Waziri anaehusika na Viwanda na biashara Mh Charles Mwijage amekua akileta utani na matamko yenye komedi linapokuja suala la ukweli wa mafanikio ya viwanda vikubwa vitakavyoingizia serikali mapato,
Mwijage amekua akiorodhesha viwanda vidogo vidogo mfano wanaogonga kokoto, watengeneza vibatari na hata wafyatua tofali za ujenzi kama ni moja ya viwanda hivyo analeta amebaki kuleta utani bungeni na majibu ya kuchekesha hata Waheshimiwa wabunge wameshindwa kumuelewa linapokuja suala la idadi ya viwanda vilivyoanzishwa na serikali, Aidha, Mh Mwijage ameshindwa kuelewa nini maana ya neno viwanda vyenye tija ya moja kwa moja na serikali amebaki kuchekesha tu miaka inakatika, akumbuke kuwa agizo la Mh Rais ni amri kwake katika kuunga mkono kaulimbiu hiyo na yeye ndio anayebeba kauli mbiu ya serikali ya viwanda kwa maana ya kuandaa mipango mikakati,mazingira mazuri ya wawekezaji viwanda, vipaumbele, ushauri wa mazingira wekezi,kutenga maeneo ya viwanda vikubwa, vidogo na vya kati, kuondoa utitiri kodi pingamizi kwa kushirikiana na taasisi nyingine husika,utitiri wa kodi zisizotabirika zinawatisha wawekezaji katika uwekezi viwanda nchini na ndio sumu ya kukwamisha viwanda, vilevile angeshauri jinsi ya kupata malighafi za viwanda, soko na fursa za uwekezaji,amebaki kuhesabu viwanda visivyo na tija na serikali, dhana ya mapinduzi ya viwanda katika nchi za Ulaya waliweka vipaumbele vya maeneo ya viwanda,malighafi,nguvukazi na masoko lakini walianza na mapinduzi ya kilimo ili wapate malighafi na wamefanikiwa sana, Aidha, ninamshauri Mh Waziri Mwijage aandae sera ya "protectionism" kwenye viwanda na bidhaa zetu, eneo la viwanda hata kimoja chenye tija kuu kwa kuishauri serikali.
Serikali kupitia Wizara ya viwanda na biashara ianze na kiwanda kikubwa kimoja tu kwanza kwa awamu hii mfano hata cha kutengeneza magurudumu/ matairi ya magari na mashine nyingine soko lipo sana tu nchini na hata jirani