Diamond hana washauri?

Hajui chochote kuhusu dini kajiandikia tu,kwanza kwa mujibu wa hiyo dini yake mtoto wa haramu (nje ya ndoa ) hawajibiki kwa lolote kwa Baba,angalau angeongelea kibinadamu angekuwa na pointi si dini. Mtoto wa haramu ni mali ya mama kwa mujibu wa hiyo dini yake na mtoto hapati dhawabu (malipo kwa mungu) kwa kumuhudumia huyo Baba, na hapati dhambi kwa kutomuhudumia. ( KUMBUKA MAMA DIAMOND NA HUYO BABA HAWAKUWA WAMEOANA)
Uislam kazii
 
Mnao mlaumu Diamond hamjapitia aliopitia ,ndio sio vizuri anavofanya but muacheni mungu ndie hakimu nyie wenyewe mna dhambi ngapi ambazo hatuzijui
Fanyeni yenu waachieni mambo yao ya kifamilia
Wanaume ishini vizuri na wapendeni watoto wenu huwezi jua atakua nani baadae
Hata km umeachana na mama ake be there kwa ajili ya mtoto wako
Ndo kinachomtesa sasa hv baba Diamond anatafuta simphathy kwenye social media

umeongea point sana, mama yake ameangaika kumlea kwa kuua vitumbua na ntilie sasa dimond ametoka baba ndio anajileta waati enzi zake alikua anauzA NYUMBA ZAO KARIAKOO ANATUMIA HELA ZOTE BILA YA KUTAMBUA KUA ANA MTOTO ANAITWA NASEEB, jamani muacheni diamond mpaka roho yake itakapoamua kumsaidia huyo baba inauma jamani acheni tu, huyo baba aliisi dimnd hatokuja kukua aliona muda hauendi
,
 
Fikiri tena, ukimaliza kufiri nakuomba ufikiri tena, nasema rudia tena kufiri, nakutaka ufikiri zaidi ya kufiri ulikofikiri,

Maneno yote aliyoyaandika mleta post hapo na kumuongoza mwenzako hasa kwa maandiko ya ki Imani ya DINI yake bado unafikiri hovyo hivyo ?

Kama umeshundwa kufikiri kwa muda huu pumzika na unywe maji maana hata swaumu...huna,

Na ukishindwa kufiri tafuta mtu akusaidie kufikiri ili ukiri kwamba ulikariri bila kufiri.
Mkuu mbona unashangaza kwani ni lazma kila mtu awe swaumu hiki kipindi "
 
wewe umepata malezi ya baba
wengine hatujapata
tunaona sawa tu, huwezi kumuonea uchungu mtu ambae hujui uchungu wake....
haiwezekani.. cjui nyie mliopata malezi nao
Like father like son,diamond nae ana roho kama ya baba yake wote wana roho mbaya
 
wewe umepata malezi ya baba
wengine hatujapata
tunaona sawa tu, huwezi kumuonea uchungu mtu ambae hujui uchungu wake....
haiwezekani.. cjui nyie mliopata malezi nao
basi asingetumia hata jina lake maana anasidia watu baki basi amsaidie nae kama mtu baki isitoshe pia ugom,vi wa wazazi si wakuingilia inaonekana dimond anaambiwa yote na mama yake wengi tu hawakulelewa na baba zao lakini wanawasaidia kwani mwenye kuhukumu ni mungu
 
Kwa mtu yoyote ambaye amelelewa kwenye familia yenye wazazi wawili ambayo baba anatimiza wajibu wake ipasavyo.....

Katika familia ambayo asilimia tisini ya mafanikio yako yametokana na juhudi za wazazi wote wawili kwa kila mmoja kutimiza wajibu wake huwezi kumuelewa huyo kijana diamond.....au huwezi kuhisi vile anavyohisi anavyomuona baba yake......

Ila kama umezaliwa kwenye familia ambayo mama yako pekee anatakiwa adamke alfajiri kwenda kutafuta vibarua ambavyo muda mwingine ni za kumdhalilisha ilimradi tu wewe kijana uweze...kula vizuri ,kuvaa vizuri , kulala pazuri na hatimaye kupata elimu nzuri....
Katika familia ambayo kilele cha mafanikio yako yametokana mahangaiko ya mama yako kipenzi aliyelazimika kubeba majukumu ya watu wawili na kufanikiwa kukufikisha hapo.....unamuelewa vyema Daimond na unaelewa vile ambavyo yeye anahisi pindi aionapo sura ya baba yake......

Nina wakumbusha wanaume wenzangu kuwa kuitwa baba hakuishiii tu kwenye kumpa mimba mwanamke bali kwenye kutimiza majukumu yake kama mzazi ambaye kwa namna moja au nyingine anahusika na upatikanaji wa mimba hiyo.....

What should I say here!! Umemaliza kila kitu
 
Back
Top Bottom