DRC Kongo: Mtanzania atekwa Bukavu. Watekaji wataka $2,000,000 wamwachie

mwanamwana

JF-Expert Member
Aug 1, 2011
1,229
4,554
*MTANZANIA ATEKWA BUKAVU - DRC*

Yusuph Athuman Kapanda, mkazi wa Nyakato Jijini Mwanza, ametekwa na waasi nchini Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo. Kapanda na wenzake wametekwa Namoya Site, iliyopo Bukavu, akiwa anafanya kazi na Kampuni ya Banro Mining Corporation Ltd. Kapanda ni mfanyakazi wa kampuni ya SGS ya Mwanza ambayo ndio iliingia mkataba na Banro kwenye maabara yao ya madini na Kapanda kupelekwa huko na SGS.

Watekaji wanadai dola za Kimarekani milioni mbili wamwachie. Duru za kibalozi zinadaiwa kusuasua kusaidia tatizo hili ambalo lina wiki mbili na siku kadhaa hadi sasa.
 
Hela yote hiyo, hao wanataka kumuua tu waseme ukweli
Ni muda sahihi wa kamanda Daudi Albert Bashite kupelekwa huko na wale jamaa alioenda nao pale Clouds Media....wakiwatishatisha na kuwakata mitama ya hapa na pale na kuwatishia kuwataja kwenye orodha ya drug dealers watamwachia tu!!!!!!!
 
Aiseee, masikini Eng. Kapanda, this is very bad news to hear. Niliwahi kufanya nae kazi, dah inauma sana. Tumuombee kwa mungu watekaji wasimdhuru. Na kwa serikali hii ya sasa dah ilivyo slow kudeal na issue kama hizi masikini wa Mungu msimamie wamuachie salama.
 
Usawa wenyewe huu TZ watekaji wanachemka. Watawatesa bure waTZ wenzetu na mzigo wasipate
 
Wamuachie TU maana farther house mwenyewe aliyopo wasitegemee kama atatia hata tsh 100

Ova
 
Wako bize wanamkingia kifua bashite
 
Hao jamaa wamekosea mahesabu, wangemteka Daudi Bashite, Magogoni wangeshaidhinisha pesa mpaka muda huu.
 

Weka Kumbukumbu zako vizuri, Bukavu iko Sud (South) Kivu Province ndipo zilipo office kuu za Banro na hakuna mgodi wowote hayo maeneo, Mgodi wa Namoya hauko Bukavu , bali upo Maniema (Manyema) Province
 
Usawa wenyewe huu TZ watekaji wanachemka. Watawatesa bure waTZ wenzetu na mzigo wasipate

Huu mzigo unatakiwa utolewe na kampuni ya SGS iliyompeleka Kapanda huko Congo!!! Serikali yetu should not get involved in the business of paying RANSOM ama sivyo waCongo watatufilisi kwa kuteka watu wetu kula kukicha!!!
 
Huu mzigo unatakiwa utolewe na kampuni ya SGS iliyompeleka Kapanda huko Congo!!! Serikali yetu should not get involved in the business of paying RAMSOM ama sivyo waCongo watatufilisi kwa kuteka watu wetu kula kukicha!!!
Duh. .mbona huo mzigo wa haja!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…