Erolink arobaini yao imefika, sasa wamepigwa chini

Mataa ya Morocco kama unaelekea Mwenge, kuna mtaa wa kwanza unaingia kulia. Ambao ukishuka nao moja kwa moja unakutana na barabara ya migombani inayoshuka kutokea Drive In (Zantel kwa sasa). Huo Mtaa ndio unaitwa Ursino.
Kila lenye kheri.
Mkuu asante sana.
 
Google inaweza ikawa msaada pia, hata wewe umemsaidia pia shukrani, mi Daslam wakuja
Sio kila mtu anaweza kutumia Google. Mfano halisi ni wewe Nguli wa Google lakini umeiona Ursino iko Oysterbay. Kutoa maelekezo hakuhitaji wakuja au wa mjini.....ni busara na ustaarabu ndio msingi wa kila Mtanzania. Siku njema.
 
Kama Erolink imefutwa kazi amepewa ISON BPO. Hapo ni sawa na kuruka mkojo kukanyaga mavi.

ISON ndio wana deal na Call centre ya Airtel. Ukimpata cust care agent wa Airtel muulize atakueleza vizuri. Kuna dogo alikuwa huko ni balaa. Ni kampuni ya manji inaendeshwa na wahindi toka india. Hapo vijana wa vodacom call centre andikeni maumivi zaidi
 
Huu ni ubinafsi, kwani wengine hata hatujui hao mnaowasema ndio kina nani daaahhh.
Ukitaka kazi za kupokea simu nenda Infinity mtaa wa ursino almaarufu mtaa alioishi Raisi mstaafu Kikwete zamani.
Nenda Quality plaza almaarufu kwa manji kampuni ya Ison BPO ina ofisi peleka maombi ya kuomba kazi ya kupokea simu. Sijui hujaelewa nini hapo
 
Ukitaka kazi za kupokea simu nenda Infinity mtaa wa ursino almaarufu mtaa alioishi Raisi mstaafu Kikwete zamani.
Nenda Quality plaza almaarufu kwa manji kampuni ya Ison BPO ina ofisi peleka maombi ya kuomba kazi ya kupokea simu. Sijui hujaelewa nini hapo
kumbe ndio kazi yao mkuu..shukrani
 
Kwani mkuu Client wao walikuwa Vodacom pekee..? huko kwingine walikobakia wanaendelea na mambo yao kama kawaida
Kwa Tanzania naona INFINITY ndio recruitment Agency inayojari staff wake kwa mshahara mzuri na mikopo, pia ongezeko la mshahara kila mwaka na wana mtaji mkubwa hata client akichelewesha salary wao hufanya malipo na baadae kupokea kutoka kwa client.....Nawapongeza hawa wengine naona ni shida tu
Hao infinity ofisi zao ziko wap dsm??
 
Hawa jamaa walikuwa wanajifanya miungu wangu wasiojali wala kuwa na ubinadamu wowote.

Wakifikiri kazi zitadumu milele. Wametuibia sana, michango yetu ya katika mifuko ya jamii walikuwa hawapeleki kwa wakati bali walikuwa wanazungusha pesa zetu hadi udai ndio wanakuwekea. Ukiumwa hawalijui hilo wala ukiuguza.

Kuna wakati walimpa ruhusa mwezetu kumpeleka mama yake India kutibiwa aliporudi wakamfukuza kazi eti kapitisha muda na ukweli ni jinsi matibabu yalivyokuwa magumu, wamefukuza watoto kwa chuki za kijinga, HR wamekuwa wakidhulumu masaa ya wakufanya kazi ya staff, ngono ndio usiseme, wamekula bonus za staff hadi kichefuchefu bila kujua yuko Mungu.

Arobaini yao imefika sasa wamepigwa chini na wamepoteza wafanyakazi takribani wote wa call centre na kuchukuliwa na muajiri mwingine.

Dhuluma huchuma dhambi, nendeni mkaanze upya.
Nan kachukua tenda ya voda upande wa customer care mkuu?? Tupeleke cv
 
Hizo Agency zote ni vichomi tu,as long kuajiriwa kunahusika malalamiko yataendelea mpk mwisho wa dunia.
 
Mataa ya Morocco kama unaelekea Mwenge, kuna mtaa wa kwanza unaingia kulia. Ambao ukishuka nao moja kwa moja unakutana na barabara ya migombani inayoshuka kutokea Drive In (Zantel kwa sasa). Huo Mtaa ndio unaitwa Ursino.
Kila lenye kheri.
Mkuu nimefanikiwa kufika. Ubarikiwe sana
 
Back
Top Bottom