gfsonwin haya ya mazingaombwe ya ZNZ tumeyadili kidogo hapa Mitazamo na tathmini ya Uchaguzi 2015 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers@Nguruvi3 ukiwa unaendelea na mada naomba uniambie hivi kilichotookea huko Zbar ni kuficha kombe mwanaharam apite ama ni ile dhana ya kwamba katiba yetu haina kipengele linachoruhusu seriikal ya mseto hivyo ingekuwa shida sana kukubali ushindi wa Maalim. ama je ni ule mtazamo wa woga kwamba zbar lazima iwe chini ya CCM kwan kinyume chake ni muungano kuvunjika?
Just dissecting ! Any concern ?
Hoja ya mabadiliko ilitumiwa na wapinzani , Rais Magufuli akaunga mkono kutokana na haja ya wakati. Tunasema Magufuli, kwasababu hakuna rekodi za CCM kuzungumzia mabadiliko
Itakuwa ngumu kumwajibisha kutokana na kuaminika' vote of confidence'
Tutaangalia awamu ya tano kwa muda uliopo, tukijadili mwelekeo unaonekana na nini tutarajie
Utaratibu tuliojiwekea miaka 50 ulikidhi haja na matakwa ya wakati huo. Mkoloni alipotoa uhuru miaka 50 iliyopita, tulijiandikia utaratibu wa kujitawala
Miaka ya 1950/60 ilitawaliwa na harakati za ukombozi. Miaka ya 1970 siasa ilitawala nguvu za dunia. Miaka ya 80, mabadiliko yakaikumba dunia kutoka sehemu mbambali. Hilo likalazimisha jiografia na siasa za dunia kubadilika(geopolitical landscape). Tulibadilika kuendana na wakati. Kwasababu za kisiasa,mabadiliko yetu hayakuambatana na mabadiliko ya taratibu kulingana na wakati. Tunajitawala kwa taratibu za zamani katika dunia mpya. Hili limepekelea kilio cha kukaa chini na kujiandikia utaratibu wetu(katiba)
Tulikuwa na katiba yenye mrengo wa kijamaa ikitumika na chama kimoja.
Kwasasa tuna mfumo wa soko huria na ubepari katika siasa za vyama vingi.Una uhakika katiba ilkuwa ya kijamaa au unaropoka tu? Tungekuwa na katiba ya kijamaa rais Mkapa angewezaje kufanya biashara Ikulu? Je, Lowasa angewezaje kufanya biashara na kujitajirisha kwa pesa za walipa kodi? Si ndio hawa viongozi walifuta Azimio la Arusha na kuanzisha Azimio la Zanzibar ambalo ndio limewatajirisha isivyo halali?
Utendaji wa shughuli ni zama hizo, leo utaratibu ule hauna nafasi katika siasa za nchi na dunia.
Ref above katiba ya USA na UK
Hilo limesababisha kukwama kwa shughuli zetu kwasababu tuna muongozo usiolingana na wakati. Katiba haielezi kuhusiana na mgawanyo wa madaraka kwa vigezo vya ukanda au ukabila. Ni mambo yaliyobuniwa bila msingi.
Wewe ni hatari sana kwa maslahi ya Watanzania, unapendelea ukabila nothing more. Unaweza kuhamia Kenya.
Tulikemea hapa duru kuwa, utamaduni huo utakapozoeleka utaleta matatizo mbele ya safati
Tulisema , mfumo wetu ulihitaji marekebisho makubwa. Kauli za wapinzani zilibezwa na CCM
Leo tunaona yote yaliyosemwa kuanza kutekelezwa tena yakionyesha ''ufanisi''. Kuandika katiba mpya ilikuwa mwanzo mzuri wa kufumua mfumo na kuusuka upya.Rasimu ya Warioba ilipigwa stop na CCM kwavile tu ilitishia masilahi yao. Katiba pendekezwa ikapingwa na wananchi, tutakwama sote . Kinachoshangaza , yale ya Rasimu ya Warioba yanaanza kutekelezwa ingawa waliyakataa hadharani
Awamu ya 5 ya ni mfano mzuri unaotuonyesha tunavyoweza kupanga mipango,lakini kikundi cha watu kupitia siasa kikatuvuruga. Tulidhamiria kuandika (katiba) , kundi la wanaCCM likatuvuruga. Leo Rais anayetoka CCM anatekeleza maoni waliyokataa CCM
Sera za wapinzani ni kuwatajirisha wezi wakubwa wa nchi hii, hakuna demokrasia huko mnachaguliwa kiongozi kutokana na mfuko wake wa pesa.
Wewe una chuki binafsi, wapinzani walitaka jambazi Sugu ndio awe rais, huyu ni mwizi anajulikana tangu wakati wa Mwalimu. Watanzania sio wajinga wa kulichagua jambazi, haiwezekani kuwa na mawazo mgando kama haya Watanzania wengi bado wana Imani na serikali iliyopo madarakani hiyo ndio demokrasi kama hupendi hama nchi.
BTW huna hoja wewe ni jipu tu linalotakiwa kupasuliwa.
Ndugu Wacha1 nadhani kuna namna maoni hayakupendezi, elewa kuwa uhuru wa mawazo na maoni ni haki ya kila mtu.
Tulitegemea kama utachangia utajibu au kufafanua hoja kwa mtazamo wako. Matusi, kashfa na kejeli hazina nafasi hapa
Kutokana na kupoteza uelekeo, umeshindwa kuelewa vitu basic kabisa.
Kwa taarifa yako UK haina KATIBA. Hili hulielewi inakuwa ngumu kujadiliana
Kilichopo mbele yetu ni kuiangalia serikali iliyoundwa.
Tafsiri fupi ya demokrasia ni ' Of the people, by the people for the people' Abraham Lincoln anasema
Hiyo ni haki yetu ikiwa na mipaka unayotuelekeza tuvuke. Huko hatuendi
Wapinzania wameshindwa uchaguzi na hawana serikali.
Kama ipo hoja juu yao, bado una nafasi ya kuijadili katika uzi unaona utafaa.
Bandiko hili ni kuangalia serikali yetu bila kujali itikadi kwa mustakabali wa Taifa.
Tutaipongeza inapodi na kuikosoa ikibidi pia.
Hakuna ubaya , ndiyo demokrasia kwa maana ya of the people for the people
Tunafahamu lengo lako ni kuharibu mtiririko ili mjadala uende unakotaka
Huko hatuendi, na tunaendelea pale tulipoachia bandiko #13
Tunataka radhi waliokwazika na kauli za maudhi za bwana Wacha1.
Tunaomba kuvumiliana , tupo tofauti na mitazamo tofauti ingawa mingine si mizamo tunayotarajia
Tunaendelea.. waziri ofisi ya nchi muungano