Dar: Ndege ndogo yaanguka Kitunda, ilikuwa inatokea Mufindi

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,500
3,481
Ndege ndogo aina ya Cessna 150G yenye usajili wa TCAA namba 5H-BOB imeanguka leo jioni katika eneo la Kitunda Mnadani/relini. Ndege hiyo ilikuwa katika hatua za mwisho kabla ya kutua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam.

Taarifa zinasema kulikuwa na watu wawili ndani ya ndege hiyo na wote wametoka wazima, hakuna majeruhi.

Mpaka sasa chanzo cha ajali hiyo hakijafahamika, vyombo vya usalama vinaendelea na uchunguzi.

FB_IMG_1599503593181.jpg
FB_IMG_1599503588086.jpg
FB_IMG_1599503582021.jpg
 
Back
Top Bottom