalifikia 97,689 kutoka 92,472 ikiwa ni kiwango kidogo cha maambukizi kuongezeka tangu Jumatano Machi 25, 2020

Kati ya wale walioambukizwa nchi nzima, 13,030 walikuwa wamepona kufikia Jumapili, ikilinganishwa na 12,384 waliokuwa wamepona Jumamosi. Watu 3,906 walikuwa ICU ikilinganishwa na 3,856 waliokuwepo siku iliyopita

MAREKANI: RAIS TRUMP AONGEZA MUDA WA WATU KUKAA NDANI

Rais Donald Trump amesema muda wa watu kujitenga kwa kukaa ndani na kutokusanyika umeongezwa hadi Aprili 30 baada ya Wataalamu kuonya kuwa vifo vinaweza kufika 100,000

Amesema, "Inakadiriwa kuwa vifo vingi vinaweza kutokea kwenye wiki mbili zijazo. Hivyo kwa wiki mbili hizo na katika kipindi hiki ni muhimu watu kufuata kanuni hizo"

Ameongeza, "Kama idadi ya vifo itabaki katika 100,000 au pungufu ya hapo (Marekani), wote tutakuwa tumefanya kazi kubwa. Hivyo ni bora kila moja kufuata Kanuni hizo ili janga hili liishe mapema."

Aidha, katika hatua nyingine Trump amesema Usalama wa Taifa walimzuia kwenda New York (Mji unaoongoza kwa maambukizi Marekani) kuhudhuria ufunguzi wa hospitali ya wagonjwa wa #COVID19

Hospitali hiyo ya muda katika Kituo cha Javits inatarajiwa kuwa na vitanda takriban 2,900 ii kukabiliana na wimbi la Wagonjwa wa #COVID_19 wanaoongezeka kwa kasi

UHISPANIA: WATU 812 WAFARIKI NDANI YA SAA 24. YAIZIDI CHINA KWA IDADI YA MAAMBUKIZI

Mamlaka zimeripoti kuwa pamoja na vifo hivyo kumekuwa na jumla ya ongezeko la wagonjwa 3,515 ndani ya saa 24 na kufanya idadi ya Wagonjwa waliorekodiwa kufikia 61,075

Jumla ya Idadi ya vifo vilivyoripotiwa nchini humo imefikia 7,340 kutoka vifo 6,528 vilivyoripotiwa Jumapili. Ni nchi ya pili kwa vifo vingi baada ya ya Italia yenye vifo 10,779

Nchi hiyo imeripoti jumla ya maambukizi 85,195 kutoka 78,797 yaliyokuwepo Jumapili na kufanya nchi hiyo kuwa na maambukizi mengi kuliko China yenye maambukizi 81,470

Aidha, wagonjwa 2,071 wamepona katika saa 24 zilizopita na kufanya idadi ya watu waliopona kuwa 16,780. Katika muda huo kulikuwa na jumla ya wagonjwa 324 waliokuwa wakihitaji uangalizi maalumu

ITALIA: MADAKTARI 61 WAFARIKI DUNIA BAADA YA KUPATA MAAMBUKIZI

Kwa mujibu wa Chama cha Madaktari nchini humo, Madaktari 61 wamefariki dunia huku Wafanyakazi wengine 8,358 wa sekta ya Afya wakiwa na maambukizi ya virusi hivyo

Kati ya Madaktari hao 61, 40 walikuwa wakifanya kazi katika Mji wa Lombary ambao ndio chimbuko la virusi hivyo Italia na ndiko kwenye maambukizi mengi

Nchi hiyo ikiwa imerekodi jumla ya maambukizi 97,689 ina karibia kuwa nchi ya pili kuwa na maambukizi mengi yaliyozidi 100,000 baada ya Marekani yenye maambukizi 144,410

Aidha, nchi hiyo ina jumla ya vifo 10,779 vilivyorekodiwa na vikiwa vinachukua takriban theluthi moja ya jumla ya vifo vyote vya #Covid19 duniani ambavyo ni 35,339

MACHI 29, 2020
CORONAVIRUS MAREKANI: MJI WA NEW YORK KUTOWEKWA KARANTINI

Rais Donald Trump amesema Mji wa New York wenye maambukizi mengi Marekani (53,455) hautawekwa karantini na kuagiza Kituo cha Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa (CDC) kutoa maelekezo kwa wasafiri

Uamuzi wake unakuja siku chache baada ya kutangaza kuwa anafikiria kuiweka Miji ya New York, New Jersey (maambukizi 11,124) na Connecticut (maambukizi 1,524) karantini ili kuzuia maambukizi ya #COVID_19

Awali, Gavana wa New York, Andrew Cuomo alipinga Mji huo kuwekwa karantini na kudai soko la hisa litaporomoka vibaya na itachukua miezi kama sio miaka kwa uchumi wa Marekani kurudi kama ulivyokuwa

Baada ya agizo hilo, CDC imewataka wananchi kutoka Miji hiyo mitatu kusitisha safari zote za ndani zisizo na umuhimu kwa muda wa siku 14. Agizo hilo halitawahusu watoa huduma za chakula, afya na fedha

ITALIA: WATU ZAIDI YA 10,000 WAFARIKI DUNIA KWA #CORONAVIRUS

Idadi ya waliopoteza maisha kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona nchini Italia imefikia 10,023 baada ya vifo 889 kuripotiwa Jumamosi

Mbali na vifo hivyo, maambukizi mapya 5,974 pia yameripotiwa ndani ya saa 24 zilizopita na nchi hiyo ina jumla ya maambukizi 92.472 mpaka sasa

Italia ina wagonjwa 70.065 na kati yao 66,209 wana hali nzuri huku wengine 3,856 wakiwa na hali mbaya. Wagonjwa waliopona #COVID_19 ni 12.384

Nchi hiyo itashusha bendera nusu mlingoti katika miji mbalimbali Machi 31 mwaka huu, ili kuwaenzi waliofariki dunia kutokana na ugonjwa huo

MACHI 27, 2020
CORONAVIRUS: MAREKANI YAIZIDI CHINA KWA IDADI YA MAAMBUKIZI

Marekani imeripoti jumla ya maambukizi 85,594 na kuwa nchi yenye maambukizi mengi zaidi ikiizidi China yenye maambukizi 81,340 na Italia yenye maambukizi 80,589

Hata hivyo italia bado inaongoza kwa vifo vilivyotokana na #Covid_19, ikiwa imetangaza vifo 8,215 ikifuatiwa na Uhispania yenye vifo 4,365 huku Marekani ikiwa na vifo 1,300 na China kuna vifo 3,292

Huko Chicago katika Gereza la Cook County lenye Wafungwa 5,400, Wafungwa 24 wamepatikana na mambukizi ya virusi vya #corona baada ya Wafungwa 89 kuonesha dalili kama za mafua na kupimwa

Aidha, Meya wa Los Angeles Eric Garcetti ameonya kuwa kwa namna maambukizi yanavyoongezeka California yenye maambukizi 4,044 inaelekea kuwa New York huku New York yenye maambukizi 38,977 inaenda kuwa kama Italia

MACHI 26, 2020
CORONAVIRUS: MWANADIPLOMASIA WA UINGEREZA AFARIKI. MAREKANI YAIDHINISHA USD TRILIONI 2

Mwanadiplomasia wa Juu wa Uingereza, Steven Dick (37) aliyekuwepo nchini Hungary amefariki Jumanne Machi 24, baada ya kupata maambukizi ya #Covid_19

Hungary ina jumla ya maambukizi 261, Vifo 10 na waliopona 28 huku Uingereza ikiwa na jumla ya maambukizi 9,529, vifo 465 na waliopona 135

Baraza la Seneti la Marekani limeidhinisha Dola za Kimarekani Trilioni 2 kwa ajili ya kusaidia mifumo ya afya, wafanyakazi na biashara zilizoathiriwa na mlipuko wa #corona

Marekani ina jumla ya maambukizi 68,489, vifo 1,032 na waliopona ni 394. Nchi hiyo ina idadi ya Watu milioni 329 na Watu 418,810 wamepimwa hiyo inamaanisha mtu mmoja kati ya 785 ameathirika

Serikali ya Urusi imeiagiza Mamlaka ya Anga nchi humo kusitisha safari zote za Kimataifa za ndege zinazoingia na kutoka nchini humo kuanzia Kesho Machi 27

Thailand imetangaza maambuki maambukizi mapya 111 na kufanya nchi hiyo kuwa na maambukizi 1,045 huku ukizuia wale wote wasio raia, Wanadiplomasia au wenye vibali vya kutofanya kazi nchini huko kutoingia

MACHI 25, 2020
CORONAVIRUS: UINGEREZA YAWATAKA WATU KUKAA NDANI. MIKUSANYIKO ZAIDI YA WAWILI MARUFUKU

Watu wanaweza kwenda kufanya mazoezi nje ya nyumba mara moja kwa siku, kusafiri kwenda na kurudi ofisini panapo ulazima, kwenda dukani kwa mahitaji muhimu na kwenda hospitali

Maduka yanayouza bidhaa zisizo za muhimu yametakiwa kufungwa na mikusanyiko ya watu zaidi ya wawili katika maeneo ya wazi imezuiwa. Watu wa familia moja ndio wameruhusiwa kukaa pamoja ndani

Iwapo watu hawatafuata maagizo hayo, Polisi wana mamlaka ya kushinikiza yafuatwe ikijumuisha kutawanya mikusanyiko na kuwatoza faini watu hao

Waziri Mkuu Boris Johnson amesema nchi hiyo kwa sasa inakabiliwa na hali ya dharura na hivyo watu kukaa nyumbani ni suala la muhimu. Hali hiyo itaendelea kwa wiki tatu chini ya uangalizi

Kwa sasa Uingereza ina jumla ya maambukizi 8,077 na jumla ya vifo ni 422 huku kukiwa na Wagonjwa 135 waliopona

ITALIA YATANGAZA VIFO 743 NDANI YA SAA 24. WHO YAITAHADHARISHA MAREKANI

Hali imeendelea kuwa mbaya nchini Italia baada ya nchi hiyo kutangaza vifo vya watu 743 ndani saa 24 zilizopita na kufanya nchi hiyo kuwa na jumla ya 6,820 vya Wagonjwa wa #covid_19

Hata hivyo, siku mbaya zaidi kwa nchi hiyo ambayo imetangaza kuwa na Maambukizi 69,176 kwa Jumanne kutoka 63,919 kwa Jumatatu, ilikuwa ni Jumamosi ilipotangaza vifo 793

Aidha, Shirika la Afya Duniani (WHO), limeitahadharisha Marekani yenye Maambukizi mengi baada ya China na Italia kuwa inaweza kuwa kitovu kipya cha Maambukizi huku Trump akisisitiza kuwa watarudi kazini baada ya wiki 3

Hadi sasa Marekani ina jumla ya maambukizi 54,867 katika Majimbo yake yote 50 huku kukiwa na jumla ya vifo 782. China ina maambukizi 81,218 na vifo 3,281
 
MORE UPDATES:

3DE4B2AA-54B1-48AC-AE03-8EC8B162B0E5.jpeg

APRILI 30, 2020
Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaonesha #COVID19 imeathiri takriban watu milioni 3.3 huku zaidi ya Wagonjwa 229,000 wakifariki dunia na wengine zaidi ya 923,000 wakipona

Marekani ndilo Taifa lililoathirika zaidi Ulimwenguni likiwa na jumla ya visa 1,159,028, vifo 62,631 huku wagonjwa waliopona wakiwa ni zaidi ya 91,447

Jumla ya visa hivyo inajumuisha katika Majimbo yote 50, na maeneo yote yaliyochini ya nchi hiyo pamoja na Wagonjwa waliorudi nchini baada ya kugundulika katika nchi nyingine, walio Magerezani na Jeshini

Jana, Aprili 29, 2020 Marekani imerekodi visa vipya 27,327 na vifo 2,611 ndani ya saa 24. Hata hivyo, namba hii inaweza kuongezeka sana kwa siku zijazo kutokana na kwamba nchi hiyo inaanza kuhesabu vifo vinavyodhaniwani vya #COVID19

Vifo vinavyodhaniwa ni vya #COVID19 ni vilivinavyotokea ambapo watu waliofariki wanahusishwa na #COVID19 na Madaktari kujiridhisha hivyo lakini bila mgonjwa kupimwa maabara
-
Idadi hiyo ya vifo inayoelezwa kupita idadi ya vifo vya Wanajeshi wa Marekani walikufa katika vita ya Vietnam (47,434), imepita makadirio ya vifo yaliyowekwa ambapo ikadiriwa vifo 60,000 vingevika Agosti 2020

APRILI 27, 2020
#CORONAVIRUS-UPDATES: Zaidi ya Wagonjwa 55,000 wamefariki nchini Marekani, ikiwa ni zaidi ya robo ya vifo vyote vilivyotokea Duniani

Huko Uingereza, Waziri Mkuu Boris Johnson anatarajiwa kurudi kazini leo baada ya kupona #COVID19. Aliruhusiwa kutoka hospitali Jumatatu ya Pasaka, Aprili 13, 2020

Aidha, nchini Uswizi baadhi ya Biashara zitaruhusiwa kufunguliwa leo, huu Italia ikipanga kulegeza baadhi ya masharti ya kupambana na CoronaVirus kuanzia Mei 4, 2020

Maduka ya maua, maduka ya vipodozi, na saluni, pamoja na hospitali zilizokuwa zimefungwa zitaruhusiwa kufunguliwa nchini Uswizi kuanzia leo huku watu wakitakiwa kufuata kanuni za usafi na umbali baina ya watu

APRILI 26, 2020
CORONAVIRUS: WATU ZAIDI YA 203,000 WAFARIKI DUNIA

Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO), watu 203,921 duniani wamepoteza maisha kutokana na janga la COVID-19

Vilevile, takriban watu 2,955,469 ulimwenguni wana maambukizi ya Virusi vya COVID-19. Aidha, Wagonjwa 814,993 wamepona hadi kufikia sasa

Mataifa yaliyoathirika zaidi duniani ni Marekani, Uhispania, Italia, Ufaransa, Ujerumani na Uingereza

Kwa upande wa Afrika, nchi zenye idadi kubwa ya waathirika mpaka sasa ni Afrika Kusini, Misri, Algeria, Cameroon na Ghana

NB: Takwimu zote ni hadi kufikia saa 2:50 asubuhi leo

UJERUMANI: IDADI YA MAAMBUKIZI YAFIKIA 154,175

Kwa mujibu wa Taasisi ya Robert Koch (RKI), Ujerumani imerekodi maambukizi mapya 1,737 na jumla ya waathirika nchini humo imefikia 154,175

Aidha, vifo vipatavyo 140 vimerekodiwa na jumla ya waliofariki dunia kutokana na Corona Virus ni 5,640. Ujerumani imepongezwa kwa namna ilivyokabiliana na maambukizi ya COVID-19, hivi sasa idadi ya wagonjwa wanaopona ni kubwa kuliko ile ya wanaoambukizwa

Nchi hiyo ilianza kulegeza masharti Aprili 20 mwaka huu, japokuwa wataalamu wameonya kuwa maambukizi yanaweza kuongezeka kama watu hawatachukua tahadhari

APRILI 25, 2020
UINGEREZA: VIFO ZAIDI YA 20,000 VYAREKODIWA HOSPITALI

Vifo vipya 813 vilivyotokea Hospitali vimetangazwa na idadi ya Wagonjwa wa COVID19 waliofariki dunia katika Hospitali mbalimbali imefikia 20,319

Takwimu za vifo za Serikali hazihusishi vifo vilivyotokea nyumbani, nyumba za uangalizi au sehemu nyingine kwenye jamii.

Takwimu hizo hukusanywa tofauti na Ofisi ya Taifa ya Takwimu kulingana na Hati za vifo

Uingereza imerekodi maambukizi 148,377 hadi kufikia leo

APRILI 24, 2020
UHISPANIA: VIFO VICHACHE ZAIDI VYAREKODIWA NDANI YA KIPINDI CHA MWEZI MMOJA

Wizara ya Afya imetangaza vifo 367 ndani ya saa 24 zilizopita, idadi ambayo ni ndogo zaidi kutokea kwa kipindi cha takriban mwezi mmoja. Uhispania imerekodi maambukizi 219,764 na vifo 22,524 hadi kufikia sasa

Waziri ya Afya, Salvador Illa amesema nchi hiyo ambayo imeongeza muda wa hali ya dharura mpaka Mei 09 mwaka huu itaendelea kuchukua tahadhari za kujikinga licha ya kuwepo na ongezeko dogo la maambukizi mapya ya Corona Virus

Aidha, kutokana na mwenendo wa mlipuko wa COVID-19 nchini humo, kuanzia Jumapili hii, watoto wataruhusiwa kutoka nje kwa muda wa saa 1 wakiwa chini ya uangalizi wa mzazi

BANGLADESH: MADAKTARI ZAIDI YA 200 WAAMBUKIZWA COVID19

Takriban madaktari 251 nchini Bangladesh wamepata maambukizi ya Corona Virus. Taasisi ya Madaktari (BDF) imelalamikia ukosefu wa vifaa kinga (PPE) kuwa chanzo cha Madaktari kupata maambukizi kutoka kwa wagonjwa

Kufuatia ongezeko la waathirika wa Corona nchini humo, Serikali imekuwa na changamoto ya kuwalinda watumishi wa afya ili wasipate maambukizi ya Virusi hivyo

Bangladesh, kama ilivyo kwa mataifa mengine duniani inakabiliwa na uhaba mkubwa wa vifaa kinga kwa ajili ya watoa huduma za afya. Nchi hiyo imerekodi maambukizi 4,186 na vifo 127 hadi sasa huku waliopona wakiwa 108

APRILI 23, 2020
MSALABA MWEKUNDU WASHAURI KUWEPO MIKAKATI YA KUSHUGHULIKIA MIILI YA WANAOFARIKI DUNIA

Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu (ICRC) imetoa wito kwa Serikali duniani kote kujiandaa na kuweka mikakati kwa ajili ya idadi kubwa ya watu wanaofariki dunia kutokana na ugonjwa wa COVID19

Imesema idadi kubwa ya vifo vinaweza kuzidi uwezo wa Mamlaka kushughulikia miili kwa ufasaha. Kamati hiyo imeeleza kuwa kukosa mikakati kunaweza kupelekea watu kuzikwa kwa pamoja, bila kuwa na rekodi ya nani amezikwa wapi

Pia imesema kuweka mipango haimaanishi watu wengi watafariki lakini ni muhimu iwepo ili kusaidia kupunguza majonzi kwa familia zilizopoteza wapendwa wao

Vilevile, imeshauri Mamlaka kuwapa kipaumbele wanaoshughulika na miili hiyo kwa kuhakikisha wana vifaa kinga muhimu ili kulinda afya zao

APRILI 21, 2020
WHO YAONYA MATAIFA KUHARAKISHA KULEGEZA MASHARTI

Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema kuondoa masharti ya wananchi kutotoka nje ili kudhibiti COVID19 ni mchakato unaotakiwa kufanywa taratibu kwani kuharakisha kufanya hivyo kunaweza kuleta maambukizi upya

Mkurugenzi wa WHO Pasifiki ya Magharibi, Takeshi Kasai amesema masharti yameonekana kufanya kazi, na watu wanatakiwa kuwa tayari kwa mfumo huo mpya wa maisha wakati huu ambapo dunia inakabiliana na janga la Coronavirus hadi pale chanjo an tiba itakapopatikana

Serikali zimetakiwa kuweka jitihada zaidi katika kudhibiti maambukizi, na WHO imeshauri masharti na tahadhari kulegezwa kwa namna ambayo italeta usawa kati ya kulinda afya za watu na kuruhusu shughuli za kiuchumi kuendelea

UK: CHANJO YA CORONAVIRUS KUANZA KUJARIBIWA ALHAMISI

Wanasayansi kutoka Chuo cha Oxford ambapo chanjo ya ugonjwa wa COVID19 inatengenezwa wamesema kuna uwezekano chanjo hiyo ikafanikiwa kwa 80% lakini pia wamekiri inaweza kushindwa

Wamesema itaanza kujaribiwa rasmi kwa binadamu siku ya Alhamisi (Aprili 23, 2020) na majaribio hayo yatagharimu Paundi Milioni 20 (sawa na takribani TZS 56,952,036,140)

APRILI 20, 2020
UFARANSA: WAZIRI MKUU ASEMA HALI INABADILIKA, MAAMBUKIZI YAANZA KUPUNGUA

Waziri Mkuu wa Ufaransa, Edouard Philippe amesema mwenendo wa ugonjwa wa COVID19 nchini humo unabadilika taratibu. Amesema dalili mojawapo kuwa mlipuko huo unaanza kupungua ni kushuka kwa idadi ya wagonjwa Hospitali

Ufaransa ni nchi ya nne kwa vifo vingi zaidi duniani kutokana na Corona Virus ikiwa imerekodi vifo 19,718 na maambukizi 152,894 hadi kufikia leo

Aidha, nchi hiyo ambayo imezuia wananchi wake kutoka nje kwa takriban wiki 5 sasa inatarajiwa kulegeza baadhi ya masharti kuanzia Mei 11 ambapo huenda biashara chache zikafunguliwa na watu kuruhusiwa kutoka huku wakiendelea kuchukua tahadhari

Hata hivyo, Philippe amesisitiza kuwa maisha hayatokuwa kama awali na watakaokutwa na COVID-19 watatakiwa kukaa nyumbani au katika hoteli zilizo chini ya uangalizi wa Serikali

UHISPANIA: WATU ZAIDI YA 200,000 WAATHIRIKA NA CORONAVIRUS

Wizara ya Afya ya Uhispania imesema nchi hiyo ina jumla ya maambukizi 200,210 ya COVID19 baada ya visa vipya 4,266 kurekodiwa leo. Kutokana na takwimu hizo, Uhispania inakuwa nchi ya pili kuathirika zaidi duniani nyuma ya Marekani

Mbali na ongezeko la wagonjwa, nchi hiyo pia imeripoti vifo vipya 399 na idadi ya waliofariki dunia kutokana na mlipuko wa Coronavirus hadi kufikia sasa ni 20,852 huku waliopona wakiwa

Kwa upande wa Ulaya, Uhispania ina idadi kubwa zaidi ya waathirika wa Virusi vya Corona ikifuatiwa na Italia ambayo imerekodi maambukizi 181,228

APRILI 16, 2020
CALIFORNIA: WAUZAJI WA MAZIWA WAYATUPA KWA KUKOSA SOKO

Wauzaji wa maziwa katika Jimbo la California wanalazimika kutupa maziwa hayo baada ya soko kupungua kutokana na kufungwa kwa migahawa na shule

Mkurugenzi Mtendaji wa Western United Dairies, Anja Raudabaugh ambaye anawakilisha takriban Wafugaji 860 amesama baada ya agizo la kukaa ndani kutolewa, migahawa ilifungwa na asilimia 50 ya Wateja ilipotea kwa usiku mmoja

Amesema migahawa mikubwa kama TGI Friday’s na Applebee’s iliyokuwa ikichukua maziwa mengi na kuwa Wateja wakubwa kwa wafugaji, iliacha kununua maziwa tangu katikati ya mwezi Machi

Aidha, Wafugaji walipata pigo zaidi baada ya Shule kufungwa na vyakula vya mchana kutotolewa shuleni jambo linalowafanya kuwa na hifadhi kubwa ya maziwa kuliko mahitaji

APRILI 15, 2020
MAREKANI YAWEKA REKODI MPYA, WATU 2,228 WAFARIKI KWA SIKU 1

Marekani imerekodi idadi kubwa ya vifo 2,228 ndani ya saa 24 na kufikia vifo 28,368 hadi sasa kwa mujibu wa Chombo cha Habari cha Reuters. Idadi kubwa ya awali ilikuwa Ijumaa ambapo vifo 2,069 vilirekodiwa

Nchi hiyo ambayo ni ya tatu kwa idadi kubwa ya watu duniani imerekodi Waathirika 606,194 hadi kufikia mapema leo idadi ambayo ni kubwa kwa mara tatu kwa nchi inayoifuata kwa Waathirika wa #COVID19

Ongezeko la vifo 2,228 halijumuishi makusudio ya Jiji la New York kujumuisha idadi ya vifo vinavyodhaniwa vimetokana na #CoronaVirus bila kupimwa

Mamlaka za New York zimeripoti vifo 3,778 vinavyodhaniwa ni kwasababu ya corona ambapo madaktari walijiridhisha ni kutokana na ugonjwa huo, na vifo 6,589 vilivyothibitishwa maabara. Ukijumlisha idadi hiyo ya vifo inafika zaidi ya 10,000

KENYA: IDADI YA WAATHIRIKA YAFIKIA 225. VIFO VYAFIKIA 10

Idadi ya waliopata maambukizi ya #COVID19 imeongezeka na kufikia 225 baada ya wagonjwa wapya 9 kuthibitika na virusi hivyo kufuatia kupimwa kwa sampuli 803 ndani ya saa 24

Waziri wa Afya, Mutahi Kagwe amesema wagonjwa wote wapya ni raia wa Kenya na hawana rekodi ya kusafiri nje ya nchi hiyo kwa hivi karibuni. Ni miongoni mwa watu waliokuwa wakifuatiliwa

Ameeleza kuwa kati ya wagonjwa hao wapya, watano wanatokea Nairobi na wanne wanatokea Mombasa na umri wao ni katika ya miaka 9 na miaka 69

Aidha, watu 12 wamepona ugonjwa huo na kuruhusiwa kutoka hospitalini; Idadi ya waliopona imefikia 53. Mtu mmoja amefariki kwa ugonjwa huo

Waziri amebainisha kuwa jumla ya watu 2,336 waliokutana na waathirika wamekuwa wakifuatiliwa, huku 1,911 wakiachiwa na wengine 455 wakiwa bado wanafuatiliwa

APRILI 14, 2020
KUNDI LA WACHUNGAJI LAMSHTAKI GAVANA WA CALIFORNIA KWA KUZUIA MIKUSANYIKO YA KIDINI

Kundi la Wachungaji kutoka Kusini mwa Jimbo la California limemshtaki Gavana Gavin Newsom na baadhi ya Watendaji kwa kuzuia Waumini kwenda Kanisani kutokana na #CoronaVirus

Mashtaka hayo yamefunguliwa jana katika Mahakama ya huko California na Kampuni ya Kisheria ya Dhillon, kwa niaba ya Walalamikaji wanne na watatu kati yao ni Wachungaji

Walalamikaji ni Dean Moffatt, Mchungaji katika Kanisa la Indio anayedaiwa kupigwa faini ya $1,000 kwa kuongoza Ibaya ya Jumapili ya Matawi; Brenda Wood, Mchngaji wa Kanisa la Riverside; Patrick Scales, Mchungaji wa Kanisa la Fontana na Wendy Gish Muumini wa kanisa la Fontana

Walalamikaji hao pia wanamshtaki Mwanasheria Mkuu wa Jimbo, Xavier Becerra na baadhi ya Watendaji wa Kaunti za Riverside na San Bernardino wakiwemo Polisi na Wafanyakazi wa sekta ya Afya

Machi 19, Newsom alitoa agizo la kwanza la kuwataka Wakazi takriban milioni 40 wa California kukaa nyumbani ili kupunguza kusambaa kwa virusi hiyo

APRILI 13, 2020
ASILIMIA 18 YA POLISI WA NEW YORK WAHOFIWA KUUNGUA #COVID19

Takriban Polisi 6,522 wa Idara ya Polisi ya New York hawakuweza kufika kazini siku ya jana kwa mujibu wa ripoti ya kila siku ya #CoronaVirus ya Idara hiyo

Ripoti hiyo imeeleza kuwa hadi sasa Polisi 2,344 na Wafanyakazi wasio Polisi 489 wa Idara hiyo ndio wamethibitika kuwa na ugonjwa wa #COVID19

Ongezeko la Wagonjwa 5,695 kwa siku ya jana kumefanya New York kuwa na zaidi ya Waathirika 104,000 na takriban vifo 6,182 vilivyorekodiwa

Kwa ujumla Marekani ndio nchi iliyoathirika zaidi duniani na virusi hivi ikiwa na jumla ya Waathirika 560,433 huku ikiwa imesharipoti vifo 22,115

APRILI 12, 2020
MAREKANI YAIZIDI ITALIA KWA VIFO

Marekani imeipita Italia kwa vifo ikiwa imerekodi vifo 20,602 na ikiwa na Waathirika takriban 529,740 kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Chuo Kikuu cha Johns Hopkins

Waathirika hao wapo katika Majimbo yote 50 ikiwemo ‘District of Columbia’ hadi sasa Jimbo pekee ambalo halijatangaza kifo cha mgonjwa wa #COVID19 ni Wyoming pekee

Takriban nusu ya vifo hivyo vimetokea New York ambapo Gavana wa sehemu hiyo, Andrew Cuomo amesema Jana kuwa Ijumaa kulitokea vifo 783 na kufanya Jimbo hilo kuwa na vifo 8,627

Aidha, kwa mujibu wa takwimu, Marekani ilikuwa na vifo 58 wiki nne zilizopita, na katika wiki 3 zilizopita ilikuwa na vifo 323. Katika wiki mbili zilizopita vifo vilifika 2,043 na wiki moja iliyopita kulikuwa na vifo 8,488

Jana, Aprili 10, 2020 Italia ilitangaza jumla ya vifo 619 vipya vinavyohusiana na #COVID_19 na kufanya Taifa hilo la Ulaya kuwa na jumla ya vifo 19,468

KENYA: MAAFISA 6 WA AFYA WAPATA MAAMBUKIZI YA #COVID19 WAKIWA KAZINI

Kwa mujibu wa Umoja wa Maafisa Kliniki wa Kenya (Kenya Union of Clinical Officers), maafisa afya wapatao 6 wamepata maambukizi ya #COVID19 wakiwa kazini

Utafiti uliofanywa hivi karibuni nchini humo umebaini 68% ya wafanyakazi wa sekta ya afya ya jamii hawana mafunzo maalum ya kukabiliana na wagonjwa wa #CoronaVirus

Katibu wa Umoja huo amesema upungufu wa barakoa na glovu ni miongoni mwa vyanzo vikubwa vilivyochangia maafisa hao sita kupata maambukizi

APRILI 11, 2020
ITALIA: TAKRIBAN MAPADRI 100 WAFARIKI DUNIA KWA CORONA VIRUS

Mapadri hao wamefariki dunia baada ya kupata maambukizi ya COVID-19. Imeelezwa kuwa asilimia kubwa ya Viongozi hao wa Dini walikuwa wastaafu

Mapadri wamekuwa wakiweka maisha yao hatarini kwa kutoa huduma za kiroho kwa wazee na Waumini walioathirika zaidi na Ugonjwa huo katika maeneo mbalimbali

Nchi ya Italia ni miongoni mwa mataifa yaliyoathirika zaidi na mlipuko wa Coronavirus ikiwa na maambukizi 147,577 na vifo 18,849 hadi kufikia jioni ya leo

MAREKANI: CORONA VIRUS YAGHARIMU MAISHA YA WATU 2000 NDANI YA SIKU MOJA

Watu 2,018 wamefariki dunia kutokana COVID-19 ndani ya siku moja, idadi hiyo ya vifo ni kubwa zaidi kurekodiwa duniani

Huenda nchi ya Marekani yenye waathirika 503,177 na vifo 18,761 hadi sasa ikaipiku Italia ambayo imerekodi vifo 18,849 kufikia leo kwa kuwa na vifo vingi zaidi

Licha ya ongezeko hilo la vifo, Wataalamu wa Kikosi Kazi cha COVID-19 kutoka Ikulu wanasisitiza kuwa makali ya mlipuko huo yameanza kupungua

Rais Donald Trump naye amesema anatarajia kuona vifo vichache zaidi vikirekodiwa tofauti na makadirio yaliyotolewa awali

KOREA KUSINI: WAGONJWA 91 WALIOPONA COVID-19 WAPATA MAAMBUKIZI

Mamlaka za Korea Kusini zimeripoti kuwa takriban watu 91 waliopona Corona Virus wamepata maambukizi kwa mara ya pili

Mkurugenzi wa Kituo cha Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa nchini humo, Jeong Eun-kyeong amesema kuna uwezekano mkubwa virusi hivyo vilikuwa vimelala (dormant) na sio kwamba watu hao wameambukizwa upya

Aidha, Wataalamu wanasema huenda vipimo walivyofanyiwa watu hao vilionesha majibu ya uongo au baadhi ya virusi vilibaki mwilini ila havikuwa na madhara

Hata hivyo, Wataalamu wa Afya wa Korea Kusini bado hawajafahamu kinachosababisha hali hiyo na undani wa jambo hilo unaendelea kuchunguzwa

Hali ya wagonjwa wa Corona kupata maambukizi baada ya kupona ni suala ambalo linahofiwa kimataifa kwakuwa nchi nyingi zinatamani walioathirika watakuwa na kinga ya mwili ya kutosha itakayowazuia kuambukizwa tena

ITALIA KUBAKI KARANTINI HADI MWEZI MEI

Waziri Mkuu wa Italia, Giuseppe Conte ametangaza kuwa muda wa wananchi kutotoka nje umeongezwa hadi Mei 3 ili kudhibiti maambukizi mapya ya COVID-19

Italia ambayo imerekodi maambukizi 147,577 na vifo 18,849 hadi kufikia leo tayari imekuwa chini ya amri hiyo kwa mwezi mmoja ma wananchi wametakiwa kubaki nyumbani

Akitangaza uamuzi huo, Conte amesema wakiacha kuchukua tahadhari zaidi, watahatarisha maendeleo waliyopata mpaka sasa na kusababisha vifo zaidi

APRILI 10, 2020
UINGEREZA: BORIS JOHNSON ATOLEWA ICU

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson ametolewa katika Chumba cha Uangalizi Maalum (ICU) na kuhamishiwa wodini huku bado akiendelea kuwa chini ya uangalizi maalum

Taarifa iliyotolewa na Ofisi yake imeeleza kuwa Johnson ambaye alilazwa baada ya hali yake kubadilika ghafla anaendelea vizuri hivi sasa.

Wanasayansi wametahadharisha kuwa Uingereza inaingia katika hatua mbaya zaidi ya mlipuko wa #Covid19 na wanatarajia vifo vingi zaidi kurekodiwa kuelekea sikukuu ya Pasaka

Jumla ya maambukizi 65,077 na vifo 7,978 vimerekodiwa hadi kufikia leo

APRILI 09, 2020
UHISPANIA KULEGEZA MASHARTI, WAZIRI MKUU ASEMA KIPINDI KIGUMU KINAPITA

Waziri Mkuu wa Uhispania, Pedro Sanchez amesema nchi hiyo inatarajia kulegeza masharti ya karantini yaliyowekwa ili kudhibiti maambukizi na Virusi vya Corona

Sanchez ambaye pia ameombe Bunge kupitisha ombi lake la kuongeza muda wa hali ya tahadhari mpaka Aprili 26 amesema kutokana na athari zilizosababishwa na janga la Covid-19, mchakato wa maisha kurejea kama zamani utachukua wa taratibu

Uhispania ni nchi ya pili iliyoathirika zaidi na janga la Corona Virus baada ya Marekani. Maambukizi 152,446 na vifo 15,238 vimerekodiwa huku wagonjwa 52,165 wakipona hadi kufikia leo

Mbali na Uhispania, mataifa mengine ya Ulaya nayo yanakifikiria kulegeza masharti mapema iwezekanavyo kutokana na wasiwasi wa uchumi kuathirika kwasababu ya kuwekwa kwa amri ya karantini

APRILI 08, 2020
UINGEREZA: WAZIRI MKUU BORIS JOHNSON APATA NAFUU

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson (55) aliyewekwa Chumba cha Uangalizi Maalum (ICU) katika Hospitali ya Mtakatifu Thomas jijini London baada ya afya yake kubadilika ghafla anaendelea vizuri baada ya kupatiwa Oxygen

Johnson aliyegundulika kuwa na maambukizi ya #Covid19 wiki mbili zilizopita alifikishwa Hospitali Jumapili. Alihamishiwa ICU baada ya hali yake ilizidi kuwa mbaya zaidi. Taarifa iliyotolewa na Ofisi yake imesema anaendelea vizuri na hajawekewa mashine za kupumulia

Kwa muda ambao Johnson amelazwa Waziri wa Mambo ya Nje, Dominic Raad ataongoza harakati za kudhibiti maambukizi ya Corona na amepewa baadhi ya mamlaka ya Waziri huyo. Hata hivyo, maamuzi yote makubwa ikiwemo kusitisha karantini yatapitishwa na Baraza

Endapo Raad atashindwa kazi hiyo, Waziri wa Fedha Rishi Sunak (39) atapewa mamlaka

MAREKANI: WATU 1,736 WAFARIKI DUNIA NDANI YA SAA 24

Marekani imeripoti vifo 1,736 vilivyotokea Jumanne, idadi kubwa zaidi kurekodiwa ndani ya siku moja, ambapo asilimia kubwa ya vifo hivyo vimetokea Jijini New York

Jumla ya waliofariki kutokana na Virusi vya Corona imefikia 12,854. Maambukizi yaliyorekodiwa nchini humo mpaka sasa ni 400,412, idadi ambayo ni kubwa zaidi duniani

Rais wa Marekani Donald Trump ametishia kusitisha kutoa fedha kwa Shirika la Afya Duniani (WHO) huku akilishutumu Shirika hilo kwa kuipendelea China na kushindwa kudhibiti mlipuko huo ambao umegharimu maisha ya watu 82,080 duniani kote

Trump amesema WHO imefanya makosa na ilitakiwa kutangaza tahadhari mapema zaidi huku akidai kuwa walitakiwa kufahamu athari za mlipuko wa #Covid19 mapema zaidi, hivyo Marekani itafanya tathmini juu ya fedha ambazo inatoa kwa Shirika hilo

APRILI 07, 2020
MADAKTARI 94 NA WAUGUZI 26 WAFARIKI DUNIA

Taarifa hiyo imetolewa leo Aprili 07, 2020 na Umoja wa Madaktari nchini humo huku Shirikisho la Wauguzi likisema licha ya Wauguzi 26 kufariki wengine 6,549 wanaugua #COVID19

Kwa mujibu wa Taasisi ya Afya nchini humo, hadi kufikia jana Aprili 06, 2020 jumla ya Wafanyakazi 12,681 wa sekta ya Afya walikuwa wanaugua ugonjwa huo

Inaelezwa kuwa ukosefu wa vifaa vya kujikinga na virusi vya corona umesababisha idadi ya wafanyakazi wanaougua ugonjwa huo kuongezeka

Mojawapo ya miundombinu bora ya afya barani Ulaya ipo Kaskazini mwa Italia lakini imeshidhwa kukidhi kuhimili wingi wa wagonjwa wa #COVID_19 wanaogundulika nchini humo

Italia imeripoti jumla ya waathirika 132,547, idadi ya vifo 16,523 na waliopona hadi sasa ni 22,837

MAREKANI: WATU ZAIDI YA 10,000 WAFARIKI DUNIA

Idadi ya vifo ambayo imerekodiwa Marekani hadi asubuhi ya leo ni 10,876. Nchi hiyo inakuwa ya tatu kwa vifo vingi zaidi duniani baada ya Uhispania (13,341) na Italia (16,523)

Wataalamu wa Afya kutoka Ikulu ya Marekani wametabiri kuwa watu 100,000 hadi 240,000 wanaweza kupoteza maisha kutokana na ugonjwa wa COVID-19 hata kama maagizo ya kukaa nyumbani yakifuatwa

Marekani imesema hali inaweza kuwa mbaya wiki hii, ambapo maambukizi na vifo vingi vitarekodiwa. Miji ya New York, New Jersey, Connecticut na Detroit inatajwa kuwa katika hatari zaidi

Hadi sasa, takriban asilimia 90 ya Wamarekani wanatekeleza agizo la kukaa nyumbani na kuepuka mikusanyiko huku majimbo nane yakiwa bado hayajatoa tamko hilo

NEW ZEALAND: WAZIRI WA AFYA ASHUSHWA CHEO BAADA YA KUIPELEKA FAMILIA BAHARINI WAKATI WA KARANTINI

Waziri Mkuu wa New Zealand, Jacinda Ardern amemshusha cheo Waziri wa Afya David Clarke kwa kukiuka taratibu zilizowekwa kudhibiti maambukizi ya #Coronavirus nchini humo na kuipeleka familia yake baharini

Waziri Ardern amesema katika mazingira ya kawaida angemfukuza kabisa kazi Clarke kwasababu kitendo alichofanya sio sawa na alitarajia atakuwa mfano kwa wengine

Clarke ametolewa katika nafasi yake ya Waziri wa Afya na sasa atakuwa katika nafasi za chini za Baraza. Katika taarifa yake, amesema hakutumia busara na anaelewa kwanini watu wamekasirishwa

New Zealand yenye watu Milioni 5 ilitangaza karantini ya nchi nzima mwishoni mwa mwezi uliopita na kufunga mipaka yake, shule, migahawa pamoja na sehemu nyingine zenye mikusanyiko ya watu

Idadi ya maambukizi iliyoripotiwa nchini humo ni 1,160 na mpaka sasa kifo kimoja kimerekodiwa

APRILI 06, 2020
UHISPANIA: IDADI YA VIFO YAPUNGUA KWA SIKU NNE MFULULIZO

Idadi ya vifo vilivyorekodiwa kutokana na maambukizi ya #Covid19 imeendelea kupungua kwa siku ya nne sasa, hali ambayo inaleta matumaini kuwa Uhispania imemaliza kipindi kigumu

Uhispania yenye jumla ya waathirika 135,032 ina idadi kubwa zaidi ya maambukizi Ulaya. Vifo 637 vimeripotiwa leo na idadi ya jumla waliofariki dunia hadi sasa ni 13,055

Mbali na Uhispania, vifo nchini Italia, Ufaransa na Ujerumani pia vimeendelea kupungua. Hii inaashiria kuwa mkakati wa watu kuwekwa karantini na kuzuia mikusanyiko umesaidia kupunguza maambukizi

Maambukizi 1,287,168 ya Virusi vya Corona yameripotiwa duniani. Watu 70,530 wamepoteza maisha kutokana na Virusi hivyo na waliopona hadi leo ni 271,887

APRILI 05, 2020
MAREKANI: WATU 1,344 WAFARIKI NDANI YA SAA 24. HALI MBAYA ZAIDI YAHOFIWA

Marekani imetangaza idadi kubwa ya vifo vilivyotokana na #COVID19 kwa siku moja huku Wataalam wakitahadharisha kuwa wiki mbili zijazo zitakuwa mtihani mkubwa katika kupambana na maambukizi nchini humo

Nchi hiyo imetangaza jumla ya vifo 1,344 vilivyorekodiwa kutokea jana Aprili 04, ikiwa ndio idadi kubwa ya vifo kutokea ndani ya saa 24 kwa Taifa moja tangu kulipuka kwa Ugonjwa huo

Idadi hiyo inapelekea Marekani kuwa na jumla ya vifo 8,496 huku kukiwa na jumla ya Waathirika 312,076, idadi kubwa ya Waathirika kuliko Taifa lolote

Mratibu wa Timu ya kukabiliana na CoronaVirus ya Ikulu ya Marekani, Dkt. Deborah Birx ametahadharisha kuwa siku chache zijazo Marekani itashuhudia mtihani wake mkubwa na zitakuwa siku muhimu sana katika mapambano hayo

Amesema “Hizi ni siku za kutokwenda dukani, kutokwenda duka la dawa, na fanya lolote uwezalo unalodhani litaiweka familia yako na marafiki zako salama na hii ni kila mtu kuhahikisha anakaa umbali wa Mita 2 kutoka kwa mwenzako na unanawa mikono”

Aidha, Rais Donald Trump ameaambia Wamarekani kujiaandaa na ongezeko kubwa la vifo vitokanavyo na #Corona katika kile alichokiita wiki mbili ngumu zijazo katika mapambano na mlipuko huo

UHISPANIA: WATU 674 WAFARIKI KWA SIKU 1. IDADI NDOGO KUTOKEA TANGU MAPEMA MACHI

Watu wengine 674 wamefariki kwa #COVID19 nchini humo kwa siku ya jana Aprili 04, ikiwa ni idadi ndogo zaidi kutokea ndani ya saa 24 tangu mwezi Machi 2020

Nchi hiyo kwa sasa ina jumla ya vifo 12,418 vilivyorekodiwa ikiwa ni nchi ya pili kwa vifo vingi baada ya Italia iliyorekodi jumla ya vifo 15,362

Pamoja na kuwa ya pili kwa vifo, takwimu zinaonesha Taifa hilo linaelekea kumaliza kipindi kigumu zaidi cha mlipuko wa ugonjwa huo ambapo sasa idadi ya vifo na Waathirika wapya inayorekodiwa inapungua

Wizara ya Afya imesema leo kuna jumla ya Wagonjwa 80,261 wa #COVID19, ikiwa idadi hiyo imeongezeka kwa Wagonjwa 1,488 kutoka Jumamosi lakini pia ndio ongezeko dogo kwa siku tangu Machi 17

Ila pia Wizara hiyo imeripoti kuwa jumla ya Wagonjwa 38,080 wamepona ugonjwa huo ikiwa ni ongezeko la Wagonjwa 4,000 kutoka idadi iliyoripotiwa jana Aprili 04, 2020

APRILI 03, 2020
#CORONAVIRUS-UPDATE:
Idadi ya Watu walioathirika na maambukizi ya virusi vya #COVID19 imezidi milioni moja Ulimwenguni kwa mujibu wa Chuo Kikuu Cha Johns Hopkins

Nchi tano zenye Waathirika wengi waliorekodiwa ni Marekani (245,184), Italia (115,242), Uhispania (112,065), Ujerumani (84,794) na China (81,620)

Lakini pia nchi tano zenye idadi kubwa ya vifo vilivyoripotiwa ni Italia (13,915), Uhispania (10,348), Marekani (6,088), Ufaransa (5,387) na China (3,322)

UHISPANIA: WATU 932 WAFARIKI NDANI YA SAA 24

Kwa mujibu wa data zilizotolewa na Wizara ya Afya nchini humo leo Aprili 03, 2020, jumla ya Watu waliofariki dunia baada ya kuugua #COVID19 imefikia 10,935

Idadi hiyo imefikiwa baada ya vifo 932 vya Wagonjwa wa #Corona kurekodiwa katika saa 24 zilizopita. Jana, Wizara hiyo ilitangaza vifo 950 vilivyotokea ndani ya saa 24

Aidha, data za Wizara hiyo zinaonesha kuwa kuna Wagonjwa 76,262 kwa sasa nchini humo, ikiwa ni ongezeko la Wagonjwa 2,770 kutokea idadi ya jana lakini pia ni ongezeko dogo tangu Machi 20

Uhispania ni moja ya nchi iliyoathirika vibaya na mlipuko wa Ugonjwa huu, ikiwa ni ya pili kwa idadi ya vifo nyuma ya Italia yenye vifo 13,915. Inashika nafasi ya pili kwa Waathiriki ikiwa na Waathirika 117,710 nyuma ya Marekani (245,380)

APRILI 02, 2020
UHISPANIA: WATU 950 WAFARIKI NDANI YA SAA 24

Kwa mujibu wa data zilizotolewa na Wizara ya Afya nchini humo leo Aprili 02, 2020, jumla ya Watu waliofariki dunia baada ya kuugua #COVID19 imefikia 10,003

Idadi hiyo imefikiwa baada ya vifo 950 vya Wagonjwa wa #Corona kurekodiwa katika saa 24 zilizopita. Hii ni idadi kuwa ya vifo kwa siku moja kutokea nchini humo

Uhispania ni moja ya nchi iliyoathirika vibaya na mlipuko wa Ugonjwa huu, ikiwa ni ya pili kwa idadi ya vifo nyuma ya Italia yenye vifo 13,155. Pia, ikiwa na maambukizi 110,238 inazifuata nchi za Marekani (215,344) na Italia (110,574) kwa maambukizi mengi

BALOZI WA UFILIPINO NCHINI LEBANON AFARIKI KWA #COVID19

Bernardita Catalla aliyekuwa Mwanadiplomasia kwa miaka 27, amefariki katika hospitali iliyopo Beirut baada ya kuugua ugonjwa wa #Covid_19

Miezi kadhaa nyuma, Balozi huyo aliongoza mpango wa kuwaondoa takriban Wafilipono 2,000 nchini Lebanon, wengi wakiwa ni Wanawake waliokuwa wakifanya kazi za ndani

Tangu Oktoba 2019, Lebanon imekuwa na migogoro ya Kisiasa na Kifedha na Wakimbizi wengi wa Kiafrika na bara la Asia wanaofanya kazi nchini humo wanalalamika kulipwa kidogo au kucheleweshewa mishahara

APRILI 01, 2020
AFRIKA: WATU 203 WAFARIKI DUNIA KWA #COVID19

Kituo cha udhibiti na kuzuia magonjwa vya Umoja wa Afrika kimesema kuwa watu 203 wamepoteza maisha baada ya kuambukizwa virusi vya #Covid19

Hadi sasa #CoronaVirus imeenea katika nchi 50 barani Afrika na jumla ya maambukizi 5,886

Mpaka sasa hakuna taarifa zozote za maambukizi nchini Lesotho, Sudani Kusini, visiwa Sao Tome na Principe, Comoro na Malawi

Afrika Kusini ina idadi kubwa ya maambukizi, ikiwa imefikia 1,353, huku watu saba wakiwa wamethibitishwa kufariki kwa #Covid19

KENYA: WAGONJWA WAPYA 22 WATHIBITISHWA. MAAMBUKIZI YAFIKIA 81

Waziri wa Afya, Mutahi Kagwe amethibitisha kuwa watu 22 wamekutwa na #CoronaVirus leo ambapo idadi hii inafanya jumla ya maambukizi kufikia 81

Kati ya wagonjwa hao 22, 18 ni raia wa Kenya, 2 raia wa Pakistan na 2 ni raia wa Cameroon. Aidha 13 kati yao ni wanaume na 9 ni wanawake

Waziri amesema wagonjwa hao wapya wamepatikana baada ya Watu 300 kupimwa na kuwa kati ya hao 22, 21 walikuwa Karantini tayari

MACHI 30, 2020
ITALIA: WATU 756 WAFARIKI NDANI YA SAA 24. IDADI YA VIFO ILIYOREKODIWA YAFIKIA 10,779

Idadi ya vifo kwa Italia ni kubwa zaidi ikilinganishwa na nchi yoyote nyingine na vifo hivyo vinachukua theluthi moja ya jumla ya vifo vyote vya #Covid19 duniani ambavyo ni 33,982

Licha ya kutokea kwa vifo 756 Jumapili, idadi ya vifo nchini humo imeonekana kupungua ambapo Jumamosi kulirekodiwa jumla ya vifo 889 na Ijumaa vifo 969 vilirekodiwa

Aidha, Idadi ya maambukizi kwa Jumapili yalifikia 97,689 kutoka 92,472 ikiwa ni kiwango kidogo cha maambukizi kuongezeka tangu Jumatano Machi 25, 2020

Kati ya wale walioambukizwa nchi nzima, 13,030 walikuwa wamepona kufikia Jumapili, ikilinganishwa na 12,384 waliokuwa wamepona Jumamosi. Watu 3,906 walikuwa ICU ikilinganishwa na 3,856 waliokuwepo siku iliyopita

MAREKANI: RAIS TRUMP AONGEZA MUDA WA WATU KUKAA NDANI

Rais Donald Trump amesema muda wa watu kujitenga kwa kukaa ndani na kutokusanyika umeongezwa hadi Aprili 30 baada ya Wataalamu kuonya kuwa vifo vinaweza kufika 100,000

Amesema, "Inakadiriwa kuwa vifo vingi vinaweza kutokea kwenye wiki mbili zijazo. Hivyo kwa wiki mbili hizo na katika kipindi hiki ni muhimu watu kufuata kanuni hizo"

Ameongeza, "Kama idadi ya vifo itabaki katika 100,000 au pungufu ya hapo (Marekani), wote tutakuwa tumefanya kazi kubwa. Hivyo ni bora kila moja kufuata Kanuni hizo ili janga hili liishe mapema."

Aidha, katika hatua nyingine Trump amesema Usalama wa Taifa walimzuia kwenda New York (Mji unaoongoza kwa maambukizi Marekani) kuhudhuria ufunguzi wa hospitali ya wagonjwa wa #COVID19

Hospitali hiyo ya muda katika Kituo cha Javits inatarajiwa kuwa na vitanda takriban 2,900 ii kukabiliana na wimbi la Wagonjwa wa #COVID_19 wanaoongezeka kwa kasi

UHISPANIA: WATU 812 WAFARIKI NDANI YA SAA 24. YAIZIDI CHINA KWA IDADI YA MAAMBUKIZI

Mamlaka zimeripoti kuwa pamoja na vifo hivyo kumekuwa na jumla ya ongezeko la wagonjwa 3,515 ndani ya saa 24 na kufanya idadi ya Wagonjwa waliorekodiwa kufikia 61,075

Jumla ya Idadi ya vifo vilivyoripotiwa nchini humo imefikia 7,340 kutoka vifo 6,528 vilivyoripotiwa Jumapili. Ni nchi ya pili kwa vifo vingi baada ya ya Italia yenye vifo 10,779

Nchi hiyo imeripoti jumla ya maambukizi 85,195 kutoka 78,797 yaliyokuwepo Jumapili na kufanya nchi hiyo kuwa na maambukizi mengi kuliko China yenye maambukizi 81,470

Aidha, wagonjwa 2,071 wamepona katika saa 24 zilizopita na kufanya idadi ya watu waliopona kuwa 16,780. Katika muda huo kulikuwa na jumla ya wagonjwa 324 waliokuwa wakihitaji uangalizi maalumu

ITALIA: MADAKTARI 61 WAFARIKI DUNIA BAADA YA KUPATA MAAMBUKIZI

Kwa mujibu wa Chama cha Madaktari nchini humo, Madaktari 61 wamefariki dunia huku Wafanyakazi wengine 8,358 wa sekta ya Afya wakiwa na maambukizi ya virusi hivyo

Kati ya Madaktari hao 61, 40 walikuwa wakifanya kazi katika Mji wa Lombary ambao ndio chimbuko la virusi hivyo Italia na ndiko kwenye maambukizi mengi

Nchi hiyo ikiwa imerekodi jumla ya maambukizi 97,689 ina karibia kuwa nchi ya pili kuwa na maambukizi mengi yaliyozidi 100,000 baada ya Marekani yenye maambukizi 144,410

Aidha, nchi hiyo ina jumla ya vifo 10,779 vilivyorekodiwa na vikiwa vinachukua takriban theluthi moja ya jumla ya vifo vyote vya #Covid19 duniani ambavyo ni 35,339

MACHI 29, 2020
CORONAVIRUS MAREKANI: MJI WA NEW YORK KUTOWEKWA KARANTINI

Rais Donald Trump amesema Mji wa New York wenye maambukizi mengi Marekani (53,455) hautawekwa karantini na kuagiza Kituo cha Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa (CDC) kutoa maelekezo kwa wasafiri

Uamuzi wake unakuja siku chache baada ya kutangaza kuwa anafikiria kuiweka Miji ya New York, New Jersey (maambukizi 11,124) na Connecticut (maambukizi 1,524) karantini ili kuzuia maambukizi ya #COVID_19

Awali, Gavana wa New York, Andrew Cuomo alipinga Mji huo kuwekwa karantini na kudai soko la hisa litaporomoka vibaya na itachukua miezi kama sio miaka kwa uchumi wa Marekani kurudi kama ulivyokuwa

Baada ya agizo hilo, CDC imewataka wananchi kutoka Miji hiyo mitatu kusitisha safari zote za ndani zisizo na umuhimu kwa muda wa siku 14. Agizo hilo halitawahusu watoa huduma za chakula, afya na fedha

ITALIA: WATU ZAIDI YA 10,000 WAFARIKI DUNIA KWA #CORONAVIRUS

Idadi ya waliopoteza maisha kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona nchini Italia imefikia 10,023 baada ya vifo 889 kuripotiwa Jumamosi

Mbali na vifo hivyo, maambukizi mapya 5,974 pia yameripotiwa ndani ya saa 24 zilizopita na nchi hiyo ina jumla ya maambukizi 92.472 mpaka sasa

Italia ina wagonjwa 70.065 na kati yao 66,209 wana hali nzuri huku wengine 3,856 wakiwa na hali mbaya. Wagonjwa waliopona #COVID_19 ni 12.384

Nchi hiyo itashusha bendera nusu mlingoti katika miji mbalimbali Machi 31 mwaka huu, ili kuwaenzi waliofariki dunia kutokana na ugonjwa huo

MACHI 27, 2020
CORONAVIRUS: MAREKANI YAIZIDI CHINA KWA IDADI YA MAAMBUKIZI

Marekani imeripoti jumla ya maambukizi 85,594 na kuwa nchi yenye maambukizi mengi zaidi ikiizidi China yenye maambukizi 81,340 na Italia yenye maambukizi 80,589

Hata hivyo italia bado inaongoza kwa vifo vilivyotokana na #Covid_19, ikiwa imetangaza vifo 8,215 ikifuatiwa na Uhispania yenye vifo 4,365 huku Marekani ikiwa na vifo 1,300 na China kuna vifo 3,292

Huko Chicago katika Gereza la Cook County lenye Wafungwa 5,400, Wafungwa 24 wamepatikana na mambukizi ya virusi vya #corona baada ya Wafungwa 89 kuonesha dalili kama za mafua na kupimwa

Aidha, Meya wa Los Angeles Eric Garcetti ameonya kuwa kwa namna maambukizi yanavyoongezeka California yenye maambukizi 4,044 inaelekea kuwa New York huku New York yenye maambukizi 38,977 inaenda kuwa kama Italia

MACHI 26, 2020
CORONAVIRUS: MWANADIPLOMASIA WA UINGEREZA AFARIKI. MAREKANI YAIDHINISHA USD TRILIONI 2

Mwanadiplomasia wa Juu wa Uingereza, Steven Dick (37) aliyekuwepo nchini Hungary amefariki Jumanne Machi 24, baada ya kupata maambukizi ya #Covid_19

Hungary ina jumla ya maambukizi 261, Vifo 10 na waliopona 28 huku Uingereza ikiwa na jumla ya maambukizi 9,529, vifo 465 na waliopona 135

Baraza la Seneti la Marekani limeidhinisha Dola za Kimarekani Trilioni 2 kwa ajili ya kusaidia mifumo ya afya, wafanyakazi na biashara zilizoathiriwa na mlipuko wa #corona

Marekani ina jumla ya maambukizi 68,489, vifo 1,032 na waliopona ni 394. Nchi hiyo ina idadi ya Watu milioni 329 na Watu 418,810 wamepimwa hiyo inamaanisha mtu mmoja kati ya 785 ameathirika

Serikali ya Urusi imeiagiza Mamlaka ya Anga nchi humo kusitisha safari zote za Kimataifa za ndege zinazoingia na kutoka nchini humo kuanzia Kesho Machi 27

Thailand imetangaza maambuki maambukizi mapya 111 na kufanya nchi hiyo kuwa na maambukizi 1,045 huku ukizuia wale wote wasio raia, Wanadiplomasia au wenye vibali vya kutofanya kazi nchini huko kutoingia

MACHI 25, 2020
CORONAVIRUS: UINGEREZA YAWATAKA WATU KUKAA NDANI. MIKUSANYIKO ZAIDI YA WAWILI MARUFUKU

Watu wanaweza kwenda kufanya mazoezi nje ya nyumba mara moja kwa siku, kusafiri kwenda na kurudi ofisini panapo ulazima, kwenda dukani kwa mahitaji muhimu na kwenda hospitali

Maduka yanayouza bidhaa zisizo za muhimu yametakiwa kufungwa na mikusanyiko ya watu zaidi ya wawili katika maeneo ya wazi imezuiwa. Watu wa familia moja ndio wameruhusiwa kukaa pamoja ndani

Iwapo watu hawatafuata maagizo hayo, Polisi wana mamlaka ya kushinikiza yafuatwe ikijumuisha kutawanya mikusanyiko na kuwatoza faini watu hao

Waziri Mkuu Boris Johnson amesema nchi hiyo kwa sasa inakabiliwa na hali ya dharura na hivyo watu kukaa nyumbani ni suala la muhimu. Hali hiyo itaendelea kwa wiki tatu chini ya uangalizi

Kwa sasa Uingereza ina jumla ya maambukizi 8,077 na jumla ya vifo ni 422 huku kukiwa na Wagonjwa 135 waliopona

ITALIA YATANGAZA VIFO 743 NDANI YA SAA 24. WHO YAITAHADHARISHA MAREKANI

Hali imeendelea kuwa mbaya nchini Italia baada ya nchi hiyo kutangaza vifo vya watu 743 ndani saa 24 zilizopita na kufanya nchi hiyo kuwa na jumla ya 6,820 vya Wagonjwa wa #covid_19

Hata hivyo, siku mbaya zaidi kwa nchi hiyo ambayo imetangaza kuwa na Maambukizi 69,176 kwa Jumanne kutoka 63,919 kwa Jumatatu, ilikuwa ni Jumamosi ilipotangaza vifo 793

Aidha, Shirika la Afya Duniani (WHO), limeitahadharisha Marekani yenye Maambukizi mengi baada ya China na Italia kuwa inaweza kuwa kitovu kipya cha Maambukizi huku Trump akisisitiza kuwa watarudi kazini baada ya wiki 3

Hadi sasa Marekani ina jumla ya maambukizi 54,867 katika Majimbo yake yote 50 huku kukiwa na jumla ya vifo 782. China ina maambukizi 81,218 na vifo 3,281
 
OKTOBA 30, 2020
MAREKANI YAREKODI VISA ZAIDI YA 91,000 NDANI YA SAA 24

Nchi hiyo imerekodi jumla ya visa vipya 91,295 na idadi ya maambukizi imefikia 8,426,568 huku waliopona hadi sasa wakiwa 2,778,552

Mbali na ongezeko hilo na maambukizi, vifo 1,021 pia vimerekodiwa katika saa 24 na waliopoteza maisha kutokana na mlipuko wa COVID19 wamefikia 228,625

Maambukizi duniani kote yamefikia 44,538,544 na Marekani inaendelea kuwa nchi iliyoathirika zaidi ikifuatiwa na India

OKTOBA 08, 2020
BRAZIL: VISA VYA CORONAVIRUS VYAFIKIA MILIONI 5

Wizara ya Afya imetangaza visa vipya 31,553 na idadi ya wenye Virusi hivyo imefikia 5,000,694. Wataalamu wana hofu ya kutokea awamu ya pili ya maambukizi kabla ya kwanza haijadhibitiwa

Licha ya idadi ya maambukizi kwa siku kupungua, Mamlaka zimekuwa zikionya kuhusu watu kutozingatia tahadhari za kujikinga, hali ambayo inaongeza uwezekano wa maambukizi mapya

Brazil ni nchi ya tatu kuathirika zaidi na mlipuko huo nyuma ya Marekani yenye visa 6,919,240 na India ambayo imerekodi visa 6,835,655 hadi sasa

SEPTEMBA 27, 2020
VISA VYA CORONAVIRUS VYAFIKIA 32,435,527

Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO), maambukizi ya COVID19 ulimwenguni yamefikia 32,435,527 huku waliopona wakiwa 22, 450,261 na vifo 986,471

Mataifa matano yaliyoathirika zaidi na mlipuko huo duniani ni Marekani-6,659,143, India-5,992,532, Brazil-4,718,115, Urusi-1,143,571 na Colombia-806,038

Aidha, maambukizi yanaongezeka kwa kazi nchini Ufaransa ambapo visa vipya 14,412 vimerekodiwa ndani ya saa 24. Wataalamu wamesema mlipuko wa pili unakuja kwa kasi kuliko walivyotarajia

SEPTEMBA 26, 2020
WHO: VIFO VYA CORONAVIRUS VINAWEZA KUFIKIA MILIONI 2

Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema vifo kutokana na COVID19 vinaweza kufikia Milioni 2 kabla ya kupatikana kwa chanjo

Mkurugenzi wa Programu za Dharura za Afya, Dkt. Mike Ryan amesema takwimu inaweza kuwa kubwa zaidi kusipokuwa na mpango wa pamoja wa kimataifa

Hadi sasa vifo 981,548 vimerekodiwa, wagonjwa 22,260,044 wamepona na maambukizi yamefikia 32.164,141 huku visa vingi zaidi vikiwa kutoka Marekani, India na Brazil

SEPTEMBA 24, 2020
UK: VISA ZAIDI YA 6,600 VYAREKODIWA NDANI YA SAA 24

Uingereza imerekodi jumla ya visa vipya 6,634, idadi ambayo ni kubwa zaidi kuripotiwa kwa siku moja tangu kuanza la mlipuko wa COVID19

Vifo 40 vimerekodiwa na kupeleka idadi ya waliopoteza maisha kutokana na virusi hivyo kufikia 41,902 huku walio na maambukizi wakifikia 416,363

Mapema wiki hii, Waziri Mkuu Boris Johnson alitangaza masharti mapya kudhibiti kasi ya mlipuko huo akisema anatarajia yatakuwepo kwa miezi 6 ijayo

SEPTEMBA 11, 2020
INDIA YAREKODI VISA ZAIDI YA 96,000 NDANI YA SAA 24

India imerekodi visa vipya 96,551 vya COVID19, idadi ambayo ni kubwa zaidi kurekodiwa duniani

Imeelezwa kuwa, maambukizi nchini humo yanaongezeka kwa kasi kuliko sehemu yoyote ulimwenguni ambapo hadi sasa visa 4,566,726 vimerekodiwa

Aidha, nchi hiyo pia imerekodi vifo zaidi ya 1,000 kwa siku 10 na jumla ya waliofariki kutokana na ugonjwa huo ni 76,336 huku waliopona wakiwa 3,542,663

SEPTEMBA 08, 2020
RAIS JINPING ASEMA CHINA ILIKUWA WAZI KUHUSU CORONAVIRUS

Rais Xi Jinping amesema China ilikabiliana na mlipuko wa COVID19 kwa uwazi na ilifanya jitihada ambazo zimesaidia kuokoa maisha ya Mamilioni ya watu ulimwenguni kote

Katika hafla maalum ya kuwatambua waliokuwa mstari wa mbele kwenye vita dhidi ya CoronaVirus, amesema China pia imetoa msaada kwa mataifa mengine yaliyoathirika na janga hilo

Jimbo la Wuhan nchini humo lilikuwa kitovu cha mlipuko wa Virusi vya Corona vilivyoathiri watu 27,138,718 na kupelekea vifo 889,029 duniani hadi sasa huku waliopona wakifikia 18,394,695

SEPTEMBA 07, 2020
INDIA INAKUWA NCHI YA 2 KUREKODI VISA VINGI ZAIDI DUNIANI

Wizara ya Afya nchini humo imetangaza ongezeko la visa vipya 90,802 leo, na idadi hiyo inafanya India kurekodi jumla ya maambukizi 4,204,613

India inaipiku Brazil (4,137,606) na kuwa nchi ya pili kuathirika zaidi na janga la COVID19 ulimwenguni baada ya Marekani ambayo ina visa 6,115,394

Vilevile, Mamlaka pia imerekodi vifo vipya 1,016 ikiwa ni siku ya 5 mfululizo kwa taifa hilo kurekodi vifo zaidi ya 1,000. Hadi sasa India imeripoti vifo 71,687 na wagonjwa 3,250,429 wamepona

AGOSTI 28, 2020
MAAMBUKIZI MAPYA YAPUNGUA KWA 20% AFRIKA

Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC) Afrika kimesema maambukizi mapya yamepungua kwa 20% katika kipindi cha wiki moja iliyopita

Hata hivyo, Kituo hicho kimeonya kuwa hali hiyo haipaswi kuchukuliwa kwa wepesi kwani inawezekana visa vimepungua kutokana na kasi ya upimaji kushuka katika baadhi ya nchi

Imeelezwa kuwa, mataifa mengi yameacha upimaji wa jumla na badala yake yamekuwa yakifanya vipimo kwenye maeneo ambayo maambukizi yameripotiwa

Afrika imerekodi visa zaidi ya Milioni 1.2 vya COVID19 na watu takriban 28,000 wamepoteza maisha

AGOSTI 27, 2020
BUNGE LA KOREA KUSINI LAFUNGWA. SERIKALI YAHIMIZA KAZI ZIFANYIKE NYUMBANI

Bunge la nchi hiyo limefungwa baada ya Mwandishi wa Habari picha kugundulika ana COVID19 jana. Watu zaidi ya 50 walikuwa karibu naye na wametakiwa kujitenga na kupima

Vilevile, katika harakati za kudhibiti maambukizi mapya ya Virusi hivyo, Korea Kusini imetoa wito kwa waajiri kuwapa ruhusa wafanyakazi wao waweze kufanya kazi nyumbani

Kumekuwa na hofu Ofisi zinaweza kuwa kitovu cha maambukizi kutokana na ongezeko la visa linalohusishwa na mikusanyiko makanisani na kwenye maandamano yaliyofanyika mapema mwezi huu

Korea Kusini imerekodi jumla ya visa 18,706 na vifo 313, wagonjwa wapatao 14,461 wamepona

AGOSTI 14, 2020
NCHI 7 ZA AFRIKA KUANZA UPIMAJI WA KINGA MWILI

Kituo cha Kudhibiti Magonjwa Afrika (CDC) kimesema wiki ijayo, mataifa 7 yanatarajiwa kuanza kufanya vipimo vya kinga ya mwili dhidi ya COVID19

Mkurugenzi wa Kituo hicho, Dkt. John Nkengasong ametaja nchi hizo kuwa ni Liberia, Sierra Leone, Zambia, Zimbabwe, Cameroon, Nigeria na Morocco

Vipimo hivyo vinafanywa kama sehemu ya jitihada za kuelewa ukubwa wa janga la CoronaVirus barani humo

Kwa mujibu wa takwimu za Chuo cha Johns Hopkins, Afrika imerekodi visa 1,084,904 hadi sasa

AGOSTI 12, 2020
'POST' ZAIDI YA MILIONI 7 ZINAZOPOTOSHA KUHUSU CORONAVIRUS ZAFUTWA FACEBOOK

Kampuni ya Facebook imesema imefuta 'post' zaidi ya Milioni 7 zinazosambaza taarifa za upotoshaji kuhusu ugonjwa wa COVID19 katika kipindi cha robo ya pili ya mwaka

Facebook imesema taarifa hizo zinaweza kuleta madhara ya kiafya kwa watu. Aidha Kampuni hiyo imesema imeweka alama ya tahadhari katika taarifa Milioni 98 ambazo sio hatarishi sana
-
Facebook ni miongoni mwa mitandao ambayo imekuwa mstari wa mbele kuondoa taarifa za kupotosha tangu kuanza kwa janga la CoronaVirus

AGOSTI 11, 2020
VISA VYA CORONAVIRUS VYAFIKIA MILIONI 20 DUNIANI

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), maambukizi ya COVID19 ulimwenguni yamefikia 20,305,200 wagonjwa waliopona ni 12,915,925 na vifo ni 741,714

Mataifa yaliyorekodi idadi kubwa zaidi ya visa ni Marekani (5,285,218), Brazil (3,057,470), India (2,269,052), Urusi (892,654) na Afrika Kusini (563,598)

Aidha, vifo vingi vimeripotiwa kutoka nchi za Marekani-168,437, Brazil-101,857, Mexico-53,003, Uingereza-46,526 na India-45,361

AGOSTI 03, 2020
MAAMBUKIZI YA COVID19 DUNIANI NI ZAIDI YA MILIONI 18

Tangu janga la CoronaVirus lipate kutokea mjini Wuhan, Desemba 2019 hadi sasa maambukizi yamefikia 18,234,936. Marekani ikiongoza kwa maambukizi ikifuatiwa na Brazil, ya tatu ikiwa India

Vifo 692,794 vimethibitika kutokana na janga la CoronaVirus Duniani. Huku watu 11,444,149 wakiripotiwa kupona

Watu 6,097,993 bado ni wagonjwa huku 65,754 kati yao wakiwa katika hali mbaya. Mamlaka za Afya zinasisitiza wananchi kuchukua tahadhari ili kuepuka maambukizi

AGOSTI 02, 2020
MAREKANI YAREKODI VISA 61,262 NDANI YA SAA 24

Marekani imerekodi visa vipya 61,262 vya COVID19 ndani ya saa 24 na maambukizi ya nchini hiyo yamefikia 4,700,765

Kwa mujibu wa takwimu za Chuo cha Johns Hopkins, Marekani imerekodi visa zaidi ya 60,000 kwa siku 5 mfululizo sasa

Nchi hiyo imeripoti visa vingi zaidi duniani na idadi ya vifo imefikia 156,498 huku wagonjwa waliopona wakiwa ni 2,290,706

Visa 17,963,710 vya COVID19 vimerekodiwa ulimwenguni kote, watu 687,596 wamepoteza maisha na 11,056,616 wamepona

AGOSTI 01, 2020
URUSI KUANZA KAMPENI KUBWA YA UTOAJI CHANJO OKTOBA

Waziri wa Afya, Mikhail Murashko amesema nchi hiyo inatarajia kuanza kampeni kubwa ya chanjo dhidi ya COVID19 ifikapo Oktoba mwaka huu

Taarifa kuhusu aina ya chanjo itakayotumika haijawekwa wazi, lakini Waziri Murashko amesema kundi la kwanza kuipata itakuwa walimu na madaktari

Inadaiwa kuwa Mamlaka zitatoa kibali cha kutumika kwa chanjo hiyo iliyotengezwa na taasisi ya utafiti iliyopo nchini humo mwezi huu na kisha itatolewa kwa ajili ya watumishi wa afya

Urusi imerekodi visa 845,443 na vifo 14,058 huku idadi ya wagonjwa waliopona hadi sasa ikiwa 646,524

MEXICO INAKUWA NCHI YA TATU KWA VIFO VINGI DUNIANI

Idadi ya waliofariki dunia kutokana na mlipuko wa CoronaVirus nchini humo imefikia 46,688 na Mexico inakuwa nchi ya 3 kurekodi vifo vingi zaidi nyuma ya Brazil na Marekani

Wizara ya afya imetangaza ongezeko la visa vipya 8,458 na vifo 688 katika saa 24 zilizopita na maambukizi yamefikia 424,637 huku wagonjwa waliopona wakiwa 278,618

Serikali ya Mexico inasema kuna uwezekano idadi halisi ya maambukizi ni kubwa kuliko takwimu zinavyoonesha

JULAI 31, 2020
BOTSWANA: MJI MKUU WAFUNGWA KWA WIKI 2

Mji Mkuu wa Botswana, Gaborone umefungwa tena kwa muda wa siku 14 kudhibiti ongezeko la maambukizi ya COVID19

Katika Mji huo na maeneo jirani watumishi wa sekta muhimu pekee ndio wataruhusiwa kutoka nyumbani na kwenda kazini huku wengine wakitoka kwa ajili ya kununua mahitaji pekee

Mikusanyiko yote imepigwa marufuku na imeelezwa kuwa hoteli, migahawa, sehemu za kufanya mazoezi pamoja na Shule zitafungwa

Tangu kuanza kwa mlipuko huo, Botswana imerekodi visa 804 na vifo 2, wagonjwa 63 wapona

JULAI 30, 2020
MAREKANI YAREKODI VIFO ZAIDI YA 150,000

Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO), Marekani ina jumla ya visa 4,509,122 na vifo 152,476 vya COVID19 na wagonjwa 2,180,726 wamepona

Taifa hilo limeathirika zaidi na mlipuko wa Virusi vya Corona kuliko nchi yeyote duniani. Idadi ya vifo imekuwa ikiongezeka kwa kasi na takriban vifo 11 vimerekodiwa ndani ya siku 11

Mbali na Marekani, Brazil ambayo ina visa 2,555,518 imerekodi vifo 90,188 hadi sasa huku waliopona wakifikia 1,787,419

Nchi nyingine zenye idadi kubwa ya maambukizi ni India (1,584,384), Urusi (828,990) na Afrika Kusini (471,123)

Duniani kote visa vimefikia 17,131,455, waliopona ni 10,430,838 na vifo ni 668,915

GAMBIA: MAKAMU WA RAIS AAMBUKIZWA COVID-19. RAIS KUJITENGA KWA WIKI 2

Makamu wa Rais wa Gambia, Isatou Touray amekutwa na maambukizi ya COVID19 na kutokana na hilo, Rais Adama Barrow atajitenga kwa muda wa siku 14

Taarifa iliyotolewa na Serikali haikuelezea kwa undani kuhusu hali ya kiafya ya Touray (65) ambaye alitangazwa kuwa Makamu wa Rais wa nchi hiyo mwaka jana

Gambia imerekodi jumla ya visa 326 na vifo 9 vya CoronaVirus, idadi ambayo ni ndogo zaidi kuripotiwa kwa ukanda wa Afrika Magharibi

JULAI 29, 2020
CHINA YAREKODI VISA ZAIDI YA 100 KWA MARA YA KWANZA TANGU APRILI

Tume ya Kitaifa ya Afya imerekodi visa vipya 101 jana, idadi ambayo ni kubwa zaidi kurekodiwa kwa saa 24 tangu Aprili mwaka huu

Katika visa hivyo, 98 ni maambukizi ya ndani ambapo 89 ni kutoka Xinjiang ambapo mlipuko mpya umeripotiwa hivi karibuni. Kisa kimoja ni kutoka Beijing na vingine vimetokea Liaoning

China ina jumla ya visa 86,783 vya COVID19, wagonjwa 80,466 wamepona na idadi ya waliofariki hadi sasa ni 4,656

JULAI 27, 2020
WHO: COVID-19 NI DHARURA MBAYA ZAIDI YA KIAFYA KUTOKEA DUNIANI

Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema janga la CoronaVirus ni dharura mbaya zaidi ya kiafya kutokea duniani

Amesema dunia inaweza kudhibiti maambukizi ya ugonjwa huo ikiwa taratibu mbalimbali za kiafya ikiwemo kuvaa barakoa zitazingatiwa huku akizipongeza nchi za Canada, China, Ujerumani na Korea Kusini kwa kudhibiti milipuko

Hadi kufikia leo, visa 16,397,921 na vifo 651, 675 huku idadi ya wagonjwa waliopona ikifikia 9,810,294. Mataifa yaliyoathirika zaidi ni Marekani, Brazil, India, Urusi na Afrika Kusini

JULAI 25, 2020
MAREKANI YAREKODI VIFO ZAIDI YA 1,000 KWA SIKU 4 MFULULIZO

Marekani imerekodi zaidi ya vifo 1,000 vinavyotokana na #COVID19 kwa siku 4 mfululizo ambapo kwa siku ya Ijumaa, Julai 24 jumla ya vifo 1,019 vilirekodiwa.

Idadi hiyo inafuatia vifo 1,140 vilivyorekodiwa Alhamisi, vifo 1,135 vilivyorekodiwa Jumatano na vifo 1,141 vilivyorekodiwa Jumanne

Aidha, kwa siku ya Ijumaa zaidi ya Wagonjwa wapya 70,000 wamethibitika ambapo maambukizi makubwa yanaonekana katika majimbo ya Arizona, California, Florida na Texas

Hata hivyo, Mshauri Mkuu wa Ikulu kuhusu Ugonjwa huo amesema ameona ishara kuwa hali mbaya imevukwa katika maeneo yaliyoathirika zaidi kwenye Majimbo ya Kusini na Magharibi mwa Marekani

Marekani imerekodi zaidi ya maambukizi 4,192,845, wagonjwa aliopona 1,972,067 na jumla ya vifo 147,127 kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO)

JULAI 17, 2020
INDIA: VISA VYA CORONAVIRUS VYAFIKIA MILIONI 1

India imerekodi visa vipya zaidi ya 34,000 ndani ya saa 24 zilizopita na idadi vya maambukizi nchini humo imefikia 1,005,760 huku vifo vikiwa 25,619 na waliopona wakiwa 636,660

Wizara ya Afya nchini India imesema maambukizi yamekuwa yakisambaa katika miji midogo na maeneo ya vijijini kutokana na masharti ya 'lockdown' kulegezwa nchini humo

India inakuwa nchi ya tatu kuwa na visa zaidi ya Milioni 1 nyuma ya Brazil yenye visa 2,014,738 na Marekani ambayo imerekodi maambukizi 3,677,036

Ulimwenguni kote, COVID19 imeathiri watu 13,937,380, wagonjwa waliopona 8,028,398 na vifo 591,793 vimerekodiwa hadi sasa

ZIMBABWE: MADAKTARI WAUNGANA NA MANESI, WATISHIA KUFANYA MGOMO

Madaktari wa Hospitali za Serikali nchini Zimbabwe wametishia kufanya mgomo, wakilalamikia malipo ya chini na ukosefu wa vifaa kinga (PPE) dhidi ya CoronaVirus

Wamedai inakuwa ngumu kwao kufanya kazi katika maeneo waliyopo kutokana na changamoto mbalimbali huku kukiwa hakuna suluhisho linalotolewa

Uamuzi wao kufanya mgomo unakuja wakati ambapo manesi takriban 15,000 wamekuwa kwenye mgomo kwa wiki mbili sasa kutokana na malipo yasiyoridhisha

Nchi hiyo imerekodi visa 1,362 na vifo 23 vya COVID19, wagonjwa waliopona ni 425

JULAI 15, 2020
GHANA: WANAFUNZI NA WAKUFUNZI ZAIDI YA 300 WAPATA MAAMBUKIZI YA CORONA

Wanafunzi na wakufunzi wapatao 300 nchini Ghana wamepata maambukizi ya COVID19. Shule za Sekondari zilifunguliwa Juni 22

Shule ya Wasichana ya Accra imeathirika zaidi, ikiripoti visa 55. Shule hiyo imewekwa karantini huku Wazazi wa Wanafunzi wakiandamana kupinga Serikali kukataa kuwaruhusu kuwaona watoto wao

Ghana ni miongoni mwa mataifa yaliyoathirika zaidi na mlipuko wa CoronaVirus barani Afrika ikirekodi visa 25,252 na vifo 139

MAREKANI: VISA VIPYA 67,417 VYA COVID19 VYARIPOTIWA

Marekani imeripoti visa vipya 67,417, idadi ambayo ni kubwa zaidi kurekodiwa ndani ya saa 24 tangu kuanza kwa mlipuko huo

Kwa mujibu wa Shirika la Afya (WHO), Nchi hiyo ambayo imeathirika zaidi kwa CoronaVirus ina jumla ya visa 3,868,873 na vifo 143,943 huku wagonjwa waliopona wakiwa 1,523,103

Utabiri mpya unakadiria nchi hiyo itakuwa na vifo 224,000 vya Corona hadi kufikia mwezi Novemba 01, mwaka huu

Hata hivyo, imeelezwa kuwa utabiri huo unaweza kubadilika ikiwa tahadhari zaidi zitachukuliwa ikiwemo uvaaji wa barakoa

JULAI 14, 2020
HONG KONG: MAMLAKA ZATANGAZA MASHARTI KUDHIBITI MLIPUKO WA COVID19

Baada ya Mamlaka kuonya hatari ya mlipuko ni kubwa, Hong Kong imejipanga kutekeleza masharti ambayo yametajwa kuwa magumu zaidi ili kudhibiti mlipuko huo

Wananchi watalazimika kuvaa barakoa kwenye usafiri wa umma na faini ya Dola 5,000 za Hong Kong itatozwa kwa watakaoshindwa kutekeleza agizo hilo

Vilevile, mikusanyiko itahusisha watu 4 pekee huku migahawa na sehemu za mazoezi (gym) zikifungwa. Wateja wataruhusiwa kuchukua chakula kwenye migahawa baada ya saa 12 jioni

Hong Kong ina visa 1,522 vya CoronaVirus ambapo visa vipya 52 viliripotiwa jana. Serikali imesema imelazimika kuweka masharti hayo kutokana na mabadiliko ya mwenendo wa mlipuko huo

JULAI 13, 2020
SRI LANKA: SERIKALI YAAGIZA KUFUNGWA KWA SHULE WIKI 1 BAADA YA KUFUNGULIWA

Serikali nchini humo imeagiza Shule zote kufungwa kuanzia leo baada ya ongezeko la visa vya COVID19. Tamko la Serikali linakuja wiki moja baada ya Shule kufunguliwa

Wizara ya Elimu imesema kutokana na muelekeo wa Mamlaka za Afya, wamefikia uamuzi wa kufunga Shule na kutoa wito kwa vyuo binafsi kufanya hivyo. Wizara hiyo imesema itachunguza mwenendo wa hali hiyo wiki ijayo

Sri Lanka imerekodi 2,631 na vifo 11 huku waliopona wakiwa ni 1,981

MEXICO INAKUWA NCHI YA 4 KWA VIFO DUNIANI

Mexico imerekodi vifo vipya 276 ndani ya saa 24 zilizopita na jumla ya vifo vilivyorekodiwa imefikia 35,006. Nchi hiyo imeipiku Italia na inakuwa ya nne kurekodi vifo vingi vya COVID19 duniani

Kwa mujibu wa Wizara ya Afya, visa vipya 4,482 vimerekodiwa Jumapili, na hadi sasa Mexico imeripoti visa 299,750 huku wagonjwa waliopona wakiwa 184,764

Ulimwenguni kote, visa vya CoronaVirus vimefikia 12,999,091, wagonjwa waliopona ni 7,314,418 na vifo vilivyorekodiwa ni 570,676

JULAI 10, 2020
WATAALAMU WA WHO KUZURU BEIJING KUCHUNGUZA CHANZO CHA VIRUSI VYA CORONA

BEIJING, Wataalamu wawili wa shirika la afya duniani WHO watazuru mji mkuu wa China, Beijing kama sehemu ya kuchunguza chanzo cha virusi vya Corona.Wataalamu hao, akiwemo wa afya ya wanyama na daktari wa kuchunguza kiini cha magonjwa watakutana na wenzao kutoka China ili kuchunguza jinsi virusi hivyo vilivyotoka kwa wanyama na kuingia kwa binadamu.

Wanasayansi wanaamini kuwa asili ya virusi vya Corona ni wanyama aina ya popo, na baadaye virusi hivyo viliambukizwa kwa wanyama wengine na hatimaye kuwafikia binadamu.

Mji wa Wuhan ndio ulikuwa kiini cha virusi hivyo mwaka jana, lakini uchunguzi wa hivi karibuni umeonyesha kuwa huenda mlipuko huo ulianzia sehemu nyengine.China imepiga marufuku biashara ya wanyama pori na kufunga baadhi ya masoko nchini humo ili kuzuia kusambaa kwa virusi hivyo.

JULAI 06, 2020

COVID-19: INDIA YASHIKA NAFASI YA TATU KATIKA NCHI ZILIZOATHIRIKA ZAIDI

India imeripoti jumla ya maambukizi 700,724 ya CoronaVirus, kwa idadi hiyo imeipita Urusi ambayo mwanzo ilikuwa ya tatu kwa kuathirika na COVID19

Wizara ya Afya ya India imesema katika muda wa saa 24 zilizopita, imekuwa na maambukizi mapya 24,000. Na hadi sasa nchi hiyo ina vifo 19,963 vya COVID19

Wataalamu wa afya wametabiri maambukizi yatafika 1,000,000 mwezi huu. Miji iliyoathiriwa zaidi ni New Delhi na Mumbai, kila mji ukiwa na zaidi ya maambukizi 100,000

Marekani ni ya kwanza kwa maambukizi ikiwa na maambukizi 2,985,490 na vifo 132,610 huku nchi ya pili ikiwa ni Brazil yenye maambukizi 1,604,585 na vifo 64,900

MAAMBUKIZI YA COVID19 YAFIKIA 11,562,878

Maambukizi ya mlipuko wa COVID19 ulioanza Desemba mwaka 2019 Wuhan China yamefikia 11,562,878

Huku kukiwa na jumla ya vifo 536,841, watu 6,537,765 wakiwa wamepona na 4,488,272 wakiwa bado na maambukizi, watu 58,527 wapo katika hali mbaya

Wataalamu wanatarajia kupeleka matokeo ya utafiti unaoonyesha kuwa CoronaVirus wanaweza kuelea hewani na wanaweza kuenezwa kwa njia ya hewa

Barua itakayokwenda Shirika la Afya Duniani imetiwa saini na wanasayansi 239

JULAI 02, 2020
MAREKANI: VISA ZAIDI YA 55,000 VYAREKODIWA NDANI YA SAA 24

Marekani imerekodi visa vipya 55,000 siku ya jana, idadi hiyo ni kubwa zaidi kurekodiwa na nchi yeyote duniani ndani ya saa 24

Hadi sasa, taifa hilo lina jumla ya visa 3,003,811 na vifo 134,432 vya CoronaVirus huku wagonjwa waliopona wakifikia 1,132,412

Wakati huo huo, Gavana wa Jimbo la Texas Greg Abbott ametangaza kuwa ni lazima kuvaa barakoa maeneo ya umma kufuatia ongezeko la visa vya COVID19

Makadirio mapya yaliyochapishwa na Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC) yanatabiri vifo takriban 148,000 nchini humo hadi kufikia Julai 25, 2020

JULAI 01, 2020
NEW ZEALAND: WAZIRI WA AFYA AJIUZULU BAADA YA KUKIUKA TARATIBU ZA KUJIKINGA NA COVID19

Aliyekuwa Waziri wa Afya nchini humo, David Clark amejiuzulu kufuatia changamoto mbalimbali za kisiasa ikiwemo kukiuka taratibu zilizowekwa na Serikali ili kujikinga na CoronaVirus

Tangu Aprili mwaka huu Clark alikosolewa vikali baada ya kwenda baharini na familia yake wakati Serikali iliamuru Wananchi kubaki nyumbani. Aliwasilisha maombi ya kujiuzulu lakini Waziri Mkuu, Jacinda Arden alimkatalia na badala yake alishushwa cheo

New Zealand imerekodi visa 1,530 na vifo 22 huku wagonjwa 1,490 wakipona. Nchi hiyo ni miongoni mwa mataifa yaliyotajwa kufanikiwa kudhibiti maambukizi ya ugonjwa huo

JUNI 29, 2020
INDIA YAREKODI VISA ZAIDI YA 10,000 KWA SIKU YA 8 MFULULIZO

India imerekodi visa vipya 19,459 ikiwa ni siku ya 8 mfululizo kwa nchi hiyo kuwa na visa zaidi ya 10,000 na maambukizi nchini humo yamefikia 549,853

Kwa mujibu wa Wizara ya Afya, visa zaidi ya 100,000 vimerekodiwa ndani ya siku 6 pekee. India imepima sampuli Milioni 8 hadi sasa, huku 170,000 zikipimwa ndani ya saa 24 zilizopita

Nchi hiyo imerekodi vifo 16,504 na wagonjwa 322,121 wamepona hadi sasa. India ni nchi ya tano kuathirika zaidi kwa CoronaVirus duniani

VISA ZAIDI YA MILIONI 10 VYAREKODIWA DUNIANI

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), visa 10,328,594 vya Corona vimerekodiwa hadi kufikia leo asubuhi

Hadi sasa wagonjwa wapatao 5,290,825 wamepona na jumla ya vifo 505,991 vimeripotiwa ulimwenguni

Nchi zilizorekodi visa vingi zaidi ni Marekani (2,719,547), Brazil (1,345,254), Urusi (634,437), India (549,197) na Uingereza (311,151)

Kwa upande wa Afrika, nchi zinazoongoza kwa maambukizi ni Afrika Kusini (138,134), Misri (65,188), Nigeria (24,567), Ghana (16,742) na Algeria (13,273)

JUNI 25, 2020
MAREKANI IMERIPOTI ZAIDI YA WAGONJWA WAPYA 34,500 NDANI YA SAA 24

Marekani ambayo ni ya kwanza kwa visa vingi ya #COVID19 Ulimwenguni, imeripoti wagonjwa wapya 34,516 na vifo vipya 751 kwa mujibu wa Chuo Kikuu John Hopkins

Kutokana na ongezeko hilo, jumla ya visa vya virusi hivyo vilivyoripotiwa nchini humo imefikia 2,381,538 huku idadi ya vifo ikifikia 121,979

Aidha, jumla ya watu 987,669 wamepona na takwimu za ugonjwa huo ni kutoka katika Majimbo yote 50, sehemu zilizochini ya Marekani na District of Columbia

JUNI 22, 2020
BRAZIL: ZAIDI YA WATU 7,000 WAMEFARIKI NDANI YA WIKI MOJA

Wizara ya Afya nchini humo imeripoti vifo vipya 641, kwa siku ya jana Juni 21, 2020. Hii inaonesha kuwa watu 7,285 wamefariki ndani ya wiki moja

Aidha, nchi hiyo ambayo sasa imerekodi jumla ya vifo 50,617, imerekodi Wagonjwa wapya 17,459 hapo jana na kufanya jumla ya visa kufikia 1,085,038

Kwa takwimu hizo Brazil ni nchi ya pili kuwa na visa vingi vya COVID19 duniani huku yenyewe na Marekani zikiwa ndizo nichi zenye visa zaidi ya milioni 1

JUNI 20,2020
BRAZIL YAREKODI VISA ZAIDI YA MILIONI 1

Mlipuko wa Corona unaendelea kushika kasi Amerika ya Kusini na Brazil inakuwa nchi ya pili duniani kurekodi visa zaidi ya Milioni 1

Wizara ya Afya imeripoti visa vipya 54,771 na kupelekea maambukizi ya nchi hiyo kufikia 1,038,568. Marekani ambayo ni nchi iliyoathitika zaidi na COVID19 ina visa 2,971,346

Aidha, vifo vipya 1,206 pia vimeripotiwa na waliofariki dunia kwa COVID19 nchini humo hadi sasa ni 49,090 huku wagonjwa waliopona wakiwa 520,360

Kwa mujibu wa Shirika la Afya (WHO) visa vya Corona vimefikia 9,441,343 duniani, wagonjwa 4,374,705 wamepona na 466,223 wamepoteza maisha

JUNI 17, 2020
BRAZIL: VISA ZAIDI YA 34,000 VYAREKODIWA NDANI YA SAA 24

Wizara ya Afya imeripoti visa vipya 34,918 vya COVID na Brazil ina jumla ya visa 923,834 hadi sasa. Kwa mujibu wa Shirika la Afya (WHO) wagonjwa 464,774 wamepona

Takwimu hizo zimetolewa wakati Afisa wa juu wa Kikosi kinachoshughulikia ugonjwa huo, Walter Braga Netto akidai mlipuko nchini humo umethibitiwa. Amesema #Brazil inafanya vizuri kuliko mataifa mengi ya Ulaya

Pamoja na ongezeko la maambukizi, vifo vipya 1,282 pia vimerekodiwa ndani ya siku moja na kupelekea idadi ya waliofariki kwa CoronaVirus kufikia 45,456

JUNI 16, 2020
VISA ZAIDI YA MILIONI 8 VYAREKODIWA, WAGONJWA MILIONI 3.9 WAPONA

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) visa 8,717,816 vimerekodiwa ulimwenguni hadi kufikia leo asubuhi. Watu 3,959,884 wamepona na vifo ni 442,387

Ripoti mpya kutoka Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa imesema wenye magonjwa sugu ikiwemo magonjwa ya Moyo na Kisukari wapo hatarini zaidi kufariki kwa COVID-19

Marekani ambayo imeathirika zaidi ina visa 2,785,732, vifo 121,545 huku waliopona wakiwa 842,659. Nchi nyingine ni Brazil (891,556) Urusi (537,210), India (343,026) na Uingereza (296,857)

Barani Afrika, nchi zilizoathirika zaidi ni Afrika Kusini (73,533), Misri (46,289), Nigeria (16,658), Ghana (11,964) na Algeria (11,031)

JUNI 15, 2020
UFARANSA KULEGEZA MASHARTI ZAIDI KUANZIA LEO

Rais Emmanuel Macron amesema masharti yaliyowekwa kudhibiti mlipuko wa COVID19 nchini humo yatalegezwa zaidi kuanzia leo ambapo safari za nchi nyingine za Ulaya zitaruhusiwa

Migahawa na hoteli zitaruhusiwa kuanza kutoa huduma nchi nzima. Mji Mkuu wa Ufaransa, Paris ambao umerekodi idadi kubwa zaidi ya visa nchini humo pia utafunguliwa

Hata hivyo, Rais Macron ameonya kuwa, japo nchi hiyo imepata ushindi wake wa kwanza dhidi ya ugonjwa huo, kuna uwezekano unaweza kurejea tena

Ufaransa ina jumla ya visa 157,223, vifo 29,407 na wagonjwa 72,859 wamepona hadi sasa

JUNI 12, 2020
MAREKANI: WAGONJWA WAPYA ZAIDI YA 22,900 WAMERIPOTIWA JANA

Marekani imeripoti wagonjwa wapya 22,921 kwa siku ya jana Juni 11, 2020 idadi inayofanya jumla ya maambukizi kwa Taifa hilo kufikia 2,654,827

Idadi hiyo inajumuisha idadi ya visa kutoka Majimbo yote 50, District of Columbia, maeneo mengine yaliyo chini ya marekani na wagonjwa Wamarekani walitoka mataifa mengine

Taifa hilo la Amerika ya Kaskazini kwa siku ya jana pia limetangaza jumla ya vifo 894 na kufanya kuwepo kwa jumla ya vifo 119,349 kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO)

Hata hivyo Marekani inayoongoza Duniani kwa idadi ya vifo na maambuki imeripoti jumla ya Wagonjwa 77,350 walipona #COVID19 hadi kufikia leo

JUNI 09, 2020
CORONAVIRUS: UGANDA YATANGAZA WAGONJWA WAPYA 11. JUMLA YA VISA YAFIKIA 657

Taifa hilo la Afrika Mashariki limetangaza ongezeko hilo la Wagonjwa ambao wote ni Waganda na wamethibitika baada ya sampuli kufanyiwa vipimo jana

Kati ya Wagonjwa hao, 5 ni Madereva wa Malori walipatikana katika mipaka ya Malaba na Elegu na 6 ni waliokuwa wakifuatiliwa na walionesha dalili katika Wilaya za Amuru na Kyotera

Sampuli zilizopimwa jana kutoka mipakani ni 1,1412, kutoka kwa waliokuwa wakifuatiliwa au kuonesha dalili ni 878 huku sampuli 46 zikitoka kwa Wafayakazi wa Afya

Aidha, Madereva wa Kigeni 34 wamekutwa na COVID19 lakini Wizara hiyo haikutaja uraia wa Madereva hao. Jumla ya Wagonjwa waliopona Uganda ni 118

JUNI 08, 2020
MEXICO: AFISA WA JUU SERIKALINI ATHIBITIKA KUWA NA COVID19 SIKU CHACHE BAADA YA KUWA PAMOJA NA RAIS

Mkurugeni wa Taasisi ya Hifadhi ya Jamii, Zoé Robledo ametangaza jana kuwa amethibitika kuwa na CoronaVirus ikiwa ni siku 2 baada ya kuonekana akiwa pamoja na Raisi wa nchi hiyo

Robledo amesema ataendelea kufanya kazi zake akiwa Karantini huku akifuta maagizo ya Madaktari wake na kwamba shughuli ya kuwafuatilia aliokuwa karibu nao inaendelea

Ijumaa, Juni 05, aliongea katika Mkutano wa Rais Andrés Manuel López Obrador ambapo pia Maafisa wa Juu wa Taifa hilo walihudhuria mkutano huo

Rais alikuwa jukwaani pamoja na Waziri wa Ulinzi, Luis Cresencio Sandoval, Waziri wa Usalama wa Ulinzi wa Wananchi, Alfonso Durazo. Walikuwa wamewekwa kwa umbali fulani ila hakuna aliyekuwa amevaa barakoa

JUNI 07, 2020
URUSI: VISA VIPYA ZAIDI YA 8,000 VYAREKODIWA NDANI YA SAA 24

Urusi imerekodi jumla ya visa 8,984 vya COVID19 na maambukizi ya nchi hiyo yameongezeka na kufikia 467,673

Pamoja na ongezeko la visa, Mamlaka pia zimesema wagonjwa 134 wamepoteza maisha ndani ya muda huo na waliofariki hadi sasa ni 5,859

Aidha, wagonjwa 226,731 nchini humo wamepona. Urusi ni la tatu kwa visa vingi zaidi duniani nyuma ya Brazil na Marekani

JUNI 05, 2020
BRAZIL IMEREKODI VIFO ZAIDI YA 34,000, INAKUWA YA TATU KWA VIFO DUNIANI

Kwa siku ya tatu mfululizo, vifo zaidi ya 1,000 vimerekodiwa ndani ya siku moja na jumla ya waliopoteza maisha imefikia 34,039. Wizara ya Afya imesema vifo vipya 1,473 vimerekodiwa jana

Pia kwa mujibu wa Wizara hiyo, visa vipya 30,925 vimeripotiwa saa 24 zilizopita na maambukizi yamefikia 615,870. Wagonjwa waliopona hadi sasa ni 274,997

Brazil yenye visa 615,870 hadi sasa inaipiku Italia na kuwa nchi ya tatu kwa vifo vingi duniani nyuma ya Uingereza na Marekani

JUNI 04, 2020
ENGLAND: KUVAA BARAKOA KWENYE USAFIRI WA UMMA ITAKUWA LAZIMA KUANZIA JUNI 15

Waziri wa Uchukuzi, Grant Shapps amesema kuanzia Juni 15, 2020 kila mtu atalazimika kuvaa barakoa awapo kwenye usafiri wa umma na watakaokiuka utaratibu huo wanaweza kulipa faini

Amesema wananchi watatakiwa kuvaa barakoa pindi watakapotumia mabasi, treni, usafiri wa anga pamoja na ule wa majini. Watoto wadogo, watu wenye ulemavu na wale walio na matatizo ya kupumua hawatolazimika kuvaa

Waziri huyo amesema kila tahadhari inapaswa kuchukuliwa kwasababu idadi ya abiria inatarajiwa kuongezeka masharti yanavyoendelea kulegezwa

UN: COVID-19 NI JANGA KUBWA ZAIDI LA KIAFYA KWA KIZAZI HIKI

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) António Guterres amesema CoronaVirus ni janga kubwa zaidi la afya ya umma na hakuna chanjo wala tiba kwa sasa

Amesema wakati wataalamu kutoka mataifa mbalimbali wanashirikiana kupata chanjo, ni muhimu kuelewa kupatikana kwa chanjo pekee haitoshi

Guterres ameeleza kuwa kinachotakiwa ni umoja ulimwenguni kote ili kila mtu aweze kupata chanjo pindi itakapopatikana

Hadi sasa visa 7,062,893 vya COVID19 vimerekodiwa duniani, wagonjwa 2,952,870 wamepona na 391,941 wamefariki dunia

BRAZIL: VIFO ZAIDI YA 1,000 VYAREKODIWA KWA SIKU YA PILI MFULULIZO

Kwa siku ya pili mfululizo, Brazil imerekodi vifo zaidi 1,000. Kwa mujibu wa Wizara ya Afya vifo 1,349 vimeripotiwa ndani ya saa 24 zilizopita

Hivi sasa, nchi hiyo ina jumla ya visa 584,562 na vifo 32,568 huku idadi ya waliopona wakiwa 266,132

Akizungumzia ongezeko la vifo vya COVID-19, Rais Jair Bolsonaro amesema kila mtu ameandikiwa kufa. Ameendelea kuvilaumu vyombo vya habari kwa kuwatia hofu wananchi

JUNI 03, 2020
BRAZIL: VIFO ZAIDI YA 1,000 VYAREKODIWA NDANI YA SAA 24

Wizara ya Afya imesema vifo 1,262 vimeripotiwa ndani ya siku moja na jumla ya waliofariki dunia kutokana na COVID19 nchini humo imefikia 31,309

Aidha, visa vipya 28,936 pia vimerekodiwa ndani ya muda huo na kufanya maambukizi kuongezeka hadi 558,237. Hadi sasa, wagonjwa 253,570 wamepona

Baadhi ya miji mikubwa nchini Brazil ikiwemo Rio de Janeiro na Sao Paulo imeanza kulegeza masharti licha ya mwenendo wa ugonjwa huo. Mji wa Sao Paulo pekee una visa 7,994

Brazil ni nchi ya pili kuathirika zaidi na mlipuko wa CoronaVirus baada ya Marekani yenye visa 2,320,476, vifo 111,417

JUNI 01, 2020
INDIA: MJI WA NEW DELHI KUFUNGWA KWA WIKI MOJA

Mipaka ya Mji Mkuu wa India, New Delhi itafungwa kwa wiki moja ili kudhibiti maambukizi ya COVID19. Hata hivyo, Waziri Arvind Kejriwa amesema usafirishaji wa bidhaa na huduma muhimu utaendelea

Maduka na saluni zote zitaendelea kutoa huduma lakini Mamlaka imeweka agizo la muda wa kutotoka ndani kuanzia saa tatu usiku mpaka saa 11 alfajiri kwa mujibu wa taratibu za Serikali

Imeelezwa kuwa, Mji huo utaruhusu safari chache mipakani lakini watumishi wa Serikali walio na utambulisho wataruhusiwa kusafiri

India imerekodi visa 191,041 hadi sasa huku waliopona wakiwa 91,907 na vifo vimefikia 5,413

BRAZIL: VISA ZAIDI YA 500,000 VYAREKODIWA

Brazil imerekodi visa vipya 16,409 ndani ya saa 24 zilizopita na jumla ya maambukizi nchini humo imefikia 514,992

Pamoja na ongezeko la maambukizi, pia vifo 480 vimerekodiwa na waliofariki dunia ni 29,314. Wagonjwa waliopona COVID19 hadi kufikia leo ni 206,555

Brazil inakuwa nchi ya mbili kwa visa vingi zaidi duniani baada ya Marekani ambayo imerekodi visa 2,183,493. Nchi nyingine zenye idadi kubwa ya maambukizi ni Urusi (405,843), Uhispania (286,509) na Uingereza (274,762)

Ulimwenguni kote, visa 6,616,154 vya CoronaVirus vimerekodiwa, waliopona ni 2,806,426 na vifo ni 373,949

MEI 31, 2020
BRAZIL IMERIPOTI VISA VIPYA 33,274 NDANI YA SAA 24

Nchi hiyo imerekodi visa 33,274 vya COVID19 kwa siku ya Jumamosi na kufanya kuwa na jumla ya visa 499,966 ikiwa ni nchi ya pili kwa visa vingi nyuma ya Marekani (2,036,110)

Pia, imerekodi vifo vipya 956 na kuwa na jumla ya vifo 28,849. Imeipita Ufaransa (28,771) kwa idadi ya vifo huku ikiwa nyuma ya Marekani (105,230), Uingereza (38,376) na Italia (33,340)

Magavana wa Majimbo wanajiandaa kulegeza masharti ya kukaa ndani ingawa Wataalam wa Afya wameonya kuwa hali mbaya zaidi ya ugonjwa huo inakuja

Rais wa Taifa hilo la Amerika ya Kusini, Jair Bolsonaro ambaye ameonekana kudharau ugonjwa huo amekosa zuio la watu kutotoka nje akisema linashusha uchumi na kusababisha ukosefu ajira

MEI 29, 2020
BRAZIL YAREKODI VISA ZAIDI YA 26,000 NA VIFO ZAIDI YA 1,150 NDANI YA SAA 24

Brazil imerekodi wagonjwa wapya 26,417 wa COVID19 jana, ikiwa ni idadi kubwa ya wagonjwa kutangazwa na nchi ndani ya saa 24. Idadi ya visa nchini humo imefikia 438,238

Pia, nchi hiyo imerekodi vifo vipya 1,156 vinavyohusiana na #CoronaVirus katika saa 24 zilizopita na kufanya nchi hiyo ya Amerika ya Kusini kuwa na jumla ya vifo 26,754. Waliopona wafikia 193,181

Wakati hayo yakijiri, Rais wa Brazil, Jair Bolsonaro ametaka shughuli za uchumi kufunguliwa akisema kufungwa kwa sekta zisizo muhimu ni fedheha mbaya kwa nchi

Magavana na Meya walichukua uamuzi wa kufunga shughuli zisizo muhimu katika majimbo yao baada ya Rais huyo kusema hatochukua hatua hiyo

Bolsonaro amesisitiza kuwa katika nchi hiyo kuna matatizo mawili, #CoronaVirus na maisha lakini pia kuna tatizo la ukosefu wa ajira hivyo anataka shughuli za uchumi kufunguliwa

MEI 25, 2020
UHISPANIA: WATALII KURUHUSIWA KUANZIA JULAI 1

Uhispania imewataka watalii kurejea nchi humo kuanzia Julai 1 mwaka huu baada ya masharti yaliyowekwa nchini humo ili kudhibiti COVID19 kuanza kulegezwa

Waziri wa Utalii, Reyes Maroto amesema ni sawa kupanga kwenda nchini humo kwa ajili ya likizo kuanzia Julai. Kufuatia mwenendo wa COVID19, inawezekana amri ya wageni kukaa karantini ya lazima kwa siku 14 ikatolewa

Uhispania ambayo ni nchi ya pili kutembelewa zaidi duniani hupata wageni takriban Milioni 80 kwa mwaka inajipanga kufungua sekta ya utalii

Mpaka sasa visa 282,852 vimerekodiwa nchini humo, waliopona ni 196,958 na vifo ni 28 752

MEI 22, 2020
UHISPANIA: MASHARTI MADRID, BARCELONA KULEGEZWA KUANZIA JUMATATU

Serikali imesema masharti yaliyowekwa kudhibiti COVID19 katika miji ya Madrid na Barcelona yataanza kulegezwa kuanzia Jumatatu ijayo baada ya maambukizi kupungua

Mapema mwezi huu, masharti yalilegezwa katika maeneo mengine ya nchi hiyo lakini Miji hiyo miwili iliendelea kufuata taratibu zote za wawili kwakuwa iliathirika zaidi na CoronaVirus

Migahawa na baa itaruhusiwa kutoa huduma kwa nusu idadi, makanisa nayo yatafunguliwa na wananchi wataruhusiwa kusafiri nje ya miji hiyo. Vilevile, shughuli za uwindaji na uvuaji samaki zitarejea

Makumbusho, kumbi za sinema, maonesho ya sanaa na baadhi ya shule nazo zitafunguliwa huku idadi ya watu ikizingatiwa

Uhispania imerekodi visa 280,117, wagonjwa 196,958 wamepona na waliofariki ni 27,940

MAREKANI: VISA VIPYA ZAIDI YA 25,000 VYATANGAZWA

Takwimu za Chuo cha John Hopkins zimeonesha kuwa visa vipya 25,294 na vifo 1,263 vimerekodiwa ndani ya saa 24 zilizopita

Hadi kufikia asubuhi ya leo wagonjwa 343,811 wa COVID19 wamepona nchini humo, huku idadi ya waliofariki ikiwa 96,465 na jumla ya visa ikifikia 1.795,587

Rais Donald Trump amesema bendera ya Marekani itapeperushwa katika majengo yote ya serikali pamoja na makumbusho za taifa kwa siku tatu zijazo kuwaenzi Wamarekani waliopoteza maisha kutokana na CoronaVirus

MEI 21, 2020
CORONAVIRUS: MAJARIBIO YA DAWA YA HYDROXYCHLOROQUINE KUANZA ULIMWENGUNI

Wafanyakazi wa Afya Uingereza na Thailand wameanza kuhusika kwenye majaribio ya kufahamu kama aina mbili za dawa za kutibu Malaria zitaweza kuzuia COVID19

Dawa hizo zinajumuisha aina ya dawa ya hydroxychloroquine ambayo Rais wa Marekani, Donald Trump alijinadi kuwa anaitumia akiamini ni nzuri

Utafiti unajumuisha zaidi ya Wafanyakazi wa Afya 40,000 wa barani Ulaya, Afrika, Asia na Amerika ya Kusini, ili kujua kama chloroquine na hydroxychloroquine inaweza kusaidia kupambana na COVID_19

Uhitaji wa hydroxychloroquine umeongezeka zaidi baada ya Rais Trump kuipigia upatu mapema Aprili na wiki hii alijinadi kuitumia licha ya tahadhari kadhaa kutoka kwa Wataalamu wa Afya

BRAZIL: VISA VIPYA ZAIDI YA 19,000 VYAREKODIWA

Brazil imeripoti idadi kubwa zaidi ya maambukizi kuwahi kutokea ndani ya saa 24 ambapo visa 19,951 vimerekodiwa

Wizara ya Afya imesema visa 19,951 vimerekodiwa jana na idadi ya maambukizi nchini humo imeongezeka na kufikia 293,357

Aidha, vifo 888 vimeripotiwa na jumla ya watu waliofariki dunia kutokana na COVID19 hadi sasa ni 18,894

Brazil inakuwa nchi ya tatu kwa visa vingi kwa #CoronaVirus nyuma ya Urusi (308,705) na Marekani (1,750,407)

MEI 20, 2020
UHISPANIA: WANANCHI WATAKIWA KUVAA BARAKOA SEHEMU ZA UMMA

Wizara ya Afya imesema wananchi watatakiwa kuvaa barakoa wakiwa sehemu za umma ambazo umbali wa futi 6.5 utakuwa vigumu kuzingatiwa

Wananchi wote kuanzia miaka 6 wametakiwa kuzingatia agizo hilo, watu wenye matatizo ya pumu na wale walio na ulemavu unaozuia uvaaji barakoa hawatohusishwa

Barakoa zote zinaruhusiwa ikiwa zinaziba pua na mdomo lakini Wizara imeshauri wananchi kutumia barakoa zilizothibitishwa kitaalamu

Uhispania imerekodi jumla ya visa 278,803, vifo 27,778 na wagonjwa waliopona ni 196,958

BRAZIL: VIFO ZAIDI YA 1,000 VYAREKODIWA KWA SIKU MOJA

Wizara ya Afya imesema vifo 1,179 vimerekodiwa ndani ya saa 24 zilizopita, idadi ambayo ni kubwa zaidi kuripotiwa nchini Brazil tangu kuanza kwa mlipuko wa Corona

Nchi hiyo ina visa 271,885 na vifo 17,983 hadi sasa, huku jumla ya wagonjwa waliopna Virusi hivyo ikiwa 106,794. Brazil imerekodi visa vingi zaidi kuliko Uingereza (248,818), Italia (226,699) na Ufaransa (180,812)

Rais wa Brazil, Jair Bolsonaro amekosolewa kwa namna anayokabiliana na janga la COVID19. Aidha, Rais wa Marekani, Donald Trump amesema anafikiria kuzuia safari za Brazil

Rais Trump amesema ni kwasababu hataki watu kuingia nchini humo na kuambukiza Wamarekani. Amesema Brazil inapitia wakati mgumu na wanaisaidia na mashine za upumuaji

MEI 19, 2020
UJERUMANI: WATUMISHI WA AFYA ZAIDI YA 20,000 WAPATA COVID19

Kituo cha Kudhibiti Magonjwa nchini humo kimesema zaidi ya watumishi wa afya 20,400 wameambukizwa CoronaVirus tangu kuanza kwa mlipuko huo

Kwa mujibu wa Taasisi ya Robert Koch, takriban watumishi 19,000 wamepona na 61 wamefariki dunia. Visa vya watumishi vinakadiriwa kuwa 11% ya maambukizi yote ya Ujerumani

Nchi hiyo imerekodi visa 177,620 na vifo 8,150 huku wagonjwa waliopona wakiwa 155,700

MAREKANI: WATU ZAIDI YA 93,000 WAFARIKI DUNIA KWA CORONAVIRUS

Nchi ya Marekani imerekodi jumla ya vifo 93,088 hadi kufikia sasa, idadi ambayo ni kubwa zaidi kuliko nchi nyingine yeyote duniani

Aidha visa 1,721,133 vya COVID19 vimeripotiwa mpaka asubuhi ya leo na wagonjwa wapatao 322,939 wakiwa wamepona

Pamoja na Marekani, nchi nyingine zenye idadi kubwa ya maambukizi ni Urusi (290,678), Uhispania (278,188), Brazil (255,368) na Uingereza (246,406)

Ulimwenguni kote, Virusi vya Corona vimeathiri watu takriban 5,064,492, wagonjwa waliopona ni 1,872,984 na vifo vilivyoripotiwa ni 321,338

MEI 18, 2020
MAREKANI: VISA VIPYA ZAIDI YA 18,000 VYAREKODIWA

Kwa mujibu wa takwimu kutoka Chuo cha John Hopkins, takriban visa vipya 18,873 na vifo 808 vimerekodiwa jana, Mei 17 2020

Hivi sasa Marekani ina jumla ya visa 1,674,644, wagonjwa waliopona ni 313,809 huku waliofariki dunia wakiwa 92,639

Bado Marekani inaendelea kuwa nchi iliyoathirika zaidi na mlipuko wa COVID19. Mataifa mengine yenye idadi kubwa ya maambukizi ni pamoja na Urusi, Uhispania, Uingereza na Brazil

Ulimwenguni kote, visa viliyorekodiwa ni 4,743,780, waliopona ni 1,698,902 na waliopoteza maisha ni 314,785

MEI 14, 2020
UGANDA: WAGONJWA 13 WAONGEZEKA, VISA VYAFIKIA 139

Wagonjwa hao wapya ni madereva wa malori waliothibitika baada ya sampuli 1,741 za madereva wa malori kupimwa #COVID19 jana Mei 13, 2020

Kati ya Wagonjwa hao wapya, Waganda ni 7, Wakenya ni 5 na mmoja ni raia wa Eritrea ambao wanaelezwa kuingia Uganda wakitokea Tanzania, Sudan Kusini na Kenya kupitia mipaka ya Mutukula, Elegu na Malaba

Aidha, Wizara ya Afya imeeleza kuwa jumla ya sampuli zilizopimwa jana ni 2,104 ambapo sampuli 363 zilikuwa za Wananchi katika jamii mbalimbali nchini humo na zote zilikutwa hazina maambukizi

Wakuu wa nchi za Afrika Mashariki waliokutana walikubaliana kuwa madereva wa malori watakuwa wakipimwa mara mbili, watapimwa nchi watokako na wataondoka ikiwa wako salama na pia watapimwa nchi wanakoenda

MEI 13, 2020
CORONAVIRUS: URUSI YAREKODI VISA ZAIDI YA 10,000 KWA SIKU YA 11 MFULULIZO

Urusi imeripoti Wagonjwa wapya 10,028 leo Mei 13 na kufanya idadi ya visa nchini humo kufikia 242,271. Watu 96 wamefariki usiku wa kuamkia leo na kufanya idadi ya vifo kufikia 2,212

Urusi inaipita Uingereza yenye visa 226,463 na kuwa nchi ya tatu kwa wingi wa visa nyuma ya Marekani yenye visa 1,490,915 na Uhispania yenye visa 269,520

Aidha, nchi hiyo imesitisha matumizi ya baadhi ya mashine za kusaidia kupumua (Ventilator) zinazotengenezwa nchini humo baada ya mashine mbili za aina hiyo kuwaka moto hospitalini

Aina hiyo ya mashine (Aventa-M) zilikuwa zinatumika katika hospitali ya St. Petersburg ambapo watu watano walifariki kutokana na moto huo, na pia zilikuwa zinatumika katika hospitali ya Moscow ambapo mtu mmoja alifariki

UGANDA: MADEREVA WANNE WA MALORI WAKUTWA NA #COVID19. YUPO MTANZANIA MMOJA

Wizara ya Afya nchini humo imesema Madereva wanne wa malori wamethibitishwa kuwa na COVID19 na kufanya idadi ya visa nchini humo kufikia 126

Wawili kati ya Wagonjwa wapya ni Waganda huku wengine wakiwa ni raia wa Kenya na Tanzania. Waganda na Mkenya wanaaminika kuingia Uganda kupitia mpaka wa Elegu na Mtanzania alipimwa katika mpaka wa Mutukula

Wamegundulika baada ya sampuli 1,478 za madereva wa malori kupimwa na Taasisi ya Utafiti wa Virusi Uganda. Hadi sasa sampuli zaidi ya 10,000 za madereva wa malori zimepimwa

Upatikanaji wa madereva wa malori wenye COVID19 imezuia hofu kati ya Waganda wengi wakiogopa madereva hao watasababisha kuenea zaidi kwa ugonjwa huo

CORONAVIRUS: BRAZIL YAREKODI VIFO 881 NDANI YA SAA 24

Wizara ya Afya imethibitisha jumla ya vifo 12,400 kutokana na COVID19 huku idadi ya visa ikifika 178,214 na kuipita Ujerumani yenye visa 173,273 huku ikiwa inaikaribia Ufaransa yenye visa 178,228

Baadhi ya nchi za Ulaya zinaanza kupunguza masharti ya zuio la kutotoka ndani, lakini mlipuko wa ugonjwa huo unazidi kuongezeka Brazil ambapo Rais Jair Bolsonaro amewakosoa Magavana kwa kutoa amri ya watu kujitenga

Wiki hii Rais Bolsonaro aliongeza mzozo baina yake na Magavana wa Majimbo baada ya kuainisha biashara kama Sehemu za Mazoezi (gyms) na saluni ni huduma muhimu hivyo zisizuiliwe

Rais huyo amesema Magavana wasiokubaliana naye katika hilo wanaweza kwenda Mahakamani huku akiwatishia kuwa atachukua hatua za kisheria kwa wale wasiofuata maagizo yake

Hata hivyo, takriban Magavana 10 wamesema hawatafuata agizo hilo. Gavana wa Rio de Janeiro, Wilson Witzel amesema "Bolsonaro anatembea kuelekea bondeni na anataka kutuchukua sisi wote pamoja naye"

MEI 11, 2020
MAREKANI YARIPOTI VIFO ZAIDI YA 80,000. UHISPANIA YAREKODI VIFO VICHACHE

Marekani imerekodi jumla ya vifo 80,807 vya COVID19 huku ikiwa na jumla ya visa 1,387,047 kutoka katika Majimbo yote 50 na sehemu zilizochini ya nchi hiyo

Taifa hilo ambalo kwa sasa ndilo linaongoza kwa idadi ya vifo na watu walioathirika na virusi hivyo limerekodi jumla ya Wagonjwa 234,916 waliopona hadi kufikia sasa

Aidha, Uhispania imerekodi vifo vipya 123 na kwa mujibu wa Wizara ya Afya idadi hiyo ya vifo ni ndogo kutokea kwa ndani ya wiki 7. Jumla ya Vifo imefikia 26,774

Idadi ya visa nchini humo imeongezeka kutoka 224,390 kwa jana, Jumapili hadi visa 268,143 kwa siku ya leo Mei 11, 2020 huku idadi ya Wagonjwa waliopona ikifikia 177,846

Huko Uturuki, maduka, saluni za aina zote zimeruhusiwa kufunguliwa baada ya kufungwa kwa takriban miezi miwili huku nchi hiyo ikihimiza masuala ya usafi zaidi

Hadi kufikia leo, nchi hiyo imerekodi jumla ya visa 138,657, vifo 3,786 huku kukiwa na zaidi ya Wagonjwa 92,691 waliopona ugonjwa huo

URUSI YAREKODI VISA VIPYA 11,656. YAWA YA TATU KWA VISA VINGI ULIMWENGUNI

Urusi imeripoti visa vipya 11,656 leo, na kufanya nchini hiyo kuwa na jumla ya visa 221,344 na kuwa ya tatu Ulimwenguni kwa visa vingi nyuma ya Marekani na Uhispania

Mji Mkuu wa nchini hiyo, Moscow umeathirika zaidi ukiwa umeripoti vifo 658 vya COVID19 kwa mwezi uliopita huku jumla ya vifo 2,009 vikiwa vimerekodiwa nchini humo

Baadhi ya wakosoaji na wataalam wamesema kiwango cha chini cha vifo cha nchini humo kinaficha idadi ya kweli ya vifo vya COVID19 vinavyotokea

Pamoja na hayo, Urusi (Russia) imeripoti kuwa jumla ya Wagonjwa 39,801 walipona. Marekani imeripoti visa 1,387,047 huku Uhispania ikiwa na visa 264,663

MEI 10,2020
VISA ZAIDI YA MILIONI NNE VYAREKODIWA DUNIANI

Visa 4,120,788 vya COVID19 vimeripotiwa ulimwenguni huku wagonjwa waliopona wakiwa 1,388,920 na jumla ya vifo ikiwa 280,144

Marekani inaendelea kuwa nchi iliyoathirika zaidi ikiripoti maambukizi 1,369,245 na vifo 80,068 huku waliopona wakifikia 217,636

Mataifa mengine ni Uhispania (262,783), Italia (218,268), Uingereza (215,260) na Urusi (198,676)

Barani Afrika, taifa la Afrika Kusini limerekodi visa 9,440, Misri (8,964), Morocco (5,911), Ghana (4,263) na Nigeria (4,151)

MEI 09, 2020
BRAZIL: VISA ZAIDI YA 10,000 VYA COVID19 VYAREKODIWA NDANI YA SAA 24

Idadi ya vifo kutokana na virusi vya corona imefikia 9,897 huku kukiwa na kesi mpya 751, za vifo nchini Brazil

Wizara ya afya imeeleza kuwa idadi ya walioambukizwa imepanda zaidi hadi kufikia 145,328 huku kukiwa na zaidi ya maambukizi 10,000 ndani ya masaa 24 zilizopita

Brazil inakuwa ni kati ya nchi zilizoathirika zaidi Latin America

MEI 07, 2020
PAKISTAN: WIZARA YA AFYA YATANGAZA VISA VIPYA ZAIDI YA 1,500

Wizara ya Afya ya Pakistan imetangaza visa vipya 1,523 vya COVID19, idadi ambayo ni kubwa zaidi kuripotiwa ndani ya saa 24. Nchi hiyo ina visa 24,073 hadi sasa na vifo vimefikia 564 baada ya watu 38 kufariki dunia

Kwa mujibu wa takwimu za Kituo cha Uendeshaji wa Kitaifa (NCOC) maeneo yaliyoathirika zaidi na mlipuko wa Corona ni Punjab, Khyber Pakhtunkhwa na Balochistan. Idadi ya wagonjwa waliopona ni 6,464

Aidha, Kituo hicho kimeshauri masharti yaliyowekwa ili kudhibiti maambukizi ya CoronaVirus kulegezwa na huduma za usafiri kurejea nchi nzima kuanzia Mei 09 mwaka huu. Pia, kimejadili kuhusu kufungua biashara kabla ya sikukuu ya Eid

MAREKANI: VISA VIPYA ZAIDI YA 24,000 VYAREKODIWA

Kwa mujibu wa takwimu za Chuo cha John Hopkins, Marekani imerekodi visa vipya 24,252 vya COVID19 na watu wapatao 2,367 wamefariki dunia kwa siku ya Jumatano pekee. Marekani ina jumla ya maambukizi 1,228,603 na vifo 73,431 hadi kufikia sasa

Marekani imerekodi visa na vifo vingi kuliko nchi nyingine yoyote duniani lakini majimbo mbalimbali ikiwemo Colorado Florida na Georgia yamelegeza baadhi ya masharti licha ya Wataalamu wa Afya kuonya inaweza kusababisha visa kuongezeka

Aidha, imeripotiwa kuwa Mwanaume wa miaka 57 kutoka nchini El Salvador amekuwa mtu wa kwanza kufariki dunia kutokana na CoronaVirus akiwa mikononi mwa Uhamiaji (ICE). Alipata maambukizi kwenye kituo kilichopo San Diego, California na kupelekwa Hospitali ambapo alifariki

MEI 06, 2020
URUSI YAREKODI VISA VIPYA ZAIDI YA 10,000 KWA SIKU YA NNE

Ndani ya saa 24 zilizopita, Urusi imerekodi visa vipya 10,559 vya COVID19. Hii inakuwa siku ya nne mfululizo kwa taifa hilo kuwa na visa zaidi ya 10,000 kwa siku moja

Licha ya ongezeko kubwa la wagonjwa, Urusi imesema idadi ya wanaopoteza maisha imekuwa ndogo kwasababu mlipuko wa Corona Virus ulichelewa kuingia nchini humo tofauti na sehemu nyingine na Mamlaka zilipata muda wa kujiandaa

Urusi ina jumla ya visa 165,929 na waliofariki dunia ni watu 1,537. Rais Vladimir Putin ameagiza amri wa wananchi kutotoka nje kuendelea kutekelezwa mpaka Jumatatu

UJERUMANI: SHULE, MADUKA KUFUNGULIWA MWEZI HUU

Katika jitihada za hali kurejea kama awali, Ujerumani itafungua Shule na maduka yaliyokuwa yamefungwa ili kudhibiti maambukizi za CoronaVirus nchini humo

Taarifa ya makubaliano baina ya Kansela Angela Merkel na Wakuu wa Mikoa imesema Shule zinatakiwa kuendelea kufundisha wanafunzi huku tahadhari za usafi na ukaribu zikizingatiwa

Awali, Wanafunzi waliokuwa wakikaribia kufanya mitihani ndio waliruhusiwa kurudi Shuleni lakini kuanzia wiki ijayo, Shule za awali na msingi zitafunguliwa

Kuhusu maduka, wamesema yanaweza kufunguliwa ila yametakiwa kuzingatia usafi, kusimamia mahali watu wanapoingia na kuepusha foleni ndefu ya huduma

Aidha, mikusanyiko ya michezo, matukio ya utamaduni na matamasha bado imepigwa marufuku. Kuna uwezekano kuwa haitaruhusiwa mpaka Agosti 31 mwaka huu

Hata hivyo, Ligi Kuu soka nchini humo, Bundesliga iliyokuwa inatarajiwa kuanza Mei 15 haitaanza baada ya Kansela kusema Wachezaji wote wa Ligi hiyo lazima wakae Karantini kwa wiki mbili kabla Ligi kuendelea

Ujerumani imerekodi visa 164,807, vifo 6,996 na Waliopona 137,400 hadi kufikia leo

MEI 05, 2020
URUSI: VISA ZAIDI YA 10,000 VYAREKODIWA NDANI YA SAA 24

Urusi imerekodi visa vipya 10,102 vya COVID19 vilivyotokea ndani ya saa 24 zilizopita na hivi sasa maambukizi yamefikia 155,370. Hii inakuwa siku ya tatu mfululizo kwa nchi hiyo kuwa na visa 10,000 kwa siku

Mji Mkuu wa Moscow umetajwa kuwa kitovu cha mlipuko huo ikiwa na takriban nusu vya visa vyote vilivyorekodiwa. Meya Sergei Sobyanin ametahadharisha uwepo na maambukizi zaidi na kuwataka wananchi kuheshimu taratibu zilizowekwa

Urusi inakuwa nchi ya saba duniani kwa idadi kubwa ya maambukizi nyuma ya Ujerumani, Ufaransa, Uingereza, Italia, Uhispania na Marekani. Licha ya ongezeko kubwa la maambukizi, Urusi imerekodi vifo vichache ikilinganishwa na mataifa mengine. Waliofariki dunia ni watu 1,451

MEI 04, 2020
JAPAN: WAZIRI MKUU AONGEZA MUDA WA HALI YA DHARURA MPAKA MEI 31

Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe amesema ni mapema sana kulegeza masharti yaliyowekwa ili kudhibiti mlipuko wa CoronaVirus, hivyo Serikali imesogeza mbele hali ya dharura hadi Mei 31, 2020

Awali, Abe alitangaza hali ya dharura kwa mwezi mmoja kuanzia Aprili 07 mwaka huu katika Mji Mkuu wa nchi hiyo, Tokyo pamoja na mikoa mingine sita lakini baadae hali hiyo ilitangazwa kwa nchi nzima ya Japan

Hadi kufikia leo, Japan imerekodi visa vya 14,877 COVID19 huku idadi ya wagonjwa waliopona ikiwa 3,981 na waliofariki dunia ni 487

ITALIA YAANZA KULEGEZA MASHARTI

Nchi ya Italia ambayo imekuwa karantini kwa takribani miezi miwili imeanza kulegeza masharti yaliyowekwa ili kuthibiti maambukizi ya COVID19 ambapo kuanzia leo, Wananchi wataruhusiwa kutembea ndani ya miji waliopo

Inakadiriwa kuwa watu wapatao Milioni 4 watarudi kazini, migahawa itafunguliwa lakini itatoa huduma za kununua na kuondoka (Takeaway) pekee. Baa, Shule, sehemu za kufanya mazoezi (gym) zitaendelea kufungwa na wananchi wote wametakiwa kuvaa barakoa

Aidha, safari za nje ya mikoa hazitaruhusiwa na watu wataruhusiwa ikiwa ni kwa ajili ya kazi, sababu za kiafya na dharura.Masharti ya misiba nayo yamelegezwa na sasa watu 15 wataruhusiwa kuhudhuria. Mikusanyiko ya ibada na harusi bado imepigwa marufuku

Italia imerekodi maambukizi 210,717 hadi kufikia leo. Idadi ya wagonjwa waliopona ni 81,654 na waliofariki dunia ni 28,884

VISA ZAIDI YA MILIONI 3. 5 VYARIPOTIWA DUNIANI

Ugonjwa wa COVID19 umeathiri takribani watu 3,566,201 duniani kote. Hadi kufikia sasa, vifo 248,285 vimeripotiwa na idadi ya wagonjwa waliopona ni 1,154,023

Marekani imeathirikia zaidi na mlipuko wa CoronaVirus ambapo visa1,188,122 vimethibitishwa na idadi ya waliofariki imefikia 68,598. Mataifa mengine yaliyoathirika kwa kiasi kikubwa ni Uhispania (247,122), Italia (210,717), Uingereza (186,599) na Ufaransa (168,693)

Rais Donald Trump amesema anaamini kuwa chanjo ya Corona itapatikana hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu. Pia ameeleza kuwa anatamani kuona shule na vyuo vikifunguliwa mwezi Septemba

Naye Kiongozi wa Kanisa Katoliki Papa Francis amewashukuru watoa huduma muhimu na kutoa wito kwa Mashirika ya Kisayansi kuendelea kutafuta chanjo ya COVID19. Amesema endapo jaribio lolote likifanikiwa, chanjo inapaswa kupatikana duniani kote

Aidha, kwa bara la Afrika, nchi ya Afrika Kusini imerekodi idadi kubwa zaidi ya maambukizi (6,783) huku ikifuatiwa na Misri (6,465), Morocco (4,903), Algeria (4,474) na Nigeria (2,558)

MEI 03, 2020
CDC: MAFUA YANAUA ILA COVID19 NI HATARI ZAIDI, HAVIPASWI KUFANANISHWA

Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa cha Marekani (CDC) kimetoa sababu za kutofananisha mafua ya kawaida na COVID19 ili kuweka sawa wanaopinga na kutaka shughuli za kiuchumi ziendelee kwa kuamini mafua ni sawa na COVID19

Kituo hicho kimesema, Mafua ya kawaida yanaweza kuambukiza kwa wastani watu 1.28 wakati CoronaVirus huambukiza wastani wa watu 2 hadi 3.Pia, Mafua ya kawaida yana chanjo, CoronaVirus haina chanjo

Aidha, tafiti za CDC zinaonesha kati ya Oktoba 2019 hadi mwanzoni mwa Aprili 2020 mafua yameua wastani wa watu 331 kwa siku huku COVID19 kuanzia Februari 6 hadi Aprli 30, ikiwa imeua wastani wa watu 769 kwa siku huko Marekani

Pia, Mafua ya kawaida watu huugua siku moja hadi nne baada ya kupata maambukizi, na huchukua siku mbili kuonesha dalili jambo linaloweza kuwafanya wakae nyumbani mara tu wajihisi wagonjwa lakini COVID19 huchukua siku 4 hadi 5 kuanza kujionesha na kupevuka kwa dalili huchukua hadi siku 14

NOVEMBA 3
MEXICO YARIPOTI MAAMBUKIZI MAPYA ZAIDI YA 5,000

Mexico’s health ministry reported on Tuesday 5,250 additional cases of the novel coronavirus and 493 more deaths in the country, bringing the official number of cases to 938,405 and the death toll to 92,593.

The government has said the real number of infected people is likely significantly higher than the confirmed cases.
 
Afrika: Nchini Ivory Coast kuna taarifa ya kufanyika kwa vipimo vya afya kwa mwanamke mmoja anayehisiwa kuwa na maambukizi ya 'Coronavirus' muda mchache baada ya kuwasili nchini humo akitokea nchini China.

====
Coronavirus: Ivory Coast tests woman for China virus. [BBC]

Health officials are dealing with a suspected case of coronavirus in Ivory Coast, the country's health ministry has announced.

An unnamed student, who returned to the West African country from Beijing on Saturday, is undergoing further tests after showing flu-like symptoms.

If confirmed, it will be the first case of the deadly virus in Africa.
 
China imetangaza kuongezwa kwa likizo ya mwaka mpya nchini humo (Lunar New Year) ili kupunguza misongamano ya watu ikiwa ni juhudi za kuhakikisha kirusi hicho kinadhibitiwa.

====
China orders public holiday extended to curb epidemic [Al Jazeera]

Chinese authorities have ordered the extension of a public holiday in an effort to contain the coronavirus epidemic.

A working group chaired by Premier Li Keqiang to tackle the outbreak decided "to reduce population flows" by extending the Spring Festival holiday which had been scheduled to end on January 30, state news agency Xinhua said.

It was not immediately clear how long the extension is.

"The meeting stressed that the country is at a crucial time in the prevention and control of the novel coronavirus outbreak, urging Party committees and governments at all levels to take more 'decisive, powerful and orderly, scientific and well-planned' measures to effective curb the spread," Xinhua reported.
 
Taiwan imetangaza kujitolea kutoa msaada kwa China ili kuweza kukabiliana na kirusi cha Corona.

====
Taiwan offers help to China to help fight coronavirus. [Al Jazeera]

Taiwan's vice president-elect on Sunday offered help to rival China to fight the new coronavirus outbreak, as authorities in the island further tightened restrictions on visitors from China to prevent its spread.

"It is incumbent upon Taiwan to take part, and help China to solve this serious epidemic, so as not to allow it to continue to spread, and that the sick can get appropriate treatment to return to help," he said.

Taiwan has close economic and cultural links with China and has so far reported four cases of the virus.
 
MPYA: Idadi ya vifo nchini China imeongezeka na kufikia 80 mpaka sasa huku idadi ya wenye maambukizi ikifikia zaidi ya 2700 ikijumuisha Hong Kong, Macau pamoja na Taiwan.

====
UPDATE: Coronavirus: China death toll climbs to 80 with more than 2,700 cases. [The Guardian]

Death toll in China has risen to 80, according to the National Health Commission (NHC). This is up from 56 yesterday. The NHC also says there are more than 2,700 infections reported (note that the commission has included Hong Kong, Macao and Taiwan in this number).

The news comes as the head of the World Health Organization, Tedros Adhanom Ghebreyesus, flies to Beijing to discuss the outbreak with authorities.
 
Muendelezo wa matukio kutokana na kirusi cha Corona tokea Jumatano wiki iliyopita mpaka Jumapili ya jana tarehe 26. Hii ni kwa mujibu wa siku taarifa ziliporipotiwa na si siku ya vipimo vilipofanyika;

SikuIdadi ya maambukizi mapyaIdadi ya vifo
Jumatano, Jan 22​
232​
11​
Alhamisi, Jan 23​
111​
1​
Ijumaa, Jan 24​
467​
16​
Jumamosi, Jan 25​
631​
14​
Jumapili, Jan 26​
731​
25​
 
MPYA: Kutoka nchini Cambodia, taarifa kutoka wizara ya afya imeeleza kuhusu uwepo wa mtu wa kwanza kabisa nchini humo kubainika kuwa na maambukizi ya 'Coronavirus'.

====
Cambodia's health minister confirms the country's first case of coronavirus. [Sky News]
 
CORONAVIRUS UPDATE:

Deaths

  • China 81

Confirmed cases
  • China 2700
  • Thailand 8
  • US 5
  • Australia 5
  • Taiwan 5
  • Japan 4
  • Singapore 4
  • South Korea 4
  • Malaysia 4
  • France 3
  • Vietnam 2
  • Cambodia 1
  • Nepal 1

[VOA/AFP]
 
MPYA: Rais wa Marekani, Donald Trump ame-tweet;

"Tuko kwenye mawasiliano ya karibu sana na China kuhusu kirusi hicho. Wachache sana wameripotiwa kuambukizwa ndani ya Marekani, lakini wapo katika uangalizi mkubwa. Tuko tayari kwa China na Rais Xi kutoa msaada wowote ambao ni muhimu. Wataalamu wetu ni wa ajabu!" - Donald J. Trump

====
"We are in very close communication with China concerning the virus. Very few cases reported in USA, but strongly on watch. We have offered China and President Xi any help that is necessary. Our experts are extraordinary!" - Donald J. Trump

1580138120677.png
 
MPYA: Beijing, China imetangaza kifo cha kwanza kabisa katika jiji hilo kutokana na kirusi cha Corona, mwanamume wa miaka 50 aliyekuwa amesafiri kwenda Wuhan tarehe 8, Januari na kurejea jijini Beijing tarehe 15.

====
Beijing has reported its first death from coronavirus. The patient was infected on January 22nd. [JPost]
 
Back
Top Bottom