Hebu tujadili kidogo kama wahanga wa escrow hizi mbili.
Kwa wale wasahaulifu niwakumbushe lile sakata lililofanya bunge kuvunja record ya kufanya kaz mpaka usiku wa manane. Lilihusu escrow ya tanesco kuibiwa kias cha sh bilion 300 hivi. japo mpaka kesho hakuna kiongozi anayesema tuliibiwa.
Sasa kuna uhaba wa sukari uliopelekea kupanda bei had kufikia sehem zingine had sh5000, zingine 3000. Kutoka bei ya awali sh1800. Japo napo ilikua inauzwa 2000.
Kwann ilipanda?? Wengi wenu mnjaua. Hii ilitokana na kaui ya mkuu wa nchi kupiga marufuku uagizaji sukari toka nje. Had sasa hali si shwari pamoja na sakasaka yote ile kwa wafanya biashara at wameficha!! sijui haijapatikana!!
Sasa nije kwenye hoja yangu. Tamko la mkuu limetolewa tar 8 murch. Mpaka sasa ni takrban miezi 5. Mnajua ni kias gani kimepotea mpaka sasa??
Tupige hesabu uchwara kidogo.
Tz tuna raia milion 50. Mie nazigawa katika familia ya watu wanne wanne. Tunapata familia milion 12.5. Hawa watu wamepata ongezeko la sukari kwa kila kilo sh 1000. Achilia mbali wanaonuna zaid ya 3000.
Hawa watakua wamepoteza sh bilion 12.5 siku wakinunua. Nagawa mwez kwa siku tano kilo moja itakua imeisha kwa matumizi kwa familia na kuwafanya wanunue tena. hivyo kuwafanya kwa mwezi kununua mara 6. Njoo nami hapa chini.
Milioni 12.5*1000=bilion 12.5 kwa siku tano!!
Bilion 12.5 *6. =bilion 75 wa mwezi hupotea. tukiendelea hv na mwez ujao na kutimiza miez 6tutapoteza bilion 450. Ila mpaka sasa tumepoteza bilion 375 ambazo ni nyingi kuliko escrow ya tanesco. Tukitimza mwaka tutapoteza bilion 900. huku escrow ya tanesco ilikua ni takrban billion 300 tu. na tusipoangalia tutajikuta hii ya sasa ndio itakua bei yetu ya kudumu na kuzd kupoteza hela zetu . japo hakuna mhasibu anayejumlisha lakn tutapoteza trillion nying na hakuna atakaye jari.
Ndugu wananchi mnajua hiz pesa zingekua mifukoni mwetu kama maagizo haya ya kukurupuka yasingetokea?? Je viongoz mnampango gani kunusuru hali hii?? Mara nyingi tunakua wakali tukisikia mtu kaiba serikalini na kufuatilia nn kitatokea kwa huyo mwizi lakn sion uchungu kutupata pale tunapoibiwa moja kwa moja sisi wenyewe kupitia mfumo mbovu. Tunaishia kukaa kimyaaaa!!
Kwa wale wenye kupinga mje na data niki kiasi gan hatujapoteza mpaka sasa,
na sio mje na hoja za jumla jumla huku watu tunaumia. maana kuna watu wanasifia viongoz hata kama wamekosea.
Kama mm nimekosea weka data zako zilizo sahihi kama mpaka sasa tumepoteza elfu kumi tu sawa, ila uwe na data. ipi ina athari kwetu esrow ya tanesco na esrow ya sukari?? ipi itapoteza hela nyingi kati ya escrow ya taesco na ya sukari??
karibu tujadili kwa hoja.