DAR: Utaratibu mbovu wa zoezi la uhakiki wa TIN, foleni bado ndefu

Mie najiuliza nini essence ya huu uhakiki!!? Maana hata kama ni suala la deadline basi useme kuna deadline kwa sababu fulani! Kwenye Uchaguzi kuna deadline kujiandikisha maana kuna Uchaguzi mbele.
Hahahaaa..... Huenda watatangaza baada ya deadline kuisha.
 
Mi mwenyewe nimeshaamua...liwalo na liwe...hamna namna...
Maana sioni mantiki...ndani ya mwaka mmoja lazima...lazima kila mwenye TIN atembelee TRA...kwa nini wasisubiri nikienda lipia road licence nimalize kila kitu badala ya kuturundika...

Afu nimeshangaa jana yule msemaji wao aliposema zoezi kwa Dar ndio linaisha...wanaamia kwingine...eeehhhh...ni mkoa kwa mkoa...basi ntaenda Moro kuhakiki...

Kuna jamaa yeye amenichekesha..amesema ataomba TIN mpya...maana wamesema watafuta za wasiohakiki....mi hata sielewi mantiki ya hili zoezi kwa kweli...au ndio fasheni...kila ofisi inahakiki...TRA utumishi...sijui wapi...
Zoezi lilianza mda mrefu sana, tangu september hadi deadline leo, kwa nini watu wasiende mwaka Jana, kama ungehakiki November haya yasingekukuta.

Lakini pia, mfanyabiashara ndio ataelewa wana maanisha nini kuhakiki TIN, dereva anaweza asielewe.
 
Afadhali nimepitia huu uzi maana mi ndio sikujua hata kama kuna uhakiki.
 
Mbn hili zoez lilikuwa lina muda tu ndug zang still kulikuwa hakuna folen we tanzanians we ar not good in time management and priority
 
Niliwapa taarifa zangu wakati najiandikisha kulipa kodi, naamini hawajazipoteza. Nikienda kwa huduma za kiofisi wahakiki, otherwise taarifa zangu zimepaswa kuwa zile zile.

Watumie anuani nilizowapa kuwasiliana nami, maana sijawahi kutumiwa hata kipeperushi na hawa jamaa kwenye box langu la posta.

Wangekuwa wanatoa tin mpya ningewaelewa.

Kama wanavyobadilisha noti.
 
Information hizo hizo kwenye:
  • Passport
  • Kitambulisho cha mpiga kura
  • Kitambulisho cha Taifa
  • TIN
Sitashangaa kesho wakianza uhakiki wa vyeti vya kuzaliwa na kutafuta information zile zile.

Ni kweli mkuu. Tatizo waafrika hatutumii akili mpaka aje mzungu atukumbushe kuwa kuna tatizo na tunahitaji kuunganisha (Integrate) mifumo yote ili kuepuka kurudia mambo yaleyale na kuunda mifumo inayo kanyagana (parallel systems). Gharama za kuendesha mifumo hii ni kubwa (transactional costs). Wataalamu wa IT tunao wengi lakini hatuwatumii.
 
TRA kwa kweli wapuuzi sana, wana data za walipa kodi wote, iweje wanawaita wananchi wote wenye TIN kuhakiki..? What..? Wana TIN zote ktk data base ya TRA, unahakiki nn, kama kuna mtu anadaiwa wana jua TIN yake, ni nani na yuko wapi wana contacts zake, wanampigia simu tu.. ila wanafanya vitu very very very LOCAL WAY, PRIMITIVE way.. how can you hakiki watu nchi nzima kwa foleni wenye TIN..? Hivi vichwa vingine vimejaa matope tupu, they have to do electronically.. na anayedaiwa anapigiwa simu tu sbb wana contacts zote za walipa kodi..

Hapa kuna ku deal linachezwa.. just wait
 
Hataa wangesema zoezi ni la miaka 10,ile cku ya mwisho kungekua na foleni na watu wangelalamika tu,tatizo watu wanakaaaaa wanangoja deadline ikifika wanaenda rundikana kwenye mifoleni na kuanza kulalamika.ha ha haaaa
 
Hataa wangesema zoezi ni la miaka 10,ile cku ya mwisho kungekua na foleni na watu wangelalamika tu,tatizo watu wanakaaaaa wanangoja deadline ikifika wanaenda rundikana kwenye mifoleni na kuanza kulalamika.ha ha haaaa
uelewi arguments za watu...watu hawataki kusikia kitu kinaitwa zoezi...bila hilo neno watu wasingejaa huko TRA with or without deadline maana deadline ingetoka wapi bila neno zoezi...?

hivi wana haraka gani kusubiri watu wanaoenda kufata huduma na kuwajazisha hizo form...kuna emergence gani? mfani mimi kila may naenda kulipa road licence na sina biashara kwa nini nikiwa nalipa wasinipe form nijaze badala ya kunikurupua now niende nikapange foleni?

Kama basi ni lazima wanede TCU wapewe shule jinsi ya kutumia online facilities...hivi wako kwenye phase goni ya e-government ambako wanarundika makaratasi (paperworks) afu waanze upya data entry?!

Hapa ukawii kusikia hata nyie mlio jaza form mnaambiwa hamkujaza...chezea makatatasi wewe...ya watu milioni...
 
Tatizo lenu mnapenda kufanya vitu kwenye deadline.. Zoez limefanyika kwa zaidi ya miezi sita haingii akilini mpaka leo hii hujamaliza kuhakiki

Kwa nini wafunge kwani hizo siku zingine watakuwa wanafanya kazi gani.
Mie walinipa TIN mwaka 2003 ya leseni. Hii miezi sita kama ni kweli unavyosema ni michache sana kurekodi watu wote waliopewa TIN kwa miaka yote hiyo. Kwanza kwani wana kazi gani zaidi ya hayo makaratasi kila siku si waendelee tuu.

Maana sasa wanatuajiri wote sasa tunafanya kazi TRA. Kwanza walioaswa kutufuata site zetu wajaze fomu zao waondoke nazo. Sio kutushindisha hapo kwao.
 
Hizo ni kazi zao sio zetu sisi. Kwani wameajiri wafanyakazi wapya kwa kazi hiyo ? Si wale wale. Basi wangekaa wamsubiri kila anayekuja kupata huduma wana mpa hayo makaratasi anajaza.
Kwanza kuna vitu sijawahi kuona application zake na kama zipo labda ni 0.03%.
Hivi fingerprint umeshaona inatumika wapi. Wanaitumiaje kwenye kitu gani hizo au wanachukua tuu kama fashion
 
Back
Top Bottom