Heavy Weight
JF-Expert Member
- Mar 1, 2014
- 888
- 883
Muaniaji wa urais wa chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump, amesema kuwa dunia ingekuwa mahala salama zaidi kama tu Saddam Hussein wa Iraq na Muammar Gaddafi wa Libya wangelikuwa hai.
Bwanyenye huyo aliyasema hayo katika mahojiano na CNN baada ya kukashifu sera za kidiplomasia za rais Barack Obama.
Trump alisema kuwa maafa yaliyoendelea mashariki ya kati yalichangiwa asilimia mia moja na sera haribifu za rais Obama na bi Hillary Clinton.
"Japo tunamlaum Muammar Gaddafi unadhani angekuwa hai magaidi wangekuwa huko? La."
'Angalia kwa makini hakuna Libya'. Libya tuliyoijua sasa imesambaratika kabisa.
Saddam alikuwa mtawala wa kiimla tunajua asingeliwaruhusu magaidi kunawiri huko Iraq.
Sasa Iraq ndio Havard ama chuo kikuu zaidi cha ugaidi duniani. Kama ni maswala ya ukiukwaji wa haki za kibinadamu kwa hakika hali ilivyo sasa ni mbaya zaidi kuliko tulivyodhani wakati huo'.
Bwanyenye huyo anaetarajiwa kutwaa tikiti ya kuwania urais ya chama hicho cha Republican amesema kuwa amepania kurudisha hadhi ya Marekani.
Aidha amesema kipengele muhimu katika utawala wake utakuwa kuimarisha uwezo Marekani kijeshi.
Amlaumu Obama kwa kugawanya taifa. Trump amesema nia ya utawala wake itakuwa kuwaunganisha wamarekani wote bila kujali tabaka.