Ewe Raia mwema wa Tanzania usidanganyike, tii Sheria bila shuruti, zingatia wito na uamuzi wa Mahakama na Wananchi kwa hekima na busara

Tlaatlaah

JF-Expert Member
May 18, 2023
19,909
21,910
Ni uzalendo wa maana sana kuitikia wito wa dola, kutii maelekezo, ilani au amri za vyombo vya ulinzi na usalama bila ukaidi, ubishi wala kiburi kwa mujibu wa sheria na katiba ya nchi..

Jitahidi sana uwe Raia mwema siku zote, muungwana, mzalendo, mtiifu kwa sheria na katiba ya nchi, na kutoa ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama ikihitajika, kamwe usikubali kuchochewa, kudanyanywa au kuhamasishwa na viongozi wa kisiasa wenye viburi na jeuri kwa dola, na wenye dhamira ya kuhatarisha au kuvuruga umoja, amani na utulivu wa wengine.

Usikubali kufundishwa ukaidi, jeuri na kiburi kwa Dola. daima, kumbuka akili za kuambiwa, ni vizuri ukanchanganya na zako.

Daima jitenge dhidi ya ukaidi kwa dola, kwasababu utaumia na utapata tabu sana ukiwa mwenyewe pekeyako na utalazimishwa kutii na kuheshimu katiba kwa shuruti na nguvu inayoweza kukusababishia madhara kimwili au kiakili.

kutii Sheria bila shuruti ndio mpango mzima wa amani na salama yako..🐒

Mungu Ibariki Tanzania
 
Tatizo sheria zenyewe zimekuwa sheria za uovu kama sheria za shetani . Vyombo vya usalama vimegeuka kuwa vyombo vya kuteka raia . Hapa raia wana wajibu wa kukaidi sheria ovu .

"When injustice becomes law , resistance becomes duty ." - Thomas Jefferson
 
Tatizo sheria zenyewe zimekuwa sheria za uovu kama sheria za shetani . Vyombo vya usalama vimegeuka kuwa vyombo vya kuteka raia . Hapa raia wana haki ya kukaidi sheria ovu .

"When injustice becomes law , resistance becomes duty ." - Thomas Jefferson
huo ni upotoshaji,

vyombo imara na vya kisasa vya ulinzi na usalama nchini vipo kwaajili ya kulinda umoja, amani, utulivu na usalama wa watu, mali zao na makazi ya wananchi na waTanzania wote...

ni upotoshaji na uchochezi chuki dhaifu na usio na madhara yoyote dhidi ya vyombo hivi muhimu vya kiuchunguzi na kiusalama..

nitoe wito kwa raia mwema yeyote mwenye taarifa zitakazowezesha kuwatia nguvuni wahalifu wa aina mbalimbali ili nchi yetu iendelee kufurahia matunda ya Amani yaliyopo 🐒
 
Hivi tanzania kuna taasisi zinaruhusiwa kuua,hata kama una kidomodomo...

Ova
nadhani kwa hisia binafsi, chuki binafsi, mihemko na ghadhabu unaweza kutuhumu taasisi au mtu yoyote kuhusika na unachofikiri,

lakini kiuhalisia hakuna zaid ya Mungu Mwenyezi Mwenyewe kuamua hatma ya kila mja wake humu duniani..

full stop!🐒
 
huo ni upotoshaji,

vyombo imara na vya kisasa vya ulinzi na usalama nchini vipo kwaajili ya kulinda umoja, amani, utulivu na usalama wa watu, mali zao na makazi ya wananchi na waTanzania wote...

ni upotoshaji na uchochezi chuki dhaifu na usio na madhara yoyote dhidi ya vyombo hivi muhimu vya kiuchunguzi na kiusalama..

nitoe wito kwa raia mwema yeyote mwenye taarifa zitakazowezesha kuwatia nguvuni wahalifu wa aina mbalimbali ili nchi yetu iendelee kufurahia matunda ya Amani yaliyopo
Hao wahalifu wakiwa wanatoka humo kwenye hivyo vyombo taarifa ukatoe wapi, kwako? Jeshi la Polisi kila taarifa ikitoka ya hali ya rushwa Nchini, wao hushika nafasi ya kwanza kila mwaka, taarifa hii wewe unaweza kuifanyia kazi hili jeshi likarudi ktk uadilifu?. Ni Umoja gani vinalinda ikiwa vinakuwa vinara vya uhalifu kila wakati? Hivyo vyombo ndio vinavyotuhumiwa kwa mauaji, upotevu wa watu, utesaji, ww una uwezo gani wa kuvirekebisha? Au ndo uchawa kila mahali ambapo sasa imekuwa fasheni?
 
nadhani kwa hisia binafsi, chuki binafsi, mihemko na ghadhabu unaweza kutuhumu taasisi au mtu yoyote kuhusika na unachofikiri,

lakini kiuhalisia hakuna zaid ya Mungu Mwenyezi Mwenyewe kuamua hatma ya kila mja wake humu duniani..

full stop!🐒
Acha kumsingizia Mungu, Mungu haamui maovu na hafurahii kifo cha mwenye dhambi, mnauwa mnateka halafu mseme mipango ya Mungu? Ona aibu basi
 
tuhuma ni hisia tu gentleman,

na saa zingine zinachochewa tu na wanasiasa wenye chuki na hasira ya kukataliwa na wananchi kwenye kura, lakini pia wanasiasa waliofilisika hoja na wanaharakati uchwara...

hakuna ukweli wowote juu ya hisia za chuki zinazojengwa dhidi ya vyombo vya Ulinzi na usalama nchini, unless una imani haba au mwepesi sana kuamini mambo ya uongo au ushirikina yanayosambazwa kwa sasa hasa na wapinzani wa serikali nchini 🐒

hata hivyo,
pamoja na na tuhuma hizo za chuki, uongo na upotoshaji, bado vyombo vya ulinzi na usalama ndio tegemeo na kimbilio la umoja, amani na utulivu wa wananchi Tanzania..

vyombo vya ulinzi na usalama nchini, vitaendelea kufanya kazi kwa bidii, usiku na mchana na kuwahakikishia waTanzania wote usalama wao, mali zao na makazi ya kwa usawa, haki na uhakika kabisa 🐒
 
Ni uzalendo wa maana sana kuitikia wito wa dola, kutii maelekezo, ilani au amri za vyombo vya ulinzi na usalama bila ukaidi, ubishi wala kiburi kwa mujibu wa sheria na katiba ya nchi..

Jitahidi sana uwe Raia mwema siku zote, muungwana, mzalendo, mtiifu kwa sheria na katiba ya nchi, na kutoa ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama ikihitajika, kamwe usikubali kuchochewa, kudanyanywa au kuhamasishwa na viongozi wa kisiasa wenye viburi na jeuri kwa dola, na wenye dhamira ya kuhatarisha au kuvuruga umoja, amani na utulivu wa wengine.

Usikubali kufundishwa ukaidi, jeuri na kiburi kwa Dola. daima, kumbuka akili za kuambiwa, ni vizuri ukanchanganya na zako.

Daima jitenge dhidi ya ukaidi kwa dola, kwasababu utaumia na utapata tabu sana ukiwa mwenyewe pekeyako na utalazimishwa kutii na kuheshimu katiba kwa shuruti na nguvu inayoweza kukusababishia madhara kimwili au kiakili.

kutii Sheria bila shuruti ndio mpango mzima wa amani na salama yako..🐒

Mungu Ibariki Tanzania
Waliotii sheria bila shuruti ,ndio hao tunasikia hawapo leo
 
Tatizo kubwa ni ukosefu wa akili ya kuweza kuchanganua mambo kwa usahii. Utawala wa Sheria unataka kufuatwa kwa Sheria na kila mtu vikiwemo hivyo vyombo vya dola. Tukiweza hili hata maendeleo endelevu yatafikiwa wa urahisi.
Tangia walipokaingiza kaneno 'tii sheria bila shuruti' ndipo maovu tunayoyasikia yalipoanza Mkuu.
 
Acha kumsingizia Mungu, Mungu haamui maovu na hafurahii kifo cha mwenye dhambi, mnauwa mnateka halafu mseme mipango ya Mungu? Ona aibu basi
ona aibu wewe unaechanganya mambo...

kwa hisia na imani yako potofu na huenda ya kishirikina unaweza hisi taasisi au mtu fulani ndie kafanya uhalifu Fulani...

lakini kiuhalisia,
anaeamua hatma yako na yangu ni Mungu Mwenyezi Mwenyewe bila mbambamba ya mtu yeyote...

sasa unakuja hapa una manga manga na chuki na mihemko yako binafsi dhidi ya ukweli ati sijui nini na nini huko, hiyo ni ushirikina useless kabisa, peleka huko kwenu 🐒
 
Waliotii sheria bila shuruti ,ndio hao tunasikia hawapo leo
wito wa vyombo vya ulinzi na usalama ni kushirikiana na raia wema kama wewe ili hatimae kuwezesha ambao unasema hawapo hatma yao ifahamike tangu mwanzo 🐒
 
nadhani kwa hisia binafsi, chuki binafsi, mihemko na ghadhabu unaweza kutuhumu taasisi au mtu yoyote kuhusika na unachofikiri,

lakini kiuhalisia hakuna zaid ya Mungu Mwenyezi Mwenyewe kuamua hatma ya kila mja wake humu duniani..

full stop!🐒
H7jawahi kusikia mtu ambaye ni mhalifu sugu mwisho wa siku inatoka amri ya kumtoa uhai
Unajuwa hiyo huwa inafanyikaga

Ova
 
wito wa vyombo vya ulinzi na usalama ni kushirikiana na raia wema kama wewe ili hatimae kuwezesha ambao unasema hawapo hatma yao ifahamike tangu mwanzo 🐒
Niliwahi kushirikiana nao, mbaya zaidi nilipokuwa napigiwa simu na kuambiwa si unajua mambo hayajakaa sawa, kama una chochote fanya mpango.
 
Kama Mungu ndiye muamuzi Wa hatima za watu basi atakuwa mkatili sana wakati Fulani. Angalia watoto wakipalestina wanavyokatwa vipande na mabomu kila siku. Wale watoto wamemkosea nini huyo Mungu hadi awapangie hatima mbaya kiasi kile?
Yes,
ndio maana nimeeleza kinagaubaga kwamba kwa hisia za chuki binafsi, mihemko na ghadhabu unaweza kutuhumu taasisi au watu unaowadhania kuangamiza wengine kumbe sio....

ghaza sio suala la kudhania au la kificho, yanafanyika mchana kweupeee, na nadhani kwa watu wa dini ya kikristo mambo yale vita yako kwenye bibilia na wao wanaweza kueleza vizuri...

hata hivyo hatma ya kuzaliwa na kufa kwa mwanadamu awae yeyote iko mikononi mwa Mungu Mwenyezi Mwenyewe 🐒
 
nadhani kwa hisia binafsi, chuki binafsi, mihemko na ghadhabu unaweza kutuhumu taasisi au mtu yoyote kuhusika na unachofikiri,

lakini kiuhalisia hakuna zaid ya Mungu Mwenyezi Mwenyewe kuamua hatma ya kila mja wake humu duniani..

full stop!🐒
Kwani wale wafanya biashara wa mahenge walivyowakamata waliwafanya nini,waliwapeleka picnic au kutembea 😄
Mwanangu we polisi uione hivyo hivyo juu juu

Ova
 
ona aibu wewe unaechanganya mambo...

kwa hisia na imani yako potofu na huenda ya kishirikina unaweza hisi taasisi au mtu fulani ndie kafanya uhalifu Fulani...

lakini kiuhalisia,
anaeamua hatma yako na yangu ni Mungu Mwenyezi Mwenyewe bila mbambamba ya mtu yeyote...

sasa unakuja hapa una manga manga na chuki na mihemko yako binafsi dhidi ya ukweli ati sijui nini na nini huko, hiyo ni ushirikina useless kabisa, peleka huko kwenu 🐒
Umbake mtoto mpaka afe halafu Mungu awe ameamua hiyo hatima? Jambazi mkubwa wewe, Kwahiyo Mungu ndiye aliyewatuma Wale waliomuua Asime? Mungu ndiye aliye waagiza wale waliomtandika Lisu zile risasi? Acha uchawi mkuu, hata kama unalipwa lakini kulipwa huko kusikufanye uwe Boga namna hiyo tumia akili kidogo. Mipango mfanye na kuratibu nyie halafu mmsingizie Mungu
 
Niliwahi kushirikiana nao, mbaya zaidi nilipokuwa napigiwa simu na kuambiwa si unajua mambo hayajakaa sawa, kama una chochote fanya mpango.
pole sana,
huenda ilikua ni zamani sana vyombo hivyo vilikua havina uewezo mzuri wa kiuchumi ukilingasha na sasa 🐒
 
Ni uzalendo wa maana sana kuitikia wito wa dola, kutii maelekezo, ilani au amri za vyombo vya ulinzi na usalama bila ukaidi, ubishi wala kiburi kwa mujibu wa sheria na katiba ya nchi..

Jitahidi sana uwe Raia mwema siku zote, muungwana, mzalendo, mtiifu kwa sheria na katiba ya nchi, na kutoa ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama ikihitajika, kamwe usikubali kuchochewa, kudanyanywa au kuhamasishwa na viongozi wa kisiasa wenye viburi na jeuri kwa dola, na wenye dhamira ya kuhatarisha au kuvuruga umoja, amani na utulivu wa wengine.

Usikubali kufundishwa ukaidi, jeuri na kiburi kwa Dola. daima, kumbuka akili za kuambiwa, ni vizuri ukanchanganya na zako.

Daima jitenge dhidi ya ukaidi kwa dola, kwasababu utaumia na utapata tabu sana ukiwa mwenyewe pekeyako na utalazimishwa kutii na kuheshimu katiba kwa shuruti na nguvu inayoweza kukusababishia madhara kimwili au kiakili.

kutii Sheria bila shuruti ndio mpango mzima wa amani na salama yako..🐒

Mungu Ibariki Tanzania
Vipi kuhusu hao wa Noah nyeusi na gari zenye namba bandia wanaokamata watu bila kuwapeleka Polisi?
 
Back
Top Bottom