Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 75,203
- 157,374
Ngoja nikumegee kidogo, hivi unajua kama Kukimbia madeni ni hatari kuliko kuyakabili? Unapokuwa na deni au madeni siku zote ni mzigo, ambao unatamani siku moja ungepata nafasi ya kuutua. Hivyo basi ni vizuri kuangalia namna ya kuutua huo mzigo.
Mimi na wewe tunakubaliana kwamba huwa tunakopa kwasababu ya kutatua shida zetu sio vinginevyo, na mara zote kama kweli uko sawa ukiwa unakopa nia na madhumi ni kuja kurudisha hicho kiasi siku moja. Hivyo basi endapo umeshindwa kurudisha kwa wakati zipo namna za kukabiliana na mdeni wako nazo ni hizi hapa:
Mimi na wewe tunakubaliana kwamba huwa tunakopa kwasababu ya kutatua shida zetu sio vinginevyo, na mara zote kama kweli uko sawa ukiwa unakopa nia na madhumi ni kuja kurudisha hicho kiasi siku moja. Hivyo basi endapo umeshindwa kurudisha kwa wakati zipo namna za kukabiliana na mdeni wako nazo ni hizi hapa:
- Dumisha mawasiliano na mdeni wako, mueleze wakati na hali uliyo nao. Usimfiche jaribu kueleza kiundani kwanini umeshindwa kulipa kwa wakati na pia muonyeshe masikitiko yako juu ya hilo.
- Toa ahadi itakayo kuweka huru, Kwa mfano Unampa mtu ahadi kuwa nitakulipa tarehe kumi na mbili, wakati wewe ni mfanya kazi na unategemea mwisho wa mwezi na huna namna yoyote ya kupata pesa hapo katikati. Wakati mwengine unaweza kutoa ahadi ilikumpa moyo mdeni wako lakini ujue unajiweka kwenye matatizo makubwa Zaidi. Kumbuka kwamba unapo mpa mtu ahadi naye anaweka mipango yake, ukitoa ahadi nyingi zisizotimia kumbuka pia unapunguza uamini kwake.
- Hakikisha unajipa muda wa kutosha, na kuwa na uhakika na ahadi unazotoa, hakuna kitu kinacho kera wadai kama ahadi nyingi zisizo na mwisho
- Punguza deni kidogo kidogo, wakati mwengine labda ni ngumu kupata pesa yote na kulipa kwa wakati lakini unaweza kuwa unapata kidogo kidogo. Nivizuri kupunguza kwani inajenga uamini Zaidi na pia huonyesha nia ya kweli ya kulipa deni.
- Usisuburi hadi mdeni wako kukupigia simu kukuuliza kuhusu “ unalipa lini”. Piga simu kabla yake na eleza maendeleo ya marejesho.
- Onana na mdeni wako uso kwa uso kama inawezeka, kuonana na mdeni wako physically inasaidia kuonyesha emotions au hisia. Hata ukimueleza jambo au kwanini umekwama kulipa deni inakuwa rahisi kukamata hisia zake pia. Pia inajenga ukaribu na heshima kwamba umeamua kumtafuta na kuongea nae.
- Pia kumbuka kwamba mdeni ni mtu, Wakati mwengine mtu baada tu ya kukopa na simu hapigi tena hata yale mahusiano ya kawaida yanapungua. Hii inaharibu sana, nayeye siku pia akija kukudai atakudai kama hakujui na hatakusiliza shida zako.
- Kwakumalizia: Hizi ni namna tu za kudili na madeni mambo yanapokuwa magumu, ila dawa kubwa ya deni ni kulipa au kutokopa.