DRC Kongo: Mtanzania atekwa Bukavu. Watekaji wataka $2,000,000 wamwachie

Je tajiri wa kiswahili atathamini watu wake hadi alipe mkwanja huo? Wale wasomali wateka wazungu huwa wanafanikiwa, sijasikia huku nchi kavu mtukio hayo kufanikiwa
 
Zipo taarifa za kutekwa kwa Mtanzania mtaalamu wa uchenguaji dhahabu anayefanyakazi na kampuni Banro ya Kongo Eng Yusuf Kapanda. Huyu ni mtaalamu muhimu sana kwa uchumi wa nchi yetu siajabu angekuwa anafanyakazi nchini tusingekuwa tunalalamika kuibiwa mchanga.

Hizi taarifa za kutisha na guogofya zinazunguka mitandaoni tunaomba Balozi Mahiga alitolee ufafanuzi na wananchi waelezwe nini kinachoendelea kuhakikisha maisha ya mtanzania mwenye elimu adimu akiokolewa na kurejeshwa nchini tayari kulitumikia taifa letu.

Nanyie wanasiasa na akina Gwajima mngeshadadia hili la kutekwa kwa mhandisi Kapanda tungewaona watu wa maana sana badala ya kuhangaika na mtu anayepambana kuondoa mateja Kinondoni.

Nategemea akina Zitto Sugu Nape kuwachana na habari za Makonda na kushinikiza serikali imrejeshe Eng.Kapanda.
 
*MTANZANIA ATEKWA BUKAVU - DRC*

Yusuph Athuman Kapanda, mkazi wa Nyakato Jijini Mwanza, ametekwa na waasi nchini Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo. Kapanda na wenzake wametekwa Namoya Site, iliyopo Bukavu, akiwa anafanya kazi na Kampuni ya Banro Mining Corporation Ltd. Kapanda ni mfanyakazi wa kampuni ya SGS ya Mwanza ambayo ndio iliingia mkataba na Banro kwenye maabara yao ya madini na Kapanda kupelekwa huko na SGS.

Watekaji wanadai dola za Kimarekani milioni mbili wamwachie. Duru za kibalozi zinadaiwa kusuasua kusaidia tatizo hili ambalo lina wiki mbili na siku kadhaa hadi sasa.
akina Lissu Mbowe Nape Kusaga Gwajima Zitto wala hawana habari na huyu mtanzania wao ni Makonda tu, hawa wanasiasa wetu washenzi sana na watu wa hovyo, wameona biashara zao za madawa ya kulevya zimeingia Luba wameungana wamekuwa wamoja huwezi jua ccm yupi na chawema ni yupi, kweli hii nchi na ya hovyo sijapata kuona. Nape ningemwona mtu wa maana kama angeongelea kutekwa huyu Mtanzania mtaalamu wa madini ya dhahabu badala yale anaenda kuongea mambo ya kilevi tu. Siajabu alikuwa bado anajanaba.
 
Lengo la kuanzisha huu uzi ni kushauri Zitto, Nape na Sugu waachane na hbari za Makonda????
habari za makonda ni upumbavu tu wakati kuna watanzania wanafia nje ya nchi wakihangaika kuiletea nchi fedha za kigeni.
 
Too sad ila unfortunately pondamali yupo busy firing and hiring mambo ya nje hajui kbs
 
Hao watekaji nao wanakosea sana badala umteke Mzungu unamteka Msukuma ambaye hata akikaa hai umri uliobakia hatailetea familia hiyo $2m
 
Ulianza kama bashite kuanzia msingi mpaka sec jina lake kufika chuo kaharibu,uzi umeanza vizur mwisho umeharibu!
 
Jiulize Wale wa tz msumbiji walisaidiwaje na serikali yao ukipata jibu tumuombee kwa Mungu huyo engineer
 
Back
Top Bottom