Diwani wa Kahe Mashariki amefanya mambo makubwa anastahili pongezi

Kifuu

Senior Member
Jan 29, 2017
150
91
Nimejaribu kufanya utafiti wakujua jinsi gani viongozi wanajibika kwa wanachi wao hapa nchini nimetembea baadhi ya mikoa ya Bara na visiwani nimempata diwani mmoja tu ambaye ameonyesha mfano wa uwongozi.

Ukifika Mkoani Kilimanjaro katika Halmashauri ya Moshi kuna kata inaitwa Kahe Mashariki Kata hii inaongozwa na diwani mdogo mwenye umri wa miaka 30, kwa tiketi ya CCM ambayo ipo jimbo la Vunjo.

Kijana huyu hapendi sana kuzungumzia mambo ya siasa zaidi atakwambia tuache siasa tufanye kazi

Niukweli kipindi cha nyuma kata hii ilikuwa hakuna anaeijua kutokana na kutopewa kipaumbele kwani wanaoishi huko nikabila dogo sana la wakahe ambao wamekuwa wakisubiri wachaga na wapare wanaamua nini?

Lakini ukienda leo utakuta mambo makubwa yaliyofanywa na Diwani huyo kijana ambaye serikali inajivunia.

Hayahapa chini ndio yanayo nifanya nikubali nayoyaandika.

1.Amefanikisha ujenzi wa vyoo vya shule za msingi.

2.ameweka baadhi ya shule umeme wa jua pamoja na TV ofisi ya walimu.

3.anajenga Kituo cha afya kwenye kata yake jambo ambalo hata mawaziri wameshindwa kufanya hivyo kwenye majimbo yao.

Hayo yote yamefanywa na fedha ambazo si za serikali nikupitia wafadhili aliyowatafuta yeye mwenye nje ya nchi.

4.Lakini haitoshi Kata ya Kahe Mashariki ndio imeongoza kwa kukusanya mapato mengi zaidi ya asilimia 53 kwenye Halmashauri ya Moshi.

5. Ndio iliyoongoza kupata tunzo za watumishi bora ndani ya Halmashauri ya Moshi.

Kwani Hayo ndio yaliyonifanya baada ya kuzunguka katika maeneo mbalimbali ya wanasiasa kuona huyu mwanasiasa kijana wa CCM na mwandishi wa habari ameongoza kufanya mambo makubwa kwa muda mfupi toka achaguliwe 2015.

Kama yupo mwingine aletwe hapa JF nae tumjadili tuone.
 
hivi kumbe kilimanjaro kuna kabila lingine la watu linaloitwa wa-kahe.. Mi nilikuwa sijui
 
Katika mambo yanayonikera hapa nchini ni kusikia habari ya mtu/taasisi/ anajitapa/wanajitapa kujenga matundu ya VYOO kweli jamani, kweli. Matundu ya vyoo, kweli karne hii tunahangaika na matundu ya vyoo.
 
bora umeona hilo. hakuna kabila la wakahe. mtoa post anajaribu kushika upepo kwa nyavu
kahe naifahamu vizuri sana, naomba aniambie ni kahe ipi anaongelea. kwa ufupi tu ni maeneo ambayo watu wengi wa mji wa moshi na wageni wanaofika hapa moshi kutafuta maisha hukimbilia kutokana na kupata viwanja kwa ajili ya makazi kwa bei ndogo sana. ila bado suala la usafiri ni changamoto haswa. haswa wakati wa mvua
 
Poor analysis !

Kahe inawatumishi wa ngapi mpaka itoe watumishi bora? Huyu diwani ni mfanyakazi wa halmashauri?

Kahe ina chanzo gani cha mapato, kuweza kuongoza Halamshauri ya Moshi kwa mapato?

Kipaumbele ni kuweka TV kwenye ofisi za walimu? kwaiyo anataka walimu wasifundishe wakeshe maofisini kutizama Isidingo The Need?

Hapo diwani wako ni saa na Zero , wapo wanyeviti wa vijiji wamefanya makubwa zaidi ya hayo. Fanya utafiti wako tena, halafu hapa JF uwe unapost vitu vyenye kichwa, sio kupost mikia..!
 
Soma vizuri hakuna palipomtaja diwani ni mtumishi.

Waliopokea zawadi niwatumishi wanaotoka Kahe Mashariki.

Kuhusu mapato jitaidi kufanya utafiti kabla ujajibu chochote Kahe Mashariki ndio inayoongoza kwa Kilimo cha mbogomboga ktk Halmashauri ya Moshi kuna ushuuru wa mazao ambao ndio umepelekea ikaongoza kwa mapato.

Kuhusu wenyeviti walete hapa tuwajue
 
Kahe mashariki
 
Hongera diwani unajua nini inapaswa kuwatendea wananchi waliokuchagua tofauti na mmoja huko maeneo ya chekereni , kagera amegeuka kuwa dalali wa mabepari kwa ardhi za wenyeji sijui huyo ni wa chama gani ila tunamfuatilia mguu kwa mguu
 
Huyo diwani atakuwa ameshirikiana na James Mbatia si ndie mbunge wa jimbo hilo!!!!
 
bora umeona hilo. hakuna kabila la wakahe. mtoa post anajaribu kushika upepo kwa nyavu
Wakahe wapo, ni kama wapare japo lugha yao iko tofauti kidogo.Wanapatika eneo kama unaelekea kiwanda cha sukari TPC vijiji vya Mabogini, Chekereni, Kahe, Samanga nk
 
kila mtu anatafuta kik ....
 
Wakahe wapo, ni kama wapare japo lugha yao iko tofauti kidogo.Wanapatika eneo kama unaelekea kiwanda cha sukari TPC vijiji vya Mabogini, Chekereni, Kahe, Samanga nk
Kahe zamani kuna baba yangu mdogo alikuwa huko anafanya kazi NAFCO hata sijui hao NAFCO walikuwa wanashughulika na nini!!! ila nakumbuka tu hilo maana alikuwa akija home lazima atuletee biskuti
 
Wakahe wapo, ni kama wapare japo lugha yao iko tofauti kidogo.Wanapatika eneo kama unaelekea kiwanda cha sukari TPC vijiji vya Mabogini, Chekereni, Kahe, Samanga nk
hawana tofauti na wapare ... nilijua Mwanga imeendelea kumbe wachovu tu...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…