EDO KUMWEMBE WEWE NI SENIOR..LAKINI KUHUSU HILI UMEFELI SANA.
Kila mtu mpenda michezo anamjua mwandishi Edo Kumwembe ambaye anaufuasi mkubwa kwenye mitandao ya kijamii. Edo Kumwembe ameonyesha kwamba yeye ana imani ndogo na akili za kushindwa kulikojaa kukata tamaa kwenye maisha.
Zaidi ya kuwa na akili hizo za kukata tamaa pia anaonekana kuwa sio mzalendo wala mwana michezo kwa kitendo chake cha wazi wazi kumtolea maneno ya kumkatisha tamaa mchezaji Himid Mao ambae ameenda nchini Denmark kwa ajili ya trial ya kucheza soka huko.
Siku ya Mei mosi mwandishi mwenzake Shaffih Dauda kupitia ukurasa wake wa instagram alipost picha ya Himid Mao akiwa airport anaelekea Denmark nakuandika kwamba tumtakie mema Himid Mao kwenye trial yake.
Kitu kizuri mashabiki wote walijitokeza kwenye comment wakimtakia mema mchezaji huyo kwenye majaribio yake. Mtu ambaye hakutegemewa kabisa licha ya kujua kwake soka akaja na roho yake ya kukatisha tamaa na kuandika, "At the age of 24...what a joke...he has already wasted his time".
Shabiki mmoja anaitwa '"1997_ELLY" akaja na kusema "Edo usimkatishe tamaa mpe moyo wa kupambana". Lakini bwana yule Edo Kumwembe na akili zake akijifanya mchambuzi wa hata future ya mtu alikazia na kusema,"Huwa naongea facts sio blah blah".
Moja) Edo Kumwembe kumbuka mifumo ya soka ya Africa na Ulaya ni tofauti, usitake Himid Mao anze soka akiwa na miaka 18 kama wakina Marcus Rashford. Huku kwetu Africa kwa mifumo yetu ambayo haina hata academy za uhakika ni ngumu sana kupeleka wachezaji Ulaya wakiwa wadogo hivyo.
Nchi za Africa Magharibi zinafanikiwa kutokana uwekezaji wa Academy zilizopo huko ndipo wanatoka wachezaji wakiwa wadogo na kwenda kuendelezwa huko.
Mbili) Ukiwa na miaka 24 sio sababu ya kwamba hautofanikiwa. George Weah alienda Ulaya akiwa na miaka 23 ambayo sio tofauti kubwa na 24. Lakini aliweza kucheza na kushinda makombe mengi na tuzo binafsi zikiwemo Ballo d'Or mwaka 95, Fifa World Player of the year 1995,UEFA Champions League top scorer 94/95 na tunzo nyingine nyingi. Kama umri umeenda kuna wakina Buffon wana miaka 39, Totti 40, Zlatan 35,Adebayo 33 na bado wanakipiga na wanategemewa na timu zao. Itakua miaka 24.
Tatu) Kikubwa kabisa kaonyesha utoto , ujinga na kukosa uzalendo. Yeye kama senior journalist tena wa michezo inabidi awe mstari wa mbele kama alivyo mwenzake Shaffih Dauda kuwa promote hawa wachezaji wapate ushabiki mkubwa kitu ambacho kinawapa moyo wakina Samatta, Ulimwengu na wengineo wakiwa uwanjani. Kwanini mashabiki wa kawaida wanafurahi Himid anaenda kujaribu nafasi lakini yeye mdau mkubwa anakuja kuleta negativities.
Lazima tuwa support vijana wetu kwasababu hata akipata mkataba wa miaka 2 mshahara atakaopata huko hauwezi kuwa sawa na mshahara atakao pata Azam. Pia mafanikio yake ni changamoto kwa vijana waliopo kama Serengeti Boys wasi aim for Simba, Yanga Azam.
Samatta, Ulimwengu na Himid wakiwa Ulaya ni motivation wa watoto wengine waliopo hapa Tanzania. Haijalishi wakina Himid wana miaka 24 au 34, cha msingi wanacheza huko na mshahara mzuri unaingia kwa ajili yao.
Cha mwisho jiangalie na wewe pia, umeona mshahara wa vyombo vya hapa Tanzania havitoshi unaenda hadi South Africa kupata pesa za ziada. Mbona husemi wewe umeshazeeka kwenye uchambuzi waisende vijana wadogo wengine. Kumbe unafata mafao zaidi, waache vijana wakajaribu kubadilisha maisha. Hakuna mwisho wa kutafuta hadi pale utakapoingia kaburini.