DED Malinyi ajenga nyumba sita za walimu

Mbona zimejengwa kama madarasa ya shule!, hatari. Bangaloo!
Kweli mkuu ziko kama madarasa kabisa hazipo katika mwonekano wa nyumba za kuishi kabisa. Zimejengwa kwa mtindo wa treni labda baadaye wanaweza wakazigeuza kuwa madarasa. Lakini nyumba za kuishi wamishi huwa zinapendeza zianapokuwa kuwa katika nafasi kila moja ikijitegemea sio kama hizi za kupeana migongo labda iwe ghorofa. Hata hivyo sio mbaya sana. Hongera!
 
*MKURUGENZI MALINYI AKAMILISHA UJENZI WA NYUMBA 6 ZA WALIMU KWA SIKU 23.*

Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Malinyi ndugu _Marcelin Ndimbwa_ amefanikiwa kukamilisha ujenzi wa nyumba 6 za walimu ambapo kila nyumba itakuwa na uwezo wa kubeba kaya/familia sita pamoja na matundu 24 ya vyoo ambao ni mradi wa SEDEP.

Ujenzi huo ulianza mara moja baada ya tangazo la mh Rais alilotoa mwishoni mwa mwezi novemba kwa kuwataka wakurugenzi wote kukamilisha ujenzi wa nyumba za walimu, ndugu Ndimbwa (Mkurugenzi Mtendaji) aliamua kufunga mkanda na kulivalia njuga ili kuhakikisha ujenzi huo unakamilika haraka iwezekanavyo na kuwa tayari kwa matumizi ya makazi hadi kufikia kipindi mkurugenzi aliendelea na shughuli za halmashauri kutokea hapo hapo site (Kwenye ujenzi wa mradi) na hatimaye ndani ya siku 23 kazi hiyo imekamilika kama inavyoonekana pichani.

Endapo miradi ya namna hiii isopokamilika kwa wakati imeelezwa moja madhara ya ni fedha kurudi World bank, hivyo ingepelekea serikali kupata hasara pamoja na kufutwa kwa msaada huu.

Tunapongeza juhudi hizi za wasaidizi na watendaji wa mh rais katika kuhakikisha serikali inatumia vema fedha za misaada pamoja na kusimamia vema mapato na matumizi ya fedha za umma na serikali yetu.

Hakika tunahitaji utendaji wa wakurugenzi wengi wa mfano wa ndugu Marcelin Ndimbwa ili kutimiza adhma ya serikali katika kuwatumikia wananchi wake kwelikweli.

View attachment 451946
View attachment 451947
View attachment 451948
acha uongo, hizi picha ni picha za madarasa.
 
Ajiandae kupandishwa cheo mwanzoni mwa mwaka
Kama anastahili why not.....Malinyi ni moja ya wilaya ambayo ni ngumu mno kwani hakuna miundombinu kabisa ila wafanyakazi kule kuanzia mkuu wa wilaya ni watu ambao wapo very much dedicated and service oriented.
 
Hapo mwl kama anavidemu utakuwa full kuchorana na kuchunguzana maishaa kwa waliooa
 
Hili nalo la kupongezwa? Kuchelewa kutimiza wajibu wako, baadae umemaliza kabla ya tarehe 31/12/2016, unajipongeza?. Halmashauri nyingi zilimaliza muda mrefu sana kazi yako
 
Yawe kama madarasa au mabanda, haijalishi ili mradi binadamu anaweza kuishi. Ukitaka nyumba ya peke ako jenga yako. Kajitahidi sana na anahitaji pongezi kwa kujenga nyumba zenye viwango vizuri tu.
 
Kweli mkuu ziko kama madarasa kabisa hazipo katika mwonekano wa nyumba za kuishi kabisa. Zimejengwa kwa mtindo wa treni labda baadaye wanaweza wakazigeuza kuwa madarasa. Lakini nyumba za kuishi wamishi huwa zinapendeza zianapokuwa kuwa katika nafasi kila moja ikijitegemea sio kama hizi za kupeana migongo labda iwe ghorofa. Hata hivyo sio mbaya sana. Hongera!
Yap kweli, kwa Malinyi ni sawa.....
 
Nyumba zina ramani mbaya ambayo haijawahi tokea duniani..Sijui wizara walitengenezewa na kapuku gani???
 
*MKURUGENZI MALINYI AKAMILISHA UJENZI WA NYUMBA 6 ZA WALIMU KWA SIKU 23.*

Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Malinyi ndugu _Marcelin Ndimbwa_ amefanikiwa kukamilisha ujenzi wa nyumba 6 za walimu ambapo kila nyumba itakuwa na uwezo wa kubeba kaya/familia sita pamoja na matundu 24 ya vyoo ambao ni mradi wa SEDEP.

Ujenzi huo ulianza mara moja baada ya tangazo la mh Rais alilotoa mwishoni mwa mwezi novemba kwa kuwataka wakurugenzi wote kukamilisha ujenzi wa nyumba za walimu, ndugu Ndimbwa (Mkurugenzi Mtendaji) aliamua kufunga mkanda na kulivalia njuga ili kuhakikisha ujenzi huo unakamilika haraka iwezekanavyo na kuwa tayari kwa matumizi ya makazi hadi kufikia kipindi mkurugenzi aliendelea na shughuli za halmashauri kutokea hapo hapo site (Kwenye ujenzi wa mradi) na hatimaye ndani ya siku 23 kazi hiyo imekamilika kama inavyoonekana pichani.

Endapo miradi ya namna hiii isopokamilika kwa wakati imeelezwa moja madhara ya ni fedha kurudi World bank, hivyo ingepelekea serikali kupata hasara pamoja na kufutwa kwa msaada huu.

Tunapongeza juhudi hizi za wasaidizi na watendaji wa mh rais katika kuhakikisha serikali inatumia vema fedha za misaada pamoja na kusimamia vema mapato na matumizi ya fedha za umma na serikali yetu.

Hakika tunahitaji utendaji wa wakurugenzi wengi wa mfano wa ndugu Marcelin Ndimbwa ili kutimiza adhma ya serikali katika kuwatumikia wananchi wake kwelikweli.

View attachment 451946
View attachment 451947
View attachment 451948
bila sha ww ndo mkurugenzi mwenyewe
 
Watu kama nyie hamkosi

Asipojenga issue akijenga bado mnatoa kasoro.

Mpongeze bas hata kidogo kwa hizi juhudi sio kila siku kuponda tu

Sawa, asije akawa amenunua mfuko mmoja wa cement kwa shilingi elfu 70....wakati tunajua ni chini ya elfu 20
 
Ina Maana Halmashauri haina wataalamu wa Michoro ya Ramani za Nyumba?

Hilo Jengo ilitakiwa lijengwe kama PEMBE NNE iliyoshikana ili kutenga vyumba vya mabachelor, na wenye familia, halafu katikati hapo kunakuwa WAZI,

Yaan, PEMBE NNE, kunatengwa vyumba 4 vya mabachelors lakini kunakuwa na jikoni hapo nje na VERANDA, halafu pia, kunakuwa na nyumba ya vyumba viwili na sebule au chumba sebule kwa wenye familia.

Waende LOLIONDO SEKONDARI huko Ngorongoro wajifunze namna nzuri ya kujenga nyumba za walimu ili ku-accommodate walimu wengi.
All in all amefanya kazi nzuri
 
Back
Top Bottom