Ikija kulipia umeme SMZ ni masikini lakini kupandisha mishahara mara 4 ndani ya miaka 5 hela wanayo!
Kutokulipa madeni ya TANESCO ni kulidhoofisha shirika la umeme na kuongeza mishahara mara nne ndani ya miaka minne kuna ashiria yafuatayo:-
1) JMT ndiyo inaipa SMZ ruzuku kuiendesha serikali tajwa.
2) Hizi peremende za Dr. Shein huku serikali yake ni mdaiwa sugu kunatia mashaka makubwa hizi peremende ni kuwanunua baadhi ya watendaji serikalini.
3) La ajabu, kutolipwa madeni ya Tanesco haiko kwenye kero za Muungano lakini mgawanyo wa mali za EAC uko kwenye kero tajwa!
4) Makovu ya kushindwa na Seif awamu ya kwanza ndiyo yanatafutiwa muarobaini kupitia hizi peremende.
5) Kuboresha masilahi ya waajiriwa hakupunguzi makali ya maisha kwa wapigakura ambao siyo waajiriwa.