Eti unitapeli kwa namna hii!!!

daaah saa kumi na moja na nusu nilipokea SMS kama hii, sema mwishoni kaniambia sijui nikachukue madudugani kama mauganga hiv yamebaki kidogo, na siyo mara ya kwanza kutumiwa, huwa nadhan labda amekosea number
 
Na mimi walinitumia hii hii SMS sijui walijuaje maana miezi sita nyuma nilimwelekeza jamaa angu kwa mganga
Hahahah jamaa inaonekana wanaotea otea..hasa term hii maisha yalivyokuwa magumu kuna wengine wakiziona hizi jumbe wanaona basi wamepata ufumbuzi.
 
mimi anipe hiyo radi tu nitembee nayo... halaf namtongoza demu mkaliiiiiii... akikataa tu nampiga nayo kwenye wowowo lake awe flat screen...!!!!
 
Maskini kuna watu hawapo jamiiforums na pengine hawana smartphone za kuwawezesha kufunguka juu ya huu utapeli sasa sipati picha niwangapi mpaka sa hivi wanaendelea kulizwa
 
Wakikutumia ujumbe tafadhali usijibu. Ukiwapa nafasi ya kuwajibu UMELIWAA. Mimi imewahi kutokea hii mwaka juzi. Zipo njia 2 wanatumia, kukutumia ujumbe au kukupigia simu na utashangaa wanakujua mpaka jina nafikiri wakati mwingine wakishachagua namba ya kuitapeli wanafanya muamala wa pesa kuangalia unatumia jina gani... Wamefanikiwa kwa hilo. Hii style ya kupigiwa simu imewaliza watu wengi ambao bado hawajajua aina ya utapeli huu. Hazijapita siku nyingi kuna dogo anaishi Dodoma katapeliwa kwa style ya kupigiwa simu. Jamaa wamepiga simu wakamwambia tuko Arusha tunaomba tufanye biashara, wewe uko wapi? Dogo akajibu nipo Dodoma. Wakamwambia kuna deal la milioni 5; tunaomba ututumie laki moja then tufakifanya biashara tutapata faida ya milioni 3. Dogo kaingia kichwa kichwa kalizwa na matukio kama haya yanatokea sana wakati mwingine ushirikina unatumika kuteka akili za watu.
 
Back
Top Bottom