Dk. Shein Afanya Uteuzi wa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, Hamad Rashid aula

Huyu Modline Castico siyo raia wa Tanzania namjua vizuri, alikuwa ni Mke wa Mzee Joel Castico ambaye alikuwa mkurugenzi wa kituo cha mikutano zanzibar ale EKOTANALI, huyu mama ni raia wa Zambia
 
Huyu Modline Castico siyo raia wa Tanzania namjua vizuri, tena aliwahi fanya dhambi mbaya Sana, akileta kelele ntaanika humu, alikuwa ni Mke wa Mzee Joel Castico ambaye alikuwa mkurugenzi wa kituo cha mikutano zanzibar ale EKOTANALI, huyu mama ni raia wa Zambia
zambi ipi ?
 
Familia ya Abeid Karume mpaka wajukuu ni matata sana!

Kila mmoja ana mtazamo wake kuhusu Zanzibar.

Kila mmoja ana mtazamo wake kuhusu Muungano.
hivyo ndivyo inavyotakiwa kwa kuwa kila mtu ana akili zake,hutakiwi kufanya maamuzi kwa kumuogopa mtu
 
Huyu Modline Castico siyo raia wa Tanzania namjua vizuri, tena aliwahi fanya dhambi mbaya Sana, akileta kelele ntaanika humu, alikuwa ni Mke wa Mzee Joel Castico ambaye alikuwa mkurugenzi wa kituo cha mikutano zanzibar ale EKOTANALI, huyu mama ni raia wa Zambia
Ss si useme........
 
Ally karume amekomalia tu mpka na yeye aupate urais, nyambafu madaraka mabaya kweli acha Fatma awachane tu hakuna namna huu uhuni lazima uendelee kusemwa.
 
Rais wa Zanzibar Dkt. Shein amteua Hamadi Rashid kuwa mjumbe wa Baraza la wawakilishi


2.jpg

Uteuzi huo wa Rais Dkt Shein umefuata baada ya leo kutoa hotuba na kuzindua Baraza la wawakilishi ambapo pamoja na mambo mengine amesisitiza umoja na mshikamano miongoni mwa wananchi.

Wengine walioteuliwa kuwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi ni pamoja na
1.Mohamed aboud Mohamed
2. Amina Salum Ali
3. Moulin Castico
4. Balozi Ali karume
5. Said Soud Said na
6. Juma Ali Khatibu

Aidha uteuzi huo umeanza hii leo tarehe 05.04.2016.
 

Attachments

  • shein.jpg
    shein.jpg
    49.6 KB · Views: 55
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, amefanya Uteuzi wa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Kwa Mujibu wa Uwezo aliopewa Chini ya Kifungu cha 66 cha Katiba ya Zanzibar ya 1984, amefanya uteuzi wa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar. Kupitia nafasi zake 10.

Mhe Mohammed Aboud Mohammed CCM.

Mhe Balozi Ali Karume.CCM

Mhe Balozi Amani Salum Ali. CCM

Mhe Moulin Castico. - CCM

Mhe Hamad Rashid Mohammed ADC

Mhe Said Soud Said - AFP

Mhe Juma Ali Khatib - ADA-TADEA.

Uteuzi huo unaaza leo tarehe 5/4/2016.
lengo la Hamad Rashid halikuwa uwakilishi , aliambiwa angekuwa makamu wa rais , halafu kingine ni kwamba irekebishwe kwamba HAMAD RASHID kateuliwa kutoka mtaani maana alishatimuliwa kihalali ndani ya ADC , ni lazima ccm ijifunze kuheshimu sheria za nchi , ya mcc yanaweza kuwa madogo yakaja makubwa zaidi , lengo si ni kumpa hamad rashid cheo ? basi inawezekana kutotumia jina la ADC na msiulizwe na yeyote , lakini kuendelea kung'ang'aniza uanachama wa hamad ADC ni kujitafutia nalumbano tu .
 
Hongera Mheshimiwa Rais, Dr. Shein, kwa uamuzi wa kuwateua wapinzani kuingia katika Baraza la Wawakilishi. Sasa ninashauri busara itumike kuteuwa mmoja wao ashike nafasi ya Makamu wa Kwanza wa Rais. Hatua hiyo itasaidia kuzima uongo na ghiliba za Seif. Wengi tunafahamu kwa uongo na unafiki wake alimwondosha mzee Aboud Jumbe madarakani. Ni fisi mwenye uchu wa madaraka aliyejivika joho la utetezi wa watu ili afanikishe ubinafsi wake.
Wapinzani ni kina nani hapo??
 
Familia ya Abeid Karume mpaka wajukuu ni matata sana!

Kila mmoja ana mtazamo wake kuhusu Zanzibar.

Kila mmoja ana mtazamo wake kuhusu Muungano.
Waowao ndo wapinzani na waowao ndo chama tawala yaani wanachekesha kweli,wameona wanogeshe siasa za Zanzibar ili tuwe tunaazisha thread kwa ajili ya Zanzibar bila hivyo Zanzibar inaweza ikapotea kwenye akili za bara.
 
Hamad Rashid karihirisha hana msimamo, kutoka kugombea Urais, unakuja kupewa uwakilishi na unakubali? Huyu jamaa kweli ni mpuuzi tu.
ulitaka afanyaje labda..mbona Dr.Slaa na Mrema waliwahi kushindwa urais wakaishia kuwa wabunge...
 
Back
Top Bottom