Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,714
- 13,464
Wadau wa haki Nchini Tanzania wanakaribishwa kujitokeza kwa wingi kuungana na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anayetarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya miaka 10 ya Haki za Binadamu, leo Mei 13, 2022 kwenye Ukumbi wa PSSSF Jijini Dar es Salaam
Shughuli hiyo inatarajiwa pia kuhudhuriwa na mabalozi kutoka Nchi 15 wadau wa maendeleo.
Mgeni Rasmi Rais Samia ameshawasili ukumbini, shughuli imeanza:
NENO KUTOKA KWA RAIS NA WADAU
HAMIS RAMADHANI ABDALLAH, KAIMU JAJI MKUU WA ZANZIBAR
Mh Rais, Niwasalimu kwa Jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Tuna kila sababu ya kuwepo hapa kwani tangu mtandao huu umefungua ofisi zake Zanziba, wametufanyia mambo mengi.
Baada ya kupewa nafasi ya Kukaimu nafasi hii, nilionana na Onesmo Ole Ngurumwa.
Mahakama zina matatizo mengi, ambapo kwa namna moja au nyingine haki za binadamu zinavizwa. ikiwamo mashauri kutosikilizwa haraka na maamuzi kutopatikana mienendo ya mashauri.
THRDC wametusaidia kujenga uwezo kwa Mahakimu na Majaji na Makadhi katika kusimamia Haki za Binadamu. Pia tulifunga nao hati ya makubaliano rasmi katika ya kusaidiana katika mambo mbalimbali kwa dhima ya kuboresha katika Mahakama zetu
Tumeshirikiana nao pia kutengeneza Needs Assessment (Mahitaji ya Mahakama) na hiyo kazi inaendelea na tunatarajia kuipokea, na hiyo ndiyo itakuwa foundation ya maboresho ya Mahakama
BI. SANDRA, KWA NIABA YA BALOZI WA SWEDEN NA UMOJA WA ULAYA
Kila nchi ina wajibu wa kulinda haki za binadamu za raia wake, kujenga, kuunga mkono na kudumisha mfumo wa kisheria unaozingatia mikataba ya haki za binadamu.
Duniani kote watetezi wa haki za binadamu wanakabiliwa na unyanyasaji, vitisho na wakati mwingine hata kuhatarisha maisha yao kwa ajili ya haki za wengine.
Wajibu wa watetezi wa haki za binadamu hutofautiana kulingana na wakati pamoja na mahali na inategemea mazingira wanayofanyia kazi. Wanaweza kuwa watetezi wa haki ya uhuru wa kuzungumza. Au watetezi wa haki ya kumiliki ardhi. Au watetezi wa haki ya kupenda. Au watetezi wa ushiriki katika uchaguzi huru na wa haki.
Baadhi ya watetezi wa haki za binadamu wanalenga katika kuhimiza serikali kutimiza wajibu wake wa haki za binadamu. Kwa mfano, kwa kutangaza taarifa za rekodi za utekelezaji wa serikali wa viwango vya haki za binadamu, na kufuatilia maendeleo yaliyopatikana.
ONESMO OLENGURUMWA, MRATIBU WA TAIFA WA THRDC
Ili tuweze kutambuliwa vizuri, tunaomba Sera inayotutambua. Tumepata changamoto nyingi ikiwemo kubambikiwa kesi
Aidha, ili Mtandao wetu ufanye vizuri, tunahitaji eneo ambalo Watetezi wote wanaweza kukutana. Hatuna eneo la kujenga
Wanachama wanafahamu wakati mwingine ilivyo changamoto kupata Vibali, wakati mwingine tunahisiwa sisi ni Wapinzani
Changamoto zimekuwa zikitukwaza na kutuzuia tusifanye kazi zetu vizuri
Tunaomba Sera inayotutambua, tumepata changamoto nyingi ikiwemo kubambikiwa kesi, kupata vibali vya kazi. Aidha, ili Mtandao wetu ufanye vizuri, tunahitaji eneo ambalo Watetezi wote wanaweza kukutana
Wakati wa uchaguzi mwaka 2020 tulipata changamoto nyingi, tunashukuru ujio wa Rais Samia Suluhu umeleta unafuu mkubwa kwa watetezi wa Haki za binadamu
DKT. NDUMBARO, WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA
Moja kati ya Haki ya Msingi ya Binadamu ni Haki ya Kuishi, bila hiyo nyingine zote hazitekelezeki
Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa akisafiri sehemu mbalimbali kupigania Haki za Kiuchumi ambazo ni miongoni mwa Haki za Binadamu
Moja ya jambo kubwa ambalo umefanya linaloonesha wewe ni mtetezi wa haki za binadamu ni kitendo cha kufungukua vyombo vya habari na kuvitaka vitende haki na waheshimu haki za binadamu
Hapo umegusa Ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ambayo inaongelea uhuru wa kutoa maoni, umeitekelezea kwa vitendo ndiyo oksijeni ya demokrasia duniani. Hata wanaoongea kinyume umekuwa muungwana kwa kuwavumilia
RAIS SAMIA SULUHU HASSAN
Mimi nilikuwa nafanya kazi zangu nilizoapa kufanya, sikujua nafanya Haki za Binadamu. Nashukuru kwa kutambua kazi nilizofanya ndani ya mwaka mmoja
Nawashukuru wote kwa kufanikisha maadhimisho haya. Nipo hapa kuwahakikishia tupo pamoja
Nakubaliana na dhana ya utetezi wa Haki za Binadamu. Serikali ni Mtetezi wa Haki za Watu katika nyanja mbalimbali
- Mtetezi Mkuu wa Haki ni Katiba
Mtetezi Mkuu wa Haki hapa Nchini ni Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Katiba hiyo ndio sheria mama, ina haki zote za wanadamu wanaoishi Tanzania, Swali langu, je, hao wanadamu tunaowatetea wanaijua hiyo katiba?
Naacha kazi kwenu, waelewesheni watu waijue katiba yao. Wanapodai haki lazima wajue wajibu wao, wakieleweshwa vizuri watajua wakibu wao kikatiba
- Tuzingatie Mila na Desturi zetu
Tanzania tuna mila na desturi zetu, tuna sheria zetu za ndani na tuna mambo ambayo tunayafanya tofauti na wengine. Kwahiyo tunapofanya utetezi tuangalie kwenye maeneo hayo.
Serikali inayo kazi kubwa kuhakikisha kwamba Haki ya kila mmoja haiingiliwi na mwingine kamailivyobainishwa kwenye Ibara ya 29 na 30 ya Katiba yetu
Hii inawezekana endapo kila mmoja atatenda wajibu wake, ndiyo mana nasema watu wafundishwe, wafahamishwe
- Tusijikite tu kwenye Haki za Kisiasa
Nilikuwa naangalia, najiuliza utetezi wa Haki. Kwa muda mrefu tulikuwa tumejielekeza kwenye kutetea Haki, lakini hata nyie wanamitandao mmejielekeza zaidi kwenye Haki za kisiasa kuliko haki nyingine.
Nilikuwa nasema, kuna tatizo kubwa la ubakaji, si Zanzibar tu hata huku, vya kike na vya kiume. Lakini sauti hazijaja juu sana kama ambavyo mnasema kuhusu haki za kisiasa.
Kuna watu wanakatwa mapanga na Panya Road, sijui kama metetea haki zao zaidi ya kusema Polisi wafanye kazi yao. Lakini je, mmejipangaje kuongea na vijana, kuwaelewesha haki na wajibu wao kama vijana?
Lakini pia kuna watu wengi wanakufa kwenye ajali, je mnafanya nini? Nimewasikia Mtandao wa Usalama barabarani lakini sauti haijaja juu kama ilivyopaswa kuwa.
- Kuhusu Kuwahamisha Wana-Ngorongoro
Wakati napita kwenye maonesho yenu, nimeona banda la Maliasili – wanasema wanatetea haki za Maliasili za Tanzania. Tuna migogoro ya Maliasili; najua mmefanya kazi, mmetoa machapisho, lakini je, tunapokwenda kuulinda urithi wa dunia uliopo Tanzania kama vile Ngorongoro, siyo mitandao yenu inayowatetea wanaoharibu urithi wa dunia waendelee kubaki na kuendelea kuharibu urithi huo wa dunia? Ni mitandao yenu. Kwa mrengo wa kusema ni Haki za Binadamu.
Lakini kumbe kuna taasisi ya Maliasili. Je, mmekaa mkazungumza mkaona lipi lina uzito? La kuacha watu waharibu urithi wa dunia na tukose ile maliasili, au tulinde maliasili na wahusika watendewe haki wapelekwe pahali pazuri?
Hilo hamjakaa mkazungumza, naliacha kwenu.
Kuna mambo mengi ya kufanyia kazi Tanzania. Njooni tufanye kazi.
- Tuachane na mambo ya "Aluta Continua!"
Nimemsikia mdogo wangu, Hassan, Mwenyekiti [wa Watetezi wa Haki za Binadamu Afrika], Aluta Continua! Nikasema hivi wana-continue na mapambano ya nini? Hivi tunapaswa kupambana au tunapaswa kukaa na kuzungumza na kufanya kazi?
Nataka niwahakikishie wanangu na ndugu zangu, kwangu mimi mapambano hakuna. Hakuna. Hakuna. Nikisikia watu wanakuja na ile Aluta Continua! – uanaharakati. Uanaharakati can be both, siwezi kuwakataza kuwa wanaharakati – mnaweza kuwa positive au negative. Lakini uanaharakati positive unajenga zaidi. Fanyeni uanaharakati, ibueni maovu yanayofanyika. Njooni tukae tuzungumze.
Waziri yupo hapa, vyombo vyetu vya usalama vipo. Ataitisha tutakaa kitako tutazungumza.
Wote hapa ni Watanzania. Hakuna wa kupambana na Serikali. Unapambana na Serikali kwa jambo gani? Hakuna. Niliwaambia wenzenu wa Vyama vya Siasa. Tunapambana kwa kitu gani? Wote tunaendesha siasa za Tanzania, wote lengo letu kujenga Tanzania. Mnajigawa mafungu mnakwenda kupambana, mnapambana kwaajili gani?
Na ndiyo maana tukasema fanyeni Harakati za Haki za Binadamu kulingana na mazingira ya Kitanzania. Mazingira ya leo. Kama mlikuwa Wanaharakati wa Aluta Continua!, badilikeni wanangu.
- Mama hapambani, anaweka mambo sawa
Msiende tena kupambana, mnapambana nan ani? Na fortunately Tanzania ina Mama – Mama anapambana? Mama hapambani. Mama anaweka tu mazingira sawa mambo yaende. Mama hapambani.
- Sera ya R Nne (4) za "Kizungu"
Nilipokuwa Marekani niliwaona wenzenu na mabango nikawaambia nimewaona. Nikawaambia nimekuja na Sera ya R 4 za Kizungu.
R No. 1 = Reconciliation. Na katika kwenda kwangu mtaniona nafanya Reconciliation. Nimeanza. Itafanyika.
R No. 2 = Resilience. Mabadiliko ya kurudi tulikokuwa. Tukae, tufanye hivyo.
R No. 3 = Reforms. Baada ya ku-reconcile na kubadilishana, sasa tufanye reforms.
R No. 4 = Rebuilding: Baada ya Reforms tutajenga tena taifa letu.
Sasa kama kuna Sera hiyo ya Serikali, nyie mnapambana na nani?
- Kama Sheria haipo vizuri semeni
Kama sheria haipo vizuri semeni, lakini msiseme kwa mapambano, semeni kwa lugha nzuri, unaweza kumrekebisha mtu kwa lugha nzuri, ukitumia lugha mbaya unaweza kumkasirisha kama mlivyokuwa mnafanya zamani,