Raisi akitokea ukanda wa pwani na visiwani yani mikoa ya Pwani, Dsm na Zenji naona kunakuwa na unafuu sana kwenye Demokrasia kuliko Raisi akitokea mikoa ya bara.
Enzi za Nyerere ilikuwa ni ngumu sana hata kusikia habari zake negative, Hii ilipelekea asifiwe kuzidi uhalisia, nakumbuka watu kama spika Sitta walicharazwa bakora hadharani lakini hili halikuwa kusemwa, Vyombo vya habari kulikuwa na uhuru mdogo sana kumkosoa, hakukuwa na vyama pinzani.
Enzi za Mwinyi mzee wa Ruksa nchi ilianza kuwa na uhuru wa maoni, ndicho kipindi aliweza kuridhia ujio wa vyama Pinzani.
Enzi za Mkapa nae huyu mzee suala la kumkosoa ilibidi ujitathmini.
Enzi za Kikwete ndipo vyama pinzani vilimea, uhuru wa moni ulikuwa upo juu sana.
Enzi za Magu fuli hata hii Jamii Forums ilitaka kufungiwa, ili uwe na ukurasa wa facebook, instagram, channel ya youtube ilibidi ulipie milioni +, magazeti kibao yalifungwa, nadhani mnaikumbuka ile kauli ya "be careful"
Enzi za Samia mambo at least yameanza kurudi kwa unafuu, hilo la tarehe 24 keshokuwa kuwaruhusu wapinzani kuandamana si jambo dogo hata kidogo