Eti! jamani ni halali kweli kwa askari wa barabarani kumpiga 30000 mwalimu wa shule.

Jindal Singh

JF-Expert Member
Sep 9, 2015
1,857
1,538
Salaam jf.
Ivi hawa askari wa barabarani hawaoni aibu kwa wafanyakazi wa umma?. Leo nimeshuhudia mwalimu akilalamika kwa askari akidai asimuandikie, baada ya kuambiwa kuwa amezidisha spidi, aisee! mwalimu alilalamika kwelikweli akisema ''jamani mie mzalendo mwenzenu'' jamaa kakomaa atakikusikia lolote, ticha ikabidi atoe kiroho upande. Sasa mimi ndo najiuliza ivi! maisha ya walimu si ndio sawa na maisha ya askari sasa mbona hawahurumiani wote si ndo wazalendo?
 

Mkuu no offence..sheria haijabagua vyeo au aina ya kazi kwa mtu anayefanya kosa barabarani..mimi sijaona kosa la huyo askari endapo kama mwalimu alizidisha speed kiukweli.Suala ni kwamba maboresho ya maslahi ya wafanyakazi wenye kipato cha chini yafanyike na si kutetea kosa.
 
Ndioo ni halali kama ana kosa
 
Wamepangiwa hesabu, halafu mwl na askari naona kama vile hawaiviani kabisa...
 
"Ukweli ni kwamba, unapokunywa bia moja ni sawa umekula matofali 2 ya kujengea kama utatumia tofali la 6inch kujengea, kwani bia 1 ni wastani wa tsh,2500 na tofali moja la watu grade ya chini ni tsh. 1200-1500 plus usafiri. Na kwakuwa wanywaji voltage hazipandi mpaka upige zaidi ya bia moja yaani lazima upige nyingi nyingi (na zile za ''waiter wazungushie!'') hapa kwa wiki unaweza kunywa kama bia 35, ukizidisha mara 1month unapata bia 140 ambazo ni sawa na tsh. 350000 ambazo unaweza pata tofali wastani wa 300, hivyo kwa kila mwezi utakuwa unaingiza tofali 300, Kwa mwaka utakuwa unaingiza tofali 3600 sawa na nyumba kamili (Self container) ya kupangisha. Hisabu hii ni kwa wanywaji daraja la kati".
Mkuu Jindal Singh inaonekana kwako uchumi hata wa basic hupiga? naona huelewi kitu kinatwa ECO system mkuu wala social interaction kwako ni kinyume, watu wanakunywa bia na nyumba zinajengwa. sema sisi wazinzi ndiyo hatuna maendeleo.
 
Akisababisha ajali na speeding yake kuwa mwalimu kutasaidia kupunguza maafa?

Wengine wanaoandikiwa faini ni madereva tu wana mshahara mdogo kuliko mwalimu.
 
Kwangu mimi naona hivyo sababu hata njaa kali lakini ukienda kwenye viwanda vya bia magunia kibao ya nafaka.
 
Kosa halina mwenyewe... Sheria ni msumeno.... Kifo hakichagui kama wewe ni mwalimu wa darasa au mwalimu wa tuition...
 

Sheria ni kwa ajili ya watanzania wote na siyo kwa walimu peke yao hivi mwalimu angefundisha wakati mabomu yakipigwa? vitu vingine angalieni mnavyosema sheria za usalama barabarani ni kwa watu wote wanatakiwa kuzifuata.
 
Endeleeni kujidanganya tu hivi unadhani huyo askari angemwandikia askari mwenzie hiyo faini?
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…