DC Mtwara hongera kwa zoezi la upandaji miti katika Shule ya Msingi Kwale

PendoLyimo

JF-Expert Member
Sep 30, 2014
956
1,038
Mkuu wa Wilaya ya Mtwara @kyobyad amezindua rasmi zoezi la upandaji miti katika shule ya msingi Kwale, iliyopo Manispaa ya Mtwara Mikindani.

Akizungumza wakati wa zoezi Hilo, KYOBYA ameeleza kuwa miti hiyo imetolewa na wakala wa Misitu (TFS), na baada ya hapo, zoezi Hilo litaendelea katika kata zote zilizopo Manispaa ya Mtwara Mikindani na kuongeza kuwa, Lengo la Wilaya hiyo ni kupanda miti Milioni 4.5.

Aidha ametumia nafasi hiyo kutoa wito kwa wakuu wa shule za Msingi na Sekondari zote kuhakikisha kwamba wanapanda miti hasa kipindi hiki Cha Mvua.

Kwa upande wake Mwakilishi wa muhifadhi wa Misitu kutoka Wilaya ya Mtwara Innocent Mkasu amesema Taasisi hiyo imetoa miti elfu kumi na sita kuashiria uzinduzi rasmi wa zoezi la upandaji miti, na kuwaomba wananchi Pamoja na taasisi zingine kwenda kuchukua miti Bure katika ofisi za TFS Ili kuendeleza uhifadhi wa misitu.

Nae Mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi Kwale mwl Costansia ameshukuru na kupongeza zoezi Hilo kufanyika katika shule hiyo, na kuongeza kuwa wamejipanga kuiendeleza miti hiyo kwa kuhakikisha inapata huduma ya maji mbolea Ili kufikia malengo ya serikali .

#nyakatizakusisimua
 
😁😁😁 hii ni baada ya mama kusema kwamba teuzi zilikuwa za kuwapima ma dc kuangalia kwanza kwa mda mchache wakoje, mkeka kamili nasikia unatoka baada ya wiki chache wa nani kafeli na nani aendelee.
 
Hongera sana Mh DC kwa kazi nzuri unayofanya huyu ni miongon mwa viongozi vijana kabisa nchini wanaoonyesha maana ya Dhamana ya uongozi hapa nchini ,hakika Mama ameupiga mwingi kuwapa vijana kama huyu dhamana ya kuongoza wilaya za pembezoni kabisa
 
Back
Top Bottom