Kuna taratibu zingine za kijinga na hazina tija yeyote kwa taifa. Hivi Ewura hapo inataka kusikiliza nini ama ndiyo vikao vys ulaji? Professor Muhongo alishasema Tanesco inazalisha na kutoza gharama mara mbili yake akimaanisha kama gharama ya uzalishaji ni shilingi 9/= kwa unit, Tanesco wanauza umeme huo kwa shillingi 18/= alisema hiyo ni super profit na alisema Tanesco lazima washushe bei. Kwa Ewura kutaka maoni ya wananchi us just no sense. Kama wakisema wanataka kuongeza kiwango cha kushusha bei, hapo naweza kuelewa, hata tukianza na 10% ni sawa, Tanesco bado watakuwa wanatengeneza faida kama siyo madudu yao ya mikataba mibovu. Hata hivyo, siyo suala la kuvutia pumzi, all the fact are out there on cost of production per unit, Ewura should move fast on this one.