Dar: Wauaji Waliomuua Askari Polisi (OCD) huko Kinyerezi, wakamatwa

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,485
SIKU moja baada ya kuuawa Mkuu wa Polisi Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma, Amedeus Malenge, watu wanaodaiwa kuhusika na tukio hilo wametiwa mbaroni.

Watuhumiwa hao walikamatwa usiku wa kuamkia jana, Kinyezi Kanga Dar es Salaam, baada ya msako mkali uliohusiha askari wa kikosi maalumu kutoka Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Jeshi la Polisi kiliambia MTANZANIA jana kuwa watuhumiwa hao walikamatwa baada ya kuhusishwa na tukio hilo la mauji ya kinyama.

Malenge ambaye ambaye alihamishiwa wilayani Uvinza akitokea Kibaha mkoani Pwani ambako alikuwa Ofisa Upelelezi wa wilaya, aliuawa juzi saa 4.00 usiku.

“Ni kweli wamekamatwa baada ya msako mkali wa polisi,” alisema mtoa taarifa huyo ambaye hakutaja kutajwa jina gazetini kwa kuwa si msemaji wa polisi na kuongeza:

“Marehemu alikuwa anapita na gari yake jirani ya nyumba yake moja ambayo bado haijaisha. Akiwa katika hilo eneo alimuona mtu mmoja ambaye walikuwa wakifahamiana akilalamika kuwa kuna watu walikuwa wanataka kumuua huku akimwita kwa jina ili amsaidie.

“Marehemu aliposhuka aliuliza ‘kulikoni mbona mnataka kumpiga, kulikoni’.

“Ghafla alitokea mtu kwa nyuma akampiga kwa shoka kichwani akafariki papo hapo”.

MTANZANIA ilipomtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilipolisi wa Ilala, Salum Hamduni kupata ufafanuzi wa suala hilo, simu yake ilipokewa na msaidizi wake ambaye alisema alikuwa kwenye majukumu ya kazi.

“Mimi si kamanda ila mimi ni msaidizi wake, kamanda yupo kwenye majukumu na kama unamhitaji atakupigia baada ya muda wa dakika 10 kutoka sasa,” alisema msaidizi huyo wa Kamanda Hamduni na kukata simu.

Chanzo: Mtanzania
 
Wauwaji wasiwe wanapelekwa mahakamani,wauwawe tu nawao..Hapa ndo huwa naona umuhimu wa kale ka utaratibu ka nchi ya saudia kakuwakata kichwa hadharani washenzi kama Hawa.
 
Bado ni watuhumiwa. Tunaomba watendewe haki yao.
Wakibainika kuua , haki yao in kifo na kinyume chake ni kweli
 
Kuna ushahidi gani kuwa ndio wauwaji?wacha sheria ichukue mkondo wake.
 
sa nne kamili(4:00)....
alimuona mtu wanae fahamiana...
akasema kulikoni mbona mnataka kumpiga..



wamejuaje aliuawa sanne kamili
hizo kauli kuna mtu alikua anarekodi?
walijuaje kuwa marehemu alimwona mtu wanae fahamiana

au hao walio kamatwa ndio wameyasema hayo ktk mahojiano?
apumzike kwa amani.
 
Mmefanya vizuri kutowataja majina kwani humu jf sasa kumetokea wanaharakati watetea dini. Ungelisikia, Ohh! Sasa mbona wa dini moja ni wengi zaidi ya dini ilee?? Unampiga mtu shoka, ati kisa kadhulumu kiwanja. Leo umekipata hicho kiwanja?? Nazidi kuamini kuwa hakuna uchawi wala majini tz. Mbona mmeacha kuyatumia hayo makitu mmerudi kutumia hata vitu vyenye ncha butu?? Ati vitu vizito!! Tumieni majini yenu na mauchawi yenu si kuua kinyama hivi.
 
Wauwaji wasiwe wanapelekwa mahakamani,wauwawe tu nawao..Hapa ndo huwa naona umuhimu wa kale ka utaratibu ka nchi ya saudia kakuwakata kichwa hadharani washenzi kama Hawa.
Sheria zetu haziruhusu utaratibu huwo! Mahakama ndio chombo pekee kinachotakiwa kutoa hukumu;
ingawa saa zingine kuna vyombo vingine vinaamua kuhukumu, kitu ambacho ni kinyume cha sheria!
 

Ninatamani usingekimbila kuandika hii habari ukasubiri kwa msemaji wa jeshi hilo juu ya hili ili upate habari za kuaminika.

Hilo gari la marehemu, alikuwa peke yake ama alikuwa na watu wengine?

Aliyesikia na kuona hayo majibishano, kwamba marehemu alisikia akiitwa jina, akashuka na kuanza kuhoji kwa nini wale watu walitaka kumpiga mwenzao, kuna nini, ninani ikiwa Marehemu alikuwa peke yake na alikufa?

Huyo aliyetaka kuuawa na wale watu, na kwa ajlili pengine ya kujihami hao wauaji, wakampiga Kamanda, yeye walimfanya nini baada ya hapo? Walimwacha aondoke na kwenda kutoa taarifa, au naye walimshughulikia?

Kama Kamanda walimkusudia, walifahamuje kwamba atapita eneo la nyumba hiyo akiwa kwenye gari?

Kama haya maswlai yangu hayana majibu, msihangaike kunijibu nitakuwa na jibu tayari na pia nitakuwa nimeshajua kwa nini habari hii imeandikwa hivi.

NI JAMBO LA HUZUNI SANA KWA KWELI. USIKUTE WALIKUWA WANATAKA KUMTOA KAFARA YA DAMU AU MAMBO MENGINE YA KIPUMBAVU TU.

HONGERENI JESHI LETU LA POLISI KWA KUFANYA KAZI KWA HARAKA NA NDANI YA MUDA. NINATAMANI NA SUALA LA KUWATAFUTA WATEKAJI WA BEN SANANE NALO LINGEFANYIKA KWA UHARAKA NA KWA KIWANGO HIKI!. MUNGU TUSAIDIE.
 
Msishangae hawa wauaji wakaibuka na mawakili wa hali ya juu wa kuwatetea.
Kila mtu ana haki ya kuwakilishwa...! Na tatizo au uzuri ni kwamba mbele ya sheria watu wote wanatakiwa wapewe treatment sawa bila kuangalia huyu ni mtuhumiwa ... mpaka mahakama itakapompata na hatia ...!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…