GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 59,949
- 119,214
Katika hali isiyo ya kawaida kabisa na ambayo imewashtua wengi muda si mrefu waandaaji wa michuano iliyojizolea umaarufu nchini ya Ndondo Cup wametoa taarifa yao kwamba kwa masikitiko makubwa na kwasababu zilizo nje ya uwezo wao mechi zote za 16 bora ambazo zilikuwa zichezwe katika uwanja wa Bandari Tandika maarufu kama Wimbledon sasa hazitachezwa tena hapo na zitachezwa katika uwanja wa Kinesi.
Ikumbukwe kuwa ujenzi wote wa uwanja huu na marekebisho yake ambayo kiukweli yameupendezesha sana huo Uwanja kwa kiasi kikubwa uliratibiwa na ' Dar es Salaam Chief ' ambaye kwa sasa hakuna asiyejua kuwa ana ' bifu ' kali sana na Clouds Media Group ( CMG ) hasa kutokana na kilichotokea ambacho kila Mtanzania anakijua.
Taarifa za ndani kabisa zinasema kwamba ' Dar es Salaam Chief ' ameamua kula sahani moja na ' projects ' zote za CMG ambazo anaona kuwa zina maslahi kwao hasa ya kuwapa ' umaarufu ' kuliko ambao anao Yeye hivyo anahakikisha ' anawakomoa ' hadi wasalimu amri Kwake kama ambavyo Africa Media Group ( AMG ) wamiliki wa Vituo vya Magic fm na Channel Ten walivyosalimu amri Kwake na kuamua ' kumlamba ' miguu hadi visigino vyake na kuendelea ' kumpamba ' na kutupilia mbali yale ' maazimio ' ya MOAT na UTPC.
Uamuzi huu utakuwa na ' athari ' kubwa sana kwa ' Waandaaji ' Clouds Media Group kwani tayari ' logistics ' zote za kuelekea hatua hii ya michuano ya 16 ya Ndondo Cup zilikuwa zimekamilika huku CMG wakiwa wametumia ' Pesa ' nyingi sana kuugharamia huo Uwanja hadi kukamilika hivyo huku wakifanya ' promo ' lakini kwa bahati mbaya sana leo ' Mamlaka ' ya Mkoa umepeleka taarifa ya kuzuia ' michuano ' hiyo isichezwe hapo kwa kutoa sababu za ' Kitoto ' kabisa ambazo hazina kichwa wa miguu.
Kwa hiki kinachoendelea na kwa ' nguvu ' ya ajabu aliyonayo ' Dar es Salaam Chief ' ambacho kilipelekea Sahara Media Group kusalimu amri Kwake, jana tena African Media Group nao wamesalimu amri naona ni suala la muda tu hata Clouds Media Group nao watasalimu amri Kwake kwani kiukweli ' Jamaa ' anatumia ' Umafia ' wa hali ya juu katika ' Kuvikomoa ' Vyombo vya Habari vya Tanzania na ' Mabosi ' wao.
Mwisho nitoe tu ' Wito ' kwa TEF, MOAT na UTPC haraka sana waje na ' tamko ' lao jingine juu ya haya yanayoendelea kwani kuna kila dalili kuwa kuna ' mpasuko ', ' usaliti ' na ' unafiki ' mkubwa unaoendelea katika Vyombo vya Habari vya Tanzania ambao usipodhibitiwa haraka utaweza hata kushusha ' Heshima ' ya Media kwa Watanzania wote.
Kwa anayetaka chanzo cha taarifa ya kutotumika tena kwa uwanja wa Bandari Tandika ' Wimbledon ' aingie katika ' Mtandao ' wa Shaffih Dauda.com ambaye kimsingi Yeye ndiyo ' Mratibu ' Mkuu wa haya mashindano pendwa ya Sports Extra Ndondo Cup isipokuwa maelezo mengine hayo ni ' mtazamo ' wangu tu wa ' Kiudukuzi '.
Poleni sana Clouds Media Group na ama hakika mwaka huu Kazi mnayo kwa ' Dar es Salaam Chief ' na sasa michuano ya Ndondo Cup 16 bora inahama kutoka kwenye ' Nyasi ' za Kisasa Bandari Tandika na inarudi ' vumbini ' Kinesi.
Nawasilisha.