Dr wa Manesi
JF-Expert Member
- Aug 19, 2024
- 349
- 571
Kila siku humu ni mashindano tu ya kuvutia utukufu wa Mungu upande wao. Waisrael wa Simiyu wakinadi kwa nguvu zote jinsi Wana wa Israel walivyobarikiwa na kwamba ole wake kwa yeyote atakayewapinga basi atapata tabu. Biblical references kama zote hutolewa. Wale Waarabu wa Nanjilinji nao hawako nyuma, huko Kuna taarifa za kubarikiwa wao tu na kwamba ndo Kuna usahihi wa Kila wanachokifanya. Qur'anic references zinamwagwa pia. Maamuma tunabaki hoi.
Huko waliko Waisrael na Waarabu wenyewe halisi Kuna ugomvi, wa miaka na miaka....hauishi. Wanachogombania haswa, kiukweli, wanakijua wao zaidi. Waisrael wa Simiyu na Waarabu wa Nanjilinji wameubeba ugomvi na wao Sasa wanaokesha tu humu wakipigana kwa vijembe vyenye kutetea Waisrael na Waarabu halisi huko mashariki ya kati katika ugomvi huo Huku wakichambua kwa kina sababu ya ugomvi huo kuliko wenyewe unaowahusu. Wanabishana na kugombana mpaka vipwenene vinawatoka na kuwamwagika. Kubwa katika vita yao hawa Waisrael wa Simiyu na Waarabu wa Nanjilinji, ni madai ya kubarikiwa kwa hao 'mabwana' zao. Hapo ndipo nami ninaposhindwa na kuamua kujitokeza kidogo....
Baraka ni nini?!!! Kwa uelewa wangu mfupi, vyovyote utakavyosema, ni kustawi, kupendeza, kuongezeka n.k kwa kitu katika nyanja mbalimbali za kimaendeleo ya maisha vikiwemo amani na hata uhai (kiimani). Je, kwao (huko kwa mabwana zao), Kuna ustawi wowote unaoendelea?!!! Kwenye baraka watu hukimbilia, je, huko kwa mabwana zao watu hukimbilia?!!!
Historia inatuambia kwa mamia ya miaka, Waisrael walihangaika na kuteseka vibaya Huku wakitangatanga Huku na kule bila kuwa na eneo Moja la kutulia Huku wakiteswa vibaya na wenyeji wao (wajerumani wa kipindi Cha Hitler wakiongoza). Baada ya kupata nchi yao 1948 mapigano na majirani hayajaisha mpaka Leo na hata hakuna dalili ya kuisha kwa mapigano hayo maana yanakwisha na kuanza tena.......yamekuwa endelevu. Kwa upande wa Waarabu (majirani wa Waisrael), hawa nao wapo kwenye mapigano ya aina mbili; wenyewe kwa wenyewe wanalipuana Kila siku na kwa miaka tele na pili ndo hiyo vita yao na Waisrael.
Waisrael na Waarabu hawa, sababu ya mapigano yasiyoisha, kwao Kila siku ni wasiwasi.....kujificha hapa au pale. Kuingia handaki hili au lile. Kuwazika hawa au wale. Majengo yanaharibiwa. Watu wanakuwa vilema. Wageni hawafikirii kwenda. Wenyeji nao wanatafuta kwa kwenda. Familia zinapoteana. Viongozi wanakuwa na makazi ya ziada nje kama tahadhali. Miundombinu ya maji nk inaharibiwa Kila siku. Watu hawachezi (mechi kadhaa za mipira zimewahi kughailishwa Israel sababu ya ukosefu wa usalama)......shida, shida, shida. Eti, nyie Waisrael wa Simiyu na Waarabu wa Nanjilinji, mbarikiwa gani anakuwa kwenye mateso hivi?!!!!!!
Kwangu Mimi, mataifa yaliyobarikiwa ni kama haya hapo;
-Qatar (dalili ya baraka zipo wazi kabisa Huku......)
-Uswatini
-Tanzania n.k
Huko kwa mabwana zenu hakuna baraka zozote, mnatupiga na kitu kizito kichwani.

- Amerika, Huku Kila raia duniani anatamani kukimbilia.
- Nchi kadhaa za ulaya
- Saudi Arabia (daima baraka zipo upande wao na watu hukimbilia huko)
- U.A.E